الدُّخان
Ad-Dukhaan: 44


بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ


حم﴿١﴾
1. Haa Miym.


وَالْكِتَابِ الْمُبِينِ﴿٢﴾
2. Na Kitabu kinachobainisha.


إِنَّا أَنزَلْنَاهُ فِي لَيْلَةٍ مُّبَارَكَةٍ ۚ إِنَّا كُنَّا مُنذِرِينَ﴿٣﴾
3. Hakika Sisi Tumeiteremsha (Qur-aan) katika usiku uliobarikiwa, hakika Sisi daima ni Wenye kuonya.


فِيهَا يُفْرَقُ كُلُّ أَمْرٍ حَكِيمٍ﴿٤﴾
4.  Katika (usiku) huo hupambanuliwa kila jambo la hikmah.


أَمْرًا مِّنْ عِندِنَا ۚ إِنَّا كُنَّا مُرْسِلِينَ﴿٥﴾
5.  Ni amri  kutoka Kwetu, hakika Sisi ndio Wenye kutuma (Rusuli).


رَحْمَةً مِّن رَّبِّكَ ۚ إِنَّهُ هُوَ السَّمِيعُ الْعَلِيمُ﴿٦﴾
6. Ni rahmah kutoka kwa Rabb wako, hakika Yeye Ndiye Mwenye kusikia yote, Mjuzi wa yote.


رَبِّ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ وَمَا بَيْنَهُمَا ۖ إِن كُنتُم مُّوقِنِينَ﴿٧﴾
7. Rabb wa mbingu na ardhi na vilivyo baina yake, mkiwa ni wenye yakini.



لَا إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ يُحْيِي وَيُمِيتُ ۖ رَبُّكُمْ وَرَبُّ آبَائِكُمُ الْأَوَّلِينَ﴿٨﴾
8. Hapana Muabudiwa wa haki ila Yeye, Anahuisha na Anafisha; Rabb wenu na Rabb wa baba zenu wa awali.


بَلْ هُمْ فِي شَكٍّ يَلْعَبُونَ﴿٩﴾
9. Bali wao wamo katika shaka wanacheza.


فَارْتَقِبْ يَوْمَ تَأْتِي السَّمَاءُ بِدُخَانٍ مُّبِينٍ﴿١٠﴾
10. Basi ngojea uangaze siku mbingu zitakapoleta moshi bayana.


يَغْشَى النَّاسَ ۖ هَـٰذَا عَذَابٌ أَلِيمٌ﴿١١﴾
11. Utawafunika watu. Hii ni adhabu iumizayo.


رَّبَّنَا اكْشِفْ عَنَّا الْعَذَابَ إِنَّا مُؤْمِنُونَ﴿١٢﴾
12. (Watasema): “Rabb wetu! Tuondoshee adhabu, hakika sisi wenye kuamini.”


أَنَّىٰ لَهُمُ الذِّكْرَىٰ وَقَدْ جَاءَهُمْ رَسُولٌ مُّبِينٌ﴿١٣﴾
13. Kutoka wapi watapata ukumbusho na hali amekwishawajia Rasuli mwenye kubainisha.


ثُمَّ تَوَلَّوْا عَنْهُ وَقَالُوا مُعَلَّمٌ مَّجْنُونٌ﴿١٤﴾
14. Kisha wakamkengeuka na wakasema: “Amefundishwa na majnuni.”


إِنَّا كَاشِفُو الْعَذَابِ قَلِيلًا ۚ إِنَّكُمْ عَائِدُونَ﴿١٥﴾
15. Hakika Sisi Tutaiondosha adhabu kidogo, lakini nyinyi hakika mtarudia vile vile.


يَوْمَ نَبْطِشُ الْبَطْشَةَ الْكُبْرَىٰ إِنَّا مُنتَقِمُونَ﴿١٦﴾
16. Siku Tutakayoshambulia mashambulio makubwa hakika Sisi ni Wenye kulipiza


وَلَقَدْ فَتَنَّا قَبْلَهُمْ قَوْمَ فِرْعَوْنَ وَجَاءَهُمْ رَسُولٌ كَرِيمٌ﴿١٧﴾
17. Na kwa yakini Tuliwatia mtihanini kabla yao watu wa Fir’awn, na aliwajia Rasuli mtukufu.


أَنْ أَدُّوا إِلَيَّ عِبَادَ اللَّـهِ ۖ إِنِّي لَكُمْ رَسُولٌ أَمِينٌ﴿١٨﴾
18. (Akiwaambia): “Wakabidhini kwangu waja wa Allaah, hakika mimi kwenu ni Rasuli mwaminifu.


وَأَن لَّا تَعْلُوا عَلَى اللَّـهِ ۖ إِنِّي آتِيكُم بِسُلْطَانٍ مُّبِينٍ﴿١٩﴾
19. “Na kwamba msitakabari mbele ya Allaah; hakika mimi nakuleteeni dalili bayana.


وَإِنِّي عُذْتُ بِرَبِّي وَرَبِّكُمْ أَن تَرْجُمُونِ﴿٢٠﴾
20. “Na hakika mimi nimejikinga kwa Rabb wangu na Rabb wenu msije kunirajimu.


وَإِن لَّمْ تُؤْمِنُوا لِي فَاعْتَزِلُونِ﴿٢١﴾
21. “Na ikiwa hamtoniamini basi nitengeni mbali”


فَدَعَا رَبَّهُ أَنَّ هَـٰؤُلَاءِ قَوْمٌ مُّجْرِمُونَ﴿٢٢﴾
22. Akamuomba Rabb wake kwamba: “Hawa watu ni wahalifu.”


فَأَسْرِ بِعِبَادِي لَيْلًا إِنَّكُم مُّتَّبَعُونَ﴿٢٣﴾
23. (Allaah Akasema): “Basi ondoka usiku na waja Wangu, hakika nyinyi ni wenye kufuatwa.”


وَاتْرُكِ الْبَحْرَ رَهْوًا ۖ إِنَّهُمْ جُندٌ مُّغْرَقُونَ﴿٢٤﴾
24. “Na acha bahari ikiwa imetulia, hakika wao ni jeshi lenye kugharikishwa.”


كَمْ تَرَكُوا مِن جَنَّاتٍ وَعُيُونٍ﴿٢٥﴾
25. Mabustani mangapi wameacha na chemchemu. 


وَزُرُوعٍ وَمَقَامٍ كَرِيمٍ﴿٢٦﴾
26. Na mimea na makazi mazuri mno.


وَنَعْمَةٍ كَانُوا فِيهَا فَاكِهِينَ﴿٢٧﴾
27. Na neema walikuwa humo wenye kuzifurahia.


كَذَٰلِكَ ۖ وَأَوْرَثْنَاهَا قَوْمًا آخَرِينَ﴿٢٨﴾
28. Hivyo ndivyo ilivyo. Na Tukawarithisha watu wengineo.


فَمَا بَكَتْ عَلَيْهِمُ السَّمَاءُ وَالْأَرْضُ وَمَا كَانُوا مُنظَرِينَ﴿٢٩﴾
29. Na hazikuwalilia mbingu na ardhi, na wala hawakua wa kupewa muhula.


وَلَقَدْ نَجَّيْنَا بَنِي إِسْرَائِيلَ مِنَ الْعَذَابِ الْمُهِينِ﴿٣٠﴾
30. Na kwa yakini Tuliwaokoa wana wa Israaiyl kutokana na adhabu ya kudhalilisha.


مِن فِرْعَوْنَ ۚ إِنَّهُ كَانَ عَالِيًا مِّنَ الْمُسْرِفِينَ﴿٣١﴾
31. Kutoka kwa Fir’awn, hakika yeye alikuwa mwenye kibri miongoni wenye kupindukia mipaka.


وَلَقَدِ اخْتَرْنَاهُمْ عَلَىٰ عِلْمٍ عَلَى الْعَالَمِينَ﴿٣٢﴾
32. Na kwa yakini Tuliwakhitari (wana wa Israaiyl) kwa elimu kuliko walimwengu wowote.


وَآتَيْنَاهُم مِّنَ الْآيَاتِ مَا فِيهِ بَلَاءٌ مُّبِينٌ﴿٣٣﴾
33. Na Tukawapa miongoni mwa Aayaat (miujiza, ishara) zilizokuwemo majaribio bayana.


إِنَّ هَـٰؤُلَاءِ لَيَقُولُونَ﴿٣٤﴾
34. Hakika hawa (Maquraysh) bila shaka wanasema.


إِنْ هِيَ إِلَّا مَوْتَتُنَا الْأُولَىٰ وَمَا نَحْنُ بِمُنشَرِينَ﴿٣٥﴾
35. “Haya si chochote isipokuwa ni mauti yetu ya awali, nasi hatutofufuliwa.


فَأْتُوا بِآبَائِنَا إِن كُنتُمْ صَادِقِينَ﴿٣٦﴾
36. “Basi tuleteeni mababu zetu mkiwa ni wakweli.”


أَهُمْ خَيْرٌ أَمْ قَوْمُ تُبَّعٍ وَالَّذِينَ مِن قَبْلِهِمْ ۚ أَهْلَكْنَاهُمْ ۖ إِنَّهُمْ كَانُوا مُجْرِمِينَ﴿٣٧﴾
37. “Je, kwani wao ni bora zaidi au kaumu ya Tubba'  na wale waliokuwa kabla yao. Tuliwaangamiza. Hakika wao walikuwa wahalifu.


وَمَا خَلَقْنَا السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ وَمَا بَيْنَهُمَا لَاعِبِينَ﴿٣٨﴾
38. Na Hatukuumba mbingu na ardhi na vilivyo baina yake kama wenye kucheza.


مَا خَلَقْنَاهُمَا إِلَّا بِالْحَقِّ وَلَـٰكِنَّ أَكْثَرَهُمْ لَا يَعْلَمُونَ﴿٣٩﴾
39. Hatukuumba viwili hivyo isipokuwa kwa haki, lakini wengi wao hawajui.


إِنَّ يَوْمَ الْفَصْلِ مِيقَاتُهُمْ أَجْمَعِينَ﴿٤٠﴾
40. Hakika Siku ya hukumu ni wakati wao maalumu uliopangwa kwa wote.


يَوْمَ لَا يُغْنِي مَوْلًى عَن مَّوْلًى شَيْئًا وَلَا هُمْ يُنصَرُونَ﴿٤١﴾
41. Siku ambayo jamaa wa karibu hatomfaa jamaa wa karibu chochote, na wala wao hawatonusuriwa.


إِلَّا مَن رَّحِمَ اللَّـهُ ۚ إِنَّهُ هُوَ الْعَزِيزُ الرَّحِيمُ﴿٤٢﴾
42. Isipokuwa yule Atakayerehemewa na Allaah.  Hakika Yeye Ndiye Mwenye enzi ya nguvu Asiyeshindika,Mwenye kurehemu.


إِنَّ شَجَرَتَ الزَّقُّومِ﴿٤٣﴾
43. Hakika mti wa az-zaqquwm.


طَعَامُ الْأَثِيمِ﴿٤٤﴾
44. Ni chakula cha mtendaji mno dhambi.


كَالْمُهْلِ يَغْلِي فِي الْبُطُونِ﴿٤٥﴾
45. Kama masazo ya zebaki nyeusi ziliyoyeyushwa inatokota matumboni.


كَغَلْيِ الْحَمِيمِ﴿٤٦﴾
46. Kama kutokota kwa maji yachemkayo.


خُذُوهُ فَاعْتِلُوهُ إِلَىٰ سَوَاءِ الْجَحِيمِ﴿٤٧﴾
47. (Itaamrishwa): “Mchukueni na msokomezeni katikati ya moto uwakao vikali mno.


ثُمَّ صُبُّوا فَوْقَ رَأْسِهِ مِنْ عَذَابِ الْحَمِيمِ﴿٤٨﴾
48. “Kisha mwagieni juu ya kichwa chake adhabu ya maji yachemkayo.”


ذُقْ إِنَّكَ أَنتَ الْعَزِيزُ الْكَرِيمُ﴿٤٩﴾
49. “Onja! Hakika wewe ni mwenye nguvu mheshimiwa.


إِنَّ هَـٰذَا مَا كُنتُم بِهِ تَمْتَرُونَ﴿٥٠﴾
50. “Hakika haya ambayo mlikuwa mkiyatilia shaka.”


إِنَّ الْمُتَّقِينَ فِي مَقَامٍ أَمِينٍ﴿٥١﴾

51. Hakika wenye taqwa wako katika mahali pa amani.


فِي جَنَّاتٍ وَعُيُونٍ﴿٥٢﴾
52. Katika Jannaat na chemchemu.


يَلْبَسُونَ مِن سُندُسٍ وَإِسْتَبْرَقٍ مُّتَقَابِلِينَ﴿٥٣﴾
53. Watavaa hariri laini na hariri nzito nyororo wakiwa wamekabiliana. 


كَذَٰلِكَ وَزَوَّجْنَاهُم بِحُورٍ عِينٍ﴿٥٤﴾
54. Hivyo ndivyo!  Na Tutawaozesha mahuwr, wanawake wa Jannah wenye macho ya kupendeza.


يَدْعُونَ فِيهَا بِكُلِّ فَاكِهَةٍ آمِنِينَ﴿٥٥﴾
55. Wataagiza humo kila aina ya matunda wakiwa katika amani.


لَا يَذُوقُونَ فِيهَا الْمَوْتَ إِلَّا الْمَوْتَةَ الْأُولَىٰ ۖ وَوَقَاهُمْ عَذَابَ الْجَحِيمِ﴿٥٦﴾
56. Hawatoonja humo mauti isipokuwa mauti yale ya awali na (Allaah) Atawakinga na adhabu ya moto uwakao vikali mno.


فَضْلًا مِّن رَّبِّكَ ۚ ذَٰلِكَ هُوَ الْفَوْزُ الْعَظِيمُ﴿٥٧﴾
57. Ni fadhila kutoka kwa Rabb wako.  Huko ndiko kufuzu adhimu.


فَإِنَّمَا يَسَّرْنَاهُ بِلِسَانِكَ لَعَلَّهُمْ يَتَذَكَّرُونَ﴿٥٨﴾
58. Basi hakika Tumeiwepesisha (Qur-aan) kwenye lisani yako ili wapate kukumbuka.


فَارْتَقِبْ إِنَّهُم مُّرْتَقِبُونَ﴿٥٩﴾
59. Basi ngojea uchunge (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم), hakika wao pia ni wenye kungojea wakichunga.