Du’aa Za Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam)

Kuomba Kinga Ya Ufakiri, Uchahe, Udhalili
Na Kinga Ya Kudhulumu Au Kudhulumiwa



 اللَّهُمَّ إِنِّي أَعُوذُ بِكَ مِنْ الْفَقْرِ وَالْقِلَّةِ وَالذِّلَّةِ وَأَعُوذُ بِكَ مِنْ أَنْ أَظْلِمَ أَوْ أُظْلَمَ

Allaahumma inniy a’uwdhu bika minal-faqri wal-qillati, wadh-dhillati, wa a’uwdhu bika min an adhwlima aw udhwlama

Ee Allaah, hakika mimi najikinga Kwako ufakiri na uchache na udhalilifu na najikinga Kwako kudhulumu au kudhulumiwa

[Abuu Daawuwd, Ahmad – Swahiyh Abuu Daawuwd (1544)]