باب تغليظ عقوبة من أمر بمعروف أَوْ نهى عن منكر وخالف قوله فعله
024 - Mlango Wa Adhabu Kali Kwa Mwenye Kuamrisha Mema Au Kukataza Maovu Kisha Kauli Yake Ikawa Kinyume Na Matendo Yake


قَالَ الله تَعَالَى:
أَتَأْمُرُونَ النَّاسَ بِالْبِرِّ وَتَنسَوْنَ أَنفُسَكُمْ وَأَنتُمْ تَتْلُونَ الْكِتَابَ ۚ أَفَلَا تَعْقِلُونَ ﴿٤٤﴾ 
Je, mnaamrisha watu watende mema na mnajisahu nafsi zenu na hali ya kuwa nyinyi mnasoma Kitabu; je hamtii akilini? [Al-Baqarah: 44]

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لِمَ تَقُولُونَ مَا لَا تَفْعَلُونَ﴿٢﴾
 Enyi walioamini! Kwanini mnasema yale msiyoyafanya?  

كَبُرَ مَقْتًا عِندَ اللَّـهِ أَن تَقُولُوا مَا لَا تَفْعَلُونَ﴿٣﴾
 Ni chukizo kubwa mno mbele ya Allaah kwamba mnasema yale msiyoyafanya. [Asw- Swaff: 2-3 ]

وَمَا أُرِيدُ أَنْ أُخَالِفَكُمْ إِلَىٰ مَا أَنْهَاكُمْ عَنْهُ ۚ
…Nami sitaki kukukhalifuni kufanya ninayokukatazeni… [Huwd: 88]



Hadiyth – 1
وعن أَبي زيد أسامة بن زيد بن حارثة رضي الله عنهما، قَالَ: سمعت رَسُول الله صلى الله عليه وسلم يقول: ((يُؤْتَى بالرَّجُلِ يَوْمَ القيَامَةِ فَيُلْقَى في النَّارِ، فَتَنْدَلِقُ أقْتَابُ بَطْنِهِ فَيدُورُ بِهَا كَمَا يَدُورُ الحِمَارُ في الرَّحَى، فَيَجْتَمِعُ إِلَيْه أهْلُ النَّارِ، فَيَقُولُونَ: يَا فُلانُ، مَا لَكَ؟ أَلَمْ تَكُ تَأمُرُ بالمعْرُوفِ وَتنهَى عَنِ المُنْكَرِ؟ فَيقُولُ: بَلَى، كُنْتُ آمُرُ بِالمَعْرُوفِ وَلا آتِيهِ، وأنْهَى عَنِ المُنْكَرِ وَآتِيهِ)). مُتَّفَقٌ عَلَيهِ
Kutoka kwa Abuu Zayd Usaamah bin Zayd bin Haarithah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kuwa amesema: Nimemsikia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi sallam) akisema: “Ataletwa mtu siku ya Qiyaamah na atiwe motoni. Matumbo yake yatatoka nje (huku ameyashika mkononi mwake) na atakuwa anazunguka nayo kama anavyozunguka punda anayesaga katika mtambo.” Watakusanyika mbele yake watu wa motoni na waseme: “Ee Fulani, una nini? Si wewe ndiye uliokuwa ukituamrisha mema na kutukataza maovu?” Atasema Fulani: “Ndio, nilikuwa nikiamrisha mema lakini mimi mwenyewe sifanyi na nilikuwa nikikataza maovu na nikiyaendea (nikifanya ninayokataza).” [Al-Bukhaariy, Muslim na Ahmad]