التَّغَابُن
At-Taghaabun: 64
بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ
يُسَبِّحُ لِلَّـهِ مَا فِي السَّمَاوَاتِ وَمَا فِي الْأَرْضِ ۖ لَهُ الْمُلْكُ وَلَهُ الْحَمْدُ ۖ وَهُوَ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ﴿١﴾
1. Vinamsabbih Allaah Pekee vilivyomo katika mbingu vilivyomo katika ardhi, ufalme ni Wake Pekee na Himidi ni Zake Pekee. Naye juu ya kila kitu ni Muweza.
هُوَ الَّذِي خَلَقَكُمْ فَمِنكُمْ كَافِرٌ وَمِنكُم مُّؤْمِنٌ ۚ وَاللَّـهُ بِمَا تَعْمَلُونَ بَصِيرٌ﴿٢﴾
2. Yeye Ndiye Ambaye Amekuumbeni, basi miongoni mwenu aliye kafiri na miongoni mwenu aliye Muumini. Na Allaah kwa yale myatendayo ni Mwenye kuona.
خَلَقَ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ بِالْحَقِّ وَصَوَّرَكُمْ فَأَحْسَنَ صُوَرَكُمْ ۖ وَإِلَيْهِ الْمَصِيرُ﴿٣﴾
3. Ameumba mbingu na ardhi kwa haki, na Akakutengenezeni sura, kisha Akafanya nzuri zaidi sura zenu, na Kwake ndio mahali pa kuishia.
يَعْلَمُ مَا فِي السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ وَيَعْلَمُ مَا تُسِرُّونَ وَمَا تُعْلِنُونَ ۚ وَاللَّـهُ عَلِيمٌ بِذَاتِ الصُّدُورِ﴿٤﴾
4. Anajua yale yaliyomo mbinguni na ardhini, na Anayajua yale mnayofanya siri na mnayoyatangaza. Na Allaah ni Mjuzi wa yaliyomo vifuani.
أَلَمْ يَأْتِكُمْ نَبَأُ الَّذِينَ كَفَرُوا مِن قَبْلُ فَذَاقُوا وَبَالَ أَمْرِهِمْ وَلَهُمْ عَذَابٌ أَلِيمٌ﴿٥﴾
5. Je, haijakufikieni habari ya wale waliokufuru kabla wakaonja matokeo ya uovu wao, na watapata adhabu iumizayo.
ذَٰلِكَ بِأَنَّهُ كَانَت تَّأْتِيهِمْ رُسُلُهُم بِالْبَيِّنَاتِ فَقَالُوا أَبَشَرٌ يَهْدُونَنَا فَكَفَرُوا وَتَوَلَّوا ۚ وَّاسْتَغْنَى اللَّـهُ ۚ وَاللَّـهُ غَنِيٌّ حَمِيدٌ﴿٦﴾
6. Hivyo kwa sababu ilikuwa wakiwafikia Rusuli wao kwa hoja bayana wakasema: “Ah! Binaadamu ndio watuongoze?” Basi wakakufuru na wakakengeuka; na Allaah Akawa hana haja nao, na Allaah ni Mkwasi, Mwenye kustahiki kuhimidiwa kwa yote.
زَعَمَ الَّذِينَ كَفَرُوا أَن لَّن يُبْعَثُوا ۚ قُلْ بَلَىٰ وَرَبِّي لَتُبْعَثُنَّ ثُمَّ لَتُنَبَّؤُنَّ بِمَا عَمِلْتُمْ ۚ وَذَٰلِكَ عَلَى اللَّـهِ يَسِيرٌ﴿٧﴾
7. Waliokufuru wamedai kwamba hawatofufuliwa kamwe. Sema: Bali hapana! Naapa kwa Rabb wangu, bila shaka mtafufuliwa, kisha mtajulishwa kwa yale mliyoyatenda, na hayo kwa Allaah ni mepesi.
فَآمِنُوا بِاللَّـهِ وَرَسُولِهِ وَالنُّورِ الَّذِي أَنزَلْنَا ۚ وَاللَّـهُ بِمَا تَعْمَلُونَ خَبِيرٌ﴿٨﴾
8. Basi muaminini Allaah na Rasuli Wake na Nuru (Qur-aan) Tuliyoiteremsha, na Allaah kwa yale myatendayo ni Mwenye upeo wa khabari za dhahiri na za kufichika.
يَوْمَ يَجْمَعُكُمْ لِيَوْمِ الْجَمْعِ ۖ ذَٰلِكَ يَوْمُ التَّغَابُنِ ۗ وَمَن يُؤْمِن بِاللَّـهِ وَيَعْمَلْ صَالِحًا يُكَفِّرْ عَنْهُ سَيِّئَاتِهِ وَيُدْخِلْهُ جَنَّاتٍ تَجْرِي مِن تَحْتِهَا الْأَنْهَارُ خَالِدِينَ فِيهَا أَبَدًا ۚ ذَٰلِكَ الْفَوْزُ الْعَظِيمُ﴿٩﴾
9. Siku Atakayokukusanyeni kwa ajili ya Siku ya mkusanyiko. Hiyo ndio Siku ya At-Taghaabun: kupata na kukosa. Basi yeyote anayemuamini Allaah na akatenda mema (Allaah) Atamfutia maovu yake na Atamuingiza Jannaat zipitazo chini yake mito ni wenye kudumu humo abadi. Huko ndiko kufuzu adhimu.
وَالَّذِينَ كَفَرُوا وَكَذَّبُوا بِآيَاتِنَا أُولَـٰئِكَ أَصْحَابُ النَّارِ خَالِدِينَ فِيهَا ۖ وَبِئْسَ الْمَصِيرُ﴿١٠﴾
10. Na wale waliokufuru na wakakadhibisha Aayaat (na ishara, dalili) Zetu hao ndio watu wa motoni ni wenye kudumu humo, na ubaya ulioje mahali pa kuishia.
مَا أَصَابَ مِن مُّصِيبَةٍ إِلَّا بِإِذْنِ اللَّـهِ ۗ وَمَن يُؤْمِن بِاللَّـهِ يَهْدِ قَلْبَهُ ۚ وَاللَّـهُ بِكُلِّ شَيْءٍ عَلِيمٌ﴿١١﴾
11. Hausibu msiba wowote isipokuwa kwa idhini ya Allaah. Na yeyote anayemuamini Allaah, (Allaah) Huuongoza moyo wake. Na Allaah kwa kila kitu ni Mjuzi.
وَأَطِيعُوا اللَّـهَ وَأَطِيعُوا الرَّسُولَ ۚ فَإِن تَوَلَّيْتُمْ فَإِنَّمَا عَلَىٰ رَسُولِنَا الْبَلَاغُ الْمُبِينُ﴿١٢﴾
12. Na mtiini Allaah na mtiini Rasuli, lakini mkikengeuka, basi hakika ni juu ya Rasuli Wetu ni ubalighisho (wa ujumbe) bayana.
اللَّـهُ لَا إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ ۚ وَعَلَى اللَّـهِ فَلْيَتَوَكَّلِ الْمُؤْمِنُونَ﴿١٣﴾
13. Allaah, hakuna Muabudiwa wa haki ila Yeye. Na kwa Allaah watawakali Waumini.
يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا إِنَّ مِنْ أَزْوَاجِكُمْ وَأَوْلَادِكُمْ عَدُوًّا لَّكُمْ فَاحْذَرُوهُمْ ۚ وَإِن تَعْفُوا وَتَصْفَحُوا وَتَغْفِرُوا فَإِنَّ اللَّـهَ غَفُورٌ رَّحِيمٌ﴿١٤﴾
14. Enyi walioamini! Hakika miongoni mwa wake zenu na watoto wenu ni maadui kwenu, basi tahadharini nao. Na mkisamehe na mkapuuza na mkayafutilia mbali, basi hakika Allaah ni Mwingi wa kughufuria, Mwenye kurehemu.
إِنَّمَا أَمْوَالُكُمْ وَأَوْلَادُكُمْ فِتْنَةٌ ۚ وَاللَّـهُ عِندَهُ أَجْرٌ عَظِيمٌ﴿١٥﴾
15. Hakika mali zenu na watoto wenu ni jaribio. Na kwa Allaah kuna ujira adhimu.
فَاتَّقُوا اللَّـهَ مَا اسْتَطَعْتُمْ وَاسْمَعُوا وَأَطِيعُوا وَأَنفِقُوا خَيْرًا لِّأَنفُسِكُمْ ۗ وَمَن يُوقَ شُحَّ نَفْسِهِ فَأُولَـٰئِكَ هُمُ الْمُفْلِحُونَ﴿١٦﴾
16. Basi mcheni Allaah muwezavyo, na sikilizeni; na tiini na toeni (kwa ajili ya Allaah) ni kheri kwa ajili ya nafsi zenu. Na yeyote anayeepushwa na ubakhili na tamaa ya uchu wa nafsi yake, basi hao ndio wenye kufaulu.
إِن تُقْرِضُوا اللَّـهَ قَرْضًا حَسَنًا يُضَاعِفْهُ لَكُمْ وَيَغْفِرْ لَكُمْ ۚ وَاللَّـهُ شَكُورٌ حَلِيمٌ﴿١٧﴾
17. Mkimkopesha Allaah karadhi mzuri, Atakuzidishieni maradufu, na Atakughufurieni. Na Allaah ni Mwenye kupokea shukurani, Mpole wa kuwavumilia waja.
عَالِمُ الْغَيْبِ وَالشَّهَادَةِ الْعَزِيزُ الْحَكِيمُ﴿١٨﴾
18. Mjuzi wa ghayb na dhahiri, Mwenye enzi ya nguvu Asiyeshindika, Mwenye hikmah wa yote.
0 Comments