الْقِيَامَة
Al-Qiyaamah: 75
بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ
لَا أُقْسِمُ بِيَوْمِ الْقِيَامَةِ﴿١﴾
1. Naapa kwa siku ya Qiyaamah.
وَلَا أُقْسِمُ بِالنَّفْسِ اللَّوَّامَةِ﴿٢﴾
2. Na Naapa kwa nafsi inayojilaumu sana.
أَيَحْسَبُ الْإِنسَانُ أَلَّن نَّجْمَعَ عِظَامَهُ﴿٣﴾
3. Je, anadhani insani kwamba Hatutoikusanya mifupa yake?
بَلَىٰ قَادِرِينَ عَلَىٰ أَن نُّسَوِّيَ بَنَانَهُ﴿٤﴾
4. Ndio! Tuna uwezo wa kusawazisha sawasawa ncha za vidole vyake .
بَلْ يُرِيدُ الْإِنسَانُ لِيَفْجُرَ أَمَامَهُ﴿٥﴾
5. Bali anataka insani aendelee kutenda dhambi na kukanusha umri wake ulobakia.
يَسْأَلُ أَيَّانَ يَوْمُ الْقِيَامَةِ﴿٦﴾
6. Anauliza ni lini hiyo siku ya Qiyaamah?
فَإِذَا بَرِقَ الْبَصَرُ﴿٧﴾
7. Basi jicho litakapoduwaa.
وَخَسَفَ الْقَمَرُ﴿٨﴾
8. Na mwezi utakapopatwa.
وَجُمِعَ الشَّمْسُ وَالْقَمَرُ﴿٩﴾
9. Na itakapojumuishwa jua na mwezi.
يَقُولُ الْإِنسَانُ يَوْمَئِذٍ أَيْنَ الْمَفَرُّ﴿١٠﴾
10. Atasema insani siku hiyo: “Wapi pa kukimbilia?”
كَلَّا لَا وَزَرَ﴿١١﴾
11. Laa hasha! Hapana mahali pa kimbilio.
إِلَىٰ رَبِّكَ يَوْمَئِذٍ الْمُسْتَقَرُّ﴿١٢﴾
12. Kwa Rabb wako siku hiyo ndio makazi ya kustakiri.
يُنَبَّأُ الْإِنسَانُ يَوْمَئِذٍ بِمَا قَدَّمَ وَأَخَّرَ﴿١٣﴾
13. Siku hiyo insani atajulishwa yale aliyoyakadimisha na aliyoyaakhirisha.
بَلِ الْإِنسَانُ عَلَىٰ نَفْسِهِ بَصِيرَةٌ﴿١٤﴾
14. Bali insani ni shahidi dhidi ya nafsi yake.
وَلَوْ أَلْقَىٰ مَعَاذِيرَهُ﴿١٥﴾
15. Japo akitoa nyudhuru.
لَا تُحَرِّكْ بِهِ لِسَانَكَ لِتَعْجَلَ بِهِ﴿١٦﴾
16. Usitikise lisani yako ili kuiharakiza (Qur-aan ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم).
إِنَّ عَلَيْنَا جَمْعَهُ وَقُرْآنَهُ﴿١٧﴾
17. Hakika ni juu Yetu kuikusanya na kukuwezesha kuisoma kwake.
فَإِذَا قَرَأْنَاهُ فَاتَّبِعْ قُرْآنَهُ﴿١٨﴾
18. Basi Tunapoisoma (kupitia Jibriyl), fuata kusomwa kwake.
ثُمَّ إِنَّ عَلَيْنَا بَيَانَهُ﴿١٩﴾
19. Kisha ni juu Yetu kuibainisha (kwako).
كَلَّا بَلْ تُحِبُّونَ الْعَاجِلَةَ﴿٢٠﴾
20. Laa hasha! Bali mnapenda uhai wa dunia.
وَتَذَرُونَ الْآخِرَةَ﴿٢١﴾
21. Na mnaiacha Aakhirah.
وُجُوهٌ يَوْمَئِذٍ نَّاضِرَةٌ﴿٢٢﴾
22. Nyuso siku hiyo zitanawiri.
إِلَىٰ رَبِّهَا نَاظِرَةٌ﴿٢٣﴾
23. Zikimtazama Rabb wake.
وَوُجُوهٌ يَوْمَئِذٍ بَاسِرَةٌ﴿٢٤﴾
24. Na nyuso (nyenginezo) siku hiyo zitakunjana.
تَظُنُّ أَن يُفْعَلَ بِهَا فَاقِرَةٌ﴿٢٥﴾
25. Zikiwa na yakini kuwa zitafikiwa na msiba unaovunja uti wa mgongo.
كَلَّا إِذَا بَلَغَتِ التَّرَاقِيَ﴿٢٦﴾
26. Laa hasha! Itakapofika (roho) mafupa ya koo.
وَقِيلَ مَنْ ۜ رَاقٍ﴿٢٧﴾
27. Na itasemwa: “Ni nani tabibu wa kumponya?”
وَظَنَّ أَنَّهُ الْفِرَاقُ﴿٢٨﴾
28. Na atakuwa na yakini kwamba hakika hivyo ni kufariki.
وَالْتَفَّتِ السَّاقُ بِالسَّاقِ﴿٢٩﴾
29. Na utakapombatanishwa muundi kwa muundi.
إِلَىٰ رَبِّكَ يَوْمَئِذٍ الْمَسَاقُ﴿٣٠﴾
30. Siku hiyo kuendeshwa ni kwa Rabb wako tu.
فَلَا صَدَّقَ وَلَا صَلَّىٰ﴿٣١﴾
31. Kwani hakusadiki (Qur-aan na Rasuli) na wala hakuswali.
وَلَـٰكِن كَذَّبَ وَتَوَلَّىٰ﴿٣٢﴾
32. Lakini alikadhibisha na akakengeuka.
ثُمَّ ذَهَبَ إِلَىٰ أَهْلِهِ يَتَمَطَّىٰ﴿٣٣﴾
33. Kisha akaenda kwa watu wake akijigamba.
أَوْلَىٰ لَكَ فَأَوْلَىٰ﴿٣٤﴾
34. Ole kwako! Tena ole kwako (ewe kafiri)!
ثُمَّ أَوْلَىٰ لَكَ فَأَوْلَىٰ﴿٣٥﴾
35. Kisha ole kwako! Tena ole kwako!
أَيَحْسَبُ الْإِنسَانُ أَن يُتْرَكَ سُدًى﴿٣٦﴾
36. Je, anadhani insani ataachwa huru bila jukumu?
أَلَمْ يَكُ نُطْفَةً مِّن مَّنِيٍّ يُمْنَىٰ﴿٣٧﴾
37. Kwani hakuwa tone kutokana na manii yanayomwagwa kwa nguvu?
ثُمَّ كَانَ عَلَقَةً فَخَلَقَ فَسَوَّىٰ﴿٣٨﴾
38. Kisha akawa pande la damu, (Allaah) Akamuumba na Akamsawazisha?
فَجَعَلَ مِنْهُ الزَّوْجَيْنِ الذَّكَرَ وَالْأُنثَىٰ﴿٣٩﴾
39. Akamfanya namna mbili; mwanamume na mwanamke?
أَلَيْسَ ذَٰلِكَ بِقَادِرٍ عَلَىٰ أَن يُحْيِيَ الْمَوْتَىٰ﴿٤٠﴾
40. Je hivyo sivyo (Allaah Anayeumba) kuwa ni Muweza wa kuhuisha wafu?
0 Comments