Hadiyth Al-Qudsiy
Hadiyth Ya 4

Binaadamu Amenikadhibisha Na Amenitukana

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ عَنْ النَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ ((قَالَ اللَّهُ كَذَّبَنِي ابْنُ آدَمَ وَلَمْ يَكُنْ لَهُ ذَلِكَ ،وَشَتَمَنِي وَلَمْ يَكُنْ لَهُ ذَلِكَ ، فَأَمَّا تَكْذِيبُهُ إِيَّايَ ، فَقَوْلُهُ لَنْ يُعِيدَنِي كَمَا بَدَأَنِي وَلَيْسَ أَوَّلُ الْخَلْقِ بِأَهْوَنَ عَلَيَّ مِنْ إِعَادَتِه ،ِ وَأَمَّا شَتْمُهُ إِيَّايَ فَقَوْلُهُ اتَّخَذَ اللَّهُ وَلَدًا وَأَنَا الْأَحَدُ الصَّمَدُ لَمْ أَلِدْ وَلَمْ أُولَدْ وَلَمْ يَكُنْ لِي كُفْئًا أَحَدٌ))البخاري والنسائ
Kutoka kwa Abu Hurayrah (Radhwiya Allaahu ‘anhu) kwamba Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam)  amesema((Allaah Amesema: Binaadamu amenikadhibisha na hana haki ya kufanya hivyo, na amenitukana na hana haki ya kufanya hivyo. Ama kunikana kwake ni kusema: Hatonirejesha (tena) kama Alivyoniumba (Hatonifufua kama vile Alivyoniumba). Na kuumba hakukuwa rahisi Kwangu kuliko kumfufua. Ama kunitukana kwake ni kule kusema: Allaah Ana mtoto wakati Mimi ni Ahad (Mmoja Pekee)Asw-Swamad (Aliyekamilika sifa za utukufu Wake, Mkusudiwa haja zote), Sikuzaa wala Sikuzaliwa na hakuna chochote kinachofanana na kulingana Nami)) [Al-Bukhaariy na An-Nasaaiy]