Ukafiri wa mwenye kuacha swala

 IJMAA YA MASWAHABA JUU YA UKAFIRI WA MWENYE KUACHA SWALA.




أقوال الصحابة في كفر تارك الصلاة وإجماعهم على ذلك.


Kauli za maswahaba juu ya ukafiri wa mwenye kuacha swala, wa wamekubaliana juu ya hilo..



🔹 قال عمر بن الخطاب :


Amesema Umar Ibn Al Khatwaab (radhiyaAllahu anhu)

لا حظ في الإسلام لمن ترك الصلاة .
وقال أيضًا : لا إسلام لمن لم يصل الصلاة .

Hana kitu katika uislam mwenye kuacha swala, na akasema tena, hana uislam ambae hatekelezi swala.


🔹وقال علي :

Amesema Aliy (radhiyaAllahu anhu).



من لم يصل فهو كافر .

Ambae haswali huyo ni kafiri.


وقال أيضًا :

Na akasema pia.

من ترك صلاة واحدة متعمدًا فقد برئ من الله وبرئ الله منه " .

Atakaecha kipindi kimoja cha swala atakuwa amejiweka mbali na Allah na Allah atakuwa amejiweka nae mbali.


🔹 وقال عبد الله بن مسعود :

Na amesema Abdillah Ibn Mas'uud (radhiyaAllahu anhu).

فإن تركها الكفر"

Ikiwa ataiacha basi amekufuru.


وقال أيضًا :

Na amesema pia.

من لم يصل فلا دين له .

Ambae haswali basi huyo hana dini.


🔹 وقال عبد الله بن عباس:

Na amesema Abdillah Ibn Abas (radhiyaAllahu anhum)

من ترك الصلاة فقد كفر.

Atakaeacha swala hakika huyo amekufuru.


🔹 وسئل جابر بن عبد الله :

Na aliulizwa Jaabir Ibn Abdillah (radhiyaAllahu anhum).

ما كان يفرق بين الكفر والإيمان عندكم من الأعمال في عهد رسول الله ؟

Ni matendo gani mlikuwa mnawatofautisha watu kati ya muumini na kafiri kipindi cha Rasulullah (swala Allahu alayhi wasalama)?

قال: الصلاة .

Akasema, Swala.


وقال أيضا :

Na akasema pia.


بين الرجل والشرك والكفر ترك الصلاة .

Kati ya mtu na ushirikina na ukafiri ni kuacha swala.


🟢 قال الحسن البصري :

Amesema Al Hasan Al Baswariyh (rahimahuAllah).


بلغني أن أصحاب رسول الله صلى الله عليه وسلم كانوا يقولون : بين العبد وبين أن يشرك فيكفر أن يدع الصلاة من غير عذر .

Nimekutana na Maswahaba wa Rasulullh (swala Allahu alayhi wasalama) walikuwa wakisema, kati ya mja na ushirikina na ukafiri ni kwamba anaacha swala bila ya udhru.


🟢 وعن عبد الله بن شقيق قال :

Na kutoka kwa Abdillah Ibn Shaqiyq Amesema.

كان أصحاب محمد لا يرون شيئًا من الأعمال تركه كفر إلا الصلاة .

Walikuwa maswahaba wa Muhammad (swala Allahu alayhi wasalama) wakiona tendo ambalo mtu akiliacha anakufuru kuliko swala.


🔸 وقال سعيد بن جبير :

Na amesema Said Ibn Jubayr

من ترك الصلاة متعمدًا فقد كفر .


Mwenye kuiacha swala pasina ya udhru atakuwa amekufuru.


🟡 وهو مذهب الشعبي ، وأيوب السختياني ، والأوزاعي ، وحماد بن زيد ، وابن المبارك ، وإسحاق بن راهويه، وأحمد.

Na hiyo ndio madhhab ya Shaabiy, na Ayuub As sakhtiyaaniy, Na Al Awzaiy, na Hamaad Ibn Zayd na Ibn Mubaaraka na Is'haaqa Ibn Raahwiyah na Imam Ahmad.


 🟣 وهو مذهب جمهور أصحاب الحديث .

Na hiyo ndio madhhab ya jumuhuur ya watu wa hadiyth.


قال ابن رجب : وكثير من علماء أهل الحديث يرى تكفير تارك الصلاة وحكاه إسحاق بن راهويه إجماعًا منهم ، حتى إنه جعل قول من قال : لا يكفر بترك هذه الأركان مع الإقرار بها من أقوال المرجئة .

Amesema Ibn Rajab, na wengi katika ulamaa wa hadiyth wanamkufurisha mwenye kuacha swala, na amelichukua hilo Is'haaqa Ibn Raahwiyah kama Ijmaa miongoni mwao, mpaka wanaona kuwa mwenye kusema hakufurishwi mwenye kuacha nguzo hii moja na akalirudia rudia kuwa mtu huyo ni murjia.


• وقال إسحاق بن راهويه كما ذكره الإمام محمد بن نصر :

Na amesema Is'haaqa Ibn Rahawiyah kama alivyotaja Imam Muhammad Ibn Naswri.


قد صح عن رسول الله أن تارك الصلاة كافر ، وكذلك كان رأي أهل العلم من لدن النبي صلى الله عليه وسلم إلى يومنا هذا ، أن تارك الصلاة عمدًا من غير عذر حتى يذهب وقتها كافر.

Imeswihi kutoka kwa Rasulullah (swala Allahu alayhi wasalama) kwamba mwenye kuacha swala ni kafiri, na hiyo ilikuwa rai ya wanachuoni toka kipindi cha Rasulullah (swala Allahu alayhi wasalamal mpaka hivi leo, kwamba mwenye kuacha kipindi cha swala pasina udhru mpaka muda wake ukapita atakuwa amekufuru.


🔴 فائدة: أما ما جاء عن بعض أهل العلم من أن تارك الصلاة لا يكفر حتى يجحد أو ينكر وجوبها فهذا الجواب عليه من وجهين:


Faida. Ama yale yaliyokuja katika baadhi ya wanachuoni kuwa mwenye kuacha swala hakufurishwi mpaka apinge uwajibu wake au aichukie uwajibu wake , jawabu hili lipo katika pande mbili.

الأول : أنه لا عبرة به لأن إجماع الصحابة قاطع بنقض مثله، فلا مذهب بعد مذهب الصحابة . Kwanza. Jibu hili halina mazingatio kwa sababu ijmaa ya maswahaba imeshahukumu mfano huo, na kwa hakika hakuna madhhab baada ya madhhab ya maswahaba. والثاني: أن الجحود والاستحلال وإنكار الوجوب لا يختص بالصلاة ، فكل الشعائر من يستحلها أو يجحدها أو ينكر وجوبها يكفر. Na pili. Ama kupinga na kuhalalisha na kuchukia uwaajibu hakuwi makhsusi kwenye swala tu, kwani kila shaair anaehalalisha au kupinga uwaajibu wake au kuchukia uwaajibu wake, anakuwa amekufuru... هذا والله اعلم.....

0 Comments