الْمَاعُون
Al-Maa’uwn: 107
بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ
أَرَأَيْتَ الَّذِي يُكَذِّبُ بِالدِّينِ ﴿١﴾
1. Je, umemuona yule anayekadhibisha malipo?
فَذَٰلِكَ الَّذِي يَدُعُّ الْيَتِيمَ ﴿٢﴾
2. Basi huyo ndiye anayemsukuma yatima.
وَلَا يَحُضُّ عَلَىٰ طَعَامِ الْمِسْكِينِ ﴿٣﴾
3. Na wala hahamasishi kulisha maskini.
فَوَيْلٌ لِّلْمُصَلِّينَ ﴿٤﴾
4. Basi Ole kwa wanaoswali ...
الَّذِينَ هُمْ عَن صَلَاتِهِمْ سَاهُونَ ﴿٥﴾
5. Ambao wanapuuza Swalaah zao.
الَّذِينَ هُمْ يُرَاءُونَ ﴿٦﴾
6. Ambao wanajionyesha (riyaa).
وَيَمْنَعُونَ الْمَاعُونَ ﴿٧﴾
7. Na wanazuia misaada ya matumizi madogodogo ya kawaida ya kila siku.
0 Comments