باب تحريم الظلم والأمر بردِّ المظالم
26 – Mlango Wa Uharamu Wa Dhulma Na Amri Ya Karudisha Vilivyodhulumiwa



قَالَ الله تَعَالَى:
مَا لِلظَّالِمِينَ مِنْ حَمِيمٍ وَلَا شَفِيعٍ يُطَاعُ﴿١٨﴾
Madhalimu hawatokuwa na rafiki wa dhati, na wala mwombezi anayetiiwa. [Ghaafir: 18]

وَمَا لِلظَّالِمِينَ مِن نَّصِيرٍ ﴿٧١﴾
Na madhalimu hawana yeyote mwenye kunusuru. [Al-Hajj: 71]



Hadiyth – 1
وعن جابر رضي الله عنه: أن رَسُول الله صلى الله عليه وسلم قَالَ: ((اتَّقُوا الظُّلْمَ؛ فَإنَّ الظُّلْمَ ظُلُمَاتٌ يَوْمَ القِيَامَةِ. وَاتَّقُوا الشُّحَّ؛ فَإِنَّ الشُّحَّ أهْلَكَ مَنْ كَانَ قَبْلَكُمْ. حَمَلَهُمْ عَلَى أنْ سَفَكُوا دِمَاءهُمْ، وَاسْتَحَلُّوا مَحَارِمَهُمْ)). رواه مسلم
Imepokewa kutoka kwa Jaabir (Radhwiya Allaahu 'anhu) kuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi sallam) amesema: “Ogopeni sana dhulma, kwani kudhulumu ni viza Siku ya Qiyaamah. Na ogopeni sana ubakhili kwani ubakhili uliwaangamiza waliokuwa kabla yenu, uliwafanya wamwage damu zao na wakahalalisha walioharamishiwa.” [Muslim]



Hadiyth – 2
وعن أَبي هريرة رضي الله عنه: أن رَسُول الله صلى الله عليه وسلم قَالَ: ((لَتُؤَدُّنَّ الحُقُوقَ إِلَى أهْلِهَا يَومَ القِيَامَةِ، حَتَّى يُقَادَ للشَّاةِ الجَلْحَاءِ مِنَ الشَّاةِ القَرْنَاءِ)). رواه مسلم
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi sallam) amesema: “Mtaendelea kutimiza haki za wenyewe Siku ya Qiyaamah mpaka kondoo asiyekuwa na pembe alipize kisasi juu ya mwenye pembe.” [Muslim]



Hadiyth – 3
وعن ابن عمر رضي الله عنهما، قال: كُنَّا نَتَحَدَّثُ عَنْ حَجَّةِ الوَدَاعِ، والنَّبيُّ صلى الله عليه وسلم بَيْنَ أَظْهُرِنَا، وَلا نَدْرِي مَا حَجَّةُ الوَدَاعِ حَتَّى حَمِدَ اللهَ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم وَأثْنَى عَلَيهِ ثُمَّ ذَكَرَ المَسْيحَ الدَّجَّال فَأطْنَبَ في ذِكْرِهِ، وَقَالَ: ((مَا بَعَثَ اللهُ مِنْ نَبيٍّ إلا أنْذَرَهُ أُمَّتَهُ، أنْذَرَهُ نُوحٌ وَالنَّبِيُّونَ مِنْ بَعْدِهِ، وَإِنَّهُ إنْ يَخْرُجْ فِيكُمْ فَما خَفِيَ عَليْكُمْ مِنْ شَأنِه فَلَيْسَ يَخْفَى عَليْكُم، إنَّ رَبَّكُمْ لَيْسَ بأعْوَرَ وإنَّهُ أعْوَرُ عَيْنِ اليُمْنَى، كَأنَّ عَيْنَهُ عِنَبَةٌ طَافِيَةٌ. ألا إنَّ الله حَرَّمَ عَلَيْكُمْ دِمَاءكُمْ وَأمْوَالَكُمْ كحُرْمَةِ يَوْمِكُمْ هَذَا، في بلدكم هذا، في شَهْرِكُمْ هَذَا، ألا هَلْ بَلّغْتُ؟)) قالُوا: نَعَمْ، قَالَ: ((اللَّهُمَّ اشْهَدْ)) ثلاثًا ((وَيْلَكُمْ- أَوْ وَيْحَكُمْ، انْظُروا: لا تَرْجعُوا بَعْدِي كُفّارًا يَضْرِبُ بَعْضُكُمْ رِقَابَ بَعْضٍ)). رواه البخاري، وروى مسلم بعضه
Imepokewa kutoka kwa ibn ‘Umar (Radhwiya Allaahu 'anhumaa) kuwa amesema: Tulikuwa tukizungumza Hijjah ya kuaga (Hijjatul Wadaa’) baina yetu wala hatujui nini Hijjah ya kuaga mpaka Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi sallam) alipomuhimidi Allaah (Subhaanahu Wa Ta'aalaa) na kumtukuza. Baada ya h\apo akamtaja Masiyh Dajjaal na kuzungumza kwa kirefu. Kisha akasema: “Kila Rasuli aliyetumwa na Allaah (Subhaanahu Wa Ta'aalaa) amewaonya Ummah wake kuhusu (Masiyh Dajjaal). Nuwh na Rusul waliokuja baada yake walionya kumhusu. Na hakika yeye atatoka miongoni mwenu, hataweza kujificha (kwani tayari mmeshamjua), ukweli wake hautafichika nanyi. Hakika Mola wenu si chogo, bali yeye ni chogo jicho lake kulia kama kwamba jicho lake ni zabibu iliyovimba. Tahadharini! Hakika Allaah (Subhaanahu Wa Ta'aalaa) Ametahadharisha kwenu damu na mali yenu kama utukufu wa siku yenu hii (siku ya Hijjah), katika mji wenu huu (yaani Makkah), katika mwezi wenu huu (Dhul Hijjah). Je, nimefikisha ujumbe? Wakasema (Maswahaba): Ndio. Akasema Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi sallam): Ee Allaah! Shuhudia – mara tatu. Ole wenu tizameni sana! Msirudi baada yangu makafiri mnakata shingo (mnauana).” [Al-Bukhaariy na Muslim amepokea baadhi yake)



Hadiyth – 4
وعن عائشة رضي الله عنها: أن رَسُول الله صلى الله عليه وسلم، قَالَ: ((مَنْ ظَلَمَ قيدَ شِبْرٍ مِنَ الأرْضِ، طُوِّقَهُ مِنْ سبْعِ أرَضينَ)). مُتَّفَقٌ عَلَيهِ.
Imepokewa kutoka kwa ‘Aaishah (Radhwiya Allaahu 'anhaa) kwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi sallam) amesema: “Atakaye dhulumu ardhi kiasi cha shubiri atabebeshwa ardhi saba (siku ya Qiyaamah) [A-Bukhaariy na Muslim]



Hadiyth – 5
وعن أَبي موسى رضي الله عنه قَالَ: قَالَ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم: ((إنَّ الله لَيُمْلِي لِلظَّالِمِ، فَإِذَا أخَذَهُ لَمْ يُفْلِتْهُ))، ثُمَّ قَرَأَ: {وكَذَلِكَ أَخْذُ رَبِّكَ إِذَا أَخَذَ الْقُرَى وَهِيَ ظَالِمَةٌ إِنَّ أَخْذَهُ أَلِيمٌ شَدِيدٌ} [هود: 102] مُتَّفَقٌ عَلَيهِ
Imepokewa na Abuu Muwsaa (Radhwiya Allaahu 'anhu) kuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi sallam) amesema: “Hakika Allaah Anampatia muda dhalimu (kwa kumcheleweshea adhabu), lakini anapomshika hatoki katika adhabu Yake. Kisha akasoma: Na hivyo ndivyo mkamato wa Rabb wako unavyokuwa Anapokamata miji na huku ikifanya dhulma. Hakika mkamato Wake unaumiza vikali. [Huwd: 102]” [Al-Bukhaariy na Muslim]



Hadiyth – 6
وعن معاذ رضي الله عنه قَالَ: بَعَثَنِي رَسُول الله صلى الله عليه وسلم فَقَالَ: ((إنَّكَ تَأتِي قَوْمًا مِنْ أهلِ الكِتَابِ فَادْعُهُمْ إِلَى شَهَادَةِ أنْ لا إلَهَ إلا الله، وَأنِّي رسولُ الله، فَإنْ هُمْ أَطَاعُوا لِذلِكَ، فَأعْلِمْهُمْ أنَّ اللهَ قَدِ افْتَرضَ عَلَيْهِمْ خَمْسَ صَلَواتٍ في كُلِّ يَوْمٍ وَلَيلَةٍ، فَإِنْ هُمْ أطَاعُوا لِذَلِكَ، فَأعْلِمْهُمْ أنَّ اللهَ قَدِ افْتَرَضَ عَلَيْهِمْ صَدَقَةً تُؤخَذُ مِنْ أغْنِيَائِهِمْ فَتُرَدُّ عَلَى فُقَرَائِهِمْ، فَإنْ هُمْ أطَاعُوا لِذَلِكَ، فَإِيَّاكَ وَكَرَائِمَ أمْوَالِهِمْ، وَاتَّقِ دَعْوَةَ المَظْلُومِ؛ فإِنَّهُ لَيْسَ بَيْنَها وَبَيْنَ اللهِ حِجَابٌ)). مُتَّفَقٌ عَلَيهِ
Mu’adh (Radhwiya Allaahu 'anhu) amesema: Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi sallam) alinituma kwa kuniambia: “Hakika utakwenda kwa (watu wa Ahlul Kitaab). Mwanzo waite katika kushuhudia na kukubali kuwa hapana Mola Apasaye kuabudiwa kwa haki ila Allaah na kuwa mimi ni Rasuli wa Allaah. Wanapokutii kwa hilo, wafahamishe kuwa Allaah Amewafaradhishia Swalaah tano kwa kila mchana na usiku. Wanapokutii kwa hilo, wafahamishe kuwa Allaah Amewafaradhishia Swadaqah (Zakaah) inayochukuliwa kutoka kwa matajiri wao na kurudishwa kwa mafakiri miongoni mwao. Wanapokutii kwa hilo, basi tahadhari sana na mali yao ya thamani. Na ogopa sana du’aa ya mwenye kudhulimiwa hiyo haina pazia na Allaah.” [Al-Bukhaariy na Muslim]



Hadiyth – 7
وعن أبي حُمَيدٍ عبد الرحمن بن سعد السَّاعِدِي رضي الله عنه قَالَ: اسْتَعْمَلَ النَّبيُّ صلى الله عليه وسلم رَجُلًا مِنَ الأزْدِ يُقَالُ لَهُ: ابْنُ اللُّتْبِيَّةِ عَلَى الصَّدَقَةِ، فَلَمَّا قَدِمَ، قَالَ: هَذَا لَكُمْ، وَهَذَا أُهْدِيَ إِلَيَّ، فَقَامَ رسولُ الله صلى الله عليه وسلم عَلَى المِنْبَرِ فَحَمِدَ الله وَأثْنَى عَلَيهِ، ثُمَّ قَالَ: ((أمَّا بَعدُ، فَإِنِّي أسْتَعْمِلُ الرَّجُلَ منْكُمْ عَلَى العَمَلِ مِمَّا وَلانِي اللهُ، فَيَأتِي فَيَقُولُ: هَذَا لَكُمْ وَهَذا هَدِيَّةٌ أُهْدِيتْ إلَيَّ، أفَلا جَلَسَ في بيت أبِيهِ أَوْ أُمِّهِ حَتَّى تَأتِيَهُ هَدِيَّتُهُ إنْ كَانَ صَادِقًا، واللهِ لا يَأخُذُ أحَدٌ مِنْكُمْ شَيئًا بِغَيرِ حَقِّهِ إلا لَقِيَ الله تَعَالَى، يَحْمِلُهُ يَوْمَ القِيَامَةِ، فَلا أعْرِفَنَّ أحَدًا مِنْكُمْ لَقِيَ اللهَ يَحْمِلُ بَعيرًا لَهُ رُغَاءٌ، أَوْ بَقَرَةً لَهَا خُوَارٌ، أَوْ شَاةً تَيْعَرُ)). ثُمَّ رفع يديهِ حَتَّى رُؤِيَ عُفْرَةُ إبْطَيْهِ، فَقَالَ: ((اللَّهُمَّ هَلْ بَلَّغْتُ)) ثلاثًا مُتَّفَقٌ عَلَيهِ
Imepokewa na Abuu Humayd, ‘Abdur-Rahmaan bin Sa’d As- Saa’iydy (Radhwiya Allaahu ‘anhu) kuwa amesema: Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alimtuma mtu kutoka katika ukoo wa Al-Azdiy aliyekuwa akiitwa inb Al-Lutbiyyah kukusanya Zakah. Aliporudi alisema: Hili ni fungo lenu na hivi nimepewa zawadi. Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alisimama juu ya mimbar, akamuhidi Allaah na kumtukuza pamoja na kumsifu, kisha akasema: “Ama baada ya haya; hakika mimi nimempa kazi mtu miongoni mwenu juu ya kazi niliyopewa mamlaka na Allaah. Mtu huyo anakuja na anasema: Hiki ni chenu na hiki ni zawadi nimepewa. Basi angekaa mmoja wenu kwenye nyumba ya baba yake, au mama yake mpaka imfikie yeye zawadi hiyo yake ikiwa hakika yeye ni mkweli. Wa-Allaahi hatochukua mmoja wenu kitu chochote bila ya haki yake ila atakutana na Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) akiwa amekibeba siku ya Qiyaamah. Hivyo, nisije nikamjua yoyote kati yenu amekutana na Allaah akiwa amebeba ngamia anayeguna, au ng’ombe anayeroroma au mbuzi (kondoo) anayelia.” Kisha akanyanyua mikono yake mpaka uonekane weupe na makwapa yake, akasema: “Ee Allaah! Je, nimefikisha.” [Al-Bukhaariy, Muslim na Ahmad]



Hadiyth – 8
عن أَبي هريرة رضي الله عنه عن النَّبيّ صلى الله عليه وسلم قَالَ: ((مَنْ كَانَتْ عِنْدَهُ مَظْلمَةٌ لأَخِيه، مِنْ عِرضِهِ أَوْ مِنْ شَيْءٍ، فَلْيَتَحَلَّلْهُ مِنْهُ اليَوْمَ قبْلَ أنْ لا يَكُونَ دِينَار وَلا دِرْهَمٌ؛ إنْ كَانَ لَهُ عَمَلٌ صَالِحٌ أُخِذَ مِنْهُ بِقَدْرِ مَظْلمَتِهِ، وَإنْ لَمْ يَكُنْ لَهُ حَسَنَاتٌ أُخِذَ مِنْ سَيِّئَاتِ صَاحِبِهِ فَحُمِلَ عَلَيهِ)). رواه البخاري
Imepokewa kutoka kwa Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu ‘anhu) kuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “Mwenye kitu cha dhulma cha nduguye kutokana na kumvunjia heshima au kitu kingine chochote, basi amuombe amhalalishie leo kabla haijafika siku ambayo hakutakuwa na dinar wala dirham; akiwa ana ‘amali njema itachukuliwa kwa kadiri ya alichodhulumu, na ikiwa hana ‘amali njema zitachukuliwa dhambi za aliyemdhulumu na kubebeshwa (yeye).” [Al-Bukhaariy]



Hadiyth – 9
وعن عبد الله بن عمرو بن العاص رضي الله عنهما عن النَّبيّ صلى الله عليه وسلم قَالَ: ((المُسْلِمُ مَنْ سَلِمَ المُسْلِمُونَ مِنْ لِسَانِهِ وَيَدِهِ، وَالمُهَاجِرُ مَنْ هَجَرَ مَا نَهَى اللهُ عَنْهُ)). مُتَّفَقٌ عَلَيهِ
Imepokewa na ‘AbduLLaah bin ‘Amru bin Al-‘Aasw (Radhwiya Allaahu ‘anhumaa) kuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “Muislamu ni yule ambaye Waislaam wamesalimika kwa ulimi na mkono wake, na Muhajir ni yule anayehama yale aliyoyakataza Allaah.” [Al-Bukhaariy na Muslim]



Hadiyth – 10
وعنه رضي الله عنه قَالَ: كَانَ عَلَى ثَقَل النَّبيِّ صلى الله عليه وسلم رَجُلٌ يُقَالُ لَهُ كِرْكِرَةُ، فَمَاتَ، فَقَالَ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم: ((هُوَ في النَّارِ)) فَذَهَبُوا يَنْظُرُونَ إِلَيْه، فَوَجَدُوا عَبَاءةً قَدْ غَلَّهَا. رواه البخاري
Kutoka kwake (Radhwiya Allaahu ‘anhu) amesema: Alikuwepo mtu mmoja akiitwa Kirkirah aliyekuwa mtunzaji wa mali ya Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) Akasema Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam): “Yeye yupo motoni”. Maswahaba wakaenda kumtazama wakapata juba alilochukua kwa khiyana.” [Al-Bukhaariy]



Hadiyth – 12
وعن أَبي بكْرة نُفَيْع بن الحارث رضي الله عنه عن النَّبيّ صلى الله عليه وسلم قَالَ: ((إنَّ الزَّمَانَ قَدِ اسْتَدَارَ كَهَيْئَته يَوْمَ خَلَقَ اللهُ السَّمَاوَاتِ وَالأَرضَ: السَّنَةُ اثْنَا عَشَرَ شَهْرًا، مِنْهَا أرْبَعَةٌ حُرُمٌ: ثَلاثٌ مُتَوالِياتٌ: ذُو القَعْدَة، وذُو الحِجَّةِ، وَالمُحَرَّمُ، وَرَجَبُ مُضَرَ الَّذِي بَيْنَ جُمَادَى وَشعْبَانَ، أيُّ شَهْر هَذَا؟)) قُلْنَا: اللهُ وَرَسُولُهُ أعْلَمُ، فَسَكَتَ حَتَّى ظَننَّا أنَّهُ سَيُسَمِّيهِ بِغَيْرِ اسْمِهِ، قَالَ: ((ألَيْسَ ذَا الحِجَّةِ؟)) قُلْنَا: بَلَى. قَالَ: ((فَأيُّ بَلَد هَذَا؟)) قُلْنَا: اللهُ ورَسُولُهُ أعْلَمُ، فَسَكَتَ حَتَّى ظَنَنَّا أنَّهُ سَيُسَمِّيهِ بِغَيرِ اسْمِهِ. قَالَ: ((ألَيْسَ البَلْدَةَ؟)) قُلْنَا: بَلَى. قَالَ: ((فَأيُّ يَوْم هَذَا؟)) قُلْنَا: اللهُ ورَسُولُهُ أعْلَمُ، فَسَكَتَ حَتَّى ظَنَنَّا أنَّهُ سَيُسَمِّيهِ بغَيرِ اسْمِهِ. قَالَ: ((ألَيسَ يَوْمَ النَّحْرِ؟)) قُلْنَا: بَلَى. قَالَ: ((فَإنَّ دِمَاءكُمْ وَأمْوَالَكُمْ وَأَعْرَاضَكُمْ عليكم حَرَامٌ، كَحُرْمَةِ يَوْمِكُمْ هَذَا في بَلَدِكُمْ هَذَا في شَهْرِكُمْ هَذَا، وَسَتَلْقُونَ رَبَّكُمْ فَيَسْألُكُمْ عَنْ أعْمَالِكُمْ، ألا فَلا تَرْجعوا بعدي كُفّارًا يَضْرِبُ بَعْضُكُمْ رِقَابَ بَعْض، ألا لَيُبَلِّغ الشَّاهِدُ الغَائِبَ، فَلَعَلَّ بَعْضَ مَنْ يَبْلُغُهُ أنْ يَكُونَ أوْعَى لَهُ مِنْ بَعْض مَنْ سَمِعَهُ))، ثُمَّ قَالَ: ((ألا هَلْ بَلَّغْتُ، ألا هَلْ بَلَّغْتُ؟)) قُلْنَا: نَعَمْ. قَالَ: ((اللَّهُمَّ اشْهَدْ)). مُتَّفَقٌ عَلَيهِ
Imepokelewa kutoka kwa Abu Bakr Nufay’ kuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa saalam) amesema: “Hakika zama (mwaka) unapita kama ilivyo siku ya Allaah Alivyoumba mbingu na ardhi: Mwaka una miezi kumi na mbili, miongoni mwayo ni miezi minne iliyo hurum (miezi ambayo vita ni haram hata wakati wa ujahiliyyah). Miezi mitatu ni ya kufuatana: Dhul Qa’dah, Dhul Hijjah na Muharram na Rajab Mundhwar, mwezi ambao upo baina ya Jumaadah na Sha’baan. Kisha akauliza: “Je, huu ni mwezi gani?” Wakasema (Maswahaba): Allaah na Rasuli Wake wanajua zaidi. Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akanyamaza mpaka tukadhania atauita kwa jina lingine. Akasema: “Je, huu si mwezi wa Dhul Hijjah?” Tukasema: Ndio. Akauliza: “Je, huu ni mji gani?” Tukasema: Allaah na Rasuli Wake wanajua zaidi. Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akanyamaza mpaka tukadhania atauita kwa jina lingine lisilikuwa jina lake. Akasema: “Je, huu si mji wa (Makkah)?” Tukasema: Ndio. Akasema: “Je, hii ni siku gani?” Tukasema: Allaah na Rasuli Wake wanajua zaidi. Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akanyamaza mpaka tukadhania kuwa ataiita kwa jina lingine. Akasema: “Je, hii si ni siku ya kuchinja?” Tukasema: Ndio. Akasema: “Hakika damu zenu, mali zenu, na heshima zenu ni haramu kwenu kama uharamu (wa kufanya dhambi) siku yenu hii, katika mji wenu huu, katika mwezi wenu huu. Na bila shaka mtakutana na Mola wenu na kuwauliza juu ya ‘amali zenu. Fahamuni! Msirudi baada yangu katika ukafiri mkiuana ninyi kwa ninyi. Jueni! Aliyehudhuria amfikishie asiyekuwepo, huenda baadhi ya watakao fikishiwa wakawa wanafahamu nzuri zaidi kuliko waliosikia.” Kisha akauliza: “Je, nimefikisha?” Tukasema: Ndio. Akasema: “Ee Allaah shuhudia (hilo).” [Al-Bukhaariy na Muslim]



Hadiyth – 11
وعن أَبي أمامة إياس بن ثعلبة الحارثي رضي الله عنه: أنَّ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم قَالَ: ((مَن اقْتَطَعَ حَقَّ امْرئ مُسْلِم بيَمينه، فَقدْ أوْجَبَ اللهُ لَهُ النَّارَ، وَحَرَّمَ عَلَيهِ الجَنَّةَ)) فَقَالَ رَجُلٌ: وإنْ كَانَ شَيْئًا يَسيرًا يَا رَسُول الله؟ فَقَالَ: ((وإنْ كَانَ قَضيبًا مِنْ أرَاك)). رواه مسلم
Imepokewa kutoka kwa Abuu Umaamah Iyaas bin Tha’labah Al-Haarithiy (Radhiya Allaah ‘anhhu) kuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “Mwenye kuchukua haki ya mtu Muislamu kwa kuapa yamini (ya uongo) imewajibika kwa Allaah kumuingiza motoni na kumharamishia Jannah.” Mtu mmoja akasema: “Hata kikiwa kitu kidogo ee Rasuli wa Allaah? Akasema: “Hata kikiwa ni kigaa cha mti Arak.” [Muslim]



Hadiyth – 12
وعن عَدِيّ بن عَميْرَةَ رضي الله عنه قَالَ: سمعت رَسُول الله صلى الله عليه وسلم يقول: ((مَنِ اسْتَعْمَلْنَاهُ مِنْكُمْ عَلَى عَمَل، فَكَتَمَنَا مِخْيَطًا فَمَا فَوْقَهُ، كَانَ غُلُولًا يَأتِي به يَومَ القِيَامَةِ)) فَقَامَ إليه رَجُلٌ أسْوَدُ مِنَ الأنْصَارِ، كَأنِّي أنْظُرُ إِلَيْهِ، فَقَالَ: يَا رَسُول الله، اقْبَلْ عَنِّي عَمَلَكَ، قَالَ: ((وَمَا لَكَ؟)) قَالَ: سَمِعْتكَ تَقُولُ كَذَا وكَذَا، قَالَ: ((وَأَنَا أقُولُه الآنَ: مَنِ اسْتَعْمَلْنَاهُ عَلَى عَمَلٍ فَلْيَجِئْ بقَليله وَكَثيره، فَمَا أُوتِيَ مِنْهُ أخَذَ، وَمَا نُهِيَ عَنْهُ انْتَهَى)). رواه مسلم
Imepokewa na ‘Adiy bin ‘Umayrah (Radhwiya Allaahu ‘anhu) kwamba nimemsikia Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akisema: “Yoyote tutakaye muajiri miongoni mwenu kwa kazi yoyote ile akawa ni mwenye kuficha sindano na zaidi yake, huo utakuwa ni wizi atakao kuja nao Siku ya Qiyaamah.” Akasema mtu mweusi mingoni mwa Answaar kana kwamba ninamtazama. Akasema: Ee Rasuli wa Allaah! Niruhusu nijiuzulu kazi yako (uliyonipa). Akamuuliza: “Kwanini?” Akajibu: Nimekusikia ukisema kadhaa na kadhaa. Akasema: “Yoyote atakayempa jukumu la kazi fulani basi alete kichache na kingi (alete chochote atakachopata). Atakachopewa atachukua, na atakachozuiliwa akiache.” [Muslim]



Hadiyth – 13
وعن عمر بن الخطاب رضي الله عنه قَالَ: لَمَّا كَانَ يَوْمُ خَيبَر أقْبَلَ نَفَرٌ مِنْ أصْحَابِ النَّبيِّ صلى الله عليه وسلم، فقَالُوا: فُلاَنٌ شَهِيدٌ، وفُلانٌ شَهِيدٌ، حَتَّى مَرُّوا عَلَى رَجُلٍ، فقالوا: فُلانٌ شَهِيدٌ. فَقَالَ النَّبيُّ صلى الله عليه وسلم: ((كَلا، إنِّي رَأيْتُهُ في النَّار في بُرْدَةٍ غَلَّهَا- أَوْ عَبَاءة-)). رواه مسلم
Imepokewa na ‘Umar bin Al-Khatwaab (Radhwiya Allaahu ‘anhu) amesema: Siku ya Vita vya Khaybar walikaribia kikundi cha Maswahaba wa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kuja kutazama waliokufa mashahidi. Wakasema: Fulani ni shahidi na fulani pia ni shahidi.” Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa salaam) akasema: “Sivyo hivyo. Hakika mimi nimemuona motoni kwa juba au gauni aliloliiba.” [Muslim]



Hadiyth – 14
وعن أَبي قتادة الحارث بن ربعي رضي الله عنه عن رَسُول الله صلى الله عليه وسلم: أَنَّهُ قَامَ فيهم، فَذَكَرَ لَهُمْ أنَّ الجِهَادَ في سبيلِ الله، وَالإِيمَانَ بالله أَفْضَلُ الأعْمَالِ، فَقَامَ رَجُلٌ، فَقَالَ: يَا رَسُولَ الله، أرَأيْتَ إنْ قُتِلْتُ في سبيلِ الله، تُكَفَّرُ عَنّي خَطَايَايَ؟ فَقَالَ لَهُ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم: ((نَعَمْ، إنْ قُتِلْتَ في سبيلِ اللهِ، وَأنْتَ صَابرٌ مُحْتَسِبٌ، مُقْبِلٌ غَيرُ مُدْبر)) ثُمَّ قَالَ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم: ((كَيْفَ قُلْتَ؟)) قَالَ: أرَأيْتَ إنْ قُتِلْتُ في سبيلِ الله، أتُكَفَّرُ عَنّي خَطَايَايَ؟ فَقَالَ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم: ((نَعمْ، وَأنْتَ صَابرٌ مُحْتَسِبٌ، مُقْبِلٌ غَيرُ مُدْبِرٍ، إلا الدَّيْنَ؛ فإنَّ جِبريلَ قَالَ لي ذلِكَ)). رواه مسلم
Imepokewa na Abuu Qataadah bin Al-Haarith bin Rab’iyy (Radhwiya Allaahu ‘anahu) kwamba Rasuli wa Allaahu (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) alisimama mbele yao, akawatajia kuwa jihaad katika njia ya Allaah na kumuamini Allaah ndio ‘amali bora. Hapo alisimama mtu akasema: Ee Rasuli wa Allaah! Waonaje nikiuliwa katika njia ya Allaah nitasamehewa madhambi yangu? Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akamwambia: “Ndio, ukiuliwa katika njia ya Allaah nawe ukawa katika hali ya kusubiri na huku unatarajia malipo (kutoka kwa Allaah), ukiwa unasonga mbele katika vita wala sio kurudi nyuma (na kukimbia).” Kisha akasema Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam): “Umesema nini?” Akasema: Ee Rasuli wa Allaah! Waonaje nikiuliwa katika njia ya Allaah nitasamehewa makossa yangu? Akasema Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam): “Ndio, ukiuliwa katika njia ya Allaah nawe ukawa katika hali ya kusubiri na huku watarajia malipo (kutoka kwa Allaah), ukiwa unasonga mbele katika vita wala sio kurudi nyuma (na kukimbia) ila deni kwani Jibriyl ameniambia hilo.” [Muslim]



Hadiyth – 15
وعن أبي هُريرةَ رضي الله عنه: أنَّ رسولَ الله صلى الله عليه وسلم قَالَ: ((أتدرونَ مَنِ المُفْلِسُ؟)) قالوا: المفْلسُ فِينَا مَنْ لا دِرهَمَ لَهُ ولا مَتَاع، فَقَالَ: ((إنَّ المُفْلسَ مِنْ أُمَّتي مَنْ يأتي يَومَ القيامَةِ بصلاةٍ وصيامٍ وزَكاةٍ، ويأتي قَدْ شَتَمَ هَذَا، وقَذَفَ هَذَا، وَأَكَلَ مالَ هَذَا، وسَفَكَ دَمَ هَذَا، وَضَرَبَ هَذَا، فيُعْطَى هَذَا مِنْ حَسَنَاتِهِ، وهَذَا مِنْ حَسناتهِ، فإنْ فَنِيَتْ حَسَناتُه قَبْل أنْ يُقضى مَا عَلَيهِ، أُخِذَ منْ خَطَاياهُم فَطُرِحَتْ عَلَيهِ، ثُمَّ طُرِحَ في النَّارِ)). رواه مسلم
Imepokewa kutoka kwa Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu ‘anhhu) kuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu Alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “Je, mnamjua Muflis?” Wakasema: Muflis kwetu sisi ni yule asiyekuwa na dirham wala mali. Akasema: “Hakika Muflis katika Ummah wangu ni yule atakayekuja Siku ya Qiyaamah akiwa ana Swalaah, Swawm na Zakaah. Na anakuja amemtusi huyu, amemsingizia huyu uzinifu, amekula mali ya huyu, amemwaga damu ya huyu na kumpiga huyu. Kila aliyedhulumiwa atapewa sehemu ya mema yake, na yule atapewa sehemu ya mema yake. Pindi mema yake yatakapomalizika kabla ya hukmu kuisha, zitachukuliwa sehemu ya dhambi zao (kulingana na alivyo dhulumu) na apewe yeye, kisha atupwe motoni.” [Muslim]



Hadiyth – 16
وعن أم سلمة رضي الله عنها: أنَّ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم قَالَ: ((إنَّمَا أنَا بَشَرٌ، وَإنَّكُمْ تَخْتَصِمُونَ إلَيَّ، وَلَعَلَّ بَعْضَكُمْ أنْ يَكُونَ أَلْحَنَ بِحُجّتِهِ مِنْ بَعْضٍ، فأَقْضِيَ لَهُ بِنَحْوِ مَا أسْمعُ، فَمَنْ قَضَيتُ لَهُ بِحَقِّ أخِيهِ فَإِنَّما أقطَعُ لَهُ قِطعةً مِنَ النَّارِ)). مُتَّفَقٌ عَلَيهِ
Imepokewa kutoka kwa ummu Salamah (Radhwiya Llaahu ‘anhaa) kuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “Hakika mimi ni mwana Aadam, nanyi mnaniletea mashtaka yenu. Na huenda baadhi yenu mkawa mahodari kutoa hoja kuliko baadhi ya wengine wenu. Nami nikampatia haki (isiyokuwa yake) kwa niliyoyasikia. Yoyote atakaye mpatia haki ya nduguye, hakika nitakuwa nimemkatia kipande cha moto. [Al-Bukhaariy na Muslim]



Hadiyth – 17
وعن ابن عمر رضي الله عنهما قَالَ: قَالَ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم: ((لَنْ يَزَالَ المُؤْمِنُ في فُسْحَةٍ مِنْ دِينهِ مَا لَمْ يُصِبْ دَمًا حَرَامًا)). رواه البخاري
Imepokewa na ibn ‘Umar (Radhwiya Allaahu ‘anhumaa) kuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “Muumin atabakia katika duara la matumaini na Iymaan madamu hatamwaga damu iliyoharamishwa.” [Al-Bukhaariy]



Hadiyth – 18
وعن خولة بنتِ عامر الأنصارية وهي امرأة حمزة رضي الله عنه وعنها، قَالَتْ: سمعت رَسُول الله صلى الله عليه وسلم يقول: ((إنَّ رِجَالًا يَتَخَوَّضُونَ في مَالِ الله بغَيرِ حَقٍّ، فَلَهُمُ النَّارُ يَومَ القِيَامَةِ)). رواه البخاري
Imepokewa kutoka kwa Khawlah bint ‘Aamir Al-Answaariyyah (Radhwiya Allaahu ‘anhaa), naye ni mke wa Hamzah bin ‘Abdul-Mutw-Twalib (Radhwiya Allaahu ‘anhumaa) kuwa amemsikia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) Akisema: “Hakika watu wanaotumia mali ya Allaah (mali ya Ummah) pasi na haki, hao wana Moto Siku ya Qiyaamah.” [Al-Bukhaariy]