التِّين
At-Tiyn: 95
بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ
وَالتِّينِ وَالزَّيْتُونِ ﴿١﴾
1. Naapa kwa tiyn na zaytuwn.
وَطُورِ سِينِينَ ﴿٢﴾
2. Na Naapa kwa mlima wa Sinai
وَهَـٰذَا الْبَلَدِ الْأَمِينِ ﴿٣﴾
3. Na Naapa kwa mji huu wa amani (Makkah).
لَقَدْ خَلَقْنَا الْإِنسَانَ فِي أَحْسَنِ تَقْوِيمٍ ﴿٤﴾
4. Kwa yakini Tumemuumba mwana Aadam katika umbile bora kabisa.
ثُمَّ رَدَدْنَاهُ أَسْفَلَ سَافِلِينَ ﴿٥﴾
5. Kisha Tukamrudisha chini kabisa ya walio chini.
إِلَّا الَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ فَلَهُمْ أَجْرٌ غَيْرُ مَمْنُونٍ ﴿٦﴾
6. Isipokuwa wale walioamini na wakatenda mema; hao watapata ujira usiokatika.
فَمَا يُكَذِّبُكَ بَعْدُ بِالدِّينِ ﴿٧﴾
7. Basi lipi bado litakalokukadhibisha kuhusu malipo?
أَلَيْسَ اللَّـهُ بِأَحْكَمِ الْحَاكِمِينَ ﴿٨﴾
8. Je, kwani Allaah Si Mwadilifu zaidi wa wanaohukumu kuliko mahakimu wote?
0 Comments