Du'aa Za  Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam)

Utangulizi




Zifuatazo ni du’aa zilothibiti kutoka kwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam). Ni busara kushikilia kusoma du’aa za Sunnah na kuacha nyinginezo zisizothibiti, kwani hizi za Sunnah ni nyingi mno zinazomtosheleza Muislamu kupata manufaa ya dunia na Aakhirah yake. Aghlabu ya du’aa za Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam)  zilikuwa ni za mukhtasari lakini ni zenye hikma na maana nzito. Amesema katika usimulizi ufuatao:

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ (رضي الله عنه)  أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ (صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ)  قَالَ:  ((فُضِّلْتُ عَلَى الأَنْبِيَاءِ بِسِتٍّ:  أُعْطِيتُ جَوَامِعَ الْكَلِمِ، وَنُصِرْتُ بِالرُّعْبِ، وَأُحِلَّتْ لِيَ الْغَنَائِمُ، وَجُعِلَتْ لِيَ الأَرْضُ طَهُورًا وَمَسْجِدًا، وَأُرْسِلْتُ إِلَى الْخَلْقِ كَافَّةً، وَخُتِمَ بِيَ النَّبِيُّونَ))
Imepokewa kutoka kwa Abu Huraryah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam)  amesema: ((Nimefadhilishwa juu ya Manabii kwa mambo sita; nimepewa ‘Jawaami’al-Kalimi’  na nimenusuriwa kwa [kutiwa] hofu [katika nyoyo za maadui] na nimehalalishiwa ghanima  na nimefanyiwa ardhi kuwa kitoharishi na masjid [mahali pa kuswali], na nimetumwa kwa viumbe wote, na Manabii wamekhitimishwa kwangu))[Muslim]

‘Jawaami’al-Kalimi’: Mjumuisho wa maana nyingi katika maneno machache

Ghanima:  Mali inayopatikana baada ya kupigana katika vita.