باب وجوب الانقياد لحكم الله تعالى
وما يقوله من دُعِيَ إلى ذلك وأُمر بمعروف أو نُهي عن منكر
017–Wajibu Wa Kuifuata Hukumu Ya Allaah (Ta'aalaa)
Na Yale Anayotakiwa Mtu Kuyasema Pindi Anapoitwa Katika Hayo,
Akaamrishwa Mema Au Akakatazwa Munkari


قال الله تعالى:
Anasema Allaah (Ta’aalaa)

فَلَا وَرَبِّكَ لَا يُؤْمِنُونَ حَتَّىٰ يُحَكِّمُوكَ فِيمَا شَجَرَ بَيْنَهُمْ ثُمَّ لَا يَجِدُوا فِي أَنفُسِهِمْ حَرَجًا مِّمَّا قَضَيْتَ وَيُسَلِّمُوا تَسْلِيمًا ﴿٦٥﴾
Basi Naapa kwa Rabb wako, hawatoamini mpaka wakufanye wewe ni mwamuzi katika yale wanayozozana baina yao, kisha wasipate katika nyoyo zao karaha katika yale uliyohukumu na wajisalimishe, kwa kujisalimisha (kikamilifu). [An-Nisaa: 65]


إِنَّمَا كَانَ قَوْلَ الْمُؤْمِنِينَ إِذَا دُعُوا إِلَى اللَّـهِ وَرَسُولِهِ لِيَحْكُمَ بَيْنَهُمْ أَن يَقُولُوا سَمِعْنَا وَأَطَعْنَا ۚ وَأُولَـٰئِكَ هُمُ الْمُفْلِحُونَ ﴿٥١﴾
Hakika kauli ya Waumini wa kweli wanapoitwa kwa Allaah na Rasuli Wake ili Awahakumu baina yao; husema: “Tumesikia na Tumetii.” Na hao ndio wenye kufaulu. [An-Nuwr: 51]


Hadiyth - 1

عن أَبي هريرة رضي الله عنه قَالَ: لَمَّا نَزَلَتْ عَلَى رَسُول الله صلى الله عليه وسلم: ((لِلَّهِ مَا فِي السَّمَاوَاتِ وَمَا فِي الْأَرْضِ وَإِنْ تُبْدُوا مَا فِي أَنْفُسِكُمْ أَوْ تُخْفُوهُ يُحَاسِبْكُمْ بِهِ اللَّهُ)) [البقرة: 284] الآية.
اشْتَدَّ ذلِكَ عَلَى أصْحَابِ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم، فَأتَوا رَسُول الله صلى الله عليه وسلم ثُمَّ بَرَكُوا عَلَى الرُّكَبِ، فَقَالُوا: أيْ رسولَ الله، كُلِّفْنَا مِنَ الأَعمَالِ مَا نُطِيقُ: الصَّلاةَ والجِهَادَ والصِّيامَ والصَّدَقَةَ، وَقَدْ أُنْزِلَتْ عَلَيْكَ هذِهِ الآيَةُ وَلا نُطيقُها. قَالَ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم: ((أتُرِيدُونَ أنْ تَقُولُوا كَمَا قَالَ أَهْلُ الكتَابَينِ مِنْ قَبْلِكُمْ: سَمِعْنَا وَعَصَيْنَا؟ بَلْ قُولُوا: سَمِعنَا وَأَطَعْنَا غُفْرَانَكَ رَبَّنَا وَإِلَيْكَ المَصِيرُ))  قَالُوا: سمعنا وأَطعنا غفرانك ربنا وإِليك المصير  
فَلَمَّا اقْتَرَأَهَا القومُ، وَذَلَّتْ بِهَا ألْسنَتُهُمْ أنْزَلَ اللهُ تَعَالَى في إثرِهَا: ((آمَنَ الرَّسُولُ بِمَا أُنْزِلَ إِلَيْهِ مِنْ رَبِّهِ وَالْمُؤْمِنُونَ كُلٌّ آمَنَ بِاللهِ وَمَلائِكَتِهِ وَكُتُبِهِ وَرُسُلِهِ لا نُفَرِّقُ بَيْنَ أَحَدٍ مِنْ رُسُلِهِ وَقَالُوا سَمِعْنَا وَأَطَعْنَا غُفْرَانَكَ رَبَّنَا وَإِلَيْكَ الْمَصِيرُ)) [البقرة: 285]

فَلَمَّا فَعَلُوا ذلِكَ نَسَخَهَا اللهُ تَعَالَى، فَأنزَلَ الله- عز وجل: ((لا يُكَلِّفُ اللهُ نَفْسًا إِلا وُسْعَهَا لَهَا مَا كَسَبَتْ وَعَلَيْهَا مَا اكْتَسَبَتْ رَبَّنَا لا تُؤَاخِذْنَا إِنْ نَسِينَا أَوْ أَخْطَأْنَا)) قَالَ: نَعَمْ
((رَبَّنَا وَلا تَحْمِلْ عَلَيْنَا إِصْرًا كَمَا حَمَلْتَهُ عَلَى الَّذِينَ مِنْ قَبْلِنَا))  قَالَ: نَعَمْ
((رَبَّنَا وَلا تُحَمِّلْنَا مَا لا طَاقَةَ لَنَا بِه))  قَالَ: نَعَمْ
((وَاعْفُ عَنَّا وَاغْفِرْ لَنَا وَارْحَمْنَا أَنْتَ مَوْلانَا فَانْصُرْنَا عَلَى الْقَوْمِ الْكَافِرِينَ)) قَالَ: نَعَمْ. رواه مسلم
Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu ‘anhu) amesema: Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa salaam) alipoteremshiwa Aayah hii: Ni vya Allaah Pekee vyote vilivyomo mbinguni na vilivyomo ardhini. Na mkidhihirisha yale yaliyomo ndani ya nafsi zenu au mkiyaficha; basi Allaah Atakuhesabuni kwayo.” Mpaka mwisho wa Aayah. [Al-Baqarah: 284]

Jambo hilo likawa zito kwa Maswahaba wa Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa salaam) wakamwendea Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa salaam) wakapiga magoti, wakasema: Ee Rasuli wa Allaah, tumekalifishwa ‘amali tunazoziweza; Swalaah, Jihaad, Swawm na kutoa Zakaah. Na kwa hakika umeteremshiwa Aayah hii, lakini hatuiwezi! Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa salaam) akawauliza: “Je, mnataka kusema kama walivyosema Ahlul-Kitaabayni (Mayahudi na Manaswara) kabla yenu? “Tumesikia na tumeasi” Bali semeni: Tumesikia na tumetii, tunakuomba maghfirah Rabb wetu Kwako ni mahali pa kuishia.”
Maswahaba walipoisoma na ndimi zao zikaandama. Allaah Aliteremsha:
 Rasuli ameamini yaliyoteremshwa kwake kutoka kwa Rabb wake na Waumini (pia wameamini). Wote wamemwamini Allaah, na Malaika Wake, na Vitabu Vyake, na Rasuli Wake. (Nao husema): “Hatutofautishi baina ya yeyote kati ya Rasuli Wake.” Na wakasema: “Tumesikia na tumetii, tunakuomba maghfirah Rabb wetu na Kwako ni mahali pa kuishia.” [Al-Baqarah: 285]

Walipofanya hivyo, Allaah Aliifuta (hukmu ya) Aayah hiyo, Akateremsha:
“Allaah Hakalifishi nafsi yoyote ila kwa kadiri ya uwezo wake. Itapata (thawabu) iliyoyachuma, na ni dhidi yake (kwa maovu) iliyojichumia. “Rabb wetu Usituchukulie tukisahau au tukikosea.” Akasema: “Na’aam”.

“Rabb wetu, Usitubebeshe mzigo kama Ulivyoubebesha juu ya wale waliokuwa kabla yetu.” Akasema: “Na’aam”.

 “Rabb wetu, Usitutwike tusiyoyaweza, na Tusamehe, na Tughufurie na Turehemu, Wewe ni Mola Mlinzi wetu, basi Tunusuru dhidi ya watu makafiri.” Akasema: “Na’aam”.  [Muslim]