Bibi Karlas Evans ni mmarekeni pia ni msomi mwenye macho ya blue na
nywele za blond, ambaye alikuwa mkirsto aliacha dini yake na kuifuata
dini hii ya haki dini ya Kiislamu ambapo watu wengi wasio Waislamu
wanaituhumu kuwa ni dini ambayo inamdhalilisha mwanamke.
Tumuache
Karlas azungumzie mwenyewe. Anaanza kwa kuelezea kwa kutoridhika kwake
kwa nadharia ya kwamba `Jesus as a God` (Yaani yesu ni Mungu). Na jinsi
gani alivyogundua ukweli wa mwanamke wa kiislam ambao ndio uliomfanya
kufuata dini ya Kiislamu.
Anaanza kwa kusema kuwa mpangilio wangu wa
kutoka katika ukristo na kuingia katika Uislamu, ulichukuwa muda mrefu
sana zaidi ya miaka 20. Ulianza tokea nina umri wa miaka 12. Nilikuwa
nikisoma katika Private school (shule ya kulipia). Tulikuwa
tukifundishwa masoma ya dini tofauti. Na nilikuwa na vitabu vya dini
tofauti, kama vile vitabu vya dini ya kikristo, kitabu kimoja cha dini
ya kiyahudi, kitabu kimoja cha Quran (dini ya Kiislamu), kitabu cha dini
ya kihindu na Kibudha.
Anasema ninakumbuka jinsi nilivyo vutiwa na
kitabu cha dini ya Kiislamu (Quran) na nikaelewa kwamba, Waislamu
hawakuwa wanafki kama wakristo (anamaanisha ameelewa hayo baada ya
kusoma vitabu vya dini zote).
Nilikumbuka mambo mawili ambayo
yamenivutia katika Quran. Jambo la kwanza ni kumuabudu Mwenyeezi Mungu
mmoja pekee. Daima Nilikuwa nina jiuliza Kwanini wakristu wanaamini
kwamba jesus (yanni Nabii Issa) ni mungu na jinsi gani wanakwenda
kinyume na maarisho ya Mwenyeezi Mungu. Jambo la pili ni Kuhusiana na
swala, si kwa sababu uislamu au wauslamu wana swali swala tano kwa siku
lakini kwa jinsi yawafuasi wengi wa dini ya kislamu wanavyoswali na
kumuabudu Mwenyezi Mungu mmoja pekee. Katika Ukiristo au dini ya
kikristo swala ni kama kutaka kitu kwa Mwenyeezi Mungu, Kwa Kusema Mungu
nipe hiki na kile basi si kufanya ibada kama katika Uislamu.
Anaedelea
Karlas kwa kuelezea, nilikwenda kusoma katika college mjini Washington
DC, ambapo huko kuna idadi kubwa ya wafuasi wa dini ya Kiislamu. Mvuto
wangu kwa dini ya Kiislamu ulikuwa bado uko palepele lakini nilikuwa
ninaona aibu kumwambia mtu yoyote nchini Marekani. Nilikuwa nikienda
msikitini, katika vituo vya Kiislamu (Islamic center) lakini niliona
aibu kuingia ndani. Nilikuwa nikiona darasa za dini na watu wanaoupenda
Uislamu lakini nilishindwa kufanya kama wao, mwisho nikaamua kununua
Quran na kuisoma mwenyewe nyumbani. Nilishangazwa sana, kila nilicho
kisoma katika Quran nilihisi kinaniingia katika moyo wangu. Na jambo
kubwa la kushangaza ni kuona jinsi mwanamke katika Uislamu alivyo pewa
haki na usawa. Nafikiri watu wengi watanicheka lakini kwa mtu ambaye
amesoma Biblia atajuwa kuwa katika Quran kuna haki mwanamke ambazo
amepewa ambazo katika biblia hakupewa. Katika Quran mwanamke anahaki ya
kumkataa mwanamume katika ndoa au kumkubali kuolewa nae. Wakati katika
ukristo hasa katika utamaduni wa Magharibi katika wakati wa miaka ya
nyuma (600CE), wanawake waliangaliwa kuwa ni mali ya mzee (baba yake).
Baba yake ndio anahaki ya kuamua kumuozesha mtoto wake wa kike, na
kuhusiana na urithi alikuwa hapati ila mtoto wa kiume mkubwa, haki hii
haikuwepo nchini Marekani ila katika karne ya 19 (akimaanisha Uislamu
ulisha fundisha hayo tokea zaidi ya miaka 1400 iliyo pita.)
Siku moja
nilipokuwa nikitazama T.V. niliona kipindi kinahusiana na (الدعوة)
ulinganiaji. kipindi hiki kilikuwa kinaonyesha jinsi mwanamke wa
kimagharibi anavyolinganiwa katika Uislamu kwa njia yeyote ile. Nilikuwa
nikikifuatilia sana kipindi hiki, na siku ambayo sikuwepo nyumbani
nilikuwa nikikirikodi. Kipindi hiki kilikuwa kikiletwa kila siku ya
ijumaa, lakini sikumbuki kilikuwa kikiletwa na chanel gani? Daima
kipindi hiki kilianza kwa kusema BismiLahi Rahmaani Raheem (kwa jina la
Mwenyeezi Mungu mwingi wa rehema na mwingi wa ukarimu). Na mwisho kabla
ya kumalizika kipindi alikuwa akionyeshwa huyo mtu aliyelinganiwa
akitamka shahada (akisilimu). Na mimi nikaitamka shahada kama ilivyokuwa
ikionyeshwa katika T.V. Ni kasema katika nafsi yangu kwa uwezo wa Allah
hivi mimi nimeshakuwa Muislamu kwa kuigiza kuitamka shahada!
nikajisemea katika nafsi yangu sijui! kwa bahati mbaya nilikuwa simjui Muislamu yoyote ili anielezee kuhusu Uislamu na nilikuwa ninaogopa kwa
familia yangu na marafiki zangu wasijue kuwa mimi nimekuwa au ninataka
kuwa Muislamu.
Mnamo mwaka 1990 au 1991 ubalozi wa Saudi Arabia
ulifanya maonyesho ya Kiislamu ya kuandika na kuchora. Nilimuuliza mmoja
kati ya watu waliokuwepo katika maonyesho ili anieleze kuhusu Uislamu.
Akanijibu mtu huyo kuwa hana nafasi ya kunieleza chochote kutokana na
msongamano wa watu, kwa hivyo sikujua niende wapi ili nipate mtu
anieleze zaidi kuhusu Uislamu. Na kujibu maswali yangu kwani niliona
aibu kwenda msikitini pia sikujua kama mwanamke anaruhusiwa kuingia
msikitini na nivae vipi ili niweze kuingia msikitini au nitakuwa ni mimi
peke yangu ambaye sijui kuongea kiarabu.
Basi nikawa naendelea
kuisoma Quran na kumuomba Mwenyeezi Mungu Mtukufu na nikaaamini kuwa
Mwenyeezi Mungu atanikubalia dua yangu.
Shauku yangu kwa kumtegemea
Mwenyeezi Mungu haikuisha japokuwa niliamua kufuata dini ya ukristo.
Lakini tatizo ni kwamba daima nilikuwa ninajiuliza kuhusu dini hii ya
Kikristo. Hasa kuhusiana na utatu na utakatifu wa Yesu na kuwa yeye ni
Mungu. Jambo ambalo nilikuwa ninahisi si la uhakika.
Ninakumbuka siku
moja tulipokuwa kanisani tunajifundisha darasa la biblia nilimuuliza
askofu kuhusu shaka yangu kuhusu Yesu kuwa ni Mungu na pia niliwauliza
mapadri tofauti lakini wote walinijibu unatakiwa kuamini tu, na mpaka
hapa nilikuwa sijasilimu lakini nilikuwa ninaamini kuwa Mwenyeezi Mungu
ni mmoja na Mtume Mohammad (swala llahu alayhi wasalam) ni Mtume wa
mwenyeezi Mungu.
Wakati nilipokuwa shuleni, nilikutana na wanafunzi
wawili ambao ni ndugu walikuwa ni Waislamu. Nilizungumza nao lakini kwa
bahati mbaya hawakujuwa kuwa mimi nilikuwa ninataka kusilimu. Kukutana
nao kwao hakukuleta faida yoyote ile. Nilijihisi katika nafsi yangu kuwa
mimi ni mfuasi wa dini zote, kwani nimesoma vitabu vya dini zote.
nilivutiwa kidogo na dini ya kiyahudi kwani nilihisi inafanana na dini
ya Kiislamu kidogo.
Baada ya miaka miwili nilijiunga na kampuni ya
sasa. Katika kampuni hiyo kulikuwa na kijana mmoja tulikuwa tukifanya
kazi pamoja. Mvulana huyu alikuwa muislamu lakini alikuwa analewa wala
haswali na nilikuwa daima ninamuuliza kwa nini hufuati maamrisho ya
dini? alikuwa hanijibu kitu. baada ya mwaka toka kuanza kufanya kazi
nikamueleza kuhusu haja yangu ya kutaka kuwa muislamu.
Siku moja
tukaenda katika kituo cha Kiislamu cha kitaifa. Kulikuwa hakuna mtu anayehusika na maswala ya uongozi ila
mtu mmoja ambaye alituambia subirini hapo baada ya muda atakuja imaam
kuswalisha swala ya isha. Lakini nikahisi uzito nikaondoka. Baada ya
wiki nne nikajaribu tena kwenda kwa mara hii nikaitamka shahada mbele ya
Imaam na kuwa muislamu. Na tokea hapo nikajifundisha kuswali jambo
ambalo nilikuwa nishajifundisha kabla ya kusilimu kwangu, kwa kupitia
internet na video, pia nikajaribu kujifundisha lugha ya kiarabu kwani
nilitamani siku moja kujuwa kuisoma Quran kwa lugha ya Kiarabu. Lakini
nilishangazwa kwa muda mfupi niliweza kujuwa kuisoma Quran ingawa
lafidhu yangu si nzuri.
Tarehe 8 October 2001 ni siku nzuri kuliko
zote katika maisha yangu kwani ndio siku ambayo niliamua kuvaa hijabu
kwa mara ya kwanza. Watu wengi kazini waliniuliza je umesilimu?
nikawajibu ndio na wengi walishangaa kwa msichana wa kimarekani ambaye
ni msomi mwenye nywele za blond na macho ya bluu kusilimu. Waliniambia
kuwa mwanamke wa Kiislamu anadhalilishwa nikawajibu kuwa Quran imempa
haki mwanamke wa Kiislamu kuliko Biblia na hili ni miongoni mwa jambo
muhimu ambalo limenifanya kuingia katika Uislamu.
Na mwisho nasema
kwamba ninaamini kuwa hapana Mola apaswae kuabudiwa kwa haki ispokuwa
Mwenyeezi Mungu Mtukufu na Mtume Muhammad (swala llahu alayhi wasalam)
ni Mjumbe wa Mwenyeezi Mungu.
Makala hii kwa Ihsani ya Tovuti ya Jamii Islam


0 Comments