watu 500 wameuawa huko Gaza Palestina kufuatia shambulio la anga lililofanywa na jeshi la utawala haramu wa Israel, dhidi ya hospitali ya Al Ahli Arab.
Kwa mujibu wa duru za Palestina, zaidi ya watu 500 wameuawa katika mashambulizi ya mabomu katika hospitali hiyo.
Mamia ya watu waliokimbia makazi yao walikuwa wamejihifadhi katika ukumbi kwenye uwanja wa hospitali, kulingana na wenyeji.
Picha zinazotoka katika hospitali ya Al Ahli Arab au Maamadani zinaonyesha matukio ya kutisha huku watu waliojeruhiwa wakitolewa nje kwa machela gizani.
Miili na magari yaliyoharibiwa yanaonekana yakiwa kwenye barabara iliyojaa vifusi.
Huku ikilaani vikali shambulio hilo baya, Harakati ya Hamas imesisitiza kuwa jinai hizo zinaonyesha tabia ya kinyama ya Wazayuni ambayo imejidhihirisha vyema.
Rais wa Palestina Mahmoud Abbas ametangaza siku tatu za maombolezo kufuatia shambulizi hilo la anga la Israel.
"Kinachoendelea sasa ni mauaji ya kimbari. Tunaitaka jumuiya ya kimataifa kuingilia haraka kuzuwia mauaji haya ya maangamizi. Ukimya haukubaliki," ilisema taarifa iliyotolewa na Harakati ya Ukombozi wa Palestina (PLO).
Shirika la Afya Duniani, WHO limelaani shambulizi na kutaka ulinzi wa haraka kwa raia na vituo vya afya katika eneo hilo la Palestina.
Mfalme Abdullah II wa Jordan amesema shambulio dhidi ya hospitali huko Gaza ni mauaji ya "kimbari” na "uhalifu wa kivita” ambao yeyote yule hawezi kunyamazia kimya.
Qatar imeyaita mashambulizi hayo kuwa ni "mauaji ya kikatili ya maangamizi" na uhalifu usio na mfano dhidi ya raia wasiokuwa na ulinzi wowote."
Saudi Arabia pia imelaani mashambulizi hayo. Kwenye taarifa yake, wizara ya mambo ya nje ya nchi hiyo imesema mashambulizi hayo ni "uvunjaji wa wazi wa sheria za kimataifa."
Katika radiamali yake kwa jinai za utawala wa Kizayuni katika mashambulizi dhidi ya Hospitali ya Maamadani huko Gaza.
picha za matukio zikionyesha hali ya hospitalini kabla ya shambulio hilo







0 Comments