Du’aa Za Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam)
Kuomba Kukunjuliwa Baraka, Rahmah, Fadhila, Rizki, Neema Ya Kudumu...
038- Ee Allaah, Himdi ni Zako zote, Ee Allaah, hakuna mwenye kuzuia…
اللَّهُمَّ لَكَ الْحَمْدُ كُلُّهُ . اللَّهُمَّ لاَ قَابِضَ لِمَا بَسَطْتَ ، وَلاَ بَاسِطَ لِمَا قَبَضْتَ ، وَلاَ هَادِيَ لِمَا أَضْلَلْتَ، وَلاَ مُضِلَّ لِمَنْ هَدَيْتَ ، وَلاَ مُعْطِيَ لِمَا مَنَعْتَ ، وَلاَ مَانِعَ لِمَا أَعْطَيْتَ، وَلاَ مُقَرِّبَ لِمَا بَاعَدْتَ، وَلاَ مُبَاعِدَ لِمَا قَرَّبْتَ. اللَّهُمَّ ابْسُطْ عَلَيْنَا مِنْ بَرَكَاتِكَ ، وَرَحْمَتِكَ، وَفَضْلِكَ، وَرِزْقِكَ.اللَّهُمَّ إِنِّي أَسْأَلُكَ النَّعِيمَ الْمُقِيمَ الَّذِي لاَ يَحُولُ وَلاَيَزُولُ. اللَّهُمَّ إِنِّي أَسْأَلُكَ النَّعِيمَ يَوْمَ الْعَيْلَةِ وَالأَمْنَ يَوْمَ الْخَوْفِ. اللَّهُمَّ إِنِّي عَائِذٌ بِكَ مِنْ شَرِّ مَا أَعْطَيْتَنَا، وَشَرِّ مَا مَنَعْتَ. اللَّهُمَّ حَبِّبْ إِلَيْنَا الإِيمَانَ وَزَيِّنْهُ فِي قُلُوبِنَا وَكَرِّهْ إِلَيْنَا الْكُفْرَ وَالْفُسُوقَ وَالْعِصْيَانَ وَاجْعَلْنَا مِنَ الرَّاشِدِينَ. اللَّهُمَّ تَوَفَّنَا مُسْلِمِينَ وَأَحْيِنَا مُسْلِمِينَ وَأَلْحِقْنَا بِالصَّالِحِينَ غَيْرَ خَزَايَا وَلاَ مَفْتُونِينَ. اللَّهُمَّ قَاتِلْ الْكَفَرَةَ الَّذِينَ يُكَذِّبُونَ رُسُلَكَ وَيَصُدُّونَ عَنْ سَبِيلِكَ، وَاجْعَلْ عَلَيْهِمْ رِجْزَكَ وَعَذَابَكَ. اللَّهُمَّ قَاتِلْ الْكَفَرَةَ الَّذِينَ أُوتُوا الْكِتَابَ إِلَهَ الْحَقِّ.
Allaahumma lakal-Hamdu kulluhu. Allaahumma laa qaabidhwa limaa basattwa, walaa baaswitwa limaa qabadhwta, walaa haadiya limaa adhw-lalta, walaa mudhwilla liman hadayta, walaa mu’-twiya limaa mana’-ta, walaa maani’a limaa a’-twayta, walaa muqarriba limaa baa’adta, walaa mubaa’idaa limaa qarrabta. Allaahumma absitw ‘alaynaa min Barakaatika, wa Rahmatika, wa fadhwlika, wa rizqika. Allaahumma inniy as-alukan-nna’iymal-muqiyma alladhiy laa yahuwlu walaa yazuwlu. Allaahumma inniy as-alukan-na’iyma yawmal-‘aylati wal amna yawmal-khawfi. Allaahumma inniy ‘aaidhum bika min sharri maa a’-twaytanaa, wa sharri maa mana’-ta. Allaahumma habbib ilaynaal-iymaana wa zayyanahu fiy quluwbina wa karrih ilaynal-kufra wal fusuwqa wal ‘iswyaana waj-‘alnaa minar-raashidiyna. Allaahumma tawaffanaa Muslimiyna wa ahyinaa Muslimiyna wa alhiqnaa bisw-Swaalihiyna ghayra khazaaya walaa maftuwniyna. Allaahumma qaatilil-kafarata alladhiyna yukadh-dhibuwna Rusulaka wa yaswudduwna ‘an Sabiylika, waj-’al ‘alayhim rijzika wa ‘adhaabika. Allaahumma qaatilil-kafarata alladhiyna uwtul-Kitaaba Ilaahal-haqq
Ee Allaah, Himdi ni Zako zote. Ee Allaah, hakuna mwenye kuzuia Ulivyovikunjua, wala mwenye kukunjua Ulivyozuia, wala mwenye kumhidi Uliyempotoa, wala kumpotoa Uliyemhidi, wala mwenye kutoa Ulichonyima, wala mwenye kunyima Ulichoruzuku, wala mwenye kukurubisha Ulichoweka mbali, wala mwenye kuweka mbali Ulichokiweka karibu. Ee Allaah tukunjulie katika baraka Zako, na Rahmah Zako, na fadhila Zako, na rizki Yako. Ee Allaah hakika mimi nakuomba neema ya kudumu isiyobadilika wala kutoweka. Ee Allaah, hakika mimi nakuomba neema siku ya shida na ufukara, na amani Siku ya khofu. Ee Allaah, hakika mimi najikinga Kwako shari Ulizotupa, na Ulizozizuwia. Ee Allaah, Pendezesha kwetu iymaan na ipambe katika nyoyo zetu, na chukiza kwetu kufru, ufasiki, uasi na tujaalie miongoni mwa waongofu. Ee Allaah, tufishe tukiwa Waislamu na tuhuishe tukiwa Waislamu na tukutanishe na waja wema bila hizaya wala kutahiniwa. Ee Allaah Wapige vita makafiri wanaokanusha Rusuli Wako na wanaozuia njia Yako, na wajaalie juu yao maangamizi Yako na adhabu Zako. Ee Allaah, Wapige vita makafiri waliopewa Kitabu. Ee Mwabudiwa wa haki [Aamiyn]
[Ahmad, na ameitoa Al-Bukhaariy katika Adaabul-Mufrad (699) na Al-Albaaniy ameipa daraja ya Swahiyh katika Takhriyj Fiqhus-Siyrah (348), Swahiyh Adaabul-Mufrad lil-Bukhaariy (538/259), na Majma’u Az-Zawaaid (6/124)].
0 Comments