Du’aa Za Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam)

Kuomba Kheri, Kuomba Kinga Za Shari, Kheri Alizoziomba Nabiy Na Shari Alizojikinga Nazo Nabiy, Kuomba Yanayokaribisha Jannah Na Kujikinga Na Yanayokaribisha Na Moto




  ‏ اللَّهُمَّ إِني أسْأَلُكَ مِنْ الْخَيْرِ كُلِّهِ عَاجِلِهِ وَآجِلِهِ مَا عَلِمْتُ مِنْهُ وَمَا لَمْ أعْلَمْ، وَأعُوذُ بِكَ مِنَ الشَّرِّ كُلِّهِ عَاجِلِهِ وَآجِلِهِ مَا عَلِمْتُ مِنْهُ وَمَا لَمْ ‏‏ أعْلَمْ،  اللَّهُمَّ إِنِّي أسْأَلُكَ مِنْ خَيْرِ مَا سَألَكَ عَبْدُكَ وَنَبِيُّكَ، وَأعُوذُ بِكَ مِنْ شَرِّ مَا استعَاذَ  بِكَ مَنْهُ عَبْدُكَ وَنَبِيُّكَ، اللَّهُمَّ إنِّي أسْأَلُكَ الْجَنَّةَ وَمَا قَرَّبَ إلَيْهَا مِنْ قَوْلٍ أوْ عَمَلٍ وَأعُوذُ بِكَ مِنْ النَّارِ وَمَا قَرَّبَ إِلَيْهَا مِنْ قَوْلٍ أوْ عَمَلٍ، وَأسْأَلُكَ أنْ تَجْعَلَ كُلَّ قَضَاءٍ قَضَيْتَهُ لِي خَيْرًا

Allaahumma inniy as-aluka minal-khayri kullihi ‘aajilihi wa aajilihi, maa ‘alimtu minhu wamaa lam a’lam. Wa a’uwdhu Bika min sharri kullihi ‘aajilihi wa aajilihi maa ‘alimtu minhu wamaa lam a’lam. Allaahumma inniy as-aluka min khayri maa saalaka ‘Abduka wa Nabiyyuka, wa a’uwdhu Bika min sharri masta’aadha Bika minhu ‘Abduka wa Nabiyyuka. Allaahumma inniy as-alukal-Jannata wamaa qarraba ilayhaa min qawlin aw ‘amal, wa a’uwdhu Bika minan-nnaari wamaa qarraba ilayhaa min qawlin aw ‘amal, wa as-aluka antaj-’ala kulla qadhwaai qadhwaytahu liy khayraa

Ee Allaah, hakika mimi nakuomba kheri zote zilizokaribu na mbali nizijuazo na nisizozijua. Najikinga Kwako shari zote za karibu na za mbali nizijuazo na nisizozijua. Ee Allaah, hakika nakuomba kheri alizokuomba mja Wako na Nabiy Wako, na najikinga Kwako shari alizojikinga nazo mja Wako na Nabiy wako. Ee Allaah, hakiki mimi nakuomba Jannah na yanayokaribisha kwayo katika kauli au amali, na najikinga Kwako Moto na yanayokaribisha kwayo katika kauli au amali, na nakuomba Ujaalie kila majaaliwa yangu [uliyonikidhia] yawe kheri

[Ibn Maajah – Ametaja katika mlango aliosimulia Hadiyth kwa anuani ya ‘Du’aa za  ‘Jawaami’ul-Kalimi’]