Du’aa Za Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam)
Kuomba Mema Kuacha Maovu Kuwapenda Maskini, Mapenzi Ya Allaah
Du’aa hii inajumuisha pia kuomba kuwapenda masikini, kuacha maovu, kuomba maghfirah na Rahmah, kuomba mauti inapotokea fitnah katika Dini. Du’aa hii amesema Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ((Hakika hii ni haki basi jifunzeni kisha muifunze))
اللَّهُمَّ إِنِّي أَسْأَلُكَ فِعْلَ الْخَيْرَاتِ وَتَرْكَ الْمُنْكَرَاتِ وَحُبَّ الْمَسَاكِينِ وَأَنْ تَغْفِرَ لِي وَتَرْحَمَنِي وَإِذَا أَرَدْتَ فِتْنَةَ قَوْمٍ فَتَوَفَّنِي غَيْرَ مَفْتُونٍ أَسْأَلُكَ حُبَّكَ وَحُبَّ مَنْ يُحِبُّكَ وَحُبَّ عَمَلٍ يُقَرِّبُنِي إِلَى حُبِّكَ
Allaahumma inniy as-aluka fi’-lal khayraati wa tarakal-munkaraati, wa hubbal masaakiyni, wa antaghfiraliy wa tarhamniy waidhaa aradta fitnata qawmin fatawaffiny ghayra maftuwnin. As-aluka hubbaka, wa hubba man yyuhibbuka, wahubba ‘amaliyy yuqarribuniy ilaa hubbika
Ee Allah, hakika mimi nakuomba kutenda mema, na kuacha maovu na kuwapenda masikini, na Unighufurie na Unirehemu, na Unapowatakia watu fitnah, basi nifishe bila ya kufitinishwa. Nakuomba mapenzi Yako, na mapenzi ya anayekupenda, na mapenzi yatakayonikaribisha katika mapenzi Yako.
[At-Tirmidhiy, Ahmad - Hadiyth Hasan]
0 Comments