نُوح
Nuwh: 71
بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ
إِنَّا أَرْسَلْنَا نُوحًا إِلَىٰ قَوْمِهِ أَنْ أَنذِرْ قَوْمَكَ مِن قَبْلِ أَن يَأْتِيَهُمْ عَذَابٌ أَلِيمٌ﴿١﴾
1. Hakika Sisi Tumemtuma Nuwh kwa kaumu yake kwamba: waonye watu wako kabla haijawafikia adhabu iumiazyo.
قَالَ يَا قَوْمِ إِنِّي لَكُمْ نَذِيرٌ مُّبِينٌ﴿٢﴾
2. (Nuwh) Akasema: “Enyi kaumu yangu! Hakika mimi kwenu ni mwonyaji bayana.
أَنِ اعْبُدُوا اللَّـهَ وَاتَّقُوهُ وَأَطِيعُونِ﴿٣﴾
3. “Kwamba muabuduni Allaah, na mcheni, na mnitii.
يَغْفِرْ لَكُم مِّن ذُنُوبِكُمْ وَيُؤَخِّرْكُمْ إِلَىٰ أَجَلٍ مُّسَمًّى ۚ إِنَّ أَجَلَ اللَّـهِ إِذَا جَاءَ لَا يُؤَخَّرُ ۖ لَوْ كُنتُمْ تَعْلَمُونَ﴿٤﴾
4. “(Allaah) Atakughufurieni madhambi yenu, na Atakuakhirisheni mpaka muda maalumu uliokadiriwa. Hakika muda uliokadiriwa na Allaah utakapokuja hautoakhirishwa, lau kama mtakuwa mnajua.”
قَالَ رَبِّ إِنِّي دَعَوْتُ قَوْمِي لَيْلًا وَنَهَارًا﴿٥﴾
5. (Nuwh) Akasema: “Rabb wangu! Hakika mimi nimewalingania watu wangu usiku na mchana.
فَلَمْ يَزِدْهُمْ دُعَائِي إِلَّا فِرَارًا﴿٦﴾
6. “Lakini haikuwazidishia wito wangu isipokuwa kukimbia.
وَإِنِّي كُلَّمَا دَعَوْتُهُمْ لِتَغْفِرَ لَهُمْ جَعَلُوا أَصَابِعَهُمْ فِي آذَانِهِمْ وَاسْتَغْشَوْا ثِيَابَهُمْ وَأَصَرُّوا وَاسْتَكْبَرُوا اسْتِكْبَارًا﴿٧﴾
7. “Na hakika mimi kila nilipowaita ili Uwaghufurie; huweka vidole vyao masikioni mwao na wakagubika nguo zao na wakashikilia (kukanusha) wakatakabari kwa majivuno makubwa.
ثُمَّ إِنِّي دَعَوْتُهُمْ جِهَارًا﴿٨﴾
8. “Kisha hakika mimi niliwalingania kwa waziwazi.
ثُمَّ إِنِّي أَعْلَنتُ لَهُمْ وَأَسْرَرْتُ لَهُمْ إِسْرَارًا﴿٩﴾
9. “Kisha hakika mimi nikawatangazia na nikawasemesha kwa siri.
فَقُلْتُ اسْتَغْفِرُوا رَبَّكُمْ إِنَّهُ كَانَ غَفَّارًا﴿١٠﴾
10. Nikasema: “Ombeni maghfirah kwa Rabb wenu; hakika Yeye ni Mwingi mno wa kughufuria.
يُرْسِلِ السَّمَاءَ عَلَيْكُم مِّدْرَارًا﴿١١﴾
11. “Atakutumieni mvua tele ya kuendelea.”
وَيُمْدِدْكُم بِأَمْوَالٍ وَبَنِينَ وَيَجْعَل لَّكُمْ جَنَّاتٍ وَيَجْعَل لَّكُمْ أَنْهَارًا﴿١٢﴾
12. “Na Atakuongezeeni mali na wana, na Atakupeni mabustani na Atakupeni mito.”
مَّا لَكُمْ لَا تَرْجُونَ لِلَّـهِ وَقَارًا﴿١٣﴾
13. Mna nini hamtaraji na hamkhofu taadhima ya Allaah?
وَقَدْ خَلَقَكُمْ أَطْوَارًا﴿١٤﴾
14. Na hali Amekuumbeni hatua baada ya hatua?
أَلَمْ تَرَوْا كَيْفَ خَلَقَ اللَّـهُ سَبْعَ سَمَاوَاتٍ طِبَاقًا﴿١٥﴾
15. Je, hamuoni vipi Allaah Ameumba mbingu saba tabaka tabaka?
وَجَعَلَ الْقَمَرَ فِيهِنَّ نُورًا وَجَعَلَ الشَّمْسَ سِرَاجًا﴿١٦﴾
16. Na Akaufanya mwezi ndani yake uwe nuru, na Akalifanya jua ni taa ya mwanga mkali.
وَاللَّـهُ أَنبَتَكُم مِّنَ الْأَرْضِ نَبَاتًا﴿١٧﴾
17. Na Allaah Amekuanzisheni vizuri katika (udongo wa) ardhi.
ثُمَّ يُعِيدُكُمْ فِيهَا وَيُخْرِجُكُمْ إِخْرَاجًا﴿١٨﴾
18. Kisha Atakurudisheni humo na Atakutoeni tena mtoke (kuwa hai).
وَاللَّـهُ جَعَلَ لَكُمُ الْأَرْضَ بِسَاطًا﴿١٩﴾
19. Na Allaah Amekufanyieni ardhi kuwa (kama) busati.
لِّتَسْلُكُوا مِنْهَا سُبُلًا فِجَاجًا﴿٢٠﴾
20. Ili mpite humo njia pana.
قَالَ نُوحٌ رَّبِّ إِنَّهُمْ عَصَوْنِي وَاتَّبَعُوا مَن لَّمْ يَزِدْهُ مَالُهُ وَوَلَدُهُ إِلَّا خَسَارًا﴿٢١﴾
21. Nuwh Akasema: “Rabb wangu! Hakika wao wameniasi, na wakafuata yule ambaye mali yake na watoto wake hawakumzidishia isipokuwa khasara.
وَمَكَرُوا مَكْرًا كُبَّارًا﴿٢٢﴾
22. “Na wakapanga njama kubwa mno.
وَقَالُوا لَا تَذَرُنَّ آلِهَتَكُمْ وَلَا تَذَرُنَّ وَدًّا وَلَا سُوَاعًا وَلَا يَغُوثَ وَيَعُوقَ وَنَسْرًا﴿٢٣﴾
23. Wakasema: “Msiwaache waabudiwa wenu; na wala msimwache Waddaa, na wala Su’waa’a, na wala Yaghuwtha, na Ya’uwqa, na Nasraa.”[1]
وَقَدْ أَضَلُّوا كَثِيرًا ۖ وَلَا تَزِدِ الظَّالِمِينَ إِلَّا ضَلَالًا﴿٢٤﴾
24. “Na wamekwishawapoteza wengi. Na wala Usiwazidishie madhalimu isipokuwa upotofu.”
مِّمَّا خَطِيئَاتِهِمْ أُغْرِقُوا فَأُدْخِلُوا نَارًا فَلَمْ يَجِدُوا لَهُم مِّن دُونِ اللَّـهِ أَنصَارًا﴿٢٥﴾
25. Kutokana na hatia zao; walizamishwa, kisha wakaingizwa motoni, basi hawakupata mwenye kuwanusuru yeyote yule badala ya Allaah.
وَقَالَ نُوحٌ رَّبِّ لَا تَذَرْ عَلَى الْأَرْضِ مِنَ الْكَافِرِينَ دَيَّارًا﴿٢٦﴾
26. Na Nuwh akasema tena: “Rabb wangu! Usimwache juu ya ardhi mkaazi yeyote yule kati ya makafiri.
إِنَّكَ إِن تَذَرْهُمْ يُضِلُّوا عِبَادَكَ وَلَا يَلِدُوا إِلَّا فَاجِرًا كَفَّارًا﴿٢٧﴾
27. “Hakika Wewe Ukiwaacha, watawapoteza waja Wako, na wala hawatozaa isipokuwa mtendaji dhambi, kafiri mkanushaji mno.
رَّبِّ اغْفِرْ لِي وَلِوَالِدَيَّ وَلِمَن دَخَلَ بَيْتِيَ مُؤْمِنًا وَلِلْمُؤْمِنِينَ وَالْمُؤْمِنَاتِ وَلَا تَزِدِ الظَّالِمِينَ إِلَّا تَبَارًا﴿٢٨﴾
28. “Rabb wangu! Nighufurie, na wazazi wangu wawili, na kila aliyeingia nyumbani mwangu mwenye kuamini, na Waumini wa kiume na Waumini wa kike, na wala Usiwazidishie madhalimu isipokuwa kuteketea kabisa.
[1] Waddaa, Su’waa’a, Yaghuwtha, Ya’uwqa, Nasraa: Majina ya masanamu waliyokuwa wakiyaabudu watu wa Nabiy Nuwh (عليه السلام)
0 Comments