الإِنْشِقَاق
Al-Inshiqaaq: 84



بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ


إِذَا السَّمَاءُ انشَقَّتْ ﴿١﴾
1. Mbingu zitakaporaruka  


وَأَذِنَتْ لِرَبِّهَا وَحُقَّتْ ﴿٢﴾
2. Na zikamsikiliza na kumtii Rabb wake na zikawajibikiwa kufanya hivyo.


وَإِذَا الْأَرْضُ مُدَّتْ ﴿٣﴾
3. Na ardhi itakapotandazwa.


وَأَلْقَتْ مَا فِيهَا وَتَخَلَّتْ ﴿٤﴾
4. Na ikatupilia mbali vile vilivyomo ndani yake na ikawa tupu.


وَأَذِنَتْ لِرَبِّهَا وَحُقَّتْ ﴿٥﴾
5. Na ikamsikiliza na kumtii Rabb wake na ikawajibikiwa kufanya hivyo.


يَا أَيُّهَا الْإِنسَانُ إِنَّكَ كَادِحٌ إِلَىٰ رَبِّكَ كَدْحًا فَمُلَاقِيهِ ﴿٦﴾
6. Ee mwana Aadam! Hakika wewe unajikusurukusuru mno kuelekea kwa Rabb wako kwa juhudi na masumbuko, basi utakutana Naye.


فَأَمَّا مَنْ أُوتِيَ كِتَابَهُ بِيَمِينِهِ ﴿٧﴾
7. Basi ama yule atakayepewa kitabu chake kwa mkono wake wa kulia.


فَسَوْفَ يُحَاسَبُ حِسَابًا يَسِيرًا ﴿٨﴾
8. Atahesabiwa hesabu ya sahali.


وَيَنقَلِبُ إِلَىٰ أَهْلِهِ مَسْرُورًا ﴿٩﴾
9. Na atageuka kwa ahli zake mwenye kufurahi.


وَأَمَّا مَنْ أُوتِيَ كِتَابَهُ وَرَاءَ ظَهْرِهِ ﴿١٠﴾
10. Na ama yule atakayepewa kitabu chake nyuma ya mgongo wake.


فَسَوْفَ يَدْعُو ثُبُورًا ﴿١١﴾
11. Ataomba kuteketea.


وَيَصْلَىٰ سَعِيرًا ﴿١٢﴾
12. Na ataingia aungue moto uliowashwa vikali mno.


إِنَّهُ كَانَ فِي أَهْلِهِ مَسْرُورًا ﴿١٣﴾
13. Hakika yeye alikuwa katika ahli zake mwenye kufurahi.


إِنَّهُ ظَنَّ أَن لَّن يَحُورَ ﴿١٤﴾
14. Hakika yeye alidhani kwamba hatorudi kwenye asili yake.


بَلَىٰ إِنَّ رَبَّهُ كَانَ بِهِ بَصِيرًا ﴿١٥﴾
15. Laa hasha! Hakika Rabb wake Amekuwa Mwenye kumuona daima.


فَلَا أُقْسِمُ بِالشَّفَقِ ﴿١٦﴾
16. Basi Naapa kwa wekundu wa kukuchwa jua.


وَاللَّيْلِ وَمَا وَسَقَ ﴿١٧﴾
17. Na Naapa kwa usiku na ambavyo umekusanya (na kugubika).


وَالْقَمَرِ إِذَا اتَّسَقَ ﴿١٨﴾
18. Na Naapa kwa mwezi unapokuwa mbalamwezi kamili.


لَتَرْكَبُنَّ طَبَقًا عَن طَبَقٍ ﴿١٩﴾
19. Bila shaka mtapitia hatua baada ya hatua.


فَمَا لَهُمْ لَا يُؤْمِنُونَ ﴿٢٠﴾
20. Basi wana nini hawaamini?


وَإِذَا قُرِئَ عَلَيْهِمُ الْقُرْآنُ لَا يَسْجُدُونَ ۩﴿٢١﴾
21. Na wanaposomewa Qur-aan, hawasujudu.


بَلِ الَّذِينَ كَفَرُوا يُكَذِّبُونَ ﴿٢٢﴾
22. Bali wale waliokufuru wanakadhibisha.


وَاللَّـهُ أَعْلَمُ بِمَا يُوعُونَ ﴿٢٣﴾
23. Na Allaah Anajua zaidi yale wanayoyakusanya ya siri.


فَبَشِّرْهُم بِعَذَابٍ أَلِيمٍ ﴿٢٤﴾
24. Basi wabashirie adhabu iumizayo.


إِلَّا الَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ لَهُمْ أَجْرٌ غَيْرُ مَمْنُونٍ ﴿٢٥﴾
25. Isipokuwa wale walioamini na wakatenda mema, watapata ujira usiokatika.