عَبَسَ
Abasa: 80


بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ


عَبَسَ وَتَوَلَّىٰ ﴿١﴾
1. Alikunja kipaji na akageuka.


أَن جَاءَهُ الْأَعْمَىٰ ﴿٢﴾
2. Alipomjia kipofu.


وَمَا يُدْرِيكَ لَعَلَّهُ يَزَّكَّىٰ ﴿٣﴾
3. Na nini kitakachokujulisha (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) huenda akatakasika?


أَوْ يَذَّكَّرُ فَتَنفَعَهُ الذِّكْرَىٰ ﴿٤﴾
4. Au atawaidhika na yamfae mawaidha?


أَمَّا مَنِ اسْتَغْنَىٰ ﴿٥﴾
5. Ama yule ajionaye amejitosheleza.


فَأَنتَ لَهُ تَصَدَّىٰ ﴿٦﴾
6. Nawe unamgeukia kumshughulikia.


وَمَا عَلَيْكَ أَلَّا يَزَّكَّىٰ ﴿٧﴾
7. Na si juu yako asipotakasika.


وَأَمَّا مَن جَاءَكَ يَسْعَىٰ ﴿٨﴾
8. Ama yule aliyekujia kwa kukimbilia.


وَهُوَ يَخْشَىٰ ﴿٩﴾
9. Naye anakhofu.


فَأَنتَ عَنْهُ تَلَهَّىٰ ﴿١٠﴾
10. Basi wewe unampuuza.


كَلَّا إِنَّهَا تَذْكِرَةٌ ﴿١١﴾
11. Laa hasha! Hakika hizi (Aayah) ni mawaidha.


فَمَن شَاءَ ذَكَرَهُ ﴿١٢﴾
12. Basi atakaye ahifadhi na awaidhike.


فِي صُحُفٍ مُّكَرَّمَةٍ ﴿١٣﴾
13.  Katika Sahifa zenye kuadhimishwa.


مَّرْفُوعَةٍ مُّطَهَّرَةٍ ﴿١٤﴾
14. Zimetukuzwa na zimetakaswa.


بِأَيْدِي سَفَرَةٍ ﴿١٥﴾
15. Katika mikono ya Malaika waandishi.


كِرَامٍ بَرَرَةٍ ﴿١٦﴾
16. Watukufu, watiifu.


قُتِلَ الْإِنسَانُ مَا أَكْفَرَهُ ﴿١٧﴾
17. Amelaaniwa na kuangamia mwana Aadam ukafiri ulioje alionao?


مِنْ أَيِّ شَيْءٍ خَلَقَهُ ﴿١٨﴾
18. Kutoka kitu gani (Allaah) Amemuumba?


مِن نُّطْفَةٍ خَلَقَهُ فَقَدَّرَهُ ﴿١٩﴾
19. Kutoka tone la manii, Amemuumba, Akamkadiria.


ثُمَّ السَّبِيلَ يَسَّرَهُ ﴿٢٠﴾
20. Kisha Akamuwepesishia njia.


ثُمَّ أَمَاتَهُ فَأَقْبَرَهُ ﴿٢١﴾
21. Kisha Akamfisha, na Akamjaalia atiwe kaburini.


ثُمَّ إِذَا شَاءَ أَنشَرَهُ ﴿٢٢﴾
22. Kisha Atakapotaka, Atamfufua.


كَلَّا لَمَّا يَقْضِ مَا أَمَرَهُ ﴿٢٣﴾
23. Laa hasha! Hakutimiza Aliyomuamuru (Allaah).


فَلْيَنظُرِ الْإِنسَانُ إِلَىٰ طَعَامِهِ ﴿٢٤﴾
24. Basi atazame mwana Aadam chakula chake.


أَنَّا صَبَبْنَا الْمَاءَ صَبًّا ﴿٢٥﴾
25. Kwamba Sisi Tumemimina maji kwa uneemefu.


ثُمَّ شَقَقْنَا الْأَرْضَ شَقًّا ﴿٢٦﴾
26. Kisha Tukairarua ardhi miraruko.


فَأَنبَتْنَا فِيهَا حَبًّا ﴿٢٧﴾
27. Tukaotesha humo nafaka.


وَعِنَبًا وَقَضْبًا ﴿٢٨﴾
28. Na mizabibu na mimea ya mboga (ikatwayo ikamea tena).


وَزَيْتُونًا وَنَخْلًا ﴿٢٩﴾
29. Na mizaituni na mitende.


وَحَدَائِقَ غُلْبًا ﴿٣٠﴾
30. Na mabustani yaliyositawi na kusongamana.


وَفَاكِهَةً وَأَبًّا ﴿٣١﴾
31. Na matunda na majani ya malisho ya wanyama.


مَّتَاعًا لَّكُمْ وَلِأَنْعَامِكُمْ ﴿٣٢﴾
32. Ni manufaa kwenu na kwa wanyama wenu wa mifugo.


فَإِذَا جَاءَتِ الصَّاخَّةُ ﴿٣٣﴾
33. Basi utakapokuja ukelele mkali wa kugofya.


يَوْمَ يَفِرُّ الْمَرْءُ مِنْ أَخِيهِ ﴿٣٤﴾
34. Siku mtu atakapomkimbia ndugu yake.


وَأُمِّهِ وَأَبِيهِ ﴿٣٥﴾
35. Na mama yake na baba yake.


وَصَاحِبَتِهِ وَبَنِيهِ ﴿٣٦﴾
36. Na mkewe na wanawe.


لِكُلِّ امْرِئٍ مِّنْهُمْ يَوْمَئِذٍ شَأْنٌ يُغْنِيهِ ﴿٣٧﴾
37. Kila mtu miongoni mwao siku hiyo atakuwa na hali ya kumtosheleza.


وُجُوهٌ يَوْمَئِذٍ مُّسْفِرَةٌ ﴿٣٨﴾
38.  Ziko nyuso siku hiyo zitanawiri.


ضَاحِكَةٌ مُّسْتَبْشِرَةٌ ﴿٣٩﴾
39. Zikicheka na kufurahika.


وَوُجُوهٌ يَوْمَئِذٍ عَلَيْهَا غَبَرَةٌ ﴿٤٠﴾
40. Na ziko nyuso siku hiyo zitakuwa na vumbi juu yake.


تَرْهَقُهَا قَتَرَةٌ ﴿٤١﴾
41. Zitafunikwa na giza totoro.


أُولَـٰئِكَ هُمُ الْكَفَرَةُ الْفَجَرَةُ ﴿٤٢﴾
42. Hao ndio makafiri waovu.