الْمَعَارِج
Al-Ma’aarij: 70



بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ


سَأَلَ سَائِلٌ بِعَذَابٍ وَاقِعٍ﴿١﴾
1. Muulizaji ameuliza kuhusu adhabu itakayotokea.


لِّلْكَافِرِينَ لَيْسَ لَهُ دَافِعٌ﴿٢﴾
2. Kwa makafiri, ambayo hakuna wa kuikinga.


مِّنَ اللَّـهِ ذِي الْمَعَارِجِ﴿٣﴾
3. Kutoka kwa Allaah Mwenye kumiliki njia za kupandia.


تَعْرُجُ الْمَلَائِكَةُ وَالرُّوحُ إِلَيْهِ فِي يَوْمٍ كَانَ مِقْدَارُهُ خَمْسِينَ أَلْفَ سَنَةٍ﴿٤﴾
4. Malaika na Ar-Ruwh (roho za viumbe au Jibriyl) wanapanda Kwake katika siku kadiri yake ni miaka khamsini elfu.


فَاصْبِرْ صَبْرًا جَمِيلًا﴿٥﴾
5. Basi subiri, subira njema (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم).


إِنَّهُمْ يَرَوْنَهُ بَعِيدًا﴿٦﴾
6. Hakika wao wanaiona (adhabu, Qiyaamah) iko mbali.


وَنَرَاهُ قَرِيبًا﴿٧﴾
7. Nasi Tunaiona  ikaribu.

يَوْمَ تَكُونُ السَّمَاءُ كَالْمُهْلِ﴿٨﴾
8. Siku mbingu zitapokuwa kama masazo ya zebaki nyeusi ziliyoyeyushwa.


وَتَكُونُ الْجِبَالُ كَالْعِهْنِ﴿٩﴾
9. Na majabali yatakuwa kama sufi iliyochambuliwa.


وَلَا يَسْأَلُ حَمِيمٌ حَمِيمًا﴿١٠﴾
10.  Na wala rafiki wadhati hatomuuliza rafiki yake wa dhati. 


يُبَصَّرُونَهُمْ ۚ يَوَدُّ الْمُجْرِمُ لَوْ يَفْتَدِي مِنْ عَذَابِ يَوْمِئِذٍ بِبَنِيهِ﴿١١﴾
11. Watafanywa waonane. Mhalifu atatamani ajitolee fidia kutokana na adhabu Siku hiyo kwa watoto wake.

وَصَاحِبَتِهِ وَأَخِيهِ﴿١٢﴾
12. Na mkewe na nduguye.


وَفَصِيلَتِهِ الَّتِي تُؤْوِيهِ﴿١٣﴾
13. Na jamaa zake wa karibu ambao wakimpa hifadhi na makazi.


وَمَن فِي الْأَرْضِ جَمِيعًا ثُمَّ يُنجِيهِ﴿١٤﴾
14. Na wale wote waliomo ardhini, kisha aokoke yeye.


كَلَّا ۖ إِنَّهَا لَظَىٰ﴿١٥﴾
15. Laa hasha! Hakika huo ni moto wenye mwako mkali.


نَزَّاعَةً لِّلشَّوَىٰ﴿١٦﴾
16. Unyofoao kwa nguvu na kuunguza kikamilifu ngozi ya kichwa na viungo vya mwili.


تَدْعُو مَنْ أَدْبَرَ وَتَوَلَّىٰ﴿١٧﴾
17. Utamwita yule aliyegeuza mgongo na akakengeuka.

وَجَمَعَ فَأَوْعَىٰ﴿١٨﴾
18. Na akakusanya (mali) kisha akayahifadhi katika makasha.


إِنَّ الْإِنسَانَ خُلِقَ هَلُوعًا﴿١٩﴾
19. Hakika insani ameumbwa ni mwenye kukosa subira na mwingi wa pupa.


إِذَا مَسَّهُ الشَّرُّ جَزُوعًا﴿٢٠﴾
20. Inapomgusa shari, anakuwa mwingi wa kusononeka, kupapatika na kuhuzunika.


وَإِذَا مَسَّهُ الْخَيْرُ مَنُوعًا﴿٢١﴾
21. Na inapomgusa kheri, mwingi wa kuzuia (kwa uchoyo).


إِلَّا الْمُصَلِّينَ﴿٢٢﴾
22. Isipokuwa wenye kuswali.


الَّذِينَ هُمْ عَلَىٰ صَلَاتِهِمْ دَائِمُونَ﴿٢٣﴾
23. Ambao wenye kudumisha Swalaah zao.


وَالَّذِينَ فِي أَمْوَالِهِمْ حَقٌّ مَّعْلُومٌ﴿٢٤﴾
24. Na wale ambao katika mali zao kuna haki maalumu.


لِّلسَّائِلِ وَالْمَحْرُومِ﴿٢٥﴾
25. Kwa ajili ya muombaji na asiyeomba kwa kujistahi


وَالَّذِينَ يُصَدِّقُونَ بِيَوْمِ الدِّينِ﴿٢٦﴾
26. Na ambao wanasadikisha Siku ya Malipo.


وَالَّذِينَ هُم مِّنْ عَذَابِ رَبِّهِم مُّشْفِقُونَ﴿٢٧﴾
27. Na wale wanaiogopa adhabu kutoka kwa Rabb wao.


إِنَّ عَذَابَ رَبِّهِمْ غَيْرُ مَأْمُونٍ﴿٢٨﴾
28. Hakika adhabu ya Rabb wao si ya kusalimika nayo. 


وَالَّذِينَ هُمْ لِفُرُوجِهِمْ حَافِظُونَ﴿٢٩﴾
29. Na ambao wanahifadhi tupu zao.


إِلَّا عَلَىٰ أَزْوَاجِهِمْ أَوْ مَا مَلَكَتْ أَيْمَانُهُمْ فَإِنَّهُمْ غَيْرُ مَلُومِينَ﴿٣٠﴾
30. Isipokuwa kwa wake zao, au wale iliyowamiliki mikono yao ya kuume, basi hao si wenye kulaumiwa.


فَمَنِ ابْتَغَىٰ وَرَاءَ ذَٰلِكَ فَأُولَـٰئِكَ هُمُ الْعَادُونَ﴿٣١﴾
31. Basi yeyote yule atakayetaka kinyume ya hayo, basi hao ndio warukao mipaka.


وَالَّذِينَ هُمْ لِأَمَانَاتِهِمْ وَعَهْدِهِمْ رَاعُونَ﴿٣٢﴾
32. Na ambao amana zao na ahadi zao ni wenye kuchunga (na kuzitimiza).


وَالَّذِينَ هُم بِشَهَادَاتِهِمْ قَائِمُونَ﴿٣٣﴾
33. Na ambao katika ushahidi wao ni wenye kusimamisha imara.


وَالَّذِينَ هُمْ عَلَىٰ صَلَاتِهِمْ يُحَافِظُونَ﴿٣٤﴾
34. Na ambao kwenye Swalaah zao ni wenye kuhifadhi.


أُولَـٰئِكَ فِي جَنَّاتٍ مُّكْرَمُونَ﴿٣٥﴾
35. Hao watakuwa kwenye Jannah wakikirimiwa.


فَمَالِ الَّذِينَ كَفَرُوا قِبَلَكَ مُهْطِعِينَ﴿٣٦﴾
36. Basi wana nini waliokufuru wanaharakiza mbele yako wakinyosha shingo zao na kukukodolea macho (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم)?

عَنِ الْيَمِينِ وَعَنِ الشِّمَالِ عِزِينَ﴿٣٧﴾
37. (Kukukalia) makundi kwa makundi kuliani na kushotoni.


أَيَطْمَعُ كُلُّ امْرِئٍ مِّنْهُمْ أَن يُدْخَلَ جَنَّةَ نَعِيمٍ﴿٣٨﴾
38. Je, anatumai kila mtu miongoni mwao kwamba ataingizwa Jannah ya neema?


كَلَّا ۖ إِنَّا خَلَقْنَاهُم مِّمَّا يَعْلَمُونَ﴿٣٩﴾
39. Laa, hasha!  Hakika Sisi Tumewaumba kutokana na kile wanachokijua.


فَلَا أُقْسِمُ بِرَبِّ الْمَشَارِقِ وَالْمَغَارِبِ إِنَّا لَقَادِرُونَ﴿٤٠﴾
40. Basi Naapa kwa Rabb wa Mashariki na Magharibi, hakika Sisi bila shaka ni Wenye kuweza.


عَلَىٰ أَن نُّبَدِّلَ خَيْرًا مِّنْهُمْ وَمَا نَحْنُ بِمَسْبُوقِينَ﴿٤١﴾
41. Kwamba Tuwabadilishe walio bora kuliko kwao, Nasi Hatushindwi.


فَذَرْهُمْ يَخُوضُوا وَيَلْعَبُوا حَتَّىٰ يُلَاقُوا يَوْمَهُمُ الَّذِي يُوعَدُونَ﴿٤٢﴾
42. Basi waachilie mbali watumbukie katika porojo na upuuzi na wacheze, mpaka wakutane na Siku yao ambayo wanaahidiwa.


يَوْمَ يَخْرُجُونَ مِنَ الْأَجْدَاثِ سِرَاعًا كَأَنَّهُمْ إِلَىٰ نُصُبٍ يُوفِضُونَ﴿٤٣﴾
43. Siku watapotoka makaburini haraka haraka kama kwamba wanakimbilia golini.


خَاشِعَةً أَبْصَارُهُمْ تَرْهَقُهُمْ ذِلَّةٌ ۚ ذَٰلِكَ الْيَوْمُ الَّذِي كَانُوا يُوعَدُونَ﴿٤٤﴾
44. Macho yao yatainama chini, udhalilifu utawafunika. Hiyo ndio ile siku waliyokuwa wakiahidiwa.