باب الإصلاح بَيْنَ الناس
031-Mlango Wa Kusuluhisha Baini Ya Watu

:قَالَ الله تَعَالَى

وَإِنِ امْرَأَةٌ خَافَتْ مِن بَعْلِهَا نُشُوزًا أَوْ إِعْرَاضًا فَلَا جُنَاحَ عَلَيْهِمَا أَن يُصْلِحَا بَيْنَهُمَا صُلْحًا ۚ وَالصُّلْحُ خَيْرٌ ۗ وَأُحْضِرَتِ الْأَنفُسُ الشُّحَّ ۚ وَإِن تُحْسِنُوا وَتَتَّقُوا فَإِنَّ اللَّـهَ كَانَ بِمَا تَعْمَلُونَ خَبِيرًا ﴿١٢٨﴾
Na ikiwa mke atakhofia kutoka kwa mumewe uonevu wa ndoa au kutengwa, basi si vibaya juu yake wakisikilizana baina yao kwa suluhu Na suluhu ni bora. Na nafsi zimewekewa uchoyo. Na mkifanya ihsaan na mkawa na taqwa, basi hakika Allaah kwa yale myatendayo ni Mwenye upeo wa khabari za dhahiri na za kufichika[An-Nisaa 128]


لَّ خَيْرَ فِي كَثِيرٍ مِّن نَّجْوَاهُمْ إِلَّا مَنْ أَمَرَ بِصَدَقَةٍ أَوْ مَعْرُوفٍ أَوْ إِصْلَاحٍ بَيْنَ النَّاسِ ۚ وَمَن يَفْعَلْ ذَٰلِكَ ابْتِغَاءَ مَرْضَاتِ اللَّـهِ فَسَوْفَ نُؤْتِيهِ أَجْرًا عَظِيمًا ﴿١١٤﴾
Hakuna khayr katika minong’ono yao mingi isipokuwa anayeamrisha swadaqah, au mema, au kusuluhisha baina ya watu. Na atakayefanya hivyo kutaka radhi za Allaah, basi Tutampa ujira adhimu. [An-Nisaa: 114]


يَسْأَلُونَكَ عَنِ الْأَنفَالِ ۖ قُلِ الْأَنفَالُ لِلَّـهِ وَالرَّسُولِ ۖ فَاتَّقُوا اللَّـهَ وَأَصْلِحُوا ذَاتَ بَيْنِكُمْ ۖ وَأَطِيعُوا اللَّـهَ وَرَسُولَهُ إِن كُنتُم مُّؤْمِنِينَ﴿١﴾
Wanakuuliza (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) kuhusu ngawira; sema: Ngawira ni ya Allaah na Rasuli. Basi mcheni Allaah na tengenezeni yaliyo baina yenu. Na mtiini Allaah na Rasuli Wake mkiwa ni Waumini. [Al-Anfaal:1]


إِنَّمَا الْمُؤْمِنُونَ إِخْوَةٌ فَأَصْلِحُوا بَيْنَ أَخَوَيْكُمْ ۚ وَاتَّقُوا اللَّـهَ لَعَلَّكُمْ تُرْحَمُونَ﴿١٠﴾
Hakika Waumini ni ndugu, basi suluhisheni baina ya ndugu zenu. Na mcheni Allaah ili mpate kurehemewa. [Al-Hujuraat:10]


Hadiyth – 1

وعن أَبي هريرة رضي الله عنه قَالَ: قَالَ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم: (( كُلُّ سُلاَمَى مِنَ النَّاسِ عَلَيهِ صَدَقَةٌ ، كُلَّ يَوْمٍ تَطْلُعُ فِيهِ الشَّمْسُ : تَعْدِلُ بَيْنَ الاثْنَينِ صَدَقَةٌ ، وَتُعينُ الرَّجُلَ في دَابَّتِهِ فَتَحْمِلُهُ عَلَيْهَا، أَوْ تَرْفَعُ لَهُ عَلَيْهَا مَتَاعَهُ صَدَقَةٌ ، وَالكَلِمَةُ الطَّيِّبَةُ صَدَقةٌ ، وَبِكُلِّ خَطْوَةٍ تَمشِيهَا إِلَى الصَّلاةِ صَدَقَةٌ ، وَتُميطُ الأَذى عَنِ الطَّريقِ صَدَقَةٌ )). مُتَّفَقٌ عَلَيهِ .

Kutoka kwa Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Kila kiungo cha mwanadamu kinafanya sadaka kila siku linapochomoza jua: Kusuluhisha kwa uadilifu baina ya watu wawili ni sadaka, kumsaidia mtu juu ya mnyama wake ukampandisha au ukamnyanyulia mzigo wake ni sadaka, kusema neno jema/zuri ni sadaka, kila hatua unayopiga kwenda kwenye Swalaah ni sadaka na kuondoa taka (uchafu) njiani ni sadaka. [Al-Bukhaariy na Muslim].


Hadiyth – 2


وعن أمِّ كُلْثُوم بنت عُقْبَة بن أَبي مُعَيط رضي الله عنها ، قَالَتْ : سمِعتُ رسول الله صلى الله عليه وسلم ، يَقُولُ : (( لَيْسَ الكَذَّابُ الَّذِي يُصْلِحُ بَيْنَ النَّاسِ فَيَنْمِي خَيراً ، أَوْ يقُولُ خَيْراً )) مُتَّفَقٌ عَلَيهِ. وفي رواية مسلم زيادة ، قَالَتْ : "وَلَمْ أسْمَعْهُ يُرْخِّصُ في شَيْءٍ مِمَّا يَقُولُهُ النَّاسُ إلاَّ في ثَلاثٍ ، تَعْنِي : الحَرْبَ ، وَالإِصْلاَحَ بَيْنَ النَّاسِ ، وَحَدِيثَ الرَّجُلِ امْرَأَتَهُ ، وَحَدِيثَ المَرْأةِ زَوْجَهَا".

Na imepokewa kutoka kwa Umm Kulthuum bint 'Uqbah bin Abuu Mu'aytw (Radhwiya Allaahu 'anhaa) kuwa nilimsikia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akisema: “Si muongo yule anayesuluhisha baina ya watu akawa anasambaza habari za kheri, au anasema kheri." [Al-Bukhaariy na Muslim].
Na katika riwaayah ya Muslim ipo ziada inayosema: "Akasema: ' Wala sijamsikia akiruhusu chochote katika uwongo kwa wanayosema watu ila katika mambo matatu, yaani katika vita, kusuluhisha baina ya watu na mazungumzo ya mwaname kwa mkewe na mke kuzungumza na mumewe."


Hadiyth – 3

وعن عائشة رضي الله عنها ، قَالَتْ : سَمِعَ رسولُ الله صلى الله عليه وسلم صَوْتَ خُصُومٍ بِالبَابِ عَاليةً أصْوَاتُهُمَا ، وَإِذَا أحَدُهُمَا يَسْتَوْضِعُ الآخَر وَيَسْتَرْفِقُهُ في شَيءٍ ، وَهُوَ يَقُولُ : والله لا أفْعَلُ، فَخَرجَ عَلَيْهِمَا رسولُ اللهِ صلى الله عليه وسلم ، فَقَالَ : (( أيْنَ المُتَأَلِّي عَلَى اللهِ لاَ يَفْعَلُ المَعْرُوفَ ؟ )) ، فَقَالَ : أَنَا يَارسولَ اللهِ ، فَلَهُ أيُّ ذلِكَ أحَبَّ . مُتَّفَقٌ عَلَيهِ .

Imepokewa na ‘Aaishah (Radhwiya Allaahu 'anhaa) amesema: Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alisikia sauti ya watu wakiteta mlangoni wakiwa wamenyanyua sauti zao. Mmoja wapo alikuwa akimwomba mwenziwe ampunguzie deni na adai kwa upole, na yule mwingine akisema:"Wa -Allaahi sikubali?" Akawatokea Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akauliza: "NI yupi aliyeapa kwa Allaah kuwa hatafanya wema?" Akasema: "Ni mimi, Ee Rasuli wa Allaah, nimempa khiyari afanye analopenda. [Al-Bukhaariy na Muslim].

Hadiyth – 4

وعن أَبي العباس سهل بن سَعد الساعِدِيّ رضي الله عنه : أنَّ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم بَلَغَهُ أنَّ َني عَمرو بن عَوْفٍ كَانَ بَيْنَهُمْ شَرٌّ ، فَخَرَجَ رسولُ الله صلى الله عليه وسلم يُصْلِحُ بَينَهُمْ في أُنَاس مَعَهُ ، فَحُبِسَ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم وَحَانَتِ الصَّلاة ، فَجَاءَ بِلالٌ إِلَى أَبي بكر رضي الله عنهما ، فَقَالَ: يَا أَبا بَكْر ، إنَّ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم قَدْ حُبِسَ وَحَانَتِ الصَّلاةُ فَهَلْ لَكَ أنْ تَؤُمَّ النَّاس ؟ قَالَ : نَعَمْ ، إنْ شِئْتَ ، فَأقَامَ بِلالٌ الصَّلاةَ ، وتَقَدَّمَ أَبُو بَكْرٍ فَكَبَّرَ وَكَبَّرَ النَّاسُ ، وَجَاءَ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم يَمشي في الصُّفُوفِ حَتَّى قَامَ في الصَّفِّ ، فَأَخَذَ النَّاسُ في التَّصْفيقِ ، وَكَانَ أَبُو بكرٍ رضي الله عنه لا يَلْتَفِتُ في الصَّلاةِ ، فَلَمَّا أكْثَرَ النَّاسُ في التَّصْفيقِ الْتَفَتَ ، فإِذَا رَسُول الله صلى الله عليه وسلم ، فَأَشَارَإِِلَيْه رسولُ الله صلى الله عليه وسلم فَرَفَعَ أَبُو بَكْر رضي الله عنه يَدَهُ فَحَمِدَ اللهَ ، وَرَجَعَ القَهْقَرَى وَرَاءهُ حَتَّى قَامَ في الصَّفِّ ، فَتَقَدَّمَ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم ، فَصَلَّى للنَّاسِ ، فَلَمَّا فَرَغَ أقْبَلَ عَلَى النَّاسِ ، فَقَالَ : (( أيُّهَا النَّاسُ ، مَا لَكُمْ حِينَ نَابَكُمْ شَيْءٌ في الصَّلاةِ أخَذْتُمْ في التَّصفيق ؟! إِنَّمَا التَّصفيق للنِّساء . مَنْ نَابَهُ شَيْءٌ في صَلاتِهِ فَلْيَقُلْ : سُبْحَانَ الله ، فَإِنَّهُ لاَ يَسْمَعُهُ أحدٌ حِينَ يقُولُ : سُبْحَانَ الله ، إلاَّ الْتَفَتَ . يَا أَبا بَكْر : مَا مَنَعَكَ أنْ تُصَلِّي بالنَّاسِ حِينَ أشَرْتُ إلَيْكَ ؟ )) ، فَقَالَ أَبُو بَكْرٍ : مَا كَانَ يَنْبَغي لابْنِ أَبي قُحَافَةَ أنْ يُصَلِّي بالنَّاسِ بَيْنَ يَدَيْ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم . مُتَّفَقٌ عَلَيهِ .


Na imepokewa kutoka kwa Abil 'Abbaas Sahl bin Sa'ad As-Saa'idiyy (Radhwiya Allaahu 'Anhu) kuwa ilimfikia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kuwa kuna mzozano baina ya vikundi vya Bani 'Amru bin 'Awf. Akatoka Rasuli wa Allaah kwenda kuwasuluhisha pamoja na kundi la maswahaba wake. Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akawa ni mwenye kuzuiliwa (baada ya hiyo sulhu kwa kualikwa karamu) na wakati wa swalaah ukafika akiwa katika hali hiyo. Bilaal alikuja kwa Abuu Bakr (Radhwiya Allaahu 'anhumaa) akamwambia: " Ee Abuu Bakr, hakika Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amezuiliwa na wakati wa swalaah umefika, utaswalisha watu?" Akasema: "Ndio ukitaka." Kwa hiyo, Bilaal akakimu swalaah, naye Abuu Bakr akajongea na kufunga swalaah, nao watu wakamfuata (kwa kupiga takbiyr ya kufungia swalaah) Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) Alikuja akiwa anapita katika safu mpaka akasimama katika safu. Watu wakaanza kupiga makofi, Naye Abuu Bakr (Radhwiya Allaahu 'anhu) alikuwa hana tabia ya kugeuka katika Swalaah yake. watu walipokithirisha kupiga makofi (Abuu Bakr) aligeuka na kumuona Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam). Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alimwashiria aendelee, Abuu Bakr (Radhwiya Allaahu 'anhu) alinyanyua mikono na kumuhimidi Allaah, kisha akarudi kinyumenyume nyuma yake mpaka akasimama kwenye safu. Hapo Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alijongea mbele na kuwaswalisha watu. Alipomaliza kuswalisha aliwaelekea watu, akasema: "Enyi watu! Mna nini nyinyi linapotendeka jambo mnaanza kupiga makofi? Hakika kupiga makofi ni kwa wanawake. Linapotendeka jambo katika Swalaah (nawe unataka kumkumbusha Imaam) basi aseme mmoja wenu: Subhaana Allaah( Ametakasika Allaah, yaani hana mapungufu yoyote yale). Hiyo ni kuwa hatasikia yeyote pindi unaposema: Subhaana Allaah ila atatizama. Ee Abuu bakr! Ni lipi liliokukataza kuwaswalisha watu nilipokuashiria?" Akasema Abuu Bakr (Radhwiya Allaahu 'anhu): "Haifalii kwa mtoto wa Abuu Quwhaafah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kuwaswalisha watu mbele ya Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam)." [Al-Bukhaariy na Muslim].