باب التعاون عَلَى البر والتقوى
021 – Mlango Wa Kusaidiana Katika Wema Na Taqwa
قَالَ الله تَعَالَى:
وَتَعَاوَنُوا عَلَى الْبِرِّ وَالتَّقْوَىٰ ۖ
Na shirikianeni katika wema na taqwa… (Al-Maaidah: 2)
وَالْعَصْرِ ﴿١﴾
Naapa kwa Al-‘Aswr (zama).
إِنَّ الْإِنسَانَ لَفِي خُسْرٍ ﴿٢﴾
Hakika mwana wa Aadam bila shaka yumo katika khasara.
إِلَّا الَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ وَتَوَاصَوْا بِالْحَقِّ وَتَوَاصَوْا بِالصَّبْرِ ﴿٣﴾
Isipokuwa wale walioamini na wakatenda mema na wakausiana haki na wakausiana subira. [Al-‘Aswr: 1-3]
Hadiyth – 1
وعن أَبي عبد الرحمن زيد بن خالد الجهني رضي الله عنه قَالَ: قَالَ رسولُ الله صلى الله عليه وسلم: ((مَنْ جَهَّزَ غَازِيًا في سَبيلِ اللهِ فَقَدْ غَزَا، وَمَنْ خَلَفَ غَازيًا في أهْلِهِ بِخَيرٍ فَقَدْ غَزَا)). مُتَّفَقٌ عَلَيهِ
Kutoka Kwa Abuu ‘Abdur-Rahmaan Zayd bin Khaalid Al-Juhaniy (Radhwiya Allaahu 'anhu) ya kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi sallam) amesema: “Yeyote atakayemtayarisha kwa kumpatia vifaa Mujahid katika njia ya Allaah ni kama yeye mwenyewe amehudhuria katika kupigana (hivyo kupata thawabu sawa). Na yeyote mwenye kuwatizama watu wanaomtegemea Mujahid (wakati ambao hayupo) ni kama pia amepigana katika vita.” [Al-Bukhaariy na Muslim]
Hadiyth – 2
وعن أَبي سعيد الخدري رضي الله عنه: أن رَسُول الله صلى الله عليه وسلم بعث بعثًا إِلَى بني لِحْيَان مِنْ هُذَيْلٍ، فَقَالَ: ((لِيَنْبَعِثْ مِنْ كُلِّ رَجُلَيْنِ أَحَدُهُمَا وَالأجْرُ بَيْنَهُمَا)). رواه مسلم
Kutoka kwa Abuu Sa’iyd Al-Khudriy (Radhwiya Allaahu 'anhu) ya kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi sallam) alituma kikosi kwa kabila la Lihyaan wa ukoo wa Hudhayl, akasema: “Atoke katika kila watu wawili mtu mmoja na ujira (thawabu) ni baina yao.” [Muslim]
Hadiyth – 3
وعن ابن عباس رضي الله عنهما: أنَّ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم لَقِيَ رَكْبًا بالرَّوْحَاءِ، فَقَالَ: ((مَنِ القَوْمُ؟)) قالوا: المسلمون، فقالوا: من أنتَ؟ قَالَ: ((رَسُول الله))، فرفعت إِلَيْه امرأةٌ صبيًا، فَقَالَتْ: ألِهَذَا حَجٌّ؟ قَالَ: ((نَعَمْ، وَلَكِ أجْرٌ)). رواه مسلم
Kutoka kwa Ibn ‘Abbaas (Radhwiya Allaahu 'anhu) ya kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi sallam) alikutana na kikundi cha watu waliokuwa wamepanda vipandio katika sehemu ya Rawhaa na akawauliza: “Hawa ni watu gani?” Wakasema: “Waislamu.” Kisha wakasema: “Wewe ni nani?” Akasema: “Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi sallam).” Mwanamke mmoja aliyekwepo alimnyanyua mtoto mdogo na kuuliza: “Je,huyu ana hijja?” Akasema Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi sallam): “Ndio, nawe pia utapata ujira (kwa hilo).” [Muslim]
Hadiyth – 4
وعن أَبي موسى الأشعري رضي الله عنه عن النَّبيّ صلى الله عليه وسلم أنَّه قَالَ: ((الخَازِنُ المُسْلِمُ الأمِينُ الَّذِي يُنفِذُ مَا أُمِرَ بِهِ فيُعْطيهِ كَامِلًا مُوَفَّرًا طَيِّبَةً بِهِ نَفْسُهُ فَيَدْفَعُهُ إِلَى الَّذِي أُمِرَ لَهُ بِهِ، أحَدُ المُتَصَدِّقين)). مُتَّفَقٌ عَلَيهِ
وفي رواية: ((الَّذِي يُعْطِي مَا أُمِرَ بِهِ))
Kutoka kwa Abuu Muwsaa Al-Ash’ariy (Radhwiya Allaahu 'anhu) ya kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi sallam) amesema “Muweka hazina Muislamu, ni yule aliye muaminifu mwenye kumpatia mtu anayestahiki haki yake kwa ukamilifu na kuwa na nafasi nzuri. Na kule kumpatia yule aliyeamriwa kwake inakuwa ni swadaqa.
Riwaya nyengine: “Yule ambaye anatoa katika yale aliyomrishwa.” [Al-Bukhaariy na Muslim]
0 Comments