الْمُرْسَلاَت
Al-Mursalaat: 77
بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ
وَالْمُرْسَلَاتِ عُرْفًا﴿١﴾
1. Naapa kwa pepo zitumwazo kwa mfuatano.
فَالْعَاصِفَاتِ عَصْفًا﴿٢﴾
2. Kisha Naapa kwa pepo zinazovuma kwa dhoruba.
وَالنَّاشِرَاتِ نَشْرًا﴿٣﴾
3. Na Naapa kwa pepo zinazotawanya mawingu na mvua.
فَالْفَارِقَاتِ فَرْقًا﴿٤﴾
4. Kisha Naapa kwa (Malaika) wanaopambanua pambanuo la haki na batili.
فَالْمُلْقِيَاتِ ذِكْرًا﴿٥﴾
5. Kisha Naapa kwa (Malaika) wanaopeleka wahyi kwa Rasuli.
عُذْرًا أَوْ نُذْرًا﴿٦﴾
6. Kwa ajili ya kuondosha udhuru au kwa ajili ya kuonya.
إِنَّمَا تُوعَدُونَ لَوَاقِعٌ﴿٧﴾
7. Hakika yale mliyoahidiwa bila shaka yatatokea tu!
فَإِذَا النُّجُومُ طُمِسَتْ﴿٨﴾
8. Basi pale nyota zitakapofutiliwa mbali mwanga wake.
وَإِذَا السَّمَاءُ فُرِجَتْ﴿٩﴾
9. Na pale mbingu zitakapofunguliwa.
وَإِذَا الْجِبَالُ نُسِفَتْ﴿١٠﴾
10. Na pale majabali yatakapopeperushiliwa mbali
وَإِذَا الرُّسُلُ أُقِّتَتْ﴿١١﴾
11. Na pale Rusuli watakapopangwa kwa wakati wake maalumu.
لِأَيِّ يَوْمٍ أُجِّلَتْ﴿١٢﴾
12. Kwa Siku gani hiyo iliyoahirishwa?
لِيَوْمِ الْفَصْلِ﴿١٣﴾
13. Kwa ajili ya Siku ya hukumu na kutenganisha.
وَمَا أَدْرَاكَ مَا يَوْمُ الْفَصْلِ﴿١٤﴾
14. Na nini kitakachokujulisha Siku ya hukumu na kutenganisha?
وَيْلٌ يَوْمَئِذٍ لِّلْمُكَذِّبِينَ﴿١٥﴾
15. Ole Siku hiyo kwa wenye kukadhibisha.
أَلَمْ نُهْلِكِ الْأَوَّلِينَ﴿١٦﴾
16. Je, kwani Hatukuangamiza watu wa awali?
ثُمَّ نُتْبِعُهُمُ الْآخِرِينَ﴿١٧﴾
17. Kisha Tukawafuatilishia wengineo?
كَذَٰلِكَ نَفْعَلُ بِالْمُجْرِمِينَ﴿١٨﴾
18. Hivyo ndivyo Tunavofanya wahalifu.
وَيْلٌ يَوْمَئِذٍ لِّلْمُكَذِّبِينَ﴿١٩﴾
19. Ole Siku hiyo kwa wenye kukadhibisha.
أَلَمْ نَخْلُقكُّم مِّن مَّاءٍ مَّهِينٍ﴿٢٠﴾
20. Je, kwani Hatukukuumbeni kutokana na maji dhalilifu (manii)?
فَجَعَلْنَاهُ فِي قَرَارٍ مَّكِينٍ﴿٢١﴾
21. Kisha Tukayaweka katika mahali pa kutulia, thabiti?
إِلَىٰ قَدَرٍ مَّعْلُومٍ﴿٢٢﴾
22. Mpaka kipimo maalumu.
فَقَدَرْنَا فَنِعْمَ الْقَادِرُونَ﴿٢٣﴾
23. Tukakadiria, basi ni wazuri walioje (Sisi) Wenye kukadiria.
وَيْلٌ يَوْمَئِذٍ لِّلْمُكَذِّبِينَ﴿٢٤﴾
24. Ole Siku hiyo kwa wenye kukadhibisha.
أَلَمْ نَجْعَلِ الْأَرْضَ كِفَاتًا﴿٢٥﴾
25. Je, kwani Hatukufanya ardhi kuwa ni chombo cha kukusanya?
أَحْيَاءً وَأَمْوَاتًا﴿٢٦﴾
26. Vilivyo hai na wafu?
وَجَعَلْنَا فِيهَا رَوَاسِيَ شَامِخَاتٍ وَأَسْقَيْنَاكُم مَّاءً فُرَاتًا﴿٢٧﴾
27. Na Tukaweka humo milima thabiti mirefu iliyojikita na Tukakunywesheni maji matamu mno?
وَيْلٌ يَوْمَئِذٍ لِّلْمُكَذِّبِينَ﴿٢٨﴾
28. Ole Siku hiyo kwa wenye kukadhibisha.
انطَلِقُوا إِلَىٰ مَا كُنتُم بِهِ تُكَذِّبُونَ﴿٢٩﴾
29. (Wataambiwa): “Nendeni kwenye yale mliyokuwa mkiyakadhibisha.
انطَلِقُوا إِلَىٰ ظِلٍّ ذِي ثَلَاثِ شُعَبٍ﴿٣٠﴾
30. “Nendeni kwenye kivuli chenye sehemu tatu.”
لَّا ظَلِيلٍ وَلَا يُغْنِي مِنَ اللَّـهَبِ﴿٣١﴾
31. Hakiwafuniki, na wala hakiwakingi na mwako wa moto.
إِنَّهَا تَرْمِي بِشَرَرٍ كَالْقَصْرِ﴿٣٢﴾
32. Hakika huo (moto) hurusha macheche mfano wa makasri.
كَأَنَّهُ جِمَالَتٌ صُفْرٌ﴿٣٣﴾
33. Kama kwamba ngamia wakubwa wa manjano.
وَيْلٌ يَوْمَئِذٍ لِّلْمُكَذِّبِينَ﴿٣٤﴾
34. Ole Siku hiyo kwa wenye kukadhibisha.
هَـٰذَا يَوْمُ لَا يَنطِقُونَ﴿٣٥﴾
35. Siku hii hawatotamka.
وَلَا يُؤْذَنُ لَهُمْ فَيَعْتَذِرُونَ﴿٣٦﴾
36. Na wala hawatopewa idhini, ili watoe nyudhuru.
وَيْلٌ يَوْمَئِذٍ لِّلْمُكَذِّبِينَ﴿٣٧﴾
37. Ole Siku hiyo kwa wenye kukadhibisha.
هَـٰذَا يَوْمُ الْفَصْلِ ۖ جَمَعْنَاكُمْ وَالْأَوَّلِينَ﴿٣٨﴾
38. Hii ni Siku ya hukumu na kutenganisha. Tumekukusanyeni pamoja na watu wa awali.
فَإِن كَانَ لَكُمْ كَيْدٌ فَكِيدُونِ﴿٣٩﴾
39. Ikiwa mnayo hila yoyote ile basi Nifanyieni.
وَيْلٌ يَوْمَئِذٍ لِّلْمُكَذِّبِينَ﴿٤٠﴾
40. Ole Siku hiyo kwa wenye kukadhibisha.
إِنَّ الْمُتَّقِينَ فِي ظِلَالٍ وَعُيُونٍ﴿٤١﴾
41. Hakika wenye taqwa wamo katika vivuli na chemchemu.
وَفَوَاكِهَ مِمَّا يَشْتَهُونَ﴿٤٢﴾
42. Na matunda katika yale wanayoyatamani.
كُلُوا وَاشْرَبُوا هَنِيئًا بِمَا كُنتُمْ تَعْمَلُونَ﴿٤٣﴾
43. (Wataambiwa): “Kuleni na kunyweni kwa furaha kwa sababu ya yale mliyokuwa mkiyatenda.”
إِنَّا كَذَٰلِكَ نَجْزِي الْمُحْسِنِينَ﴿٤٤﴾
44. Hakika hivyo ndivyo Tunavyowalipa wafanyao ihsani.
وَيْلٌ يَوْمَئِذٍ لِّلْمُكَذِّبِينَ﴿٤٥﴾
45. Ole Siku hiyo kwa wenye kukadhibisha.
كُلُوا وَتَمَتَّعُوا قَلِيلًا إِنَّكُم مُّجْرِمُونَ﴿٤٦﴾
46. (Enyi Makafiri): “Kuleni na stareheni kidogo (duniani), hakika nyinyi ni wahalifu.”
وَيْلٌ يَوْمَئِذٍ لِّلْمُكَذِّبِينَ﴿٤٧﴾
47. Ole Siku hiyo kwa wenye kukadhibisha.
وَإِذَا قِيلَ لَهُمُ ارْكَعُوا لَا يَرْكَعُونَ﴿٤٨﴾
48. Na walipokuwa wakiambiwa “Rukuuni (mswali),” hawakuwa wakirukuu.
وَيْلٌ يَوْمَئِذٍ لِّلْمُكَذِّبِينَ﴿٤٩﴾
49. Ole Siku hiyo kwa wenye kukadhibisha.
فَبِأَيِّ حَدِيثٍ بَعْدَهُ يُؤْمِنُونَ﴿٥٠﴾
50. Basi kauli gani baada ya hii (Qur-aan) wataiamini?
0 Comments