الضُّحى
Adhw-Dhwuhaa: 93
بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ
وَالضُّحَىٰ ﴿١﴾
1. Naapa kwa dhuha.
وَاللَّيْلِ إِذَا سَجَىٰ ﴿٢﴾
2. Na Naapa kwa usiku unapotanda kiza na kutulia.
مَا وَدَّعَكَ رَبُّكَ وَمَا قَلَىٰ ﴿٣﴾
3. Rabb wako Hakukutelekeza na wala Hakukuchukia (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم).
وَلَلْآخِرَةُ خَيْرٌ لَّكَ مِنَ الْأُولَىٰ ﴿٤﴾
4. Na bila shaka Aakhirah ni kheri kwako kuliko ya awali (dunia).
وَلَسَوْفَ يُعْطِيكَ رَبُّكَ فَتَرْضَىٰ ﴿٥﴾
5. Na bila shaka Rabb wako Atakupa na utaridhika.
أَلَمْ يَجِدْكَ يَتِيمًا فَآوَىٰ ﴿٦﴾
6. Je, kwani Hakukukuta yatima, Akakupa makazi?
وَوَجَدَكَ ضَالًّا فَهَدَىٰ ﴿٧﴾
7. Na Akakukuta mpotevu Akakuongoza?
وَوَجَدَكَ عَائِلًا فَأَغْنَىٰ ﴿٨﴾
8. Na Akakukuta mhitaji, Akakutosheleza?
فَأَمَّا الْيَتِيمَ فَلَا تَقْهَرْ ﴿٩﴾
9. Kwa hivyo basi yatima usimuonee.
وَأَمَّا السَّائِلَ فَلَا تَنْهَرْ ﴿١٠﴾
10. Na muulizaji usimkaripie.
وَأَمَّا بِنِعْمَةِ رَبِّكَ فَحَدِّثْ ﴿١١﴾
11. Na neema ya Rabb wako ihadithie.
0 Comments