باب الحث عَلَى الازدياد من الخير في أواخر العمر
012 – Mlango Wa Mahimizo Ya Kuzidisha Kutenda Khayr Mwisho Wa Umri
قَالَ الله تَعَالَى:
Anasema Allaah (Ta’aalaa):
أَوَلَمْ نُعَمِّرْكُم مَّا يَتَذَكَّرُ فِيهِ مَن تَذَكَّرَ وَجَاءَكُمُ النَّذِيرُ ۖ
“Je, kwani Hatukukupeni umri wa kukumbuka mwenye kukumbuka humo? [Faatwir: 37]
قَالَ ابن عباس والمُحَقِّقُونَ: أَو لَمْ نُعَمِّرْكُمْ سِتِّينَ سَنَةً؟ وَيُؤَيِّدُهُ الحديث الَّذِي سنذْكُرُهُ إنْ شاء الله تَعَالَى، وقيل: معناه ثماني عَشْرَة سَنَةً، وقيل: أرْبَعينَ سَنَةً، قاله الحسن والكلبي ومسروق ونُقِلَ عن ابن عباس أيضًا. وَنَقَلُوا أنَّ أَهْلَ المدينَةِ كانوا إِذَا بَلَغَ أَحَدُهُمْ أربْعينَ سَنَةً تَفَرَّغَ للعِبادَةِ
‘Abdullaah bin ‘Abbaas (Radhwiya Allaahu ‘anhumaa) na ‘Ulamaa wenye tahakiki wamesema: “Je, hatukuwapa umri wa miaka sitini?” Kauli hii inatiliwa nguvu na Hadiyth itakayokuja in shaa Allaah (Ta’aalaa). Na imesemekana kuwa, maana yake ni: Miaka kumi na nane, na pia imesemekana ni miaka arobaini. Kauli hii imesemwa na Al-Hasan, Al-Kalbiy na Masruwq. Vile vile imenukuliwa kutoka kwa ‘Abdullaah bin ‘Abbaas wakaeleza kuwa: Watu wa Madiynah ilikuwa mtu akitimiza umri wa miaka arobaini, hujihusisha na ‘Ibaadah pekee.
Hadiyth – 1
عن أبي هريرةَ رضي الله عنه عن النَّبيّ صلى الله عليه وسلم قَالَ: ((أعْذَرَ الله إِلَى امْرِئٍ أَخَّرَ أجَلَهُ حَتَّى بَلَغَ سِتِّينَ سَنَةً)). رواه البخاري
Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu ‘anhu) amesema: Amepokea kutoka kwa Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “Allaah Hakumbakishia udhuru mtu Aliyemuakhirishia mauti yake hata akafikia umri wa miaka sitini.” [Al-Bukhaariy]
Hadiyth – 2
عن ابن عباس رضي الله عنهما، قَالَ: كَانَ عمر رضي الله عنه يُدْخِلُنِي مَعَ أشْيَاخِ بَدرٍ فكأنَّ بَعْضَهُمْ وَجَدَ في نفسِهِ، فَقَالَ: لِمَ يَدْخُلُ هَذَا معنا ولَنَا أبْنَاءٌ مِثلُهُ؟! فَقَالَ عُمَرُ: إنَّهُ منْ حَيثُ عَلِمْتُمْ! فَدعانِي ذاتَ يَومٍ فَأدْخَلَنِي مَعَهُمْ فما رَأيتُ أَنَّهُ دعاني يَومَئذٍ إلا لِيُرِيَهُمْ، قَالَ: مَا تقُولُون في قولِ الله تعالى: {إِذَا جَاءَ نَصْرُ اللهِ وَالْفَتْحُ} [النصر: 1].
فَقَالَ بعضهم: أُمِرْنَا نَحْمَدُ اللهَ وَنَسْتَغْفِرُهُ إِذَا نَصَرنَا وَفَتحَ عَلَيْنَا، وَسَكتَ بَعْضُهُمْ فَلَمْ يَقُلْ شَيئًا. فَقَالَ لي: أَكَذلِكَ تقُول يَا ابنَ عباسٍ؟ فقلت: لا. قَالَ: فما تقول؟ قُلْتُ: هُوَ أجَلُ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم أعلَمَهُ لَهُ، قَالَ: {إِذَا جَاءَ نَصْرُ اللهِ وَالْفَتْحُ} وذلك علامةُ أجَلِكَ {فَسَبِّحْ بِحَمْدِ رَبِّكَ وَاسْتَغْفِرْهُ إِنَّهُ كَانَ تَوَّابًا} [النصر: 3].
فَقَالَ عمر رضي الله عنه: مَا أعلم مِنْهَا إلا مَا تقول. رواه البخاري
‘Abdullaah bin ‘Abbaas (Radhwiya Allaahu ‘anhu) amesema: ‘Umar (Radhwiya Allaahu ‘anhu) alikuwa akiniingiza katika mashauri pamoja na wazee waliopigana katika Vita vya Badr, basi kana kwamba mmoja wao alikasirika moyoni mwake, akauliza: Mbona huyu anaingia pamoja na sisi na wakati sisi tunao watoto kama yeye? ‘Umar akamwambia: Huyu ni kama mnavyomjua! Siku moja akaniita na kuniingiza pamoja nao. Sikuona siku hiyo kuwa ameniita ila ni kwa ajili ya kutaka kuwaonesha wao. Akawauliza: Mnasemaje kuhusu kauli ya Allaah “Pindi itakapokuja Nusura ya Allaah na ushindi?” Baadhi yao walisema: Tumeamriwa tumuhimidi Allaah na tumuombe maghfirah Allaah Atakapotunusuru na Kutupa ushindi. Baadhi yao walinyamaza wala hawakusema kitu. Akaniuliza: Nawe unasema hivyo hivyo ee Ibn ‘Abbaas? Nikamjibu: Hapana. Akasema: Unasemaje? Nikamwambia: Hayo ni mauti ya Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam), Allaah Alimjulisha Akamwambia: “Pindi itakapokuja Nusura ya Allaah na ushindi.” Hiyo ndiyo alama ya mauti yako, “Basi sabbih kwa Himidi za Rabb wako na muombe maghfirah; hakika Yeye daima ni Tawwaabaa (Mwingi mno wa kupokea tawbah).” [An-Naswr]
‘Umar (Radhwiya Allaahu ‘anhu) akasema: Hivyo ulivyosema ndivyo ninavyojua. [Al-Bukhaariy]
Hadiyth – 3
عن عائشة رضي الله عنها، قَالَتْ: مَا صلّى رَسُول الله صلى الله عليه وسلم صلاةً بَعْدَ أنْ نَزَلتْ عَلَيهِ: {إِذَا جَاءَ نَصْرُ اللهِ وَالْفَتْحُ} إلا يقول فِيهَا: ((سُبحَانَكَ رَبَّنَا وَبِحَمْدِكَ، اللَّهُمَّ اغْفِرْ لي)). مُتَّفَقٌ عَلَيه
وفي رواية في الصحيحين عنها: كَانَ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم يُكْثِرُ أنْ يقُولَ في ركُوعِه وسُجُودهِ: ((سُبْحَانَكَ اللَّهُمَّ رَبَّنَا وبِحَمدِكَ، اللَّهُمَّ اغْفِرْ لِي)).
وفي رواية لمسلم: كَانَ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم يُكثِرُ أنْ يَقُولَ قَبلَ أنْ يَمُوتَ: {إذا جَاءَ نَصْرُ اللهِ وَالْفَتْحُ} … إِلَى آخِرِ السورة.
وفي رواية لَهُ: كَانَ رسولُ الله صلى الله عليه وسلم يُكثِرُ مِنْ قَولِ: ((سبْحَانَ اللهِ وَبِحَمدِهِ أسْتَغفِرُ اللهَ وأتُوبُ إِلَيْهِ)). قَالَتْ: قُلْتُ: يَا رسولَ اللهِ، أَراكَ تُكثِرُ مِنْ قَولِ سُبحَانَ اللهِ وَبِحَمدهِ أسْتَغْفِرُ اللهَ وأتُوبُ إِلَيْه؟ فَقَالَ: ((أخبَرَني رَبِّي أنِّي سَأرَى عَلامَةً في أُمَّتي فإذا رَأيْتُها أكْثَرْتُ مِنْ قَولِ: سُبْحَانَ اللهِ وبِحَمدهِ أسْتَغْفرُ اللهَ وَأَتُوبُ إِلَيْه فَقَدْ رَأَيْتُهَا: {إِذَا جَاءَ نَصْرُ اللهِ وَالْفَتْحُ} فتح مكّة، {وَرَأَيْتَ النَّاسَ يَدْخُلُونَ فِي دِينِ اللهِ أَفْوَاجًا * فَسَبِّحْ بِحَمْدِ رَبِّكَ وَاسْتَغْفِرْهُ إِنَّهُ كَانَ تَوَّابًا}))
‘Aaishah (Radhwiya Allaahu ‘anhu) amesema: Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) hakuswali Swalaah yoyote baada ya kuteremka Suwrah hii “Pindi itakapokuja Nusura ya Allaah na ushindi.” Isipokuwa alikuwa akisema: “Kutakasika ni Kwako Rabb wetu, Ee Rabb nisamehe.” [Al-Bukhaariy na Muslim]
Riwaayah nyingine ya Swahiyh Al-Bukhaariy na Swahiyh Muslim; Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa akikithirisha kusema katika rukuu yake na sujuwd yake: “Kutakasika ni Kwako Rabb wetu, Ee Rabb nisamehe.”
Riwaayah nyingine ya Muslim imesema: Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa akikithirisha kusema kabla ya kuondoka kwake duniani. “Pindi itakapokuja Nusura ya Allaah na ushindi.” Mpaka mwisho wa Aayah. [An-Naswr]
Riwaayah nyingine tena ya Muslim imesema: Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa akikithirisha kusema: “Kutakasika ni kwa Allaah na shukurani zote ni Zake, namuomba Allaah msamaha na ninatubia Kwake.” Nikamuuliza Ee Rasuli wa Allaah, nakuona unakithirisha kusema: Kutakasika ni kwa Allaah na shukurani zote ni Zake, namuomba Allaah msamaha na ninatubia Kwake. Akajibu: Rabb wangu Ameniambiwa kuwa mimi nitaona alama katika Ummah wangu, nitakapoiona nikithirishe kusema: “Kutakasika ni kwa Allaah na shukurani zote ni Zake, namuomba Allaah msamaha na ninatubia Kwake.” Nami nimeshaiona: “Pindi itakapokuja Nusura ya Allaah na ushindi, na utawaona watu wanaingia katika Dini ya Allaah makundi makundi, basi sabbih kwa Himidi za Rabb (Mola) wako na muombe maghfirah; hakika Yeye daima ni Tawwaabaa (Mwingi mno wa kupokea tawbah).” [An-Naswr]
Hadiyth – 4
عن أنس رضي الله عنه قَالَ: إنَّ اللهَ عز وجل تَابَعَ الوَحيَ عَلَى رسولِ الله صلى الله عليه وسلم قَبلَ وَفَاتهِ حَتَّى تُوُفِّيَ أكْثَرَ مَا كَانَ الوَحْيَ عَلَيِّه. مُتَّفَقٌ عَلَيه
Anas (Radhwiya Allaahu ‘anhu) amesema: Allaah Alimteremshia Wahyi Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kwa wingi kabla ya kufariki kwake, alipofariki Wahyi ulikuwa umeshateremka mwingi.” [Al-Bukhaariy na Muslim]
Hadiyth – 5
عن جابر رضي الله عنه قَالَ: قَالَ رسول الله صلى الله عليه وسلم: ((يُبْعَثُ كُلُّ عَبْدٍ عَلَى مَا مَاتَ عَلَيهِ)). رواه مسلم
Jaabir (Radhwiya Allaahu ‘anhu) amesema: Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “Kila mja atafufuliwa katika hali aliyokufa nayo.” [Muslim]
0 Comments