الْمُمْتَحِنَة
Al-Mumtahinah: 60
بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ
يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا تَتَّخِذُوا عَدُوِّي وَعَدُوَّكُمْ أَوْلِيَاءَ تُلْقُونَ إِلَيْهِم بِالْمَوَدَّةِ وَقَدْ كَفَرُوا بِمَا جَاءَكُم مِّنَ الْحَقِّ يُخْرِجُونَ الرَّسُولَ وَإِيَّاكُمْ ۙ أَن تُؤْمِنُوا بِاللَّـهِ رَبِّكُمْ إِن كُنتُمْ خَرَجْتُمْ جِهَادًا فِي سَبِيلِي وَابْتِغَاءَ مَرْضَاتِي ۚ تُسِرُّونَ إِلَيْهِم بِالْمَوَدَّةِ وَأَنَا أَعْلَمُ بِمَا أَخْفَيْتُمْ وَمَا أَعْلَنتُمْ ۚ وَمَن يَفْعَلْهُ مِنكُمْ فَقَدْ ضَلَّ سَوَاءَ السَّبِيلِ﴿١﴾
1. Enyi walioamini! Msifanye adui Wangu na adui wenu kuwa marafiki wandani mkiwapa mapenzi, na hali wamekwishakufuru yaliyokujieni ya haki; wanamfukuza Rasuli pamoja nanyi kwa sababu mmemuamini Allaah Rabb wenu; Mnapotoka kwa ajili ya jihaad katika njia Yangu na kutafuta radhi Zangu mnawapa siri kwa mapenzi, na hali Mimi Najua zaidi yale mnayoyaficha na yale mnayoyadhihirisha. Na yeyote atakayefanya hivyo miongoni mwenu, basi kwa yakini amepotea njia ya sawa.
إِن يَثْقَفُوكُمْ يَكُونُوا لَكُمْ أَعْدَاءً وَيَبْسُطُوا إِلَيْكُمْ أَيْدِيَهُمْ وَأَلْسِنَتَهُم بِالسُّوءِ وَوَدُّوا لَوْ تَكْفُرُونَ﴿٢﴾
2. Wakikushindeni watakuwa ni maadui kwenu, na watakunyosheeni mikono yao na ndimi zao kwa uovu, na watatamani lau mngekufuru.
لَن تَنفَعَكُمْ أَرْحَامُكُمْ وَلَا أَوْلَادُكُمْ ۚ يَوْمَ الْقِيَامَةِ يَفْصِلُ بَيْنَكُمْ ۚ وَاللَّـهُ بِمَا تَعْمَلُونَ بَصِيرٌ﴿٣﴾
3. Hawatokufaeni jamaa zenu wa uhusiano wa damu, na wala watoto wenu Siku ya Qiyaamah (Allaah) Atapambanua baina yenu; na Allaah kwa yale myatendayo ni Mwenye kuona.
قَدْ كَانَتْ لَكُمْ أُسْوَةٌ حَسَنَةٌ فِي إِبْرَاهِيمَ وَالَّذِينَ مَعَهُ إِذْ قَالُوا لِقَوْمِهِمْ إِنَّا بُرَءَآؤُاْ مِنكُمْ وَمِمَّا تَعْبُدُونَ مِن دُونِ اللَّـهِ كَفَرْنَا بِكُمْ وَبَدَا بَيْنَنَا وَبَيْنَكُمُ الْعَدَاوَةُ وَالْبَغْضَاءُ أَبَدًا حَتَّىٰ تُؤْمِنُوا بِاللَّـهِ وَحْدَهُ إِلَّا قَوْلَ إِبْرَاهِيمَ لِأَبِيهِ لَأَسْتَغْفِرَنَّ لَكَ وَمَا أَمْلِكُ لَكَ مِنَ اللَّـهِ مِن شَيْءٍ ۖ رَّبَّنَا عَلَيْكَ تَوَكَّلْنَا وَإِلَيْكَ أَنَبْنَا وَإِلَيْكَ الْمَصِيرُ﴿٤﴾
4. Kwa yakini mna kigezo kizuri kwa Ibraahiym na wale walio pamoja naye, walipowaambia watu wao: “Hakika sisi tumejitenga nanyi na yale mnayoyaabudu badala ya Allaah, tunakukanusheni, na umedhihirika baina yetu na baina yenu uadui na bughudha abadi mpaka mumuamini Allaah Pekee.” Isipokuwa kauli ya Ibraahiym kwa baba yake: “Nitakuombea maghfirah, na wala sikumilikii chochote kile mbele ya Allaah. Rabb wetu! Tumetawakali Kwako, na Kwako Tunarudia kutubia, na Kwako ni mahali pa kuishia.
رَبَّنَا لَا تَجْعَلْنَا فِتْنَةً لِّلَّذِينَ كَفَرُوا وَاغْفِرْ لَنَا رَبَّنَا ۖ إِنَّكَ أَنتَ الْعَزِيزُ الْحَكِيمُ﴿٥﴾
5. “Rabb wetu! Usitujaalie kuwa mtihani kwa wale waliokufuru, na Tughufurie Rabb wetu; hakika Wewe ni Mwenye enzi ya nguvu Asiyeshindika, Mwenye hikmah wa yote.”
لَقَدْ كَانَ لَكُمْ فِيهِمْ أُسْوَةٌ حَسَنَةٌ لِّمَن كَانَ يَرْجُو اللَّـهَ وَالْيَوْمَ الْآخِرَ ۚ وَمَن يَتَوَلَّ فَإِنَّ اللَّـهَ هُوَ الْغَنِيُّ الْحَمِيدُ﴿٦﴾
6. Kwa yakini imekuwa kwenu kigezo kizuri katika mwenendo wao kwa mwenye kumtaraji Allaah na Siku ya Mwisho. Na yeyote atakayekengeuka, basi hakika Allaah Ndiye Mkwasi, Mwenye kustahiki kuhimidiwa kwa yote.
عَسَى اللَّـهُ أَن يَجْعَلَ بَيْنَكُمْ وَبَيْنَ الَّذِينَ عَادَيْتُم مِّنْهُم مَّوَدَّةً ۚ وَاللَّـهُ قَدِيرٌ ۚ وَاللَّـهُ غَفُورٌ رَّحِيمٌ﴿٧﴾
7. Asaa Allaah Akajaalia mapenzi baina yenu na baina ya wale mlio na uadui nao; na Allaah ni Muweza wa yote, na Allaah ni Mwingi wa kughufuria, Mwenye kurehemu.
لَّا يَنْهَاكُمُ اللَّـهُ عَنِ الَّذِينَ لَمْ يُقَاتِلُوكُمْ فِي الدِّينِ وَلَمْ يُخْرِجُوكُم مِّن دِيَارِكُمْ أَن تَبَرُّوهُمْ وَتُقْسِطُوا إِلَيْهِمْ ۚ إِنَّ اللَّـهَ يُحِبُّ الْمُقْسِطِينَ﴿٨﴾
8. Allaah Hakukatazeni kuwafanyia wema na uadilifu wale wasiokupigeni vita katika Dini, na wala hawakukutoeni kutoka majumbani mwenu. Hakika Allaah Anapenda wafanyao uadilifu.
إِنَّمَا يَنْهَاكُمُ اللَّـهُ عَنِ الَّذِينَ قَاتَلُوكُمْ فِي الدِّينِ وَأَخْرَجُوكُم مِّن دِيَارِكُمْ وَظَاهَرُوا عَلَىٰ إِخْرَاجِكُمْ أَن تَوَلَّوْهُمْ ۚ وَمَن يَتَوَلَّهُمْ فَأُولَـٰئِكَ هُمُ الظَّالِمُونَ﴿٩﴾
9. Hakika Allaah Anakukatazeni tu kuhusu wale waliokupigeni vita katika Dini, na wakakutoeni kutoka majumbani mwenu, na wakasaidiana juu ya kukutoeni ndio msiwafanye urafiki nao. Na yeyote atakayewafanya marafiki, basi hao ndio madhalimu.
يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا إِذَا جَاءَكُمُ الْمُؤْمِنَاتُ مُهَاجِرَاتٍ فَامْتَحِنُوهُنَّ ۖ اللَّـهُ أَعْلَمُ بِإِيمَانِهِنَّ ۖ فَإِنْ عَلِمْتُمُوهُنَّ مُؤْمِنَاتٍ فَلَا تَرْجِعُوهُنَّ إِلَى الْكُفَّارِ ۖ لَا هُنَّ حِلٌّ لَّهُمْ وَلَا هُمْ يَحِلُّونَ لَهُنَّ ۖ وَآتُوهُم مَّا أَنفَقُوا ۚ وَلَا جُنَاحَ عَلَيْكُمْ أَن تَنكِحُوهُنَّ إِذَا آتَيْتُمُوهُنَّ أُجُورَهُنَّ ۚ وَلَا تُمْسِكُوا بِعِصَمِ الْكَوَافِرِ وَاسْأَلُوا مَا أَنفَقْتُمْ وَلْيَسْأَلُوا مَا أَنفَقُوا ۚ ذَٰلِكُمْ حُكْمُ اللَّـهِ ۖ يَحْكُمُ بَيْنَكُمْ ۚ وَاللَّـهُ عَلِيمٌ حَكِيمٌ﴿١٠﴾
10. Enyi walioamini! Wanapokujieni Waumini wa kike Muhaajiraat basi wajaribuni. Allaah Mjuzi zaidi wa iymaan zao. Kisha mkiwatambua kuwa ni Waumini basi msiwarejeshe kwa makafiri. Wao si wake halaal kwao, na wala wao waume hawahalaliki kwao. Na wapeni (makafiri mahari) waliyotoa. Na wala si dhambi kufunga nao nikaah mkiwapa mahari yao. Na wala msiwaweke wanawake makafiri katika fungamano la ndoa; na takeni mlichotoa (katika mahari), nao watake walichotoa. Hiyo ndio hukumu ya Allaah, Anahukumu baina yenu, na Allaah ni Mjuzi wa yote, Mwenye hikmah wa yote.
وَإِن فَاتَكُمْ شَيْءٌ مِّنْ أَزْوَاجِكُمْ إِلَى الْكُفَّارِ فَعَاقَبْتُمْ فَآتُوا الَّذِينَ ذَهَبَتْ أَزْوَاجُهُم مِّثْلَ مَا أَنفَقُوا ۚوَاتَّقُوا اللَّـهَ الَّذِي أَنتُم بِهِ مُؤْمِنُونَ﴿١١﴾
11. Na kama akikutorokeni yeyote kati ya wake zenu kurejea kwa makafiri kisha ikatokea kuwa mmelipiza mkashinda na kupata ngawira, basi wapeni wale walioondokewa na wake zao mfano wa walichotoa (mahari); na mcheni Allaah Ambaye nyinyi Kwake mnamuamini.
يَا أَيُّهَا النَّبِيُّ إِذَا جَاءَكَ الْمُؤْمِنَاتُ يُبَايِعْنَكَ عَلَىٰ أَن لَّا يُشْرِكْنَ بِاللَّـهِ شَيْئًا وَلَا يَسْرِقْنَ وَلَا يَزْنِينَ وَلَا يَقْتُلْنَ أَوْلَادَهُنَّ وَلَا يَأْتِينَ بِبُهْتَانٍ يَفْتَرِينَهُ بَيْنَ أَيْدِيهِنَّ وَأَرْجُلِهِنَّ وَلَا يَعْصِينَكَ فِي مَعْرُوفٍ ۙفَبَايِعْهُنَّ وَاسْتَغْفِرْ لَهُنَّ اللَّـهَ ۖ إِنَّ اللَّـهَ غَفُورٌ رَّحِيمٌ﴿١٢﴾
12. Ee Nabiy! Wakikujia Waumini wa kike wanafungamana nawe ahadi ya utiifu kwamba hawatomshirikisha Allaah na chochote, na wala hawatoiba, na wala hawatozini, na wala hawataua watoto wao, na wala hawatoleta usingiziaji wa kashfa walioizua baina ya mikono yao na miguu yao na wala hawatakuasi katika mema; basi pokea ahadi yao ya utiifu, na waombee maghfirah kwa Allaah. Hakika Allaah ni Mwingi wa kughufuria, Mwenye kurehemu.
يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا تَتَوَلَّوْا قَوْمًا غَضِبَ اللَّـهُ عَلَيْهِمْ قَدْ يَئِسُوا مِنَ الْآخِرَةِ كَمَا يَئِسَ الْكُفَّارُ مِنْأَصْحَابِ الْقُبُورِ﴿١٣﴾
13. Enyi walioamini! Msiwafanye marafiki watu ambao Allaah Amewaghadhibikia, wamekwishakata tamaa na (thawabu za) Aakhirah kama walivyokwishakata tamaa makafiri na watu wa makaburini.
0 Comments