Du’aa Za Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam)

Kuomba Uhai Au Mauti Yakiwa Na Khayr,
Kumkhofu Allaah Kwa  Siri Na Dhahiri...

 026-Ee Allaah naomba kwa ujuzi Wako wa ghaibu na uwezo…


اللَّهُمَّ بِعِلْمِكَ الْغَيْبَ وَقُدْرَتِكَ عَلَى الْخَلْقِ أحْيِنِي مَا عَلِمْتَ الْحَيَاةَ خَيْرًا لِي، وَتَوَفَّنِي إِذَا عَلِمْتَ الْوَفَاةَ خَيْرًا ‏‏ لِي، ‏‏ اللَّهُمَّ إِنِّي أسْأَلُكَ خَشْيَتَكَ فِي الْغَيْبِ وَالشَّهَادَةِ، وَأسْأَلُكَ كَلِمَةَ الْحَقِّ فِي الرِّضَا وَالْغَضَبِ، وَأسْأَلُكَ ‏الْقَصْدَ‏ ‏فِي الْغِنَى وَالْفَقْرِ، وَأسْألُكَ نَعِيمًا لا‏ ‏يَنْفَدُ،‏ ‏وَأسْألُكَ قُرَّةَ عَيْنٍ لا تَنْقَطِعُ وَأسْألُكَ الرِّضَاءَ بَعْدَ الْقَضَاءِ، وَأسْألُكَ بَرْدَ الْعَيْشِ بَعْدَ الْمَوْتِ وَأسْألُكَ لَذَّةَ النَّظَرِ ِإِلَى وَجْهِكَ وَالشَّوْقَ إِلَى لِقَائِكَ فِي غَيْرِ ضَرَّاءَ مُضِرَّةٍ وَلا فِتْنَةٍ مُضِلَّةٍ، اللَّهُمَّ ‏‏زَيِّنَّا بِزِينَةِ الإِيمَانِ وَاجْعَلْنَا هُدَاةً مُهْتَدِينَ

Allaahumma bi‘ilmikal-ghayba wa qudratika ‘alal-khalqi, ahyiniy maa ‘alimtal-hayaata khayral-liy, wa tawaffaniy idhaa ‘alimtal-wafaata khayral-liy. Allaahumma inniy as-aluka khash-yataka fil-ghaybi wash-shahaadah, wa as-aluka kalimatal-haqqi fir-ridhwaa wal-ghadhwabi, wa as-alukal-qaswda fil-ghinaa wal-faqri, wa as-aluka na’iyman-llaa yanfadu, wa as-aluka qurrata ‘aynin-llaa tanqatwi’u, wa as-alukar-ridhwaa ba’-dal-qadhwaai, wa as-aluka bardal-‘ayshi ba’-dal-mawti,  wa as-aluka laddhatan-nadhwari ilaa Wajhika, wash-shawqa ilaa liqaaika fiy ghayri dhwarraai mudhwirratin walaa fitnatin mudhwillatin. Allaahumma zayyinaa biziynatil-iymaani waj-’alnaa hudaatan muhtadiyna.

Ee Allaah naomba kwa ujuzi Wako wa ghaibu na uwezo Wako juu viumbe, nihuishe ikiwa Unajua uhai ni khayr kwangu, na nifishe ikiwa Unajua kufa ni khayr kwangu. Ee Allaah, nakuomba khofu Yako katika siri na dhahiri, na nakuomba Unifanye mkweli katika kauli wakati wa furaha na ghadhabu, na nakuomba unifanye wastani wakati wa utajiri na umasikini, na nakuomba neema isiyokoma, na kitulizo cha macho kisichokatika, na nakuomba niridhike Uliyonikidhia na nakuomba maisha mepesi baada ya mauti, na nakuomba ladha ya kuutazama Wajihi Wako na shauku ya kukutana Nawe, pasi na madhara yanayodhuru au fitna itakayosababisha upotofu. Ee Allaah, tupambie kwa pambo la iymaan na tujaalie wenye kuongoza na kuongoka.

[Swahiyh Sunan An-Nasaaiy (1/280/281), Ahmad (4/364) kwa isnaad nzuri]