باب الصدق
004 – Mlango Wa Ukweli
قَالَ الله تَعَالَى:
يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اتَّقُوا اللَّـهَ وَكُونُوا مَعَ الصَّادِقِينَ
Enyi walioamini! Mcheni Allaah na kuweni pamoja na wakweli. [At-Tawbah: 119]
وَالصَّادِقِينَ وَالصَّادِقَاتِ
Na wanaume wakweli na wanawake wakweli. [Al-Ahzaab: 33]
فَلَوْ صَدَقُوا اللَّـهَ لَكَانَ خَيْرًا لَّهُمْ
Basi kama wangekuwa wakweli kwa Allaah, bila shaka ingalikuwa kheri kwao. [Muhammad: 21]
Hadiyth – 1
عن ابن مسعود رضي الله عنه عن النَّبيّ صلى الله عليه وسلم، قَالَ: ((إنَّ الصِّدقَ يَهْدِي إِلَى البرِّ، وإنَّ البِرَّ يَهدِي إِلَى الجَنَّةِ، وإنَّ الرَّجُلَ لَيَصدُقُ حَتَّى يُكْتَبَ عِنْدَ اللهِ صِدِّيقًا. وَإِنَّ الكَذِبَ يَهْدِي إِلَى الفُجُورِ، وَإِنَّ الفُجُورَ يَهدِي إِلَى النَّارِ، وَإِنَّ الرَّجُلَ لَيَكْذِبُ حَتَّى يُكتَبَ عِنْدَ الله كَذَّابًا)). مُتَّفَقٌ عَلَيه
‘Abdullaah bin Mas’uwd (Radhwiya Allaahu ‘anhu) amepokea kutoka kwa Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kuwa amesema: “Hakika ukweli unaongoza katika wema, na hakika wema unaongoza Jannah na mtu ataendelea kusema ukweli mpaka aandikiwe mbele ya Allaah kuwa ni mkweli. Na hakika uongo unaongoza katika uovu, na hakika uovu unapeleka motoni, na mtu ataendelea kusema uongo mpaka aandikiwe mbele ya Allaah kuwa ni muongo,” [Al-Bukhaariy na Muslim]
Hadiyth – 2
عن أبي محمد الحسن بنِ عليِّ بن أبي طالب رضي الله عنهما قَالَ: حَفظْتُ مِنْ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم: ((دَعْ مَا يَرِيبُكَ إِلَى مَا لا يَرِيبُكَ؛ فإنَّ الصِّدقَ طُمَأنِينَةٌ، وَالكَذِبَ رِيبَةٌ)). رواه الترمذي، وَقالَ: ((حديث صحيح))
Abuu Muhammad, Al-Hasan bin ‘Alliy bin Abiy Twaalib (Radhwiya Allaahu ‘anhumaa) amesema: Nimehifadhi kutoka kwa Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) maneno haya: “Acha linalokutia shaka ufuate lisilokutia shaka; hakika ukweli ni utulivu na uongo ni mashaka.” [At-Tirmidhiy, na amesema Hadiyth hii ni Hasan]
Hadiyth – 3
عن أبي سفيانَ صَخرِ بنِ حربٍ رضي الله عنه في حديثه الطويلِ في قصةِ هِرَقْلَ، قَالَ هِرقلُ: فَمَاذَا يَأَمُرُكُمْ؟ يعني: النَّبيّ صلى الله عليه وسلم قَالَ أبو سفيانَ: قُلْتُ: يقولُ: ((اعْبُدُوا اللهَ وَحدَهُ لا تُشْرِكوُا بِهِ شَيئًا، وَاتْرُكُوا مَا يَقُولُ آبَاؤُكُمْ، ويَأْمُرُنَا بالصَلاةِ، وَالصِّدْقِ، والعَفَافِ، وَالصِّلَةِ)). مُتَّفَقٌ عَلَيه
Abuu Sufyaan, Swakhr bin Harb (Radhwiya Allaahu ‘anhu) amehadithia katika Hadiyth yake ndefu katika kisa cha Hiraqli (Heraclius). Hiraqli akauliza: Anawaamrisha nini? Yaani Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) nikasema: Anatuambia: “Muabuduni Allaah Mmoja Pekee wala msimshirikishe kwa chochote. Na muwache walivyokuwa wakiabudu baba zenu.” Na akituamuru kuswali, kusema kweli, kujiepusha na machafu na kuunga undugu.” [Al-Bukhaariy na Muslim]
Hadiyth – 4
عن أبي ثابت، وقيل: أبي سعيد، وقيل: أبي الوليد، سهل بن حُنَيْفٍ وَهُوَ بدريٌّ رضي الله عنه: أنَّ النَّبيّ صلى الله عليه وسلم قَالَ: ((مَنْ سَأَلَ الله تَعَالَى الشَّهَادَةَ بِصِدْقٍ بَلَّغَهُ اللهُ مَنَازِلَ الشُّهَدَاءِ وَإِنْ مَاتَ عَلَى فِرَاشِهِ)). رواه مسلم
Abuu Thaabit, na inasemekana: Abiy Sa’iyd, na inasemekana: Abil Waliyd, Sahl bin Hunayf (Radhwiya Allaahu ‘anhu) naye ni mpiganaji wa vita vya Badr amesimulia kuwa: Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “Atakayemuomba Allaah kufa kifo cha shaahid kwa ukweli, Allaah Atamfikisha daraja za Mashuhadaa hata akifa kitandani mwake.” [Muslim]
Hadiyth – 5
عن أبي هريرةَ رضي الله عنه قَالَ: قَالَ رَسُولُ الله صلى الله عليه وسلم: ((غَزَا نبيٌّ مِنَ الأنْبِياءِ صَلَوَاتُ اللهِ وَسَلاَمُهُ عَلَيْهمْ فَقَالَ لِقَومهِ: لاَ يَتْبَعَنِّي رَجُلٌ مَلَكَ بُضْعَ امْرَأةٍ وَهُوَ يُريدُ أنْ يَبْنِي بِهَا وَلَمَّا يَبْنِ بِهَا، وَلا أحَدٌ بَنَى بُيُوتًا لَمْ يَرْفَعْ سُقُوفَهَا، وَلا أحَدٌ اشْتَرَى غَنَمًا أَوْ خَلِفَاتٍ وَهُوَ يَنْتَظِرُ أَوْلادَها. فَغَزا فَدَنَا مِنَ القَرْيَةِ صَلاةَ العَصْرِ أَوْ قَريبًا مِنْ ذلِكَ، فَقَالَ لِلشَّمْسِ: إِنَّكِ مَأمُورَةٌ وَأنَا مَأمُورٌ، اللَّهُمَّ احْبِسْهَا عَلَيْنَا، فَحُبِسَتْ حَتَّى فَتَحَ اللهُ عَلَيهِ، فَجَمَعَ الغَنَائِمَ فَجَاءتْ- يعني النَّارَ- لِتَأكُلَهَا فَلَمْ تَطعَمْها، فَقَالَ: إنَّ فِيكُمْ غُلُولًا، فَلْيُبايعْنِي مِنْ كُلِّ قَبيلةٍ رَجُلٌ، فَلَزِقَتْ يد رجل بِيَدِهِ فَقَالَ: فِيكُمُ الغُلُولُ فلتبايعني قبيلتك، فلزقت يد رجلين أو ثلاثة بيده، فقال: فيكم الغلول، فَجَاؤُوا بِرَأْس مثل رأس بَقَرَةٍ مِنَ الذَّهَبِ، فَوَضَعَهَا فَجاءت النَّارُ فَأكَلَتْها. فَلَمْ تَحلَّ الغَنَائِمُ لأحَدٍ قَبْلَنَا، ثُمَّ أحَلَّ الله لَنَا الغَنَائِمَ لَمَّا رَأَى ضَعْفَنا وَعَجْزَنَا فَأحَلَّهَا لَنَا)). مُتَّفَقٌ عَلَيه
Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu ‘anhu) amesema: Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “Kuna Nabiy mmoja alitaka kwenda kupigana jihaad, akawaambia qaumu yake: “Yeyote aliyeoa na hajamleta mkewe kwake lakini ana niyyah ya kufanya hivyo au yule aliyejenga kuta za nyumba lakini hajati paa, au yule aliyenunua mbuzi au ngami wenye mimba anangojea wazae, basi anifuate kwa kujiunga katika jihaad.” Baada ya hapo akaanza kuelekea na mujaahidina wake katika mji aliokusudia. Alipofika hapo karibu na mji karibu na Swalaah ya Alasiri, aliliambia jua: “Hakika wewe unafuata amri za Allaah, name nimeamrishwa, Ee Rabb, lizuie kwa ajili yetu.” Likazuiliwa mpaka Allaah Alipompa ushindi. Akazikusanya ghanima, moto ukaja ili upate kuziteketeza, lakini haukuweza kuziteketeza. Akawaambia: “Hakika kati yenu kuna aliyefanya khiyana, kwa hiyo katika kila kabila anbai (afunge kiapo cha ahadi) mtu mmoja.” Mkono wa mtu mmoja ukanata katika mkono wake. Akawaambia: “Kwenu kuna khiyana, kwa hivyo kabila lako lote linibai” Mikono ya watu wawili au watatu ikanata kwenye mkono wake.” Akawaambia: “Kwenu kuna khiyana,” Wakaleta dhahabu mfano wa kichwa cha ng’ombe. Yule Nabiy akaiweka, moto ukaja na ukaiteketeza. Ghanima haikuhalalishwa kwa yoyote kabla yetu. Kisha Allaah Akatuhalalishia ghanima Alipoona udhaifu wetu na ajizi yetu (na kukosa hila), Akatuhalalishia.” [Al-Bukhaariy na Muslim]
Hadiyh – 6
عن أبي خالد حَكيمِ بنِ حزامٍ رضي الله عنه قَالَ: قَالَ رسولُ الله صلى الله عليه وسلم: ((البَيِّعَانِ بالخِيَار مَا لَمْ يَتَفَرَّقَا، فَإنْ صَدَقا وَبيَّنَا بُوركَ لَهُمَا في بيعِهمَا، وإنْ كَذَبَا وَكَتَمَا مُحِقَتْ بركَةُ بَيعِهِما)). مُتَّفَقٌ عَلَيهِ
Abuu Khaalid, Hakiym bin Hizaam (Radhwiya ALlaahu ‘anhu) amesema: Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amasema: “Wenye kuuziana wapo katika khiyari kabla hawajaachana. Watakaposema kweli na wakabainisha (kasoro au upungufu wa bidhaa), watabarikiwa katika biashara yao. Na wakificha na wakasema uongo; basi itaondolewa baraka ya biashara yao.” [Al-Bukhaariy na Muslim]
0 Comments