الْحَدِيد
Al-Hadiyd: 57



بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ



سَبَّحَ لِلَّـهِ مَا فِي السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ ۖ وَهُوَ الْعَزِيزُ الْحَكِيمُ ﴿١﴾
1. Vimemsabbi Allaah Pekee vilivyomo katika mbingu na ardhi Naye Ndiye Mwenye enzi ya nguvu Asiyeshindika, Mwenye hikmah wa yote.


لَهُ مُلْكُ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ ۖ يُحْيِي وَيُمِيتُ ۖ وَهُوَ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ ﴿٢﴾
2. Ni Wake Pekee ufalme wa mbingu na ardhi, Anahuisha na Anafisha, Naye juu ya kila kitu ni Muweza.


هُوَ الْأَوَّلُ وَالْآخِرُ وَالظَّاهِرُ وَالْبَاطِنُ ۖ وَهُوَ بِكُلِّ شَيْءٍ عَلِيمٌ ﴿٣﴾
3. Yeye Ndiye wa Awali hakuna kitu kabla Yake, na wa Mwisho hakuna kitu baada Yake, na Aliye juu hakuna kitu juu Yake, na Aliye karibu, hakuna kitu kilichokaribu kuliko Yeye, Naye kwa kila kitu ni Mjuzi.


هُوَ الَّذِي خَلَقَ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ فِي سِتَّةِ أَيَّامٍ ثُمَّ اسْتَوَىٰ عَلَى الْعَرْشِ ۚ يَعْلَمُ مَا يَلِجُ فِي الْأَرْضِ وَمَا يَخْرُجُ مِنْهَا وَمَا يَنزِلُ مِنَ السَّمَاءِ وَمَا يَعْرُجُ فِيهَا ۖ وَهُوَ مَعَكُمْ أَيْنَ مَا كُنتُمْ ۚ وَاللَّـهُ بِمَا تَعْمَلُونَ بَصِيرٌ ﴿٤﴾
4. “Yeye Ndiye Aliyeumba mbingu na ardhi katika siku sita, kisha Istawaa juu ya ‘Arsh[1] Anajua yale yanayoingia ardhini, na yale yatokayo humo, na yale yanayoteremka kutoka mbinguni, na yale yanayopanda humo, Naye Yu Pamoja nanyi (kwa ujuzi Wake) popote mlipo. Na Allaah ni Mwenye kuona yote myatendayo.


لَّهُ مُلْكُ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ ۚ وَإِلَى اللَّـهِ تُرْجَعُ الْأُمُورُ ﴿٥﴾
5. Ni Wake Pekee ufalme wa mbingu na ardhi, kwa Allaah Pekee yanarejeshwa mambo yote.


يُولِجُ اللَّيْلَ فِي النَّهَارِ وَيُولِجُ النَّهَارَ فِي اللَّيْلِ ۚ وَهُوَ عَلِيمٌ بِذَاتِ الصُّدُورِ ﴿٦﴾
6. Anauingiza usiku katika mchana, na Anaingiza mchana katika usiku, Naye ni Mjuzi wa yaliyomo vifuani.


آمِنُوا بِاللَّـهِ وَرَسُولِهِ وَأَنفِقُوا مِمَّا جَعَلَكُم مُّسْتَخْلَفِينَ فِيهِ ۖ فَالَّذِينَ آمَنُوا مِنكُمْ وَأَنفَقُوا لَهُمْ أَجْرٌ كَبِيرٌ﴿٧﴾
7. Muaminini Allaah na Rasuli Wake, na toeni kutokana na yale Aliyokufanyieni kuwa warithi kwayo. Basi wale walioamini miongoni mwenu, na wakatoa, watapata ujira mkubwa.


وَمَا لَكُمْ لَا تُؤْمِنُونَ بِاللَّـهِ ۙ وَالرَّسُولُ يَدْعُوكُمْ لِتُؤْمِنُوا بِرَبِّكُمْ وَقَدْ أَخَذَ مِيثَاقَكُمْ إِن كُنتُم مُّؤْمِنِينَ ﴿٨﴾
8. Na mna nini nyinyi hamumuamini Allaah, na hali Rasuli anakuiteni ili mumuamini Rabb wenu, na hali Amekwishachukua fungamano lenu mkiwa nyinyi ni Waumini.


هُوَ الَّذِي يُنَزِّلُ عَلَىٰ عَبْدِهِ آيَاتٍ بَيِّنَاتٍ لِّيُخْرِجَكُم مِّنَ الظُّلُمَاتِ إِلَى النُّورِ ۚ وَإِنَّ اللَّـهَ بِكُمْ لَرَءُوفٌ رَّحِيمٌ ﴿٩﴾
9. Yeye Ndiye Yule Anayemteremshia mja Wake Aayaat bayana ili Akutoeni katika viza na kukuingizeni kwenye Nuru. Na hakika Allaah kwenu ni Mwenye huruma mno, Mwenye kurehemu.


وَمَا لَكُمْ أَلَّا تُنفِقُوا فِي سَبِيلِ اللَّـهِ وَلِلَّـهِ مِيرَاثُ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ ۚ لَا يَسْتَوِي مِنكُم مَّنْ أَنفَقَ مِن قَبْلِ الْفَتْحِ وَقَاتَلَ ۚ أُولَـٰئِكَ أَعْظَمُ دَرَجَةً مِّنَ الَّذِينَ أَنفَقُوا مِن بَعْدُ وَقَاتَلُوا ۚ وَكُلًّا وَعَدَ اللَّـهُ الْحُسْنَىٰ ۚوَاللَّـهُ بِمَا تَعْمَلُونَ خَبِيرٌ ﴿١٠﴾
10. Na mna nini hata hamtoi katika njia ya Allaah, na hali urithi wa mbingu na ardhi ni wa Allaah Pekee. Hawi sawa miongoni mwenu aliyetoa kabla ya Ushindi (wa Makkah) na akapigana. Hao watapata daraja kuu kabisa kuliko wale waliotoa baadae na wakapigana.  Na wote Allaah Amewaahidi malipo mazuri kabisa. Na Allaah kwa yale myatendayo ni Mwenye upeo wa khabari za dhahiri na za kufichika.


مَّن ذَا الَّذِي يُقْرِضُ اللَّـهَ قَرْضًا حَسَنًا فَيُضَاعِفَهُ لَهُ وَلَهُ أَجْرٌ كَرِيمٌ ﴿١١﴾
11. Nani ambaye atamkopesha Allaah karadha nzuri kisha (Allaah) Amuongezee maradufu na apate ujira mtukufu.



يَوْمَ تَرَى الْمُؤْمِنِينَ وَالْمُؤْمِنَاتِ يَسْعَىٰ نُورُهُم بَيْنَ أَيْدِيهِمْ وَبِأَيْمَانِهِم بُشْرَاكُمُ الْيَوْمَ جَنَّاتٌ تَجْرِي مِن تَحْتِهَا الْأَنْهَارُ خَالِدِينَ فِيهَا ۚ ذَٰلِكَ هُوَ الْفَوْزُ الْعَظِيمُ ﴿١٢﴾
12. Siku utakayowaona Waumini wa kiume na Waumini wa kike, nuru zao zinakimbilia mbele yao na kuliani kwao; (wataambiwa): “Bishara njema kwenu leo! Jannaat zipitazo chini yake mito, ni wenye kudumu humo. Huko ndiko kufuzu adhimu.”


يَوْمَ يَقُولُ الْمُنَافِقُونَ وَالْمُنَافِقَاتُ لِلَّذِينَ آمَنُوا انظُرُونَا نَقْتَبِسْ مِن نُّورِكُمْ قِيلَ ارْجِعُوا وَرَاءَكُمْ فَالْتَمِسُوا نُورًا فَضُرِبَ بَيْنَهُم بِسُورٍ لَّهُ بَابٌ بَاطِنُهُ فِيهِ الرَّحْمَةُ وَظَاهِرُهُ مِن قِبَلِهِ الْعَذَابُ ﴿١٣﴾
13. Siku wanafiki wa kiume na wanafiki wa kike watakapowaambia wale walioamini: “Tungojeeni, tupate mwangaza kutokana na nuru yenu!” (Wataambiwa): “Rudini nyuma yenu, na mtafute huko nuru (yenu)!” Kisha utawekwa ukutwa baina yao wenye mlango, ndani mna rahmah na nje kwa upande wake wa mbele mna adhabu.


يُنَادُونَهُمْ أَلَمْ نَكُن مَّعَكُمْ ۖ قَالُوا بَلَىٰ وَلَـٰكِنَّكُمْ فَتَنتُمْ أَنفُسَكُمْ وَتَرَبَّصْتُمْ وَارْتَبْتُمْ وَغَرَّتْكُمُ الْأَمَانِيُّ حَتَّىٰ جَاءَ أَمْرُ اللَّـهِ وَغَرَّكُم بِاللَّـهِ الْغَرُورُ ﴿١٤﴾
14. (Wanafiki) Watawaita: “Je, kwani hatukuwa pamoja nanyi?” Watasema: “Ndio! Lakini nyinyi mmezifitini nafsi zenu, na mkangojea kuangaza yatusibu misiba; na mkatia shaka, na yakakughururini matumaini ya uongo mpaka ikaja amri ya Allaah; na akakughuruni mdanganyifu (Ibliys) kuhusu Allaah.


فَالْيَوْمَ لَا يُؤْخَذُ مِنكُمْ فِدْيَةٌ وَلَا مِنَ الَّذِينَ كَفَرُوا ۚ مَأْوَاكُمُ النَّارُ ۖ هِيَ مَوْلَاكُمْ ۖ وَبِئْسَ الْمَصِيرُ ﴿١٥﴾
15. Basi leo haitochukuliwa kutoka kwenu fidia na wala kutoka kwa waliokufuru. Makazi yenu ni moto, hayo ndio yanayostahiki kwenu, na ubaya ulioje mahali pa kuishia.


أَلَمْ يَأْنِ لِلَّذِينَ آمَنُوا أَن تَخْشَعَ قُلُوبُهُمْ لِذِكْرِ اللَّـهِ وَمَا نَزَلَ مِنَ الْحَقِّ وَلَا يَكُونُوا كَالَّذِينَ أُوتُوا الْكِتَابَ مِن قَبْلُ فَطَالَ عَلَيْهِمُ الْأَمَدُ فَقَسَتْ قُلُوبُهُمْ ۖ وَكَثِيرٌ مِّنْهُمْ فَاسِقُونَ ﴿١٦﴾
16. Je, haujafika wakati kwa walioamini kwamba zinyenyekee nyoyo zao kwa kumdhukuru Allaah na yale yaliyoteremka ya haki, na wala wasiwe kama wale waliopewa Kitabu kabla, ukawatawilikia muda, kisha zikawa ngumu nyoyo zao? Na wengi miongoni mwao ni mafasiki.


اعْلَمُوا أَنَّ اللَّـهَ يُحْيِي الْأَرْضَ بَعْدَ مَوْتِهَا ۚ قَدْ بَيَّنَّا لَكُمُ الْآيَاتِ لَعَلَّكُمْ تَعْقِلُونَ ﴿١٧﴾
17. Jueni kwamba Allaah Anahuisha ardhi baada ya kufa kwake. Amekwishakubainishieni Aayaat ili mpate kutia akilini.


إِنَّ الْمُصَّدِّقِينَ وَالْمُصَّدِّقَاتِ وَأَقْرَضُوا اللَّـهَ قَرْضًا حَسَنًا يُضَاعَفُ لَهُمْ وَلَهُمْ أَجْرٌ كَرِيمٌ ﴿١٨﴾
18. Hakika wanaume watoao swadaqah na wanawake watoao swadaqah na wakamkopesha Allaah karadha mzuri, Atawazidishia maradufu, na watapa ujira mtukufu.


وَالَّذِينَ آمَنُوا بِاللَّـهِ وَرُسُلِهِ أُولَـٰئِكَ هُمُ الصِّدِّيقُونَ ۖ وَالشُّهَدَاءُ عِندَ رَبِّهِمْ لَهُمْ أَجْرُهُمْ وَنُورُهُمْ ۖوَالَّذِينَ كَفَرُوا وَكَذَّبُوا بِآيَاتِنَا أُولَـٰئِكَ أَصْحَابُ الْجَحِيمِ ﴿١٩﴾
19. Na wale waliomwamini Allaah na Rusuli Wake, hao ndio Asw-Swiddiquwn (waliosadikisha) na Mashuhadaa mbele ya Rabb wao. Watapa ujira wao na nuru yao. Na wale waliokufuru na wakakadhibisha Aayaat Zetu hao ni watu wa moto uwakao vikali mno.


اعْلَمُوا أَنَّمَا الْحَيَاةُ الدُّنْيَا لَعِبٌ وَلَهْوٌ وَزِينَةٌ وَتَفَاخُرٌ بَيْنَكُمْ وَتَكَاثُرٌ فِي الْأَمْوَالِ وَالْأَوْلَادِ ۖ كَمَثَلِ غَيْثٍ أَعْجَبَ الْكُفَّارَ نَبَاتُهُ ثُمَّ يَهِيجُ فَتَرَاهُ مُصْفَرًّا ثُمَّ يَكُونُ حُطَامًا ۖ وَفِي الْآخِرَةِ عَذَابٌ شَدِيدٌ وَمَغْفِرَةٌ مِّنَ اللَّـهِ وَرِضْوَانٌ ۚ وَمَا الْحَيَاةُ الدُّنْيَا إِلَّا مَتَاعُ الْغُرُورِ ﴿٢٠﴾
20. Jueni kwamba uhai wa dunia ni mchezo na pumbao na mapambo, na kufakharishana baina yenu na kushindana kukithiri katika mali na watoto; ni kama mfano wa mvua inayowafurahisha wakulima mimea yake, kisha yananyweya, basi utayaona yamepiga manjano, kisha yanakuwa mabua yaliyonyauka na kupondekapondeka.  Na Aakhirah kuna adhabu kali, na maghfirah kutoka kwa Allaah na radhi. Na uhai wa dunia si chochote isipokuwa ni sterehe fupi za kughuri.


سَابِقُوا إِلَىٰ مَغْفِرَةٍ مِّن رَّبِّكُمْ وَجَنَّةٍ عَرْضُهَا كَعَرْضِ السَّمَاءِ وَالْأَرْضِ أُعِدَّتْ لِلَّذِينَ آمَنُوا بِاللَّـهِ وَرُسُلِهِ ۚ ذَٰلِكَ فَضْلُ اللَّـهِ يُؤْتِيهِ مَن يَشَاءُ ۚ وَاللَّـهُ ذُو الْفَضْلِ الْعَظِيمِ ﴿٢١﴾
21. Shindaneni kukimbilia maghfirah ya Rabb wenu na Jannah, upana wake kama upana wa mbingu na ardhi, imeandaliwa kwa wale waliomwamini Allaah na Rusuli Wake. Hiyo ni fadhila ya Allaah, Humpa Amtakaye. Na Allaah ni Mwenye fadhila adhimu.


مَا أَصَابَ مِن مُّصِيبَةٍ فِي الْأَرْضِ وَلَا فِي أَنفُسِكُمْ إِلَّا فِي كِتَابٍ مِّن قَبْلِ أَن نَّبْرَأَهَا ۚ إِنَّ ذَٰلِكَ عَلَى اللَّـهِ يَسِيرٌ ﴿٢٢﴾
22. Hausibu msiba wowote katika ardhi au katika nafsi zenu isipokuwa umo katika Kitabu kabla hatujautokezesha. Hakika hayo kwa Allaah ni mepesi.


لِّكَيْلَا تَأْسَوْا عَلَىٰ مَا فَاتَكُمْ وَلَا تَفْرَحُوا بِمَا آتَاكُمْ ۗ وَاللَّـهُ لَا يُحِبُّ كُلَّ مُخْتَالٍ فَخُورٍ ﴿٢٣﴾
23. Ili msisononeke juu ya yale yaliyokuondokeeni na wala msifurahie kwa yale Aliyokupeni (Allaah); na Allaah Hapendi kila mwenye kujinata, anayejifakharisha.


الَّذِينَ يَبْخَلُونَ وَيَأْمُرُونَ النَّاسَ بِالْبُخْلِ ۗ وَمَن يَتَوَلَّ فَإِنَّ اللَّـهَ هُوَ الْغَنِيُّ الْحَمِيدُ ﴿٢٤﴾
24. Ambao wanaofanya ubakhili na wanaamrisha watu ubakhili. Na atakayekenguka, basi hakika Allaah Ndiye Mkwasi, Mwenye kustahiki kuhimidiwa kwa yote.


لَقَدْ أَرْسَلْنَا رُسُلَنَا بِالْبَيِّنَاتِ وَأَنزَلْنَا مَعَهُمُ الْكِتَابَ وَالْمِيزَانَ لِيَقُومَ النَّاسُ بِالْقِسْطِ ۖ وَأَنزَلْنَا الْحَدِيدَ فِيهِ بَأْسٌ شَدِيدٌ وَمَنَافِعُ لِلنَّاسِ وَلِيَعْلَمَ اللَّـهُ مَن يَنصُرُهُ وَرُسُلَهُ بِالْغَيْبِ ۚ إِنَّ اللَّـهَ قَوِيٌّ عَزِيزٌ ﴿٢٥﴾
25. Kwa yakini Tuliwapeleka Rusuli Wetu kwa hoja bayana, na Tukateremsha pamoja nao Kitabu na Miyzaan (shariy’ah) ili watu wasimamie kwa uadilifu. Na Tukateremsha chuma chenye nguvu shadidi na manufaa kwa watu, na ili Allaah Ajue nani atakayeinusuru (Dini Yake) na Rusuli Wake hali ya kuwa ni ghayb. Hakika Allaah ni Mwenye nguvu zote, Mwenye enzi ya nguvu Asiyeshindika.


وَلَقَدْ أَرْسَلْنَا نُوحًا وَإِبْرَاهِيمَ وَجَعَلْنَا فِي ذُرِّيَّتِهِمَا النُّبُوَّةَ وَالْكِتَابَ ۖ فَمِنْهُم مُّهْتَدٍ ۖ وَكَثِيرٌ مِّنْهُمْ فَاسِقُونَ﴿٢٦﴾
26. Na kwa yakini Tulimtuma Nuwh, na Ibraahiym, na Tukaweka katika dhuriya wao Unabii na Kitabu. Basi miongoni mwao wako waongofu, na wengi wao ni mafasiki.


ثُمَّ قَفَّيْنَا عَلَىٰ آثَارِهِم بِرُسُلِنَا وَقَفَّيْنَا بِعِيسَى ابْنِ مَرْيَمَ وَآتَيْنَاهُ الْإِنجِيلَ وَجَعَلْنَا فِي قُلُوبِ الَّذِينَ اتَّبَعُوهُ رَأْفَةً وَرَحْمَةً وَرَهْبَانِيَّةً ابْتَدَعُوهَا مَا كَتَبْنَاهَا عَلَيْهِمْ إِلَّا ابْتِغَاءَ رِضْوَانِ اللَّـهِ فَمَا رَعَوْهَا حَقَّ رِعَايَتِهَا ۖ فَآتَيْنَا الَّذِينَ آمَنُوا مِنْهُمْ أَجْرَهُمْ ۖ وَكَثِيرٌ مِّنْهُمْ فَاسِقُونَ ﴿٢٧﴾
27. Kisha Tukawafuatisha baada yao, Rusuli Wetu, na Tukamfuatisha ‘Iysaa mwana wa Maryam, na Tukampa Injiyl. Na Tukaweka katika nyoyo za wale waliomfuata upole na rahmah na uruhubani (maisha ya utawa); wameyaanzisha wao wenyewe Hatukuwaandikia hayo juu yao isipokuwa ni kutafuta radhi za Allaah. Lakini hawakuuchunga ipasavyo kuchungwa. Basi Tukawapa wale walioamini miongoni mwao ujira wao, na wengi wao ni mafasiki.


يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اتَّقُوا اللَّـهَ وَآمِنُوا بِرَسُولِهِ يُؤْتِكُمْ كِفْلَيْنِ مِن رَّحْمَتِهِ وَيَجْعَل لَّكُمْ نُورًا تَمْشُونَ بِهِ وَيَغْفِرْ لَكُمْ ۚ وَاللَّـهُ غَفُورٌ رَّحِيمٌ ﴿٢٨﴾
28. Enyi walioamini! Mcheni Allaah, na muaminini Rasuli Wake. (Allaah) Atakupeni sehemu mbili kati ya rahmah Zake, na Atakuwekeeni nuru mnatembea nayo, na Atakughufurieni; na Allaah ni Mwingi wa kughufuria, Mwenye kurehemu.


لِّئَلَّا يَعْلَمَ أَهْلُ الْكِتَابِ أَلَّا يَقْدِرُونَ عَلَىٰ شَيْءٍ مِّن فَضْلِ اللَّـهِ ۙ وَأَنَّ الْفَضْلَ بِيَدِ اللَّـهِ يُؤْتِيهِ مَن يَشَاءُۚ وَاللَّـهُ ذُو الْفَضْلِ الْعَظِيمِ ﴿٢٩﴾
29. Ili wajue Ahlul-Kitaabi kwamba hawana uwezo wa chochote katika fadhila za Allaah, na kwamba fadhila zimo Mkononi mwa Allaah Humpa Amtakaye, na Allaah ni Mwenye fadhila adhimu.


 
[1] Istawaa: Yuko juu kwa namna inayolingana na Utukufu Wake Yeye Mwenyewe Allaah.