الأَعْلى
Al-A’laa: 87
بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ
سَبِّحِ اسْمَ رَبِّكَ الْأَعْلَى ﴿١﴾
1. Sabbih Jina la Rabb wako Mwenye ‘Uluwa Ametukuka kabisa kuliko vyote.
الَّذِي خَلَقَ فَسَوَّىٰ ﴿٢﴾
2. Ambaye Ameumba (kila kitu) kisha Akasawazisha.
وَالَّذِي قَدَّرَ فَهَدَىٰ ﴿٣﴾
3. Na Ambaye Amekadiria na Akaongoza.
وَالَّذِي أَخْرَجَ الْمَرْعَىٰ ﴿٤﴾
4. Na Ambaye Ametoa malisho.
فَجَعَلَهُ غُثَاءً أَحْوَىٰ ﴿٥﴾
5. Kisha Akayafanya majani makavu, meusi.
سَنُقْرِئُكَ فَلَا تَنسَىٰ ﴿٦﴾
6. Tutakusomesha (Qur-aan ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) basi hutoisahau.
إِلَّا مَا شَاءَ اللَّـهُۚ إِنَّهُ يَعْلَمُ الْجَهْرَ وَمَا يَخْفَىٰ ﴿٧﴾
7. Isipokuwa yale Ayatakayo Allaah; hakika Yeye Anayajua ya jahara na yale yanayofichikana.
وَنُيَسِّرُكَ لِلْيُسْرَىٰ ﴿٨﴾
8. “Na Tutakuwepesishia kwa yaliyo mepesi”
فَذَكِّرْ إِن نَّفَعَتِ الذِّكْرَىٰ ﴿٩﴾
9. Basi kumbusha ikiwa kunafaa ukumbusho.
سَيَذَّكَّرُ مَن يَخْشَىٰ ﴿١٠﴾
10. Atakumbuka yule anayeogopa.
وَيَتَجَنَّبُهَا الْأَشْقَى ﴿١١﴾
11. Na atajiepusha nayo fedhuli.
الَّذِي يَصْلَى النَّارَ الْكُبْرَىٰ ﴿١٢﴾
12. Ambaye atauingia na kuungua moto mkubwa kabisa.
ثُمَّ لَا يَمُوتُ فِيهَا وَلَا يَحْيَىٰ ﴿١٣﴾
13. Kisha hatokufa humo, na wala hatokuwa hai.
قَدْ أَفْلَحَ مَن تَزَكَّىٰ ﴿١٤﴾
14. Hakika amefaulu ambaye amejitakasa.
وَذَكَرَ اسْمَ رَبِّهِ فَصَلَّىٰ ﴿١٥﴾
15. Na akadhukuru Jina la Rabb wake na akaswali.
بَلْ تُؤْثِرُونَ الْحَيَاةَ الدُّنْيَا ﴿١٦﴾
16. Bali mnahiari uhai wa dunia.
وَالْآخِرَةُ خَيْرٌ وَأَبْقَىٰ ﴿١٧﴾
17. Na hali Aakhirah ni bora zaidi ya kudumu.
إِنَّ هَـٰذَا لَفِي الصُّحُفِ الْأُولَىٰ ﴿١٨﴾
18. Hakika haya bila shaka yamo katika maandiko tukufu ya awali.
صُحُفِ إِبْرَاهِيمَ وَمُوسَىٰ ﴿١٩﴾
19. Maandiko tukufu ya Ibraahiym na Muwsaa.
0 Comments