الصًّفَّات
Asw-Swaffaat: 37
بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ
وَالصَّافَّاتِ صَفًّا ﴿١﴾
1. Naapa kwa (Malaika) wanaojipanga safusafu.
فَالزَّاجِرَاتِ زَجْرًا ﴿٢﴾
2. Na Naapa kwa (Malaika) wanaosukumiza mbali mawingu.
فَالتَّالِيَاتِ ذِكْرًا ﴿٣﴾
3. Na Naapa kwa (Malaika) wanaosoma maneno ya Allaah.
إِنَّ إِلَـٰهَكُمْ لَوَاحِدٌ ﴿٤﴾
4. Hakika Muabudiwa wenu wa haki wenu ni Mmoja.
رَّبُّ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ وَمَا بَيْنَهُمَا وَرَبُّ الْمَشَارِقِ ﴿٥﴾
5. Rabb wa mbingu na ardhi na vilivyo baina yake na Rabb wa mapambazuko.
إِنَّا زَيَّنَّا السَّمَاءَ الدُّنْيَا بِزِينَةٍ الْكَوَاكِبِ ﴿٦﴾
6. Hakika Sisi Tumeipamba mbingu ya dunia kwa mapambo ya nyota.
وَحِفْظًا مِّن كُلِّ شَيْطَانٍ مَّارِدٍ ﴿٧﴾
7. Na hifadhi kutokana na kila shaytwaan asi.
لَّا يَسَّمَّعُونَ إِلَى الْمَلَإِ الْأَعْلَىٰ وَيُقْذَفُونَ مِن كُلِّ جَانِبٍ ﴿٨﴾
8. Hawawezi kusikiliza kundi la juu lilotukuzwa, kwani wanavurumsihwa kila upande.
دُحُورًا ۖ وَلَهُمْ عَذَابٌ وَاصِبٌ ﴿٩﴾
9. Wakifukuziliwa mbali, na watapata adhabu ya kuendelea.
إِلَّا مَنْ خَطِفَ الْخَطْفَةَ فَأَتْبَعَهُ شِهَابٌ ثَاقِبٌ ﴿١٠﴾
10. Isipokuwa yule atakayenyakua kitu kwa kuiba basi inamwandama kimondo kiwakacho.
فَاسْتَفْتِهِمْ أَهُمْ أَشَدُّ خَلْقًا أَم مَّنْ خَلَقْنَا ۚ إِنَّا خَلَقْنَاهُم مِّن طِينٍ لَّازِبٍ ﴿١١﴾
11. Basi waulize: “Je, wao ni viumbe wenye nguvu zaidi, au wale Tuliowaumba?” Hakika Sisi Tumewaumba kutokana na udongo unaonata.
بَلْ عَجِبْتَ وَيَسْخَرُونَ ﴿١٢﴾
12. Bali umestaajabu, nao wanafanya dhihaki.
وَإِذَا ذُكِّرُوا لَا يَذْكُرُونَ ﴿١٣﴾
13. Na wanapokumbushwa, hawakumbuki.
وَإِذَا رَأَوْا آيَةً يَسْتَسْخِرُونَ ﴿١٤﴾
14. Na wanapoona Aayah, (muujiza, dalili) wanazidi kufanya masikhara kudhihaki.
وَقَالُوا إِنْ هَـٰذَا إِلَّا سِحْرٌ مُّبِينٌ ﴿١٥﴾
15. Na wanasema: “Hii si chochote isipokuwa ni sihiri bayana.”
أَإِذَا مِتْنَا وَكُنَّا تُرَابًا وَعِظَامًا أَإِنَّا لَمَبْعُوثُونَ ﴿١٦﴾
16. “Je, hivi tukifa, na tukawa vumbi na mifupa, hivi sisi tutafufuliwa?”
أَوَآبَاؤُنَا الْأَوَّلُونَ ﴿١٧﴾
17. “Je, pia na baba zetu wa awali?”
قُلْ نَعَمْ وَأَنتُمْ دَاخِرُونَ ﴿١٨﴾
18. Sema: “Naam na hali nanyi madhalili.”
فَإِنَّمَا هِيَ زَجْرَةٌ وَاحِدَةٌ فَإِذَا هُمْ يَنظُرُونَ ﴿١٩﴾
19. Kwani huo ni ukelele (wa baragumu) mmoja tu, basi mara hao wanatazama!
وَقَالُوا يَا وَيْلَنَا هَـٰذَا يَوْمُ الدِّينِ ﴿٢٠﴾
20. Na watasema: “Ole wetu! Hii ni Siku ya Malipo.”
هَـٰذَا يَوْمُ الْفَصْلِ الَّذِي كُنتُم بِهِ تُكَذِّبُونَ ﴿٢١﴾
21. (Waatambiwa): “Hii ndio Siku ya hukumu ambayo mlikuwa mkiikadhibisha.”
احْشُرُوا الَّذِينَ ظَلَمُوا وَأَزْوَاجَهُمْ وَمَا كَانُوا يَعْبُدُونَ ﴿٢٢﴾
22. (Malaika wataamrishwa): “Wakusanyeni wale waliodhulumu na wenziwao na yale waliyokuwa wakiyaabudu.”
مِن دُونِ اللَّـهِ فَاهْدُوهُمْ إِلَىٰ صِرَاطِ الْجَحِيمِ ﴿٢٣﴾
23. “Badala ya Allaah, basi waongozeni kwenye njia ya moto uwakao vikali mno.”
وَقِفُوهُمْ ۖ إِنَّهُم مَّسْئُولُونَ ﴿٢٤﴾
24. “Wasimamisheni, hakika wao ni wenye kuulizwa.”
مَا لَكُمْ لَا تَنَاصَرُونَ ﴿٢٥﴾
25. (Wataulizwa): “Mna nini hamnusuriani?”
بَلْ هُمُ الْيَوْمَ مُسْتَسْلِمُونَ ﴿٢٦﴾
26. Bali wao leo wamesalimu amri.
وَأَقْبَلَ بَعْضُهُمْ عَلَىٰ بَعْضٍ يَتَسَاءَلُونَ ﴿٢٧﴾
27. Na watakabiliana wenyewe kwa wenyewe kuulizana.
قَالُوا إِنَّكُمْ كُنتُمْ تَأْتُونَنَا عَنِ الْيَمِينِ ﴿٢٨﴾
28. Watasema: “Hakika nyinyi mlikuwa mkitujia kutoka kuliani (kutushinda nguvu).”
قَالُوا بَل لَّمْ تَكُونُوا مُؤْمِنِينَ ﴿٢٩﴾
29. Watasema: “Bali nyinyi wenyewe hamkuwa wenye kuamini.
وَمَا كَانَ لَنَا عَلَيْكُم مِّن سُلْطَانٍ ۖ بَلْ كُنتُمْ قَوْمًا طَاغِينَ ﴿٣٠﴾
30. “Na hatukuwa na madaraka juu yenu, bali mlikuwa watu wapindukao mipaka kuasi.”
فَحَقَّ عَلَيْنَا قَوْلُ رَبِّنَا ۖ إِنَّا لَذَائِقُونَ ﴿٣١﴾
31. “Basi ikahakiki juu Yetu kauli ya Rabb wetu; hakika sisi bila ni wenye kuonja (adhabu).
فَأَغْوَيْنَاكُمْ إِنَّا كُنَّا غَاوِينَ ﴿٣٢﴾
32. “Kisha tukakupotoeni hakika sisi tulikuwa wenye kupotoka.”
فَإِنَّهُمْ يَوْمَئِذٍ فِي الْعَذَابِ مُشْتَرِكُونَ ﴿٣٣﴾
33. Basi hakika wao Siku hiyo katika adhabu ni wenye kushirikiana.
إِنَّا كَذَٰلِكَ نَفْعَلُ بِالْمُجْرِمِينَ ﴿٣٤﴾
34. Hakika hivyo ndivyo Tuwafanyavo wahalifu.
إِنَّهُمْ كَانُوا إِذَا قِيلَ لَهُمْ لَا إِلَـٰهَ إِلَّا اللَّـهُ يَسْتَكْبِرُونَ ﴿٣٥﴾
35. Hakika wao walipokuwa wakiambiwa: “Laa ilaaha illa Allaah”, Hapana Muabudiwa wa haki ila Allaah, hutakabari.
وَيَقُولُونَ أَئِنَّا لَتَارِكُو آلِهَتِنَا لِشَاعِرٍ مَّجْنُونٍ ﴿٣٦﴾
36. Na wanasema: “Je, sisi kweli tuache waabudiwa wetu kwa ajili ya mshairi majnuni?!”
بَلْ جَاءَ بِالْحَقِّ وَصَدَّقَ الْمُرْسَلِينَ ﴿٣٧﴾
37. Bali (Nabiy Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) amekuja kwa haki, na amewasadikisha Rusuli (waliotangulia).
إِنَّكُمْ لَذَائِقُو الْعَذَابِ الْأَلِيمِ ﴿٣٨﴾
38. Hakika nyinyi (makafiri) bila shaka ni wenye kuionja adhabu iumizayo.
وَمَا تُجْزَوْنَ إِلَّا مَا كُنتُمْ تَعْمَلُونَ ﴿٣٩﴾
39. Na hamlipwi isipokuwa yale mliyokuwa mkiyatenda.
إِلَّا عِبَادَ اللَّـهِ الْمُخْلَصِينَ ﴿٤٠﴾
40. Isipokuwa waja wa Allaah
waliokhitariwa kwa ikhlasi zao.
أُولَـٰئِكَ لَهُمْ رِزْقٌ مَّعْلُومٌ ﴿٤١﴾
41. Hao watapata riziki maalumu.
فَوَاكِهُ ۖ وَهُم مُّكْرَمُونَ ﴿٤٢﴾
42. Matunda; nao ni wenye kukirimiwa
فِي جَنَّاتِ النَّعِيمِ ﴿٤٣﴾
43. Katika Jannaat za neema.
عَلَىٰ سُرُرٍ مُّتَقَابِلِينَ ﴿٤٤﴾
44. Juu ya makochi ya enzi wakikabiliana.
يُطَافُ عَلَيْهِم بِكَأْسٍ مِّن مَّعِينٍ ﴿٤٥﴾
45. Wanazungushiwa gilasi za mvinyo kutoka chemchemu.
بَيْضَاءَ لَذَّةٍ لِّلشَّارِبِينَ ﴿٤٦﴾
46. Nyeupe, ya ladha kwa wanywaji.
لَا فِيهَا غَوْلٌ وَلَا هُمْ عَنْهَا يُنزَفُونَ ﴿٤٧﴾
47. Hamna humo madhara yoyote na wala wao kwayo hawataleweshwa.
وَعِندَهُمْ قَاصِرَاتُ الطَّرْفِ عِينٌ ﴿٤٨﴾
48. Na watakuwa nao wanawake wenye staha wanaoinamisha macho, wenye macho mapana mazuri ya kuvutia.
كَأَنَّهُنَّ بَيْضٌ مَّكْنُونٌ ﴿٤٩﴾
49. (Wanyororo, watakasifu) kama kwamba mayai yaliyohifadhiwa.
فَأَقْبَلَ بَعْضُهُمْ عَلَىٰ بَعْضٍ يَتَسَاءَلُونَ ﴿٥٠﴾
50. Basi watakabiliana wenyewe kwa wenyewe wakiulizana.
قَالَ قَائِلٌ مِّنْهُمْ إِنِّي كَانَ لِي قَرِينٌ ﴿٥١﴾
51. Aseme msemaji miongoni mwao: “Hakika mimi nilikuwa na rafiki mwandani.”
يَقُولُ أَإِنَّكَ لَمِنَ الْمُصَدِّقِينَ ﴿٥٢﴾
52. Aliyekuwa akiniambia: “Je, hivi wewe ni miongoni mwa wanaosadiki?
أَإِذَا مِتْنَا وَكُنَّا تُرَابًا وَعِظَامًا أَإِنَّا لَمَدِينُونَ ﴿٥٣﴾
53. “Je tutakapokufa, tukawa vumbi na mifupa, eti hakika sisi tutahukumiwa na kulipwa kikamilifu?”
قَالَ هَلْ أَنتُم مُّطَّلِعُونَ ﴿٥٤﴾
54. Atasema: “Je, nyinyi mnachungulia (motoni)?”
فَاطَّلَعَ فَرَآهُ فِي سَوَاءِ الْجَحِيمِ ﴿٥٥﴾
55. Basi atachunuglia atamuona (rafiki yake) yuko katikati ya moto uwakao vikali mno.
قَالَ تَاللَّـهِ إِن كِدتَّ لَتُرْدِينِ ﴿٥٦﴾
56. Atasema: “Wa-Allaahi! Ulikaribia bila shaka kuniangamiza!
وَلَوْلَا نِعْمَةُ رَبِّي لَكُنتُ مِنَ الْمُحْضَرِينَ ﴿٥٧﴾
57. “Na lau kama si neema ya Rabb wangu, bila shaka ningelikuwa miongoni mwa wahudhurishwao (motoni).”
أَفَمَا نَحْنُ بِمَيِّتِينَ ﴿٥٨﴾
58. “Je, sisi hatutakufa tena.”
إِلَّا مَوْتَتَنَا الْأُولَىٰ وَمَا نَحْنُ بِمُعَذَّبِينَ ﴿٥٩﴾
59. “Isipokuwa mauti yetu ya awali, nasi hatutaadhibiwa.”
إِنَّ هَـٰذَا لَهُوَ الْفَوْزُ الْعَظِيمُ ﴿٦٠﴾
60. Hakika huku ndiko kufuzu adhimu.
لِمِثْلِ هَـٰذَا فَلْيَعْمَلِ الْعَامِلُونَ ﴿٦١﴾
61. Kwa mfano kama huu, basi watende wenye kutenda.
أَذَٰلِكَ خَيْرٌ نُّزُلًا أَمْ شَجَرَةُ الزَّقُّومِ ﴿٦٢﴾
62. Je hiyo (Jannah) ni mapokezi bora au mti wa zaqquwm (motoni)?[1]
إِنَّا جَعَلْنَاهَا فِتْنَةً لِّلظَّالِمِينَ ﴿٦٣﴾
63. Hakika Sisi Tumeufanya (zaqquwm) kuwa ni jaribio kwa madhalimu.
إِنَّهَا شَجَرَةٌ تَخْرُجُ فِي أَصْلِ الْجَحِيمِ ﴿٦٤﴾
64. Hakika huo ni mti unaotoka katika kina cha moto uwakao vikali mno.
طَلْعُهَا كَأَنَّهُ رُءُوسُ الشَّيَاطِينِ ﴿٦٥﴾
65. Mashada ya matunda yake kama kwamba ni vichwa vya mashaytwaan.
فَإِنَّهُمْ لَآكِلُونَ مِنْهَا فَمَالِئُونَ مِنْهَا الْبُطُونَ ﴿٦٦﴾
66. Basi hakika wao watakula humo na watajaza matumbo yao kwayo.
ثُمَّ إِنَّ لَهُمْ عَلَيْهَا لَشَوْبًا مِّنْ حَمِيمٍ ﴿٦٧﴾
67. Kisha hakika wao watapata mchanganyiko wa maji yachemkayo.
ثُمَّ إِنَّ مَرْجِعَهُمْ لَإِلَى الْجَحِيمِ ﴿٦٨﴾
68. Kisha marejeo yao bila shaka yatakuwa kuelekea kwenye moto uwakao vikali mno.
إِنَّهُمْ أَلْفَوْا آبَاءَهُمْ ضَالِّينَ ﴿٦٩﴾
69. Hakika wao waliwakuta baba zao wamepotoka.
فَهُمْ عَلَىٰ آثَارِهِمْ يُهْرَعُونَ ﴿٧٠﴾
70. Basi na wao wakaharakiza kufuata athari zao.
وَلَقَدْ ضَلَّ قَبْلَهُمْ أَكْثَرُ الْأَوَّلِينَ ﴿٧١﴾
71. Na kwa yakini walipotoka kabla yao watu wengi wa awali.
وَلَقَدْ أَرْسَلْنَا فِيهِم مُّنذِرِينَ ﴿٧٢﴾
72. Na kwa yakini Tuliwatumia waonyaji.
فَانظُرْ كَيْفَ كَانَ عَاقِبَةُ الْمُنذَرِينَ ﴿٧٣﴾
73. Basi tazama vipi ilikuwa hatima ya walioonywa?
إِلَّا عِبَادَ اللَّـهِ الْمُخْلَصِينَ ﴿٧٤﴾
74. Isipokuwa waja wa Allaah
waliokhitariwa kwa ikhlasi zao.
وَلَقَدْ نَادَانَا نُوحٌ فَلَنِعْمَ الْمُجِيبُونَ ﴿٧٥﴾
75. Na kwa yakini Nuwh alituita (tumnusuru). Basi uzuri ulioje wa Wanaoitikia.
وَنَجَّيْنَاهُ وَأَهْلَهُ مِنَ الْكَرْبِ الْعَظِيمِ ﴿٧٦﴾
76. Tukamuokoa na ahli zake kutokana na janga kubwa mno.
وَجَعَلْنَا ذُرِّيَّتَهُ هُمُ الْبَاقِينَ ﴿٧٧﴾
77. Na Tukajaalia dhuria wake wao ndio wenye kubakia.
وَتَرَكْنَا عَلَيْهِ فِي الْآخِرِينَ ﴿٧٨﴾
78. Na Tukamuachia (sifa nzuri) kwa karne za baadaye.
سَلَامٌ عَلَىٰ نُوحٍ فِي الْعَالَمِينَ ﴿٧٩﴾
79. Amani iwe juu ya Nuwh ulimwenguni.
إِنَّا كَذَٰلِكَ نَجْزِي الْمُحْسِنِينَ ﴿٨٠﴾
80. Hakika hivyo ndivyo Tunavyolipa wafanyao ihsaan.
إِنَّهُ مِنْ عِبَادِنَا الْمُؤْمِنِينَ ﴿٨١﴾
81. Hakika yeye ni miongoni mwa waja Wetu Waumini.
ثُمَّ أَغْرَقْنَا الْآخَرِينَ ﴿٨٢﴾
82. Kisha Tukawagharikisha wengineo.
وَإِنَّ مِن شِيعَتِهِ لَإِبْرَاهِيمَ ﴿٨٣﴾
83. Na hakika katika waliomfuata njia yake (ya tawhiyd) bila shaka ni Ibraahiym.
إِذْ جَاءَ رَبَّهُ بِقَلْبٍ سَلِيمٍ ﴿٨٤﴾
84. Alipomjia Rabb wake kwa moyo uliosalimika.
إِذْ قَالَ لِأَبِيهِ وَقَوْمِهِ مَاذَا تَعْبُدُونَ ﴿٨٥﴾
85. Alipomwambia baba yake na watu wake: “Mnaabudu nini?”
أَئِفْكًا آلِهَةً دُونَ اللَّـهِ تُرِيدُونَ ﴿٨٦﴾
86. “Je, kwa uzushi tu, mnataka waabudiwa badala ya Allaah?”
فَمَا ظَنُّكُم بِرَبِّ الْعَالَمِينَ ﴿٨٧﴾
87. “Basi nini dhana yenu kuhusu Rabb wa walimwengu?”
فَنَظَرَ نَظْرَةً فِي النُّجُومِ ﴿٨٨﴾
88. Akatazama mtazamo katika nyota.
فَقَالَ إِنِّي سَقِيمٌ ﴿٨٩﴾
89. Akasema: “Hakika mimi ni mgonjwa.”
فَتَوَلَّوْا عَنْهُ مُدْبِرِينَ ﴿٩٠﴾
90. Wakaachana naye wakimgeukilia mbali kwenda zao.
فَرَاغَ إِلَىٰ آلِهَتِهِمْ فَقَالَ أَلَا تَأْكُلُونَ ﴿٩١﴾
91. Akaenda kwa siri kwa waabudiwa wao; akasema: “Mbona hamli?
مَا لَكُمْ لَا تَنطِقُونَ ﴿٩٢﴾
92. “Mna nini! Mbona hamsemi?”
فَرَاغَ عَلَيْهِمْ ضَرْبًا بِالْيَمِينِ ﴿٩٣﴾
93. Akayakabili kwa siri akawapiga kwa mkono wa kulia.
فَأَقْبَلُوا إِلَيْهِ يَزِفُّونَ ﴿٩٤﴾
94. (Washirikina) Wakamjia wakiharakiza mbio.
قَالَ أَتَعْبُدُونَ مَا تَنْحِتُونَ ﴿٩٥﴾
95. Akasema: “Je, mnaabudu vile mnavyovichonga?
وَاللَّـهُ خَلَقَكُمْ وَمَا تَعْمَلُونَ ﴿٩٦﴾
96. “Na hali Allaah Amekuumbeni pamoja na vile mnavyovifanya?
قَالُوا ابْنُوا لَهُ بُنْيَانًا فَأَلْقُوهُ فِي الْجَحِيمِ ﴿٩٧﴾
97. Wakasema: “Mjengeeni jengo kisha mtupeni katika moto uwakao vikali mno.”
فَأَرَادُوا بِهِ كَيْدًا فَجَعَلْنَاهُمُ الْأَسْفَلِينَ ﴿٩٨﴾
98. Wakamkusudia hila lakini Tukawafanya wao ndio wa chini kabisa.
وَقَالَ إِنِّي ذَاهِبٌ إِلَىٰ رَبِّي سَيَهْدِينِ ﴿٩٩﴾
99. Akasema: “Hakika mimi ni mwenye kwenda kwa Rabb wangu Ataniongoza.
رَبِّ هَبْ لِي مِنَ الصَّالِحِينَ ﴿١٠٠﴾
100. “Rabb wangu! Nitunukie miongoni mwa Swalihina.”
فَبَشَّرْنَاهُ بِغُلَامٍ حَلِيمٍ ﴿١٠١﴾
101. Basi Tukambashiria ghulamu mpole.
فَلَمَّا بَلَغَ مَعَهُ السَّعْيَ قَالَ يَا بُنَيَّ إِنِّي أَرَىٰ فِي الْمَنَامِ أَنِّي أَذْبَحُكَ فَانظُرْ مَاذَا تَرَىٰ ۚ قَالَ يَا أَبَتِ افْعَلْ مَا تُؤْمَرُ ۖ سَتَجِدُنِي إِن شَاءَ اللَّـهُ مِنَ الصَّابِرِينَ ﴿١٠٢﴾
102. Alipofikia makamo ya kwenda na kurudi pamoja naye; akasema: “Ee mwanangu! Hakika mimi nimeona ndoto usingizini kwamba mimi nakunchinja, basi tazama unaonaje?” (Ismaa’iyl) Akasema: “Ee baba yangu! Fanya yale uliyoamrishwa, utanikuta In Shaa Allaah miongoni mwa wanaosubiri.”
فَلَمَّا أَسْلَمَا وَتَلَّهُ لِلْجَبِينِ ﴿١٠٣﴾
103. Basi wote wawili walipojisalimisha, na akamlaza kifudifudi juu ya kipaji.
وَنَادَيْنَاهُ أَن يَا إِبْرَاهِيمُ ﴿١٠٤﴾
104. Na tukamwita: “Ee Ibraahiym.
قَدْ صَدَّقْتَ الرُّؤْيَا ۚإِنَّا كَذَٰلِكَ نَجْزِي الْمُحْسِنِينَ﴿١٠٥﴾
105. “Kwa yakini umesadikisha ndoto.” Hakika Sisi hivyo ndivyo Tunavyowalipa wafanyao ihsaan.
إِنَّ هَـٰذَا لَهُوَ الْبَلَاءُ الْمُبِينُ ﴿١٠٦﴾
106. Hakika hii bila shaka ni jaribio bayana.
وَفَدَيْنَاهُ بِذِبْحٍ عَظِيمٍ ﴿١٠٧﴾
107. Na Tukamfidia kwa dhabihu adhimu.
وَتَرَكْنَا عَلَيْهِ فِي الْآخِرِينَ ﴿١٠٨﴾
108. Na Tukamuachia (sifa nzuri) kwa karne za baadaye.
سَلَامٌ عَلَىٰ إِبْرَاهِيمَ ﴿١٠٩﴾
109. Amani iwe juu ya Ibraahiym.
كَذَٰلِكَ نَجْزِي الْمُحْسِنِينَ ﴿١١٠﴾
110. Hakika hivyo ndivyo Tunavyolipa wafanyao ihsaan.
إِنَّهُ مِنْ عِبَادِنَا الْمُؤْمِنِينَ ﴿١١١﴾
111. Hakika yeye ni miongoni mwa waja Wetu Waumini.
وَبَشَّرْنَاهُ بِإِسْحَاقَ نَبِيًّا مِّنَ الصَّالِحِينَ ﴿١١٢﴾
112. Na Tukambashiria Is-haaq; Nabiy miongoni mwa Swalihina.
وَبَارَكْنَا عَلَيْهِ وَعَلَىٰ إِسْحَاقَ ۚ وَمِن ذُرِّيَّتِهِمَا مُحْسِنٌ وَظَالِمٌ لِّنَفْسِهِ مُبِينٌ ﴿١١٣﴾
113. Na Tukambarikia yeye na Is-haaq; na katika vizazi vyao wawili kuna mhisani na aliyejidhulumu nafsi yake waziwazi.
وَلَقَدْ مَنَنَّا عَلَىٰ مُوسَىٰ وَهَارُونَ ﴿١١٤﴾
114. Na kwa yakini Tuliwafanyia fadhila Muwsaa na Haaruwun.
وَنَجَّيْنَاهُمَا وَقَوْمَهُمَا مِنَ الْكَرْبِ الْعَظِيمِ ﴿١١٥﴾
115. Na Tukawaokoa wote wawili na watu wao kutokana na janga kuu.
وَنَصَرْنَاهُمْ فَكَانُوا هُمُ الْغَالِبِينَ ﴿١١٦﴾
116. Na Tukawanusuru, basi wakawa wao ndio wenye kushinda.
وَآتَيْنَاهُمَا الْكِتَابَ الْمُسْتَبِينَ ﴿١١٧﴾
117. Na Tukawapa Kitabu kinachojibainisha chenyewe waziwazi.
وَهَدَيْنَاهُمَا الصِّرَاطَ الْمُسْتَقِيمَ ﴿١١٨﴾
118. Na Tukawaongoza njia iliyonyooka.
وَتَرَكْنَا عَلَيْهِمَا فِي الْآخِرِينَ ﴿١١٩﴾
119. Na Tukawaachia (sifa nzuri) kwa karne za baadaye.
سَلَامٌ عَلَىٰ مُوسَىٰ وَهَارُونَ ﴿١٢٠﴾
120. Amani iwe juu ya Muwsaa na Haaruwn.
إِنَّا كَذَٰلِكَ نَجْزِي الْمُحْسِنِينَ ﴿١٢١﴾
121. Hakika hivyo ndivyo Tunavyolipa wafanyao ihsaan.
إِنَّهُمَا مِنْ عِبَادِنَا الْمُؤْمِنِينَ ﴿١٢٢﴾
122. Hakika wao wawili ni miongoni mwa waja Wetu Waumini.
وَإِنَّ إِلْيَاسَ لَمِنَ الْمُرْسَلِينَ ﴿١٢٣﴾
123. Na hakika Iliyaasa bila shaka ni miongoni mwa Rusuli.
إِذْ قَالَ لِقَوْمِهِ أَلَا تَتَّقُونَ ﴿١٢٤﴾
124. Alipowaambia watu wake: “Je, hamtokuwa na taqwa?
أَتَدْعُونَ بَعْلًا وَتَذَرُونَ أَحْسَنَ الْخَالِقِينَ ﴿١٢٥﴾
125. “Mnamwomba (sanamu linaloitwa) ba’laa, na mnaacha Mbora wa wenye kuumba?”
اللَّـهَ رَبَّكُمْ وَرَبَّ آبَائِكُمُ الْأَوَّلِينَ ﴿١٢٦﴾
126. “Allaah Ndiye Rabb wenu na Rabb wa baba zenu wa awali.”
فَكَذَّبُوهُ فَإِنَّهُمْ لَمُحْضَرُونَ ﴿١٢٧﴾
127. Wakamkadhibisha, basi wao bila shaka watahudhurishwa (kuadhibiwa).
إِلَّا عِبَادَ اللَّـهِ الْمُخْلَصِينَ ﴿١٢٨﴾
128. Isipokuwa waja wa Allaah
waliokhitariwa kwa ikhlasi zao.
وَتَرَكْنَا عَلَيْهِ فِي الْآخِرِينَ ﴿١٢٩﴾
129. Na Tukamuachia (sifa nzuri) kwa karne za baadaye.
سَلَامٌ عَلَىٰ إِلْ يَاسِينَ ﴿١٣٠﴾
130. Amani iwe juu ya Ilyaasiyn.
إِنَّا كَذَٰلِكَ نَجْزِي الْمُحْسِنِينَ ﴿١٣١﴾
131. Hakika hivyo ndivyo Tunavyolipa wafanyao ihsaan.
إِنَّهُ مِنْ عِبَادِنَا الْمُؤْمِنِينَ ﴿١٣٢﴾
132. Hakika yeye ni miongoni mwa waja Wetu Waumini.
وَإِنَّ لُوطًا لَّمِنَ الْمُرْسَلِينَ ﴿١٣٣﴾
133. Na hakika Luwtw bila shaka ni miongoni mwa Rusuli.
إِذْ نَجَّيْنَاهُ وَأَهْلَهُ أَجْمَعِينَ ﴿١٣٤﴾
134. Tulipomuokoa na ahli zake wote.
إِلَّا عَجُوزًا فِي الْغَابِرِينَ ﴿١٣٥﴾
135. Isipokuwa (mkewe) Bi mkongwe katika waliobakia nyuma.
ثُمَّ دَمَّرْنَا الْآخَرِينَ ﴿١٣٦﴾
136. Kisha Tukawadamirisha wengineo.
وَإِنَّكُمْ لَتَمُرُّونَ عَلَيْهِم مُّصْبِحِينَ ﴿١٣٧﴾
137. Nanyi bila shaka mnawapitia asubuhi.
وَبِاللَّيْلِ ۗ أَفَلَا تَعْقِلُونَ ﴿١٣٨﴾
138. Na usiku. Je, basi hamtii akilini?
وَإِنَّ يُونُسَ لَمِنَ الْمُرْسَلِينَ ﴿١٣٩﴾
139. Na hakika Yuwnus bila shaka ni miongoni mwa Rusuli.
إِذْ أَبَقَ إِلَى الْفُلْكِ الْمَشْحُونِ ﴿١٤٠﴾
140. Alipokimbilia katika merikebu iliyosheheni.
فَسَاهَمَ فَكَانَ مِنَ الْمُدْحَضِينَ ﴿١٤١﴾
141. Akapiga kura akawa miongoni mwa walioshindwa.
فَالْتَقَمَهُ الْحُوتُ وَهُوَ مُلِيمٌ ﴿١٤٢﴾
142. Basi samaki kubwa likammeza hali ya kuwa ni mwenye kulaumiwa.
فَلَوْلَا أَنَّهُ كَانَ مِنَ الْمُسَبِّحِينَ ﴿١٤٣﴾
143. Na lau kama hakuwa miongoni mwa wenye kumsabbih Allaah.
لَلَبِثَ فِي بَطْنِهِ إِلَىٰ يَوْمِ يُبْعَثُونَ ﴿١٤٤﴾
144. Angelibakia tumboni mwake mpaka Siku watakayofufuliwa.
فَنَبَذْنَاهُ بِالْعَرَاءِ وَهُوَ سَقِيمٌ ﴿١٤٥﴾
145. Basi Tukamtupa kwenye ardhi tupu ufukweni (alipomcheua samaki) naye akiwa mgonjwa.
وَأَنبَتْنَا عَلَيْهِ شَجَرَةً مِّن يَقْطِينٍ ﴿١٤٦﴾
146. Na Tukamuoteshea mti unaotambaa aina ya mung’unya.
وَأَرْسَلْنَاهُ إِلَىٰ مِائَةِ أَلْفٍ أَوْ يَزِيدُونَ ﴿١٤٧﴾
147. Na Tukamtuma kwa (watu wake) laki moja au wanaozidi.
فَآمَنُوا فَمَتَّعْنَاهُمْ إِلَىٰ حِينٍ ﴿١٤٨﴾
148. Wakaamini, basi Tukawastarehesha kwa muda.
فَاسْتَفْتِهِمْ أَلِرَبِّكَ الْبَنَاتُ وَلَهُمُ الْبَنُونَ ﴿١٤٩﴾
149. Waulize (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم): “Je, Rabb wako ndio ana mabanati, na wao ndio wana watoto wa kiume?”
أَمْ خَلَقْنَا الْمَلَائِكَةَ إِنَاثًا وَهُمْ شَاهِدُونَ ﴿١٥٠﴾
150. Au, je Tumewaumba Malaika kuwa wanawake; nao ni wenye kushuhudia?
أَلَا إِنَّهُم مِّنْ إِفْكِهِمْ لَيَقُولُونَ ﴿١٥١﴾
151. Tanabahi! Hakika wao kwa uzushi wanasema:
وَلَدَ اللَّـهُ وَإِنَّهُمْ لَكَاذِبُونَ ﴿١٥٢﴾
152. “Allaah Amezaa.” Na hakika wao bila shaka ni waongo!
أَصْطَفَى الْبَنَاتِ عَلَى الْبَنِينَ ﴿١٥٣﴾
153. Je, Amekhitari mabanati kuliko wana wa kiume?
مَا لَكُمْ كَيْفَ تَحْكُمُونَ ﴿١٥٤﴾
154. Mna nini! Vipi mnahukumu?
أَفَلَا تَذَكَّرُونَ ﴿١٥٥﴾
155. Je, hamkumbuki?
أَمْ لَكُمْ سُلْطَانٌ مُّبِينٌ ﴿١٥٦﴾
156. Je, mna hoja bayana (ya mnayodai)?
فَأْتُوا بِكِتَابِكُمْ إِن كُنتُمْ صَادِقِينَ ﴿١٥٧﴾
157. Basi leteni kitabu chenu mkiwa ni wakweli.
وَجَعَلُوا بَيْنَهُ وَبَيْنَ الْجِنَّةِ نَسَبًا ۚ وَلَقَدْ عَلِمَتِ الْجِنَّةُ إِنَّهُمْ لَمُحْضَرُونَ ﴿١٥٨﴾
158. Na wakafanya baina Yake (Allaah) na baina ya majini unasaba. Na hali majini wamekwishajua kwamba wao bila shaka watahudhurishwa (kuadhibiwa).
سُبْحَانَ اللَّـهِ عَمَّا يَصِفُونَ ﴿١٥٩﴾
159. Subhaana Allaah, Utakasifu ni wa Allaah kutokana na yale wanayoyavumisha.
إِلَّا عِبَادَ اللَّـهِ الْمُخْلَصِينَ ﴿١٦٠﴾
160. Isipokuwa waja wa Allaah waliokhitariwa kwa ikhlasi zao.
فَإِنَّكُمْ وَمَا تَعْبُدُونَ ﴿١٦١﴾
161. Basi hakika nyinyi na vile mnavyoabudu.
مَا أَنتُمْ عَلَيْهِ بِفَاتِنِينَ ﴿١٦٢﴾
162. Hamuwezi kupotosha.
إِلَّا مَنْ هُوَ صَالِ الْجَحِيمِ ﴿١٦٣﴾
163. Isipokuwa yule ambaye amehukumiwa kuingia na kuungua katika moto uwakao vikali mno.
وَمَا مِنَّا إِلَّا لَهُ مَقَامٌ مَّعْلُومٌ ﴿١٦٤﴾
164. Na “Hakuna miongoni mwetu (Malaika) isipokuwa ana mahali maalumu.”
وَإِنَّا لَنَحْنُ الصَّافُّونَ ﴿١٦٥﴾
165. “Na hakika sisi bila shaka tutajipanga safu.”
وَإِنَّا لَنَحْنُ الْمُسَبِّحُونَ ﴿١٦٦﴾
166. “Na hakika sisi bila shaka ni wenye kumsabbih Allaah.”
وَإِن كَانُوا لَيَقُولُونَ ﴿١٦٧﴾
167. Na hakika (washirikina) walikuwa wakisema:
لَوْ أَنَّ عِندَنَا ذِكْرًا مِّنَ الْأَوَّلِينَ ﴿١٦٨﴾
168. “Lau tungelikuwa na ukumbusho kama walivyokuwa wa mwanzo.”
لَكُنَّا عِبَادَ اللَّـهِ الْمُخْلَصِينَ ﴿١٦٩﴾
169. “Bila shaka tungelikuwa waja wa Allaah
waliokhitariwa kwa ikhlasi zao. .”
فَكَفَرُوا بِهِ ۖ فَسَوْفَ يَعْلَمُونَ ﴿١٧٠﴾
170. Lakini wakaikanusha (Qur-aan), basi karibuni watakuja kujua.
وَلَقَدْ سَبَقَتْ كَلِمَتُنَا لِعِبَادِنَا الْمُرْسَلِينَ ﴿١٧١﴾
171. Kwa yakini limekwishasabiki Neno Letu kwa waja Wetu, Rusuli (waliotumwa).
إِنَّهُمْ لَهُمُ الْمَنصُورُونَ ﴿١٧٢﴾
172. Kwamba hakika wao bila shaka ndio wenye kunusuriwa.
وَإِنَّ جُندَنَا لَهُمُ الْغَالِبُونَ ﴿١٧٣﴾
173. Na kwamba hakika jeshi Letu ndilo litakaloshinda.
فَتَوَلَّ عَنْهُمْ حَتَّىٰ حِينٍ ﴿١٧٤﴾
174. Basi waachilie mbali mpaka muda.
وَأَبْصِرْهُمْ فَسَوْفَ يُبْصِرُونَ ﴿١٧٥﴾
175. Na watazame tu, nao karibuni watakuja ona.
أَفَبِعَذَابِنَا يَسْتَعْجِلُونَ ﴿١٧٦﴾
176. Je, wanaharakiza adhabu Yetu?
فَإِذَا نَزَلَ بِسَاحَتِهِمْ فَسَاءَ صَبَاحُ الْمُنذَرِينَ ﴿١٧٧﴾
177. Basi itakapoteremka uwanjani mwao, ubaya ulioje wa asubuhi ya walioonywa.
وَتَوَلَّ عَنْهُمْ حَتَّىٰ حِينٍ ﴿١٧٨﴾
178. Na waachilie mbali mpaka muda.
وَأَبْصِرْ فَسَوْفَ يُبْصِرُونَ ﴿١٧٩﴾
179. Na tazama tu, nao karibuni watakuja ona.
سُبْحَانَ رَبِّكَ رَبِّ الْعِزَّةِ عَمَّا يَصِفُونَ ﴿١٨٠﴾
180. Subhaana Rabbika! Utakasifu ni wa Rabb wako, Rabb Mtukufu kutokana na yale wanayoyavumisha.
وَسَلَامٌ عَلَى الْمُرْسَلِينَ ﴿١٨١﴾
181. Na amani iwe juu ya Rusuli.
وَالْحَمْدُ لِلَّـهِ رَبِّ الْعَالَمِينَ ﴿١٨٢﴾
182. Na AlhamduliLLaah, Himidi Anastahiki Allaah Rabb wa walimwengu.
[1] Mti mchungu wa karaha kabisa motoni.
0 Comments