Du’aa Za Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam)

 Sayyid Al-Istighfaar  Du'aa Kubwa Kabisa Ya Kuomba Maghfirah Kuliko Zote



 اللّهـمَّ أَنْتَ رَبِّـي لا إلهَ إلاّ أَنْتَ، خَلَقْتَنـي وَأَنا عَبْـدُك، وَأَنا عَلـى عَهْـدِكَ وَوَعْـدِكَ ما اسْتَـطَعْـت، أَعـوذُبِكَ مِنْ شَـرِّ ما صَنَـعْت، أَبـوءُ لَـكَ بِنِعْـمَتِـكَ عَلَـيَّ وَأَبـوءُ بِذَنْـبي فَاغْفـِرْ لي فَإِنَّـهُ لا يَغْـفِرُ الذُّنـوبَ إِلاّ أَنْتَ

Allaahumma Rabbiy laa ilaaha illa Anta Khalaqtaniy wa-ana ‘abduka wa-anaa ‘alaa ‘ahdika wawa’dika mastatwa’tu, a’uwdhu bika minsharri maa swana’tu, abuu laka bini’matika ‘alayya waabuu bidhambiy, faghfirliy fainnahu laa yaghfirudh dhunuwba illaa Anta

Ee Allaah, Wewe ni Rabb wangu, hapana Muabudiwa wa haki ila Wewe, umeniumba nami ni mja Wako, nami niko juu ya  ahadi Yako, na agano Lako, kiasi cha uwezo wangu, najikinga Kwako dhidi ya shari ya nilichokifanya, nakiri  Kwako kwa kunineemesha, na nakiri kwa madhambi yangu, basi nakuomba unighufurie kwani hakuna anayeghufuria  madhambi ila Wewe  [Al-Bukhaariy, Abu Daawuwd, At-Tirmidhiy, An-Nasaaiy, Ibn Maajah, Ahmad - Sayyidul-Istighfaar - Du’aa kuu ya kuomba Maghfirah. Atakayesema jioni akafariki ataingia Jannah, atakayesema asubuhi akafariki ataingia Jannah.