025 – Mlango Wa Amri Ya kurudisha Amana
باب الأمر بأداء الأمانة

قَالَ الله تَعَالَى:

إِنَّ اللَّـهَ يَأْمُرُكُمْ أَن تُؤَدُّوا الْأَمَانَاتِ إِلَىٰ أَهْلِهَا
Hakika Allaah Anakuamrisheni kurudisha amana kwa wenyewe. [An-Nisaa: 58]


إِنَّا عَرَضْنَا الْأَمَانَةَ عَلَى السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ وَالْجِبَالِ فَأَبَيْنَ أَن يَحْمِلْنَهَا وَأَشْفَقْنَ مِنْهَا وَحَمَلَهَا الْإِنسَانُ ۖ إِنَّهُ كَانَ ظَلُومًا جَهُولًا ﴿٧٢﴾
Hakika Sisi Tulihudhurisha amana kwa mbingu na ardhi na majabali vikakataa kuibeba na vikaiogopa; lakini insani akaibeba. Hakika yeye amekuwa dhalimu mno, jahili mno. [Al-Ahzaab: 72]



Hadiyth – 1
وعن أَبي هريرة رضي الله عنه: أن رَسُول الله صلى الله عليه وسلم قَالَ: ((آيةُ المُنافقِ ثلاثٌ: إِذَا حَدَّثَ كَذَبَ، وَإِذَا وَعدَ أخْلَفَ، وَإِذَا اؤْتُمِنَ خَانَ)). مُتَّفَقٌ عَلَيهِ
وفي رواية: ((وَإِنْ صَامَ وَصَلَّى وَزَعَمَ أنَّهُ مُسْلِمٌ))
Imepokewa kutoka kwa Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) ya kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi sallam) amesema: “Alama za mtu mnafiki ni tatu: Anaposema husema uongo, na napoahidi hatakelezi, na anapoaminiwa hufanya khiyana” [Al-Bukhaariy na Muslim]
Riwaayah nyingine: “Japokuwa atafunga na kuswali na akajichukulia kuwa yeye ni Muislamu.”




Hadiyth – 2
وعن حذيفة بن اليمان رضي الله عنه قَالَ: حدثنا رَسُول الله صلى الله عليه وسلم حدِيثَينِ قَدْ رأيْتُ أحَدَهُمَا وأنا أنتظرُ الآخر: حدثنا أن الأمانة نَزلت في جَذرِ قلوبِ الرجال، ثُمَّ نزل القرآن فعلموا مِنَ القرآن، وعلِموا من السنةِ.
ثُمَّ حدّثنا عن رفع الأمانة، فَقَالَ: ((يَنَامُ الرَّجُلُ النَّوْمَةَ فَتُقْبَضُ الأَمَانَةُ مِنْ قَلْبهِ، فَيَظَلُّ أثَرُهَا مِثلَ الوَكْتِ، ثُمَّ يَنَامُ النَّومَةَ فَتُقْبَضُ الأَمَانَةُ مِنْ قَلْبهِ، فَيَظَلُّ أثَرُهَا مِثلَ أَثَرِ المَجْلِ، كَجَمْرٍ دَحْرَجْتَهُ عَلَى رِجْلِكَ فَنَفِطَ، فَتَرَاهُ مُنْتَبرًا وَلَيسَ فِيهِ شَيءٌ)) ثُمَّ أخَذَ حَصَاةً فَدَحْرَجَهُ عَلَى رِجْلِهِ ((فَيُصْبحُ النَّاسُ يَتَبَايعُونَ، فَلا يَكَادُ أحدٌ يُؤَدّي الأَمَانَةَ حَتَّى يُقَالَ: إنَّ في بَني فُلانٍ رَجُلًا أمينًا، حَتَّى يُقَالَ لِلرَّجُلِ: مَا أجْلَدَهُ! مَا أَظْرَفَهُ! مَا أعْقَلَهُ! وَمَا في قَلْبِهِ مِثْقَالُ حَبَّة مِن خَرْدَل مِنْ إيمَان وَلَقدْ أتَى عَلَيَّ زَمَانٌ وَمَا أُبَالِي أيُّكُمْ بَايَعْتُ: لَئن كَانَ مُسْلِمًا لَيَرُدَّنَّهُ عليَّ دِينهُ، وَإنْ كَانَ نَصْرانِيًّا أَوْ يَهُودِيًا لَيَرُدَّنَّهُ عَلَيَّ سَاعِيهِ، وَأَمَّا اليَوْمَ فَمَا كُنْتُ أُبَايعُ مِنْكُمْ إلا فُلانًا وَفُلانًا)). مُتَّفَقٌ عَلَيهِ
Imepokewa kutoka kwake Hudhayfah bin Al-Yamaan (Radhwiya Allaahu 'anhu) ya kwamba: Ametuhadithia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi sallam) Hadiyth mbili, nami nimeiona Hadiyth moja kati ya hizo mbili na ninangoja kuiona hiyo ya pili. Alituhadithia ya kwamba, amana iliteremshwa na kukita katika mioyo ya watu. Wakati Qur-aan iliteremshwa waliweza kuelimishwa kwa Qur-aan na Sunnah. Kisha akatuhadithia kuhusu kunyanyuliwa amanah, akasema: “Analala mtu usiku na anapoamka na anajikuta kuwa amatolewa uaminifu katika moyo wake na kubakishwa kivuli chake tu. Kisha analala tena usiku na uaminifu unaondolewa katika moyo wake na kubakia alama ndogo mfano wa lenge lenge kama anapoguswa mmoja wenu na moto katika mguu wake na hivyo kupata lenge lenge ambalo linapasuka basi ndani huwa tupu kabisa.” Kisha akachukua vijiwe na kuanza kujipiga mguu wake: “Watu watakuwa wanapambazukia katika biashara (kuuza na kununua), lakini hakuna hata mmoja atayetekeleza uaminifu (kurudisha amanah), mpaka imesemwe, hakika katika ukoo fulani kuna mtu muaminifu, mpaka pia isemwe kwa mtu (ambaye ni hodari katika mambo ya dunia). Tazama jinsi gani alivyo hodari, jinsi gani alivyo mzuri, na jinsi gani alivyo na akili, lakini kwenye moyo wake hana hata chembe ya iymaan.” Hakika nimefikiwa na wakati ambapo sikujali mtu gani ninayefanya naye biashara. Akiwa ni Musilamu basi Dini yake ni dhamana tosha kwangu, na akiwa ni Naswara, au Myahudi  basi (mzazi) au walii wake atatimiza amana hiyo (ni dhamana tosha). Lakini ama leo sifanyi biashara miongoni mwenu isipokuwa fulani na fulani.  [Al-Bukhaariy na Muslim]



Hadiyth – 3
وعن حُذَيفَة وأبي هريرة رضي الله عنهما قالا: قَالَ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم: ((يَجمَعُ اللهُ تبَارَكَ وَتَعَالَى النَّاسَ فَيَقُومُ المُؤمِنُونَ حَتَّى تُزْلَفَ لَهُمُ الجَنَّةُ، فَيَأتُونَ آدَمَ صَلَواتُ اللهِ عَلَيهِ، فَيقُولُونَ: يَا أَبَانَا اسْتَفْتِحْ لَنَا الجَنَّةَ، فَيقُولُ: وَهَلْ أخْرَجَكُمْ مِنَ الجَنَّةِ إلا خَطيئَةُ أبيكُمْ! لَسْتُ بِصَاحِبِ ذلِكَ، اذْهَبُوا إِلَى ابْنِي إِبْراهيمَ خَلِيل اللهِ.
قَالَ: فَيَأتُونَ إبرَاهِيمَ فَيَقُولُ إبراهيم: لَسْتُ بِصَاحِبِ ذلِكَ إِنَّمَا كُنْتُ خَليلًا مِنْ وَرَاءَ وَرَاءَ، اعْمَدُوا إِلَى مُوسَى الَّذِي كَلَّمَهُ الله تَكليمًا. فَيَأتُونَ مُوسَى، فَيَقُولُ: لستُ بِصَاحِبِ ذلِكَ، اذْهَبُوا إِلَى عِيسى كلمةِ اللهِ ورُوحه، فيقول عيسى: لستُ بصَاحبِ ذلِكَ.
فَيَأتُونَ مُحَمَّدًا صلى الله عليه وسلم فَيَقُومُ فَيُؤذَنُ لَهُ، وتُرْسَلُ الأَمَانَةُ وَالرَّحِمُ فَيَقُومانِ جَنْبَتَي الصِّرَاطِ يَمِينًا وَشِمَالًا فَيَمُرُّ أوَّلُكُمْ كَالبَرْقِ)) قُلْتُ: بأبي وَأمِّي، أيُّ شَيءٍ كَمَرِّ البَرقِ؟ قَالَ: ((ألَمْ تَرَوا كَيْفَ يمُرُّ وَيَرْجِعُ في طَرْفَةِ عَيْن، ثُمَّ كَمَرّ الرِّيحِ، ثُمَّ كَمَرِّ الطَّيْرِ، وَأَشَدِّ الرِّجَال تَجْري بهمْ أعْمَالُهُمْ، وَنَبيُّكُمْ قَائِمٌ عَلَى الصِّراطِ، يَقُولُ: رَبِّ سَلِّمْ سَلِّمْ، حَتَّى تَعْجِزَ أعْمَالُ العِبَادِ، حَتَّى يَجِيء الرَّجُلُ لا يَسْتَطِيعُ السَّيْرَ إلا زَحْفًا، وَفي حَافَتي الصِّراطِ كَلاَلِيبُ معَلَّقَةٌ مَأمُورَةٌ بِأخْذِ مَنْ أُمِرَتْ بِهِ، فَمَخْدُوشٌ نَاجٍ، وَمُكَرْدَسٌ في النَّارِ)) وَالَّذِي نَفْسُ أَبي هُرَيْرَةَ بِيَدِهِ، إنَّ قَعْرَ جَهَنَّمَ لَسَبْعُونَ خَرِيفًا. رواه مسلم
Imepokewa kutoka kwa Hudhayfah na Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu 'anhumaa) ya kwamba: Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi sallam) amesema: “Allaah (Subhaanahu Wa Ta'aalaa) Atawakusanya watu. Watasimama waumini mpaka watakuja karibu na Jannah, na hapo watamuendea Aadam (‘Alayhis Salaam) na kumwambia: “Ee Aadam baba yetu, tufungulie Jannah. Atasema: Ni kosa la baba yenu ndio lililowatoa nyinyi katika Jannah. Mimi sina uwezo wa kuwasaidia, hivyo nendeni kwa mtoto wangu Ibraahiym (‘Alayhis Salaam), ni kipenzi cha Allaah (Subhaanahu Wa Ta'aalaa). Amasema: Watakwenda kwa Ibraahiym (‘Alayhis Salaam), na watamwambia. Atasema: Mimi sina uwezo, hakika mimi nilikuwa kipenzi tu na wala sina darja hiyo ya juu. Nendeni kwa Muwsaa ambaye Allaah (Subhaanahu Wa Ta'aalaa) Alizungumza naye kwa uwazi kabisa. Watakuja kwa Muwsaa (‘Alayhis Salaam), naye atasema: Mimi si mwenyewe wa jambo hilo. Hapo watakuja kwa Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa salaam). Atasimama mbele ya Allaah (Subhaanahu Wa Ta'aalaa) na atakubaliwa kuwatetea watu. Itatumwa amana na kuunganisha kizazi, nazo zitasimama pembezoni mwa Swiraatw (njia) kulia na kushoto. Wa mwanzo wenu watapita kama umeme. Nikasema: Baba yangu na mama yangu wawe fidia kwako unamaanisha nini? Akasema: “Huoni cheche za umeme zinazokwenda na kurudi katika kupepesa jicho? Kisha watapita kama upepo, kisha kama ndege, na wengine kwa kasi ya watu wanaokimbia, na tofauti hii (ya kasi) itakuwa kwa sababu ya ‘amali za kila mmoja wenu. Na Rasuli wenu (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi sallam) atakuwa amesimama juu ya Swiraatw, anasema: Mola wangu! Wasalimishe, wasalimishe. Mpaka matendo ya waja yashindwe, mpaka mtu aje hawezi kupita isipokuwa kwa kutambaa na katika pande zote mbili za Swiraatw kuna koleo zimening’ing’izwa, ambazo zimeamriwa (na Allaah Subhaanahu Wa Ta'aalaa). Yule atakayekwaruzwa atakuwa ni mwenye kufaulu na wasiokuwa wao wataingia motoni. Na yule ambaye kwamba nafsi ya Abuu Hurayrah ipo mikononi Mwake, hakika urefu wa Jahannam ni masafa miaka sabini. [Muslim]



Hadiyth – 4
وعن أَبي خُبيب- بضم الخاء المعجمة- عبد الله بن الزبير رضي الله عنهما، قَالَ: لَمَّا وَقفَ الزُّبَيْرُ يَوْمَ الجَمَل دَعَانِي فَقُمْتُ إِلَى جَنْبه، فَقَالَ: يَا بُنَيَّ، إنَّهُ لا يُقْتَلُ اليَومَ إلا ظَالِمٌ أَوْ مَظْلُومٌ، وَإنِّي لا أراني إلا سَأُقْتَلُ اليوم مظلومًا، وإنَّ مِنْ أكبرَ هَمِّي لَدَيْنِي، أفَتَرَى دَيْننا يُبقي من مالِنا شَيئًا؟ ثُمَّ قَالَ: يَا بُنَيَّ، بعْ مَا لَنَا وَاقْضِ دَيْنِي، وَأوْصَى بِالثُّلُثِ وَثُلُثِهِ لِبَنِيهِ، يعني لبني عبد الله بن الزبير ثُلُثُ الثُّلُث. قَالَ: فَإنْ فَضَلَ مِنْ مَالِنَا بَعْدَ قَضَاءِ الدَّينِ شَيء فَثُلُثُه لِبَنِيكَ. قَالَ هِشَام: وَكَانَ بَعْضُ وَلَدِ عَبْدِ اللهِ قَدْ وَازى بَعْضَ بَنِي الزُّبَيْرِ خُبيبٍ وَعَبَّادٍ، وَلهُ يَوْمَئذٍ تِسْعَةُ بَنينَ وَتِسْعُ بَنَات.
قَالَ عَبدُ الله: فَجَعلَ يُوصينِي بدَيْنِهِ وَيَقُولُ: يَا بُنَيَّ، إنْ عَجَزْتَ عَن شَيْءٍ مِنْهُ فَاسْتَعِنْ عَلَيهِ بِمَوْلاَيَ. قَالَ: فَوَاللهِ مَا دَرَيْتُ مَا أرَادَ حَتَّى قُلْتُ: يَا أبَتِ مَنْ مَوْلاَكَ؟ قَالَ: الله. قَالَ: فَوَاللهِ مَا وَقَعْتُ في كُرْبةٍ مِنْ دَيْنِهِ إلا قُلْتُ: يَا مَوْلَى الزُّبَيْرِ اقْضِ عَنْهُ دَيْنَهُ فَيَقْضِيَهُ. قَالَ: فَقُتِلَ الزُّبَيْرُ وَلَم يَدَعْ دِينَارًا وَلا دِرْهمًا إلا أرَضِينَ، مِنْهَا الغَابَةُ وإحْدَى عَشْرَةَ دَارًا بالمَدِينَةِ، وَدَارَيْنِ بالبَصْرَةِ، ودَارًا بالكُوفَةِ، ودَارًا بمِصْرَ.
قَالَ: وَإِنَّمَا كَانَ دَيْنُهُ الَّذِي كَانَ عَلَيهِ أنَّ الرَّجُلَ كَانَ يَأتِيهِ بالمال، فَيَسْتَودِعُهُ إيَّاهُ، فَيَقُولُ الزُّبَيْرُ: لا، وَلَكِنْ هُوَ سَلَفٌ إنِّي أخْشَى عَلَيهِ الضَّيْعَةَ. وَمَا وَليَ إمَارَةً قَطُّ وَلا جِبَايَةً، ولا خراجًا، وَلا شَيئًا إلا أنْ يَكُونَ في غَزْوٍ مَعَ رسولِ الله صلى الله عليه وسلم أَوْ مَعَ أَبي بَكْرٍ وَعُمَرَ وَعُثْمَانَ رضي الله عنهم، قَالَ عَبدُ الله: فَحَسَبْتُ مَا كَانَ عَلَيهِ مِن الدَّيْنِ فَوَجَدْتُهُ ألْفيْ ألْفٍ وَمئَتَي ألْف ‍! فَلَقِيَ حَكِيمُ بنُ حِزَام عَبْدَ الله بْنَ الزُّبَيْرِ، فَقَالَ: يَا ابْنَ أخِي، كَمْ عَلَى أخي مِنَ الدَّيْنِ؟ فَكَتَمْتُهُ وَقُلْتُ: مِائَةُ ألْف. فَقَالَ حَكيمٌ: واللهِ مَا أرَى أمْوَالَكُمْ تَسَعُ هذِهِ. فَقَالَ عَبْدُ اللهِ: أرَأيْتُكَ إنْ كَانَتْ ألْفَي ألف وَمائَتَيْ ألْف؟ قَالَ: مَا أرَاكُمْ تُطيقُونَ هَذَا، فَإنْ عَجَزْتُمْ عَنْ شَيءٍ مِنْهُ فَاسْتَعِينُوا بي.
قَالَ: وَكَانَ الزُّبَيرُ قَد اشْتَرَى الغَابَةَ بِسَبْعِينَ ومائة ألف، فَبَاعَهَا عَبدُ اللهِ بِألْفِ ألْف وَسِتّمِائَةِ ألْف، ثُمَّ قَامَ فَقَالَ: مَنْ كَانَ لَهُ عَلَى الزُّبَيرِ شَيْء فَلْيُوافِنَا بِالغَابَةِ، فَأتَاهُ عَبدُ اللهِ بنُ جَعفَر، وَكَانَ لَهُ عَلَى الزُّبَيرِ أرْبَعمائةِ ألْف، فَقَالَ لعَبدِ الله: إنْ شِئْتُمْ تَرَكْتُهَا لَكمْ؟ قَالَ عَبدُ الله: لا، قَالَ: فَإنْ شِئتُمْ جَعَلْتُمُوهَا فِيمَا تُؤَخِّرُونَ إنْ إخَّرْتُمْ، فَقَالَ عَبدُ الله: لا، قَالَ: فَاقْطَعُوا لِي قطْعَةً، قَالَ عَبدُ الله: لَكَ مِنْ هاهُنَا إِلَى هَاهُنَا. فَبَاعَ عَبدُ اللهِ مِنهَا فَقَضَى عَنْهُ دَينَه وَأوْفَاهُ، وَبَقِيَ مِنْهَا أرْبَعَةُ أسْهُم وَنِصْفٌ، فَقَدِمَ عَلَى مُعَاوِيَة وَعنْدَهُ عَمْرُو بْنُ عُثْمَانَ، وَالمُنْذِرُ بْنُ الزُّبَيْرِ، وَابْنُ زَمْعَةَ، فَقَالَ لَهُ مُعَاويَةُ: كَمْ قُوِّمَتِ الغَابَةُ؟ قَالَ: كُلُّ سَهْم بمائَة ألف، قَالَ: كَمْ بَقِيَ مِنْهَا؟ قَالَ: أرْبَعَةُ أسْهُم وَنصْفٌ، فَقَالَ المُنْذِرُ بْنُ الزُّبَيرِ: قَدْ أخَذْتُ مِنْهَا سَهمًا بِمائَةِ ألف، قَالَ عَمْرُو بْنُ عُثْمَانَ: قَدْ أخَذْتُ مِنْهَا سَهْمًا بمائَةِ ألْف. وَقالَ ابْنُ زَمْعَةَ: قَدْ أخَذْتُ سَهْمًا بِمائَةِ ألْف، فَقَالَ مُعَاويَةُ: كَمْ بَقِيَ مِنْهَا؟ قَالَ: سَهْمٌ ونصْفُ سَهْم، قَالَ: قَدْ أخَذْتُهُ بخَمْسِينَ وَمائَةِ ألْف. قَالَ: وَبَاعَ عَبدُ الله بْنُ جَعفَر نَصيبهُ مِنْ مَعَاوِيَةَ بستِّمِائَةِ ألْف.
فَلَمَّا فَرَغَ ابْنُ الزُّبَيرِ مِنْ قَضَاءِ دَيْنِهِ، قَالَ بَنُو الزُّبَيرِ: اقسمْ بَينَنَا ميراثَنا، قَالَ: وَاللهِ لا أقْسِمُ بَيْنَكُمْ حَتَّى أنَادِي بالمَوْسم أرْبَعَ سنينَ: ألا مَنْ كَانَ لَهُ عَلَى الزُّبَيرِ دَيْنٌ فَلْيَأتِنَا فَلْنَقْضِهِ. فَجَعَلَ كُلّ سَنَةٍ يُنَادِي في المَوْسِمِ، فَلَمَّا مَضَى أرْبَعُ سنينَ قَسَمَ بيْنَهُمْ وَدَفَعَ الثُّلُثَ. وَكَانَ للزُّبَيْرِ أرْبَعُ نِسْوَةٍ، فَأصَابَ كُلَّ امرَأةٍ ألْفُ ألف وَمِئَتَا ألْف، فَجَميعُ مَالِه خَمْسُونَ ألف ألْف وَمِئَتَا ألْف. رواه البخاري
Imepokwa kutoka kwa Abuu Khubayd, ‘Abdullaah bin Az-Zubayr (Radhwiya Allaahu 'anhumaa) ya kwamba: Aliposimama Az-Zubayr katika vita vya Ngamia, aliniita nami nikasimama ubavuni mwake. Alinambia: Ewe mtoto wangu! Hautauliwa leo isipokuwa dhalimu au aliyedhulumiwa. Nami nina hakika ya kuwa nitauliwa leo kwa dhulma. Na hakika hamu yangu kubwa ni deni langu. Je, unafikiria kutabakia chochote katika mali baada ya kulipa deni? Kisha akasema: Ewe mtoto wangu! Uza rasimali yangu na ulipe deni langu. Na nausia ya kwamba thuluthi ya thuluthi (1/9) iwe ni ya watoto wako (yaani ‘Abdullaah bin Az-Zubayr), kwa kile kitakachobakia. Baada ya hii ikiwa kutabakia chochote basi thuluthi itakuwa ni ya watoto wako. Amasema Hishaam: Na walikuwa baadhi ya watoto wa ‘Abdullaah ni rika moja na watoto wa Az-Zubayr, kama Khubayb na ‘Abbaad, na wakati huo alikuwa na vijana tisa na mabinti tisa. Akasema: Ewe mtoto wangu! Ukishindwa kulipa deni langu basi takamsaada kwa Bwana wangu. Akasema: Naapa kwa Allaah! Sikufahamu alilokusudia mpaka nilipouuliza: Ewe baba yangu! Nani bwana wako? Akasema: Allaah. Akasema tena (‘Abdullaah): Naapa kwa Allaah! Sijapatwa tena na shida ya deni lake isipokuwa nilikuwa nasema, Ee Bwana wa Az-Zubayr mwondoshee deni lake, Naye Allaah (Subhaanahu Wa Ta'aalaa) Alikuwa anamuondoshea. Az-Zubayr (Radhwiya Allaahu 'anhu) aliuliwa siku hiyo na hakuacha hata dinari moja wala dirhamu isipokuwa vipande viwili vya ardhi, moja katika hiyo ikiwa katika sehemu ya Ghaabah na nyumba kumi na moja Madiynah, na nyumba mbili Basrah, na nyumba moja Kufah, na nyumba moja Misri. Na kwa hakika deni lake lilitokana na watu waliokuwa wakimjia ili awahifadhie mali zao, lakini Az-Zubayr alikuwa anawaambia: Hapana! Siwezi jukumu hilo kwani huenda ikapotea lakini naweza kuichukua hiyo amana kama deni juu yangu. Yeye hakukubali nafasi ya uongozi wala wadhifa wa kukusanya kodi wala kitu chengine chochote isipokuwa ile ngawira aliyopatiwa katika vita alivyopigana wakati wa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi sallam), au Abu Bakr, au ‘Umar, au ‘Uthmaan (Radhwiya Allaahu 'anhum). Akasema (‘Abdullaah): Nikahesabu deni lake na jumla ikafika million mbili na laki mbili. Nilikutana na Hakiym bin Hizaam, naye akasema: Ewe mtoto wa ndugu yangu! Ndugu yangu anadenia la kiasi gani? Nikaficha hilo kwa kusema: Laki moja. Akasema Hakiym: Kwa Allaah, sidhani ya kwamba mali yenu itafikia kiwango hicho. Nikasema: Unaonaje deni likiwa ni milioni mbili na laki mbili? Akasema: Sidhani ya kwamba mtaweza kuubeba mzigo huo, hivyo mkiwa na uzito wa aina yoyote njooni kwangu kwa msaada. Az-Zubayr alikuwa ameinunua ile ardhi ya Ghaabah kwa laki moja na elfu sabini, nami nikauza kwa milioni moja na laki sita. Kisha akasimama ‘Abdullaah na kunadi Az-Zubayr atukute katika ardhi ya Ghaabah. Akaja ‘Abdullaah bin Ja’far, ambaye alikuwa anamdai Az-Zubayr laki nne. Alimwambia ibn Zubayr: Mkipenda nitawaachia deni hilo? Nikasema: Hapana, Akasema: Ikiwa mnataka nitawapatia muda wa kunilipa. Akasema ibn Zubayr: Hapana. Akasema ibn Ja’far basi nikatie kipande cha ardhi. Akasema ‘Abdullaah: Kipande chako ni kuanzia hapa mpaka hapa. Kwa njia hii ‘Abdullaah alimlipia baba yake deni. Baada ya hapo ikabaki ardhi yenye kipimo cha siham nne na nusu. Akaja Mu’awiyyah pamoja naye ni ‘Amru bin ‘Uthmaan na Al-Mundhir bin Az-Zubayr na ibn Zam’ah. Akasema Mu’awiyyah: Hii Ghaabah ni bei gani? Akasema: Kila siham ni laki moja. Akasema: Imebakia kiasi gani? Akasema: Siham nne na nusu. Hapo akasema Mundhir bin Zubayr: Mimi nimechukua sihim moja kwa bei hiyo ya laki moja. Akasema ‘Amru bin ‘Uthmaan: Nami nachukua sihim moja kwa bei hiyo ya laki moja. Na akasema ibn Zam’ah: Nami nimechukua sihim moja kwa bei ya laki moja. Akasema Mu’awiyyah: Imebaki kiasi gani cha ardhi? Akasema (‘Abdullaah): Sihim moja na nusu. Akasema Mu’awiyyah: Nimeichukua kwa laki moja na nusu. Baadae ‘Abdullaah bin Ja’far alimuuzia Mu’awiyyah sehemu yake ya ardhi kwa laki sita. ‘Abdullaah bin Zubayr alipomaliza shughuli hii yote ya kulipa madeni ya baba yake, walimjia warithi wa Az-Zubayr  na kumwambia: Tupatie fungu letu la mirathi. Akasema: Naapa kwa Allaah! Sitagawa mirathi mpaka mwanzo ninadi katika msimu wa Hijjah kwa miaka minne mfululizo. Mtu yoyote anayemdai Az-Zubayr basi atujie tumrudishie haki yake. Akajaalia kuwa ananadi kila mwaka katika msimu wa Hijjah. Ilipomalizika miaka minne aligawanya pesa zilizobakia baina yao akalipa thuluthi. Az-Zubayr alikuwa na wake wanne, hivyo kila mmke alipata milioni moja na laki mbili, kwani jumla ya mali yake yote ilikuwa milioni khamsini na laki mbili. [Al-Bukhaariy)