
Vipimo
Viazi 4
Vitunguu nyasi vilokatwakatwa 3 miche
Kitunguu maji kilokatwakatwa 1
Chumvi 1 kijiko cha chai
Bizari ya pilau nzima ( jeera) 1 kijiko cha chai
Mafuta Nusu kilo
Manda za tayari 10 - 20
Yai 1 au 2
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
Menya viazi, vioshe vikate slesi kisha vikatekate vipande vidogo vidogo.

Chemsha maji kidogo ukiwa umeyatia chumvi , kisha vimimine viazi ndani ya maji yawache paka uwone tena yachemka kwa mara ya pili acha kwa dakika 10 - 15, kisha ondoa jikoni.
Mimina katika chujio uchuje maji .
Roweka bizari kwenye maji kwa muda wa dakika 20 hivi.
Chukua bakuli kubwa lenye nafasi mimina viazi, vtunguu nyasi na maji, chumvi, mafuta vijiko 2 – 3 vya supu, na bizari. Changanya vizuri.
Tandaza manda mezani au kwenye kibao fanya mkunjo wa sambusa kisha paka yai kwa brashi, kunja upate pembe moja . Tazama picha.

Jaza viazi sehemu ulokunja kisha funga sambusa.


Tia mafuta katika karai, yakipata moto, tia sambusa ziikaange hadi zigeuke rangi ya dhahabu.
Zitoe na zichuje mafuta tayari kuliwa

0 Comments