الشَّرْح
Ash-Sharh: 94
بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ
أَلَمْ نَشْرَحْ لَكَ صَدْرَكَ ﴿١﴾
1. Je, kwani Hatukukupanulia kifua chako kukubainishia (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم)?
وَوَضَعْنَا عَنكَ وِزْرَكَ ﴿٢﴾
2. Na Tukakuondolea mzigo wako (wa dhambi)?
الَّذِي أَنقَضَ ظَهْرَكَ ﴿٣﴾
3. Ambao ulithakilisha mgongo wako?
وَرَفَعْنَا لَكَ ذِكْرَكَ ﴿٤﴾
4. Na Tukakutukuzia kutajwa kwako?
فَإِنَّ مَعَ الْعُسْرِ يُسْرًا ﴿٥﴾
5. Basi hakika pamoja na kila gumu kuna wepesi.
إِنَّ مَعَ الْعُسْرِ يُسْرًا ﴿٦﴾
6. Hakika pamoja na kila ugumu kuna wepesi.
فَإِذَا فَرَغْتَ فَانصَبْ ﴿٧﴾
7. Basi utakapopata faragha fanya juhudi katika ‘ibaadah.
وَإِلَىٰ رَبِّكَ فَارْغَب ﴿٨﴾
8. Na kwa Rabb wako elemea kwa raghba (kutakabaliwa).
0 Comments