اللَّيْل
Al-Layl: 92



بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ


وَاللَّيْلِ إِذَا يَغْشَىٰ ﴿١﴾
1. Naapa kwa usiku unapofunika.


وَالنَّهَارِ إِذَا تَجَلَّىٰ ﴿٢﴾
2. Na Naapa kwa mchana unapodhihirika mwanga.


وَمَا خَلَقَ الذَّكَرَ وَالْأُنثَىٰ ﴿٣﴾
3. Na Naapa kwa Aliyeumba dume na kike.


إِنَّ سَعْيَكُمْ لَشَتَّىٰ ﴿٤﴾
4. Hakika juhudi zenu bila shaka ni tofauti tofauti.


فَأَمَّا مَنْ أَعْطَىٰ وَاتَّقَىٰ ﴿٥﴾
5. Basi yule anayetoa (mali) na akamcha Allaah.


وَصَدَّقَ بِالْحُسْنَىٰ ﴿٦﴾
6. Na akasadikisha Al-Husnaa; jazaa na laa ilaaha illa Allaah. 


فَسَنُيَسِّرُهُ لِلْيُسْرَىٰ ﴿٧﴾
7. “Basi Tutamuwepesishia kwa yaliyo mepesi”


وَأَمَّا مَن بَخِلَ وَاسْتَغْنَىٰ ﴿٨﴾
8. Ama yule afanyaye ubakhili na akajiona amejitosheleza.


وَكَذَّبَ بِالْحُسْنَىٰ ﴿٩﴾
9. Na akakadhibisha Al-Husnaa; anayowajibika kuyasadiki.


فَسَنُيَسِّرُهُ لِلْعُسْرَىٰ ﴿١٠﴾
10. Na Tutamuwepesishia kwa yaliyo magumu”.


وَمَا يُغْنِي عَنْهُ مَالُهُ إِذَا تَرَدَّىٰ ﴿١١﴾
11. Na itamsaidia nini mali yake atakapoporomoka kuangamia (motoni).


إِنَّ عَلَيْنَا لَلْـهُدَىٰ ﴿١٢﴾
12. Hakika ni juu Yetu (kubainisha) mwongozo.


وَإِنَّ لَنَا لَلْآخِرَةَ وَالْأُولَىٰ ﴿١٣﴾
13. Na hakika ni Yetu Sisi ya Aakhirah na ya awali (dunia).


فَأَنذَرْتُكُمْ نَارًا تَلَظَّىٰ ﴿١٤﴾
14. Basi Nimekutahadharisheni moto wenye mwako mkali mno.


لَا يَصْلَاهَا إِلَّا الْأَشْقَى ﴿١٥﴾
15. Hatouingia kuungua isipokuwa muovu mkubwa.


الَّذِي كَذَّبَ وَتَوَلَّىٰ ﴿١٦﴾
16. Ambaye amekadhibisha na akakengeuka mbali.


وَسَيُجَنَّبُهَا الْأَتْقَى ﴿١٧﴾
17. Na ataepushwa nao mwenye taqwa kabisa.


الَّذِي يُؤْتِي مَالَهُ يَتَزَكَّىٰ ﴿١٨﴾
18. Ambaye anatoa mali yake kujitakasa.


وَمَا لِأَحَدٍ عِندَهُ مِن نِّعْمَةٍ تُجْزَىٰ ﴿١٩﴾
19. Na hali hakuna mmoja yeyote aliyemfanyia fadhila yoyote hata amlipe.


إِلَّا ابْتِغَاءَ وَجْهِ رَبِّهِ الْأَعْلَىٰ ﴿٢٠﴾
20. Isipokuwa kutaka Wajihi wa Rabb wake Aliyetukuka.


وَلَسَوْفَ يَرْضَىٰ ﴿٢١﴾
21. Na bila shaka atakuja kuridhika.