الْكَوْثَر
Al-Kawthar: 108



بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ


إِنَّا أَعْطَيْنَاكَ الْكَوْثَرَ ﴿١﴾
1. Hakika Sisi Tumekupa (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) Al-Kawthar (Mto katika Jannah).


فَصَلِّ لِرَبِّكَ وَانْحَرْ ﴿٢﴾
2. Basi swali kwa ajili ya Rabb wako na chinja kwa ajili Yake.


إِنَّ شَانِئَكَ هُوَ الْأَبْتَرُ ﴿٣﴾
3. Hakika mbaya wako, yeye ndiye atakayekatiliwa mbali (kizazi na kila kheri).