الْبُرُوج
Al-Buruwj: 85
بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ
وَالسَّمَاءِ ذَاتِ الْبُرُوجِ ﴿١﴾
1. Naapa kwa mbingu zenye sayari kubwa zilizodhahiri.
وَالْيَوْمِ الْمَوْعُودِ ﴿٢﴾
2. Na Naapa kwa Siku iliyoahidiwa (ya Qiyaamah).
وَشَاهِدٍ وَمَشْهُودٍ ﴿٣﴾
3. Na Naapa kwa shahidi na kinachoshuhudiwa.
قُتِلَ أَصْحَابُ الْأُخْدُودِ ﴿٤﴾
4. Wamelaaniwa na kuangamia watu wa mahandaki.
النَّارِ ذَاتِ الْوَقُودِ ﴿٥﴾
5. Yenye moto uliojaa vichochezi moto.
إِذْ هُمْ عَلَيْهَا قُعُودٌ ﴿٦﴾
6. Pale walipokuwa wamekaa hapo.
وَهُمْ عَلَىٰ مَا يَفْعَلُونَ بِالْمُؤْمِنِينَ شُهُودٌ ﴿٧﴾
7. Nao walikuwa ni wenye kushuhudia juu ya yale waliyowafanyia Waumini.
وَمَا نَقَمُوا مِنْهُمْ إِلَّا أَن يُؤْمِنُوا بِاللَّـهِ الْعَزِيزِ الْحَمِيدِ ﴿٨﴾
8. Na hawakuwachukia isipokuwa kwa vile wamemwamini Allaah Mwenye enzi ya nguvu Asiyeshindika, Mwenye kustahiki kuhimidiwa kwa yote.
الَّذِي لَهُ مُلْكُ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِۚ وَاللَّـهُ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ شَهِيدٌ ﴿٩﴾
9. Ambaye Pekee Ana ufalme wa mbingu na ardhi; na Allaah juu ya kila kitu ni Shahidi.
إِنَّ الَّذِينَ فَتَنُوا الْمُؤْمِنِينَ وَالْمُؤْمِنَاتِ ثُمَّ لَمْ يَتُوبُوا فَلَهُمْ عَذَابُ جَهَنَّمَ وَلَهُمْ عَذَابُ الْحَرِيقِ ﴿١٠﴾
10. Hakika wale waliowatesa motoni Waumini wa kiume na Waumini wa kike kisha hawakutubu, watapata adhabu ya Jahannam, na watapata adhabu ya kuunguza.
إِنَّ الَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ لَهُمْ جَنَّاتٌ تَجْرِي مِن تَحْتِهَا الْأَنْهَارُۚ ذَٰلِكَ الْفَوْزُ الْكَبِيرُ ﴿١١﴾
11. Hakika wale walioamini na wakatenda mema watapata Jannaat zipitazo chini yake mito. Huko ndiko kufuzu kukubwa.
إِنَّ بَطْشَ رَبِّكَ لَشَدِيدٌ ﴿١٢﴾
12. Hakika mkamato wa kuadhibu wa Rabb wako bila shaka ni mkali.
إِنَّهُ هُوَ يُبْدِئُ وَيُعِيدُ ﴿١٣﴾
13. Hakika Yeye Ndiye Anayeanzisha asili (ya uumbaji) na Atayerudisha.
وَهُوَ الْغَفُورُ الْوَدُودُ ﴿١٤﴾
14. Naye ni Mwingi wa kughufuria, Mwenye upendo halisi.
ذُو الْعَرْشِ الْمَجِيدُ ﴿١٥﴾
15. Mwenye ‘Arsh; Mwenye utukufu kamili, enzi, wingi wa vipawa, fadhila na ukarimu.
فَعَّالٌ لِّمَا يُرِيدُ ﴿١٦﴾
16. Mwingi wa kufanya Atakalo.
هَلْ أَتَاكَ حَدِيثُ الْجُنُودِ ﴿١٧﴾
17. Je, imekujia hadithi ya majeshi? -
فِرْعَوْنَ وَثَمُودَ ﴿١٨﴾
18. Ya Fir’awn na kina Thamuwd?
بَلِ الَّذِينَ كَفَرُوا فِي تَكْذِيبٍ ﴿١٩﴾
19. Bali wale waliokufuru wamo katika kukadhibisha.
وَاللَّـهُ مِن وَرَائِهِم مُّحِيطٌ ﴿٢٠﴾
20. Na Allaah Amewazunguka (kwa Ujuzi Wake) nyuma yao.
بَلْ هُوَ قُرْآنٌ مَّجِيدٌ ﴿٢١﴾
21. Bali hii ni Qur-aan Majiyd; adhimu, karimu, yenye kheri, baraka na ilmu tele.
فِي لَوْحٍ مَّحْفُوظٍ ﴿٢٢﴾
22. Katika Ubao Uliohifadhiwa.
0 Comments