الْعَلَق
Al-‘Alaq: 96
بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ
اقْرَأْ بِاسْمِ رَبِّكَ الَّذِي خَلَقَ ﴿١﴾
1. Soma kwa Jina la Rabb wako Aliyeumba.
خَلَقَ الْإِنسَانَ مِنْ عَلَقٍ ﴿٢﴾
2. Amemuumba mwana Aadam kutokana na pande la damu linaloning’inia.
اقْرَأْ وَرَبُّكَ الْأَكْرَمُ ﴿٣﴾
3. Soma na Rabb wako ni Mkarimu kushinda wote.
الَّذِي عَلَّمَ بِالْقَلَمِ ﴿٤﴾
4. Ambaye Aliyefunza kwa kalamu.
عَلَّمَ الْإِنسَانَ مَا لَمْ يَعْلَمْ ﴿٥﴾
5. Amemfunza mwana Aadam ambayo asiyoyajua.
كَلَّا إِنَّ الْإِنسَانَ لَيَطْغَىٰ ﴿٦﴾
6. Laa hasha! Hakika mwana Aadam bila shaka amepindukia mipaka kuasi.
أَن رَّآهُ اسْتَغْنَىٰ ﴿٧﴾
7. Kwa kuwa amejiona amejitosheleza.
إِنَّ إِلَىٰ رَبِّكَ الرُّجْعَىٰ ﴿٨﴾
8. Hakika kwa Rabb wako ni marejeo.
أَرَأَيْتَ الَّذِي يَنْهَىٰ ﴿٩﴾
9. Je, umemuona yule anayekataza?
عَبْدًا إِذَا صَلَّىٰ ﴿١٠﴾
10. Mja pale anaposwali?
أَرَأَيْتَ إِن كَانَ عَلَى الْهُدَىٰ ﴿١١﴾
11. Je, umeona kama alikuwa katika Uongofu?
أَوْ أَمَرَ بِالتَّقْوَىٰ ﴿١٢﴾
12. Au ameamrisha kuhusu taqwa?
أَرَأَيْتَ إِن كَذَّبَ وَتَوَلَّىٰ ﴿١٣﴾
13. Je, unaonaje! Kama amekadhibisha na akakengeuka?
أَلَمْ يَعْلَم بِأَنَّ اللَّـهَ يَرَىٰ ﴿١٤﴾
14. Je, hajui kwamba hakika Allaah Anaona?
كَلَّا لَئِن لَّمْ يَنتَهِ لَنَسْفَعًا بِالنَّاصِيَةِ ﴿١٥﴾
15. Laa hasha! Asipoacha, bila shaka Tutamburuta kwa nywele za paji la uso.
نَاصِيَةٍ كَاذِبَةٍ خَاطِئَةٍ ﴿١٦﴾
16. Paji la usio linalokadhibisha lenye hatia.
فَلْيَدْعُ نَادِيَهُ ﴿١٧﴾
17. Basi na aite timu yake.
سَنَدْعُ الزَّبَانِيَةَ ﴿١٨﴾
18. Nasi Tutawaita Az-Zabaaniyah Malaika wa adhabu.
كَلَّا لَا تُطِعْهُ وَاسْجُدْ وَاقْتَرِب ۩﴿١٩﴾
19. Laa hasha! Usimtii; na sujudu na kurubia (kwa Allaah).
0 Comments