الشَّمْس
Ash-Shams: 91
بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ
وَالشَّمْسِ وَضُحَاهَا ﴿١﴾
1. Naapa kwa jua na mwangaza wake.
وَالْقَمَرِ إِذَا تَلَاهَا ﴿٢﴾
2. Na Naapa kwa mwezi unapoliandama.
وَالنَّهَارِ إِذَا جَلَّاهَا ﴿٣﴾
3. Na Naapa kwa mchana unapolidhihirisha.
وَاللَّيْلِ إِذَا يَغْشَاهَا ﴿٤﴾
4. Na Naapa kwa usiku unapolifunika.
وَالسَّمَاءِ وَمَا بَنَاهَا ﴿٥﴾
5. Na Naapa kwa mbingu na Aliyezijenga.
وَالْأَرْضِ وَمَا طَحَاهَا ﴿٦﴾
6. Na Naapa kwa ardhi na Aliyeitandaza.
وَنَفْسٍ وَمَا سَوَّاهَا ﴿٧﴾
7. Na Naapa kwa nafsi na Aliyeisawazisha.
فَأَلْهَمَهَا فُجُورَهَا وَتَقْوَاهَا ﴿٨﴾
8. Kisha Akaitambulisha uovu wake na taqwa yake.
قَدْ أَفْلَحَ مَن زَكَّاهَا ﴿٩﴾
9. Kwa yakini amefaulu yule aliyeitakasa.
وَقَدْ خَابَ مَن دَسَّاهَا ﴿١٠﴾
10. Na kwa yakini amepita patupu aliyeifisidi.
كَذَّبَتْ ثَمُودُ بِطَغْوَاهَا ﴿١١﴾
11. Kina Thamuwd walikadhibisha (Rasuli wao) kwa upindukaji mipaka ya kuasi kwao.
إِذِ انبَعَثَ أَشْقَاهَا ﴿١٢﴾
12. Pale alipochomoka haraka muovu wao mkuu.
فَقَالَ لَهُمْ رَسُولُ اللَّـهِ نَاقَةَ اللَّـهِ وَسُقْيَاهَا ﴿١٣﴾
13. Rasuli wa Allaah (Swaalih عليه السلام) aliwaambia: (Msimdhuru) “Ngamia jike wa Allaah, na kinywaji chake.”
فَكَذَّبُوهُ فَعَقَرُوهَا فَدَمْدَمَ عَلَيْهِمْ رَبُّهُم بِذَنبِهِمْ فَسَوَّاهَا ﴿١٤﴾
14. Lakini walimkadhibisha na wakamuua; basi Rabb wao Akawaangamiza kwa sababu ya dhambi zao, na Akayafanya mateketezi yao sawasawa kwa wote.
وَلَا يَخَافُ عُقْبَاهَا ﴿١٥﴾
15. Na wala (Allaah) Hakhofu hatima yake.
0 Comments