Mamlaka nchini Madagascar imefunga shule na kudhibiti shughuli za kawaida kabla ya kuwasili kwa Kimbunga Freddy siku ya Jumanne.
Ofisi ya kitaifa ya kushughulikia hali ya dharura imetuma mahema, kamba, misumeno ya minyororo na vifaa vingine kwa wilaya hizo za mashariki ambazo zina uwezekano mkubwa wa kuathirika.
Dhoruba hiyo ilisababisha uharibifu mdogo katika nchi jirani ya Mauritius siku ya Jumatatu, na kusababisha mafuriko katika hoteli zilizo ufuoni.


0 Comments