Du’aa Za Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam)

Kuomba Kutengenezewa Dini, Dunia Na Aakhirah,
Kuzidishiwa Kheri Katika Uhai, Kuepushwa Na Shari Za Mauti


  



اللَّهُمَّ أَصْلِحْ لِي دِينِي الَّذِي هُوَ عِصْمَةُ أَمْرِي، وَأَصْلِحْ لِي دُنْيَايَ الَّتِي فِيهَا مَعَاشِي، وَأَصْلِحْ لِي آخِرَتِي الَّتِي فِيهَا مَعَادِي، وَاجْعَلْ الْحَيَاةَ زِيَادَةً لِي فِي كُلِّ خَيْر، وَاجْعَلْ الْمَوْتَ رَاحَةً لِي مِنْ كُلِّ شَرٍّ

Allaahumma aswlih-liy diyni-lladhiy huwa ‘iswmatu amriy, wa aswlih-liy dunyaaya-llatiy fiyhaa ma’aashiy, wa aswlih-liy Aakhirati-llaty fiyhaa ma’aadiy, waj-’alil-hayaata ziyaadatan-lliy fiy kulli khayr, waj-’alil-mawta raahatan-lliy min kulli sharr.

Ee Allaah, nitengenezee Dini yangu ambayo ndio asasi ya mambo yangu, na nitengenezee dunia yangu ambayo humo ni maisha yangu, na nitengenezee Aakhirah yangu ambayo humo ni marejeo yangu, na Jaalia uhai wangu uwe wenye ziada ya kila kheri, na Jaalia mauti kwangu yawe ya raha kutokana na  kila shari

[Muslim]