باب التقوى
006 – Riyaadhw Asw-Swaalihiyn: Mlango Wa Taqwa – Kumkhofu Allaah

يَقُولُ اللهُ تَعَالَى:
يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اتَّقُوا اللَّـهَ حَقَّ تُقَاتِهِ وَلَا تَمُوتُنَّ إِلَّا وَأَنتُم مُّسْلِمُونَ
Enyi walioamini! Mcheni Allaah kama apasavyo kuogopwa na wala msife isipokuwa nyinyi (mmeshakuwa) ni Waislaam (wanaojisalimisha kwa Allaah). [Aal-‘Imraan: 102]
فَاتَّقُوا اللَّـهَ مَا اسْتَطَعْتُم
Basi mcheni Allaah muwezavyo. [At-Taghaabun: 16]

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اتَّقُوا اللَّـهَ وَقُولُوا قَوْلًا سَدِيدًا
Enyi walioamini! Mcheni Allaah na semeni kauli nyoofu ya haki. [Al-Ahzaab: 70]

وَمَن يَتَّقِ اللَّـهَ يَجْعَل لَّهُ مَخْرَجًا
Na yeyote anayemcha Allaah; Humjaalia njia ya kutoka (shidani).

وَيَرْزُقْهُ مِنْ حَيْثُ لَا يَحْتَسِبُ ۚ وَمَن يَتَوَكَّلْ عَلَى اللَّـهِ فَهُوَ حَسْبُهُ
Na Atamruzuku kutoka njia ambayo hatizamii. Na yeyote anayetawakali kwa Allaah, basi Yeye Humtosheleza. [At-Twalaaq: 2-3]

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا إِن تَتَّقُوا اللَّـهَ يَجْعَل لَّكُمْ فُرْقَانًا وَيُكَفِّرْ عَنكُمْ سَيِّئَاتِكُمْ وَيَغْفِرْ لَكُمْ ۗ وَاللَّـهُ ذُو الْفَضْلِ الْعَظِيمِ
Enyi walioamini! Mkimcha Allaah Atakupeni upambanuo wa haki na batili, na Atakufutieni maovu yenu, na Atakughufurieni. Na Allaah ni Mwenye fadhila adhimu. [Al-Anfaal: 29]

Hadiyth – 1

عن أبي هريرةَ رضي الله عنه قَالَ: قِيلَ: يَا رسولَ الله، مَنْ أكرمُ النَّاس؟ قَالَ: ((أَتْقَاهُمْ)). فقالوا: لَيْسَ عن هَذَا نسألُكَ، قَالَ: ((فَيُوسُفُ نَبِيُّ اللهِ ابنُ نَبِيِّ اللهِ ابنِ نَبيِّ اللهِ ابنِ خليلِ اللهِ)) قالوا: لَيْسَ عن هَذَا نسألُكَ، قَالَ: ((فَعَنْ مَعَادِنِ العَرَبِ تَسْأَلوني؟ خِيَارُهُمْ في الجَاهِليَّةِ خِيَارُهُمْ في الإِسْلامِ إِذَا فقُهُوا)). مُتَّفَقٌ عَلَيه
Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu ‘anhu) amesema: Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) aliulizwa: Yaa Rasula-Allaah, ni nani bora katika watu? Akajibu: “Ni yule aliyewazidi kwa kumcha Allaah.” Wakamwambia: Hatukuulizi kuhusu hili. Akawaambia: “Basi ni Yuwusuf Nabiy wa Allaah, Ibn Nabiy wa Allaah, ibn Nabiy wa Allaah, Ibn Khaliyl wa Allaah.” Wakasema: Hatukuulizi kuhusu hili. Akasema: “Mwaniuliza kuhusu koo za Waarabu? Wabora wao katika ujahiliyyah ndio wabora wao katika Uislamu iwapo watafahamu Dini.” [Al-Bukhaariy na Muslim]


Hadiyth -2

عن أبي سعيد الخدري رضي الله عنه عن النَّبيّ صلى الله عليه وسلم قَالَ: ((إنَّ الدُّنْيَا حُلْوَةٌ خَضِرةٌ، وإنَّ اللهَ مُسْتَخْلِفُكُمْ فِيهَا فَيَنْظُرَ كَيفَ تَعْمَلُونَ، فَاتَّقُوا الدُّنْيَا وَاتَّقُوا النِّسَاء؛ فإنَّ أَوَّلَ فِتْنَةِ بَنِي إسرائيلَ كَانَتْ في النِّسَاءِ)). رواه مسلم
Abuu Sa’iyd Al-Khudriy (Radhwiya Allaahu ‘anhu) amepokea kutoka kwa Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “Hakika dunia ni tamu rangi ya kijani, Hakika Allaah Amewatawalisha humo ili Awatazame mtakayotenda. Basi ogopeni dunia na waogopeni wanawake; hakika fitnah (mtihani) ya mwanzo kwa wana wa Israiyl ilikuwa ni katika wanawake.” [Muslim]


Hadiyth – 3
عن ابن مسعودٍ رضي الله عنه: أنَّ النَّبيّ صلى الله عليه وسلم كَانَ يقول: ((اللَّهُمَّ إنِّي أَسألُكَ الهُدَى، وَالتُّقَى، وَالعَفَافَ، وَالغِنَى)). رواه مسلم
‘Abdullaah bin Mas’uwd (Radhwiya Allaahu ‘anhu) amesimulia: Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa akiomba: “Ee Rabb, nakuomba uongofu na taqwa na kuepuka mabaya na ukwasi.” [Muslim]


Hadiyth – 4
عن أبي طريفٍ عدِيِّ بن حاتمٍ الطائيِّ رضي الله عنه، قَالَ: سمعتُ رسولَ الله صلى الله عليه وسلم يقول: ((مَنْ حَلَفَ عَلَى يَمِينٍ ثُمَّ رَأَى أتْقَى للهِ مِنْهَا فَليَأتِ التَّقْوَى)). رواه مسلم
Abuu Twariyf ‘Adiyyi bin Haatim At-Twaaiyy (Radhwiya Allaahu ‘anhu) amesema: Nilimsikia Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akisema: “Atakayeapa yamini kisha akaona linalomridhisha zaidi Allaah kulikoni aliloliapia, basi afanye linalomridhisha Allaah.” [Muslim]


Hadiyth – 5
عن أبي أُمَامَةَ صُدَيّ بنِ عجلانَ الباهِلِيِّ رضي الله عنه قَالَ: سَمِعتُ رسولَ الله صلى الله عليه وسلم يَخْطُبُ في حجةِ الوداعِ، فَقَالَ: ((اتَّقُوا الله وَصلُّوا خَمْسَكُمْ، وَصُومُوا شَهْرَكُمْ، وَأَدُّوا زَكاةَ أَمْوَالِكُمْ، وَأَطِيعُوا أُمَرَاءكُمْ تَدْخُلُوا جَنَّةَ رَبِّكُمْ)). رواه الترمذي، في آخر كتابِ الصلاةِ، وَقالَ: (حديث حسن صحيح)
Abuu Umaamah, Swudayy bin ‘Ajlaan Al-Baahiliyy (Radhwiya Allaahu ‘anhu) amesema: Nilimsikia Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akikhutubia katika Hajjatil-Widaa’i akasema: “Mcheni Allaaah, swalini Swalaah zenu tano, fungeni Swawm mwezi wenu, toeni Zakaah za mali yenu na watiini viongozi wenu, mtaingia Jannah ya Rabb wenu.” [At-Tirmidhiy, na amesema: Hadiyth hii ni Hasan Swahiyh]