الزَّلْزَلَة
Al-Zalzalah: 99



بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ


إِذَا زُلْزِلَتِ الْأَرْضُ زِلْزَالَهَا ﴿١﴾
1. Itakapotetemeshwa ardhi zilzala yake (ya mwisho).


وَأَخْرَجَتِ الْأَرْضُ أَثْقَالَهَا ﴿٢﴾
2. Na itakapotoa ardhi mizigo yake.


وَقَالَ الْإِنسَانُ مَا لَهَا ﴿٣﴾
3. Na mwana Aadam akasema: “Ina nini?”


يَوْمَئِذٍ تُحَدِّثُ أَخْبَارَهَا ﴿٤﴾
4. Siku hiyo itahadithia habari zake.


بِأَنَّ رَبَّكَ أَوْحَىٰ لَهَا ﴿٥﴾
5. Kwa kuwa Rabb wako Ameifunulia ilhamu.


يَوْمَئِذٍ يَصْدُرُ النَّاسُ أَشْتَاتًا لِّيُرَوْا أَعْمَالَهُمْ ﴿٦﴾
6. Siku hiyo watatoka watu makundi mbalimbali wamefarikiana ili waonyeshwe ‘amali zao.


فَمَن يَعْمَلْ مِثْقَالَ ذَرَّةٍ خَيْرًا يَرَهُ ﴿٧﴾
7. Basi yule atakayetenda kheri uzito wa chembe (au sisimizi) ataiona.


وَمَن يَعْمَلْ مِثْقَالَ ذَرَّةٍ شَرًّا يَرَهُ ﴿٨﴾
8. Na yule atakayetenda shari uzito wa chembe (au sisimizi) ataiona.