Du’aa Za Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam)
Kuomba Mapenzi Ya Allaah Na Mapenzi Ya Watakaokunufaisha Kwa Allaah



Du’aa kutafuta mapenzi ya Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa)


اللَّهُمَّ ارْزُقْنِي حُبَّكَ وَحُبَّ مَنْ يَنْفَعُنِي حُبُّهُ عِنْدَكَ اللَّهُمَّ مَا رَزَقْتَنِي مِمَّا أُحِبُّ فَاجْعَلْهُ قُوَّةً لِي فِيمَا تُحِبُّ اللَّهُمَّ مَا زَوَيْتَ عَنِّي مِمَّا أُحِبُّ فَاجْعَلْهُ فَرَاغًا لِي فِيمَا تُحِبُّ


Allaahummar-zuqniy hubbaka wa hubba man yanfa’aniy hubbuhu ‘indaka. Allaahumma maa razaqtaniy mimmaa uhibbu faj-’alhu quwwatal-lliy fiymaa tuhibbu. Allaahumma maa zawayta ‘anniy mimmaa uhibbu faj-’alhu faraaghal-lliy fiymaa Tuhibbu

Ee Allaah, niruzuku mapenzi Yako, na mapenzi ya atakayeninufaisha mapenzi yake Kwako. Ee Allaah Uliyoniruzuku kati ya niyapendayo, basi yajaalie yawe ni nguvu kwangu kwa Uyapendayo. Ee Allaah, Uliyoniondoshea kati ya niyapendayo, basi yajaalie kuwa ni wasa’aa kwangu katika Uyapendayo

[At-Tirmidhiy  (5/523 ) na ameipa daraja ya Hasan]