Nasiha: Swiyaam Tarehe 9 na 10 Al-Muharram zimesisitizwa na fadhila zake ni kufutiwa madhambi ya mwaka mzima kwa dalili kauli ya Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam):
((صِيَامُ يَوم عاشوراء إنِّي أحْتَسبُ علَى اللهِ أن يُكفِّرَ السَّنةَ التِي قبلَه)) رواه مسلم
"Swawm ya siku ya 'Ashuraa, nategemea kutoka kwa Allaah Ayafute madhambi ya mwaka uliotangulia." [Muslim]
Asiyejaaliwa kufunga tarehe 9 basi asikose Swawm ya tarehe 10 Al-Muharram pekee.


0 Comments