الْقَصَص
Al-Qaswasw: 28
بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ
طسم ﴿١﴾
1. Twaa Siyn Miym.
تِلْكَ آيَاتُ الْكِتَابِ الْمُبِينِ ﴿٢﴾
2. Hizi ni Aayaat za Kitabu kinachobainisha.
نَتْلُو عَلَيْكَ مِن نَّبَإِ مُوسَىٰ وَفِرْعَوْنَ بِالْحَقِّ لِقَوْمٍ يُؤْمِنُونَ ﴿٣﴾
3. Tunakusomea (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) baadhi ya habari za Muwsaa na Fir’awn kwa haki kwa watu wanaoamini.
إِنَّ فِرْعَوْنَ عَلَا فِي الْأَرْضِ وَجَعَلَ أَهْلَهَا شِيَعًا يَسْتَضْعِفُ طَائِفَةً مِّنْهُمْ يُذَبِّحُ أَبْنَاءَهُمْ وَيَسْتَحْيِي نِسَاءَهُمْ ۚ إِنَّهُ كَانَ مِنَ الْمُفْسِدِينَ ﴿٤﴾
4. Hakika Fir’awn alitakabari katika ardhi, na akawafanya watu wake makundi mbali mbali, akikandamiza kundi miongoni mwao, akiwachinja watoto wao wa kiume na akiacha hai wanawake wao. Hakika yeye alikuwa miongoni mwa mafisadi.
وَنُرِيدُ أَن نَّمُنَّ عَلَى الَّذِينَ اسْتُضْعِفُوا فِي الْأَرْضِ وَنَجْعَلَهُمْ أَئِمَّةً وَنَجْعَلَهُمُ الْوَارِثِينَ ﴿٥﴾
5. Na Tukataka Tuwafanyie fadhila wale waliokandamizwa katika ardhi; na Tuwafanye viongozi na Tuwafanye wenye kurithi.
وَنُمَكِّنَ لَهُمْ فِي الْأَرْضِ وَنُرِيَ فِرْعَوْنَ وَهَامَانَ وَجُنُودَهُمَا مِنْهُم مَّا كَانُوا يَحْذَرُونَ ﴿٦﴾
6. Na Tuwamakinishe kwa uwezo katika ardhi, na Tumwonyeshe Fir’awn na Haamaan na majeshi yao miongoni mwao yale waliyokuwa wakitahadhari.
وَأَوْحَيْنَا إِلَىٰ أُمِّ مُوسَىٰ أَنْ أَرْضِعِيهِ ۖ فَإِذَا خِفْتِ عَلَيْهِ فَأَلْقِيهِ فِي الْيَمِّ وَلَا تَخَافِي وَلَا تَحْزَنِي ۖ إِنَّا رَادُّوهُ إِلَيْكِ وَجَاعِلُوهُ مِنَ الْمُرْسَلِينَ ﴿٧﴾
7. Na Tukamtia ilhamu mama yake Muwsaa kwamba: “Mnyonyeshe. Lakini utakapomkhofia, basi mtupe katika mto na wala usikhofu wala usihuzunike. Hakika Sisi Tutamrudisha kwako, na Tutamfanya miongoni mwa Rusuli”.
فَالْتَقَطَهُ آلُ فِرْعَوْنَ لِيَكُونَ لَهُمْ عَدُوًّا وَحَزَنًا ۗ إِنَّ فِرْعَوْنَ وَهَامَانَ وَجُنُودَهُمَا كَانُوا خَاطِئِينَ ﴿٨﴾
8. Basi wakamwokota watu wa Fir’awn ili awe adui kwao na (sababu ya) huzuni. Hakika Fir’awn na Haamaan na majeshi yao walikuwa wenye makosa.
وَقَالَتِ امْرَأَتُ فِرْعَوْنَ قُرَّتُ عَيْنٍ لِّي وَلَكَ ۖ لَا تَقْتُلُوهُ عَسَىٰ أَن يَنفَعَنَا أَوْ نَتَّخِذَهُ وَلَدًا وَهُمْ لَا يَشْعُرُونَ ﴿٩﴾
9. Na mke wa Fir’awn akasema: “Kiburudisho cha macho kwangu na kwako; usimuue, asaa akatufaa, au tumfanye mwana.” Nao hawatambui.
وَأَصْبَحَ فُؤَادُ أُمِّ مُوسَىٰ فَارِغًا ۖ إِن كَادَتْ لَتُبْدِي بِهِ لَوْلَا أَن رَّبَطْنَا عَلَىٰ قَلْبِهَا لِتَكُونَ مِنَ الْمُؤْمِنِينَ﴿١٠﴾
10. Na ukawa moyo uliojaa hisia wa mama yake Muwsaa mtupu! Alikaribia kumdhihirisha (kuwa ni mwanawe) lau kama Tusingeutia nguvu moyo wake ili awe miongoni mwa Waumini.
وَقَالَتْ لِأُخْتِهِ قُصِّيهِ ۖ فَبَصُرَتْ بِهِ عَن جُنُبٍ وَهُمْ لَا يَشْعُرُونَ ﴿١١﴾
11. Akamwambia dada yake (Muwsaa): “Mfuatilie!” Akamtazama kwa mbali nao hawatambui.
وَحَرَّمْنَا عَلَيْهِ الْمَرَاضِعَ مِن قَبْلُ فَقَالَتْ هَلْ أَدُلُّكُمْ عَلَىٰ أَهْلِ بَيْتٍ يَكْفُلُونَهُ لَكُمْ وَهُمْ لَهُ نَاصِحُونَ﴿١٢﴾
12. Na Tulimharamishia akatae kabisa wanyonyeshaji tangu mwanzo, mpaka akasema: “Je, nikuelekezeni kwa watu wa nyumba watakaomlea kwa ajili yenu, nao watakuwa wenye kumweka vyema kidhati?
فَرَدَدْنَاهُ إِلَىٰ أُمِّهِ كَيْ تَقَرَّ عَيْنُهَا وَلَا تَحْزَنَ وَلِتَعْلَمَ أَنَّ وَعْدَ اللَّـهِ حَقٌّ وَلَـٰكِنَّ أَكْثَرَهُمْ لَا يَعْلَمُونَ﴿١٣﴾
13. Basi Tukamrudisha kwa mama yake ili yaburudike macho yake na wala asihuzunike, na ili ajue kwamba ahadi ya Allaah ni kweli, lakini wengi wao hawajui.
وَلَمَّا بَلَغَ أَشُدَّهُ وَاسْتَوَىٰ آتَيْنَاهُ حُكْمًا وَعِلْمًا ۚ وَكَذَٰلِكَ نَجْزِي الْمُحْسِنِينَ ﴿١٤﴾
14. Na alipofikia umri wa kupevuka na akaimarika sawasawa, Tulimpa hikma na elimu. Na hivyo ndivyo Tunavyowalipa wafanyao ihsaan.
وَدَخَلَ الْمَدِينَةَ عَلَىٰ حِينِ غَفْلَةٍ مِّنْ أَهْلِهَا فَوَجَدَ فِيهَا رَجُلَيْنِ يَقْتَتِلَانِ هَـٰذَا مِن شِيعَتِهِ وَهَـٰذَا مِنْ عَدُوِّهِ ۖ فَاسْتَغَاثَهُ الَّذِي مِن شِيعَتِهِ عَلَى الَّذِي مِنْ عَدُوِّهِ فَوَكَزَهُ مُوسَىٰ فَقَضَىٰ عَلَيْهِ ۖ قَالَ هَـٰذَا مِنْ عَمَلِ الشَّيْطَانِ ۖ إِنَّهُ عَدُوٌّ مُّضِلٌّ مُّبِينٌ ﴿١٥﴾
15. Na akaingia mjini wakati watu wake wako katika mighafiliko, akakuta humo watu wawili wanapigana; mmoja ni miongoni mwa kundi lake, na mwengine miongoni mwa adui wake. Akamsaidia kumuokoa yule ambaye katika kundi lake dhidi ya yule ambaye ni katika adui wake, Muwsaa akampiga ngumi, akamuua. Akasema: “Hii ni kutokana na kitendo cha shaytwaan. Hakika yeye ni adui mpotoaji bayana.”
قَالَ رَبِّ إِنِّي ظَلَمْتُ نَفْسِي فَاغْفِرْ لِي فَغَفَرَ لَهُ ۚ إِنَّهُ هُوَ الْغَفُورُ الرَّحِيمُ ﴿١٦﴾
16. Akasema: “Rabb wangu! Hakika mimi nimejidhulumu nafsi yangu, basi Nighufurie; Akamghufuria. Hakika Yeye ni Mwingi wa kughufuria, Mwenye kurehemu.
قَالَ رَبِّ بِمَا أَنْعَمْتَ عَلَيَّ فَلَنْ أَكُونَ ظَهِيرًا لِّلْمُجْرِمِينَ ﴿١٧﴾
17. Akasema: “Rabb wangu! Kwa Uliyonineemesha; sitokuwa kamwe msaidizi kwa wahalifu.”
فَأَصْبَحَ فِي الْمَدِينَةِ خَائِفًا يَتَرَقَّبُ فَإِذَا الَّذِي اسْتَنصَرَهُ بِالْأَمْسِ يَسْتَصْرِخُهُ ۚ قَالَ لَهُ مُوسَىٰ إِنَّكَ لَغَوِيٌّ مُّبِينٌ ﴿١٨﴾
18. Akapambaukiwa kuwa mwenye khofu katika mji ule anaangaza kwa tahadhari. Basi mara yule aliyemuomba amnusuru jana anampigia kelele amsaidie. Muwsaa akamwambia: “Hakika wewe ni mpotofu bayana”.
فَلَمَّا أَنْ أَرَادَ أَن يَبْطِشَ بِالَّذِي هُوَ عَدُوٌّ لَّهُمَا قَالَ يَا مُوسَىٰ أَتُرِيدُ أَن تَقْتُلَنِي كَمَا قَتَلْتَ نَفْسًا بِالْأَمْسِۖ إِن تُرِيدُ إِلَّا أَن تَكُونَ جَبَّارًا فِي الْأَرْضِ وَمَا تُرِيدُ أَن تَكُونَ مِنَ الْمُصْلِحِينَ ﴿١٩﴾
19. Kisha alipotaka amkamate yule aliye adui wao wote wawili, akasema: “Ee Muwsaa! Je, unataka kuniua kama ulivyomuua mtu jana? Hutaki lolote isipokuwa unataka uwe jabari katika nchi, na wala hutaki kuwa miongoni mwa wasuluhishaji.”
وَجَاءَ رَجُلٌ مِّنْ أَقْصَى الْمَدِينَةِ يَسْعَىٰ قَالَ يَا مُوسَىٰ إِنَّ الْمَلَأَ يَأْتَمِرُونَ بِكَ لِيَقْتُلُوكَ فَاخْرُجْ إِنِّي لَكَ مِنَ النَّاصِحِينَ ﴿٢٠﴾
20. Akaja mtu kutoka pande ya mbali ya mji ule akiwa anakimbia; akasema: “Ee Muwsaa! Hakika wakuu wanashauriana dhidi yako ili wakuue; basi toka hakika mimi ni miongoni mwa wanaokunasihi.”
فَخَرَجَ مِنْهَا خَائِفًا يَتَرَقَّبُ ۖ قَالَ رَبِّ نَجِّنِي مِنَ الْقَوْمِ الظَّالِمِينَ ﴿٢١﴾
21. Basi akatoka humo akiwa na khofu anaangaza kwa tahadhari. Akasema: “Rabb wangu! Niokoe na watu madhalimu.”
وَلَمَّا تَوَجَّهَ تِلْقَاءَ مَدْيَنَ قَالَ عَسَىٰ رَبِّي أَن يَهْدِيَنِي سَوَاءَ السَّبِيلِ ﴿٢٢﴾
22. Na alipoelekea upande wa wa Madyan, akasema: “Asaa Rabb wangu Akaniongoza njia iliyo sawa.”
وَلَمَّا وَرَدَ مَاءَ مَدْيَنَ وَجَدَ عَلَيْهِ أُمَّةً مِّنَ النَّاسِ يَسْقُونَ وَوَجَدَ مِن دُونِهِمُ امْرَأَتَيْنِ تَذُودَانِ ۖ قَالَ مَا خَطْبُكُمَا ۖ قَالَتَا لَا نَسْقِي حَتَّىٰ يُصْدِرَ الرِّعَاءُ ۖ وَأَبُونَا شَيْخٌ كَبِيرٌ ﴿٢٣﴾
23. Alipofikia maji ya Madyan; alikuta kundi la watu linanywesha maji (wanyama wao), na akakuta kando yake wanawake wawili wanawazuia (wanyama wao); Akasema: “Mna nini?” Wakasema: “Hatunyweshi mpaka waondoke wachungaji, na baba yetu ni mtu mzima sana.”
فَسَقَىٰ لَهُمَا ثُمَّ تَوَلَّىٰ إِلَى الظِّلِّ فَقَالَ رَبِّ إِنِّي لِمَا أَنزَلْتَ إِلَيَّ مِنْ خَيْرٍ فَقِيرٌ ﴿٢٤﴾
24. Basi akawanyweshea, kisha akageuka kwenda kivulini, akasema: “Rabb wangu! Hakika mimi ni mhitajia wa kheri yoyote Utakayoniteremshia.”
فَجَاءَتْهُ إِحْدَاهُمَا تَمْشِي عَلَى اسْتِحْيَاءٍ قَالَتْ إِنَّ أَبِي يَدْعُوكَ لِيَجْزِيَكَ أَجْرَ مَا سَقَيْتَ لَنَا ۚ فَلَمَّا جَاءَهُ وَقَصَّ عَلَيْهِ الْقَصَصَ قَالَ لَا تَخَفْ ۖ نَجَوْتَ مِنَ الْقَوْمِ الظَّالِمِينَ ﴿٢٥﴾
25. Basi akamjia mmoja kati ya wanawake wawili akitembea kwa kuona hayaa; akasema: “Baba yangu anakwita ili akulipe ujira wa kutunyweshea.” Basi alipomfikia na akamsimulia visa vyake; alisema: “Usikhofu, umeokoka na watu madhalimu.”
قَالَتْ إِحْدَاهُمَا يَا أَبَتِ اسْتَأْجِرْهُ ۖ إِنَّ خَيْرَ مَنِ اسْتَأْجَرْتَ الْقَوِيُّ الْأَمِينُ ﴿٢٦﴾
26. Mmoja wao akasema: “Ee baba yangu, muajiri! Hakika mbora uwezaye kumwajiri ni mwenye nguvu mwaminifu.”
قَالَ إِنِّي أُرِيدُ أَنْ أُنكِحَكَ إِحْدَى ابْنَتَيَّ هَاتَيْنِ عَلَىٰ أَن تَأْجُرَنِي ثَمَانِيَ حِجَجٍ ۖ فَإِنْ أَتْمَمْتَ عَشْرًا فَمِنْ عِندِكَ ۖ وَمَا أُرِيدُ أَنْ أَشُقَّ عَلَيْكَ ۚ سَتَجِدُنِي إِن شَاءَ اللَّـهُ مِنَ الصَّالِحِينَ ﴿٢٧﴾
27. Akasema: “Mimi nataka nikuozeshe mmoja wapo wa binti zangu hawa wawili kwa sharti kuwa unitumikie miaka minane; ukitimiza kumi, basi ni kutoka kwako. Na wala sitaki kukutia mashakani; utanikuta In Shaa Allaah miongoni mwa Swalihina.”
قَالَ ذَٰلِكَ بَيْنِي وَبَيْنَكَ ۖ أَيَّمَا الْأَجَلَيْنِ قَضَيْتُ فَلَا عُدْوَانَ عَلَيَّ ۖ وَاللَّـهُ عَلَىٰ مَا نَقُولُ وَكِيلٌ ﴿٢٨﴾
28. (Muwsaa) Akasema: “Hayo ni baina yangu na baina yako. Muda wowote kati ya miwili nitakaoutimiza basi hakuna uadui juu yangu. Na Allaah juu ya yale tunayoyasema ni Mdhamini.”
فَلَمَّا قَضَىٰ مُوسَى الْأَجَلَ وَسَارَ بِأَهْلِهِ آنَسَ مِن جَانِبِ الطُّورِ نَارًا قَالَ لِأَهْلِهِ امْكُثُوا إِنِّي آنَسْتُ نَارًا لَّعَلِّي آتِيكُم مِّنْهَا بِخَبَرٍ أَوْ جَذْوَةٍ مِّنَ النَّارِ لَعَلَّكُمْ تَصْطَلُونَ ﴿٢٩﴾
29. Basi Muwsaa alipotimiza muda, akasafiri pamoja na ahli zake, akaona moto upande wa jabali. Akawaambia ahli zake: “Bakieni; hakika mimi nimeona moto, huenda nikakuleteeni kutoka humo habari, au kijinga cha moto ili mpate kuota moto.”
فَلَمَّا أَتَاهَا نُودِيَ مِن شَاطِئِ الْوَادِ الْأَيْمَنِ فِي الْبُقْعَةِ الْمُبَارَكَةِ مِنَ الشَّجَرَةِ أَن يَا مُوسَىٰ إِنِّي أَنَا اللَّـهُ رَبُّ الْعَالَمِينَ ﴿٣٠﴾
30. Basi alipoufikia, akaitwa kutoka upande wa kulia wa bonde katika sehemu iliyobarikiwa kutoka mtini kwamba: “Ee Muwsaa! Hakika Mimi ni Allaah, Rabb wa walimwengu.”
وَأَنْ أَلْقِ عَصَاكَ ۖ فَلَمَّا رَآهَا تَهْتَزُّ كَأَنَّهَا جَانٌّ وَلَّىٰ مُدْبِرًا وَلَمْ يُعَقِّبْ ۚ يَا مُوسَىٰ أَقْبِلْ وَلَا تَخَفْ ۖ إِنَّكَ مِنَ الْآمِنِينَ ﴿٣١﴾
31. Na tupa fimbo yako!” Basi alipoiona inataharuki kama kwamba ni nyoka; aligeuka kukimbia bila kutazama nyuma wala hakurudi. “Ee Muwsaa! Njoo mbele, na wala usikhofu! Hakika wewe ni miongoni mwa waliokuwa katika amani.”
اسْلُكْ يَدَكَ فِي جَيْبِكَ تَخْرُجْ بَيْضَاءَ مِنْ غَيْرِ سُوءٍ وَاضْمُمْ إِلَيْكَ جَنَاحَكَ مِنَ الرَّهْبِ ۖ فَذَانِكَ بُرْهَانَانِ مِن رَّبِّكَ إِلَىٰ فِرْعَوْنَ وَمَلَئِهِ ۚ إِنَّهُمْ كَانُوا قَوْمًا فَاسِقِينَ ﴿٣٢﴾
32. “Ingiza mkono wako kifuani katika uwazi wa nguo yako, utatoka kuwa mweupe bila ya dhara yoyote. Na ambatisha ubavuni mwako kujikinga na khofu. Hizo ni dalili mbili za wazi kutoka kwa Rabb wako kwa Fir’awn na wakuu wake; hakika wao walikuwa watu mafasiki.”
قَالَ رَبِّ إِنِّي قَتَلْتُ مِنْهُمْ نَفْسًا فَأَخَافُ أَن يَقْتُلُونِ ﴿٣٣﴾
33. Akasema: “Rabb wangu! Hakika mimi nimeua mtu miongoni mwao, na nakhofu wataniua.”
وَأَخِي هَارُونُ هُوَ أَفْصَحُ مِنِّي لِسَانًا فَأَرْسِلْهُ مَعِيَ رِدْءًا يُصَدِّقُنِي ۖ إِنِّي أَخَافُ أَن يُكَذِّبُونِ ﴿٣٤﴾
34. “Na kaka yangu Haaruwn yeye ana ufasaha zaidi wa lisani kuliko mimi, basi mpeleke pamoja nami, kama msaidizi wangu anisadikishe; hakika mimi nakhofu watanikadhibisha.”
قَالَ سَنَشُدُّ عَضُدَكَ بِأَخِيكَ وَنَجْعَلُ لَكُمَا سُلْطَانًا فَلَا يَصِلُونَ إِلَيْكُمَا ۚ بِآيَاتِنَا أَنتُمَا وَمَنِ اتَّبَعَكُمَا الْغَالِبُونَ ﴿٣٥﴾
35. (Allaah) Akasema: “Tutautia nguvu mkono wako kwa kaka yako, na Tutakupeni madaraka, basi hawatakufikilieni. Kwa sababu ya Aayaat (ishara, dalili) Zetu, nyinyi wawili na watakaokufuateni mtashinda.
فَلَمَّا جَاءَهُم مُّوسَىٰ بِآيَاتِنَا بَيِّنَاتٍ قَالُوا مَا هَـٰذَا إِلَّا سِحْرٌ مُّفْتَرًى وَمَا سَمِعْنَا بِهَـٰذَا فِي آبَائِنَا الْأَوَّلِينَ﴿٣٦﴾
36. Basi Muwsaa alipowajia (kina Fir’awn) kwa Aayaat (ishara, dalili) Zetu bayana; wakasema: “Hii si chochote isipokuwa ni sihiri iliyotungwa; na hatukusikia haya kwa baba zetu wa awali.”
وَقَالَ مُوسَىٰ رَبِّي أَعْلَمُ بِمَن جَاءَ بِالْهُدَىٰ مِنْ عِندِهِ وَمَن تَكُونُ لَهُ عَاقِبَةُ الدَّارِ ۖ إِنَّهُ لَا يُفْلِحُ الظَّالِمُونَ ﴿٣٧﴾
37. Muwsaa akasema: “Rabb wangu Anajua zaidi yule ajaye kwa mwongozo kutoka Kwake, na yule atakayekuwa na hatima njema ya makazi Aakhirah; hakika madhalimu hawafaulu.”
وَقَالَ فِرْعَوْنُ يَا أَيُّهَا الْمَلَأُ مَا عَلِمْتُ لَكُم مِّنْ إِلَـٰهٍ غَيْرِي فَأَوْقِدْ لِي يَا هَامَانُ عَلَى الطِّينِ فَاجْعَل لِّي صَرْحًا لَّعَلِّي أَطَّلِعُ إِلَىٰ إِلَـٰهِ مُوسَىٰ وَإِنِّي لَأَظُنُّهُ مِنَ الْكَاذِبِينَ ﴿٣٨﴾
38. Fir’awn akasema: “Enyi wakuu! Sijui kama mnaye mwabudiwa badala yangu; basi niwashie moto ewe Haamaan juu ya unichomee udongo ili unifanyie mnara mrefu ili nimwangalie Ilaah wa Muwsaa, na hakika mimi bila shaka namdhania ni miongoni mwa waongo.”
وَاسْتَكْبَرَ هُوَ وَجُنُودُهُ فِي الْأَرْضِ بِغَيْرِ الْحَقِّ وَظَنُّوا أَنَّهُمْ إِلَيْنَا لَا يُرْجَعُونَ ﴿٣٩﴾
39. (Fir’awn) Akatakabari yeye na jeshi lake katika ardhi bila ya haki, na wakadhania kwamba wao Kwetu hawatorejeshwa.
فَأَخَذْنَاهُ وَجُنُودَهُ فَنَبَذْنَاهُمْ فِي الْيَمِّ ۖ فَانظُرْ كَيْفَ كَانَ عَاقِبَةُ الظَّالِمِينَ ﴿٤٠﴾
40. Basi Tukamchukua na jeshi lake, Tukawatupilia mbali baharini; basi tazama vipi ilikuwa hatima ya madhalimu.
وَجَعَلْنَاهُمْ أَئِمَّةً يَدْعُونَ إِلَى النَّارِ ۖ وَيَوْمَ الْقِيَامَةِ لَا يُنصَرُونَ ﴿٤١﴾
41. Na Tukawafanya viongozi wanaolingania motoni; na Siku ya Qiyaamah hawatonusuriwa.
وَأَتْبَعْنَاهُمْ فِي هَـٰذِهِ الدُّنْيَا لَعْنَةً ۖ وَيَوْمَ الْقِيَامَةِ هُم مِّنَ الْمَقْبُوحِينَ ﴿٤٢﴾
42. Na Tukawafuatishia laana katika dunia hii; na Siku ya Qiyaamah wao ni miongoni mwa wenye kubaidishwa (rahmah ya Allaah).
وَلَقَدْ آتَيْنَا مُوسَى الْكِتَابَ مِن بَعْدِ مَا أَهْلَكْنَا الْقُرُونَ الْأُولَىٰ بَصَائِرَ لِلنَّاسِ وَهُدًى وَرَحْمَةً لَّعَلَّهُمْ يَتَذَكَّرُونَ ﴿٤٣﴾
43. Na kwa yakini Tulimpa Muwsaa Kitabu baada ya kuwa Tumeshaangamiza karne za awali kiwe ni kifumbuzi macho kwa watu, na mwongozo na rahmah ili wakumbuke.
وَمَا كُنتَ بِجَانِبِ الْغَرْبِيِّ إِذْ قَضَيْنَا إِلَىٰ مُوسَى الْأَمْرَ وَمَا كُنتَ مِنَ الشَّاهِدِينَ ﴿٤٤﴾
44. Na wala hukuweko (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) kando ya Magharibi (ya jabali) Tulipomkidhia Muwsaa amri, na wala hukuwa miongoni mwa walioshuhudia.
وَلَـٰكِنَّا أَنشَأْنَا قُرُونًا فَتَطَاوَلَ عَلَيْهِمُ الْعُمُرُ ۚ وَمَا كُنتَ ثَاوِيًا فِي أَهْلِ مَدْيَنَ تَتْلُو عَلَيْهِمْ آيَاتِنَا وَلَـٰكِنَّا كُنَّا مُرْسِلِينَ ﴿٤٥﴾
45. Lakini Tulianzisha karne nyingi ukawatawilikia umri. Na wala hukuwa mkaazi katika watu wa Madyan ukiwasomea Aayaat Zetu, lakini Sisi Tulikuwa Watumaji (Rusuli).
وَمَا كُنتَ بِجَانِبِ الطُّورِ إِذْ نَادَيْنَا وَلَـٰكِن رَّحْمَةً مِّن رَّبِّكَ لِتُنذِرَ قَوْمًا مَّا أَتَاهُم مِّن نَّذِيرٍ مِّن قَبْلِكَ لَعَلَّهُمْ يَتَذَكَّرُونَ ﴿٤٦﴾
46. Na wala hukuwa (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) kando ya jabali Tuliponadi, lakini ni rahmah kutoka kwa Rabb wako ili uonye watu ambao hawakufikiwa na mwonyaji yeyote kabla yako ili wapate kukumbuka.
وَلَوْلَا أَن تُصِيبَهُم مُّصِيبَةٌ بِمَا قَدَّمَتْ أَيْدِيهِمْ فَيَقُولُوا رَبَّنَا لَوْلَا أَرْسَلْتَ إِلَيْنَا رَسُولًا فَنَتَّبِعَ آيَاتِكَ وَنَكُونَ مِنَ الْمُؤْمِنِينَ ﴿٤٧﴾
47. Na usije ukawasibu msiba kwa yale iliyotanguliza mikono yao, wakasema: “Rabb wetu! Kwanini Hukututumia Rasuli tukafuata Aayaat Zako, na tuwe miongoni mwa Waumini.”
فَلَمَّا جَاءَهُمُ الْحَقُّ مِنْ عِندِنَا قَالُوا لَوْلَا أُوتِيَ مِثْلَ مَا أُوتِيَ مُوسَىٰ ۚ أَوَلَمْ يَكْفُرُوا بِمَا أُوتِيَ مُوسَىٰ مِن قَبْلُ ۖ قَالُوا سِحْرَانِ تَظَاهَرَا وَقَالُوا إِنَّا بِكُلٍّ كَافِرُونَ ﴿٤٨﴾
48. Basi ilipowajia haki kutoka Kwetu, walisema: “Mbona hakupewa mfano wa yale aliyopewa Muwsaa? Je, kwani hawakuyakufuru yale aliyopewa Muwsaa kabla? Wakasema: “Sihri mbili; (Tawraat na Qur-aan) zimesaidiana.” Na wakasema: “Hakika sisi kwa vyote viwili ni wenye kuvikanusha.”
قُلْ فَأْتُوا بِكِتَابٍ مِّنْ عِندِ اللَّـهِ هُوَ أَهْدَىٰ مِنْهُمَا أَتَّبِعْهُ إِن كُنتُمْ صَادِقِينَ ﴿٤٩﴾
49. Sema: “Leteni Kitabu kutoka kwa Allaah ambacho ni mwongozo zaidi kuliko hivyo viwili nikifuate, mkiwa ni wakweli.
فَإِن لَّمْ يَسْتَجِيبُوا لَكَ فَاعْلَمْ أَنَّمَا يَتَّبِعُونَ أَهْوَاءَهُمْ ۚ وَمَنْ أَضَلُّ مِمَّنِ اتَّبَعَ هَوَاهُ بِغَيْرِ هُدًى مِّنَ اللَّـهِ ۚإِنَّ اللَّـهَ لَا يَهْدِي الْقَوْمَ الظَّالِمِينَ ﴿٥٠﴾
50. Na wasipokuitikia basi juwa kwamba hakika wanafuata hawaa zao. Na nani mpotofu zaidi kuliko yule aliyefuata hawaa zake bila ya Mwongozo kutoka kwa Allaah? Hakika Allaah Haongoi watu madhalimu.
وَلَقَدْ وَصَّلْنَا لَهُمُ الْقَوْلَ لَعَلَّهُمْ يَتَذَكَّرُونَ ﴿٥١﴾
51. Na kwa yakini Tumewafuatilishia na kuwateremshia sehemu kwa sehemu ya Neno ili wapate kukumbuka.
الَّذِينَ آتَيْنَاهُمُ الْكِتَابَ مِن قَبْلِهِ هُم بِهِ يُؤْمِنُونَ ﴿٥٢﴾
52. Wale Tuliowapa Kitabu kabla yake, wao wanaiamini (Qur-aan).
وَإِذَا يُتْلَىٰ عَلَيْهِمْ قَالُوا آمَنَّا بِهِ إِنَّهُ الْحَقُّ مِن رَّبِّنَا إِنَّا كُنَّا مِن قَبْلِهِ مُسْلِمِينَ ﴿٥٣﴾
53. Na wanaposomewa husema: “Tumeiamini, hakika hiyo ni haki kutoka Rabb wetu, hakika Sisi kabla yake tumekuwa Waislamu.”
أُولَـٰئِكَ يُؤْتَوْنَ أَجْرَهُم مَّرَّتَيْنِ بِمَا صَبَرُوا وَيَدْرَءُونَ بِالْحَسَنَةِ السَّيِّئَةَ وَمِمَّا رَزَقْنَاهُمْ يُنفِقُونَ ﴿٥٤﴾
54. Hao watapewa ujira wao mara mbili kwa vile walivyosubiri, na wanazuia ubaya kwa wema, na katika vile Tulivyowaruzuku hutoa.
وَإِذَا سَمِعُوا اللَّغْوَ أَعْرَضُوا عَنْهُ وَقَالُوا لَنَا أَعْمَالُنَا وَلَكُمْ أَعْمَالُكُمْ سَلَامٌ عَلَيْكُمْ لَا نَبْتَغِي الْجَاهِلِينَ﴿٥٥﴾
55. Na wanaposikia maneno ya upuuzi hujitenga nayo; na husema: “Sisi tuna ‘amali zetu, nanyi mna ‘amali zenu. Salaamun ‘alaykum! Amani iwe juu yenu hatutafuti majahili.”
إِنَّكَ لَا تَهْدِي مَنْ أَحْبَبْتَ وَلَـٰكِنَّ اللَّـهَ يَهْدِي مَن يَشَاءُ ۚ وَهُوَ أَعْلَمُ بِالْمُهْتَدِينَ ﴿٥٦﴾
56. Hakika wewe huwezi kumhidi umpendaye; lakini Allaah Humhidi Amtakaye, Naye Anawajua zaidi wenye kuongoka.
وَقَالُوا إِن نَّتَّبِعِ الْهُدَىٰ مَعَكَ نُتَخَطَّفْ مِنْ أَرْضِنَا ۚ أَوَلَمْ نُمَكِّن لَّهُمْ حَرَمًا آمِنًا يُجْبَىٰ إِلَيْهِ ثَمَرَاتُ كُلِّ شَيْءٍ رِّزْقًا مِّن لَّدُنَّا وَلَـٰكِنَّ أَكْثَرَهُمْ لَا يَعْلَمُونَ ﴿٥٧﴾
57. Wakasema: “Tukifuata Mwongozo pamoja nawe tutanyakuliwa kutoka ardhi yetu. Je, kwani hatukuwamakinisha mahali patukufu, na pa amani ambako huletewa mazao ya kila kitu kuwa ni riziki kutoka Kwetu; lakini wengi wao hawajui.
وَكَمْ أَهْلَكْنَا مِن قَرْيَةٍ بَطِرَتْ مَعِيشَتَهَا ۖ فَتِلْكَ مَسَاكِنُهُمْ لَمْ تُسْكَن مِّن بَعْدِهِمْ إِلَّا قَلِيلًا ۖ وَكُنَّا نَحْنُ الْوَارِثِينَ ﴿٥٨﴾
58. Na miji mingapi Tumeiangamiza imepinduka mipaka mno ya kanusha haki na neema za maisha yake? Basi hayo ni masikani yao yasiyokaliwa baada yao isipokuwa kidogo tu. Na Tukawa Sisi Warithi.
وَمَا كَانَ رَبُّكَ مُهْلِكَ الْقُرَىٰ حَتَّىٰ يَبْعَثَ فِي أُمِّهَا رَسُولًا يَتْلُو عَلَيْهِمْ آيَاتِنَا ۚ وَمَا كُنَّا مُهْلِكِي الْقُرَىٰ إِلَّا وَأَهْلُهَا ظَالِمُونَ ﴿٥٩﴾
59. Na Rabb wako Hakuwa Mwenye kuangamiza miji mpaka Apeleke katika miji mikuu yake Rasuli awasomee Aayaat Zetu. Na Hatukuwa Wenye kuangamiza miji isipokuwa watu wake wawe madhalimu.
وَمَا أُوتِيتُم مِّن شَيْءٍ فَمَتَاعُ الْحَيَاةِ الدُّنْيَا وَزِينَتُهَا ۚ وَمَا عِندَ اللَّـهِ خَيْرٌ وَأَبْقَىٰ ۚ أَفَلَا تَعْقِلُونَ ﴿٦٠﴾
60. Na chochote mlichopewa katika vitu, basi ni starehe za uhai wa dunia na mapambo yake. Na yaliyoko kwa Allaah ni bora zaidi na yakubakia. Je, basi hamtii akilini?
أَفَمَن وَعَدْنَاهُ وَعْدًا حَسَنًا فَهُوَ لَاقِيهِ كَمَن مَّتَّعْنَاهُ مَتَاعَ الْحَيَاةِ الدُّنْيَا ثُمَّ هُوَ يَوْمَ الْقِيَامَةِ مِنَ الْمُحْضَرِينَ ﴿٦١﴾
61. Je, yule Tuliyemuahidi ahadi nzuri kisha yeye atakutana nayo, ni sawa na yule Tuliyemstarehesha starehe za uhai wa dunia, kisha yeye Siku ya Qiyaamah ni miongoni mwa watakaohudhurishwa?
وَيَوْمَ يُنَادِيهِمْ فَيَقُولُ أَيْنَ شُرَكَائِيَ الَّذِينَ كُنتُمْ تَزْعُمُونَ ﴿٦٢﴾
62. Na Siku (Allaah) Atakayowaita; Atasema: “Wako wapi hao mliokuwa mnadai kwa dhana kuwa ni washirika Wangu? “
قَالَ الَّذِينَ حَقَّ عَلَيْهِمُ الْقَوْلُ رَبَّنَا هَـٰؤُلَاءِ الَّذِينَ أَغْوَيْنَا أَغْوَيْنَاهُمْ كَمَا غَوَيْنَا ۖ تَبَرَّأْنَا إِلَيْكَ ۖ مَا كَانُوا إِيَّانَا يَعْبُدُونَ ﴿٦٣﴾
63. Watasema wale iliyowathibitikia kauli: “Rabb wetu! Hawa ndio wale tuliowapotoa. Tumewapotoa kama tulivyopotoka. Tumejitoa hatiani mbele Yako, hawakuwa wakituabudu sisi.”
وَقِيلَ ادْعُوا شُرَكَاءَكُمْ فَدَعَوْهُمْ فَلَمْ يَسْتَجِيبُوا لَهُمْ وَرَأَوُا الْعَذَابَ ۚ لَوْ أَنَّهُمْ كَانُوا يَهْتَدُونَ ﴿٦٤﴾
64. Na itasemwa: “Iteni washirika wenu.” Watawaita lakini hawatowaitikia; na wataiona adhabu, laiti wao wangelikuwa wameongoka.
وَيَوْمَ يُنَادِيهِمْ فَيَقُولُ مَاذَا أَجَبْتُمُ الْمُرْسَلِينَ ﴿٦٥﴾
65. Na Siku (Allaah) Atakapowaita, Atasema: “Mliwajibu nini Rusuli?
فَعَمِيَتْ عَلَيْهِمُ الْأَنبَاءُ يَوْمَئِذٍ فَهُمْ لَا يَتَسَاءَلُونَ ﴿٦٦﴾
66. Basi zitawafichikia habari Siku hiyo, nao hawatoweza kuulizana.
فَأَمَّا مَن تَابَ وَآمَنَ وَعَمِلَ صَالِحًا فَعَسَىٰ أَن يَكُونَ مِنَ الْمُفْلِحِينَ ﴿٦٧﴾
67. Ama yule aliyetubu na akaamini na akatenda mema, basi asaa akawa miongoni mwa waliofaulu.
وَرَبُّكَ يَخْلُقُ مَا يَشَاءُ وَيَخْتَارُ ۗ مَا كَانَ لَهُمُ الْخِيَرَةُ ۚ سُبْحَانَ اللَّـهِ وَتَعَالَىٰ عَمَّا يُشْرِكُونَ ﴿٦٨﴾
68. Na Rabb wako Anaumba na Anachagua Atakavyo. Haikuwa wao wana khiari yoyote. Subhaana-Allaah Utakasifu ni wa Allaah na Ametukuka kwa ‘Uluwa kutokana na yale yote wanayomshirikisha.
وَرَبُّكَ يَعْلَمُ مَا تُكِنُّ صُدُورُهُمْ وَمَا يُعْلِنُونَ ﴿٦٩﴾
69. Na Rabb wako Anayajua yale yanayoficha vifua vyao, na yale wanayoyafichua.
وَهُوَ اللَّـهُ لَا إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ ۖ لَهُ الْحَمْدُ فِي الْأُولَىٰ وَالْآخِرَةِ ۖ وَلَهُ الْحُكْمُ وَإِلَيْهِ تُرْجَعُونَ ﴿٧٠﴾
70. Naye ni Allaah, Hakuna Muabudiwa wa haki ila Yeye. Ni Zake Pekee Himidi za mwanzoni (duniani) na za Aakhirah. Na hukumu ni Yake Pekee, na Kwake Pekee mtarejeshwa.
قُلْ أَرَأَيْتُمْ إِن جَعَلَ اللَّـهُ عَلَيْكُمُ اللَّيْلَ سَرْمَدًا إِلَىٰ يَوْمِ الْقِيَامَةِ مَنْ إِلَـٰهٌ غَيْرُ اللَّـهِ يَأْتِيكُم بِضِيَاءٍ ۖ أَفَلَا تَسْمَعُونَ ﴿٧١﴾
71. Sema: “Je, mnaonaje kama Allaah Angelikufanyieni usiku unaendelea daima dawamu mpaka Siku ya Qiyaamah, nani mwabudiwa ghairi ya Allaah Atakayekuleteeni mwanga? Je, basi hamsikii?”
قُلْ أَرَأَيْتُمْ إِن جَعَلَ اللَّـهُ عَلَيْكُمُ النَّهَارَ سَرْمَدًا إِلَىٰ يَوْمِ الْقِيَامَةِ مَنْ إِلَـٰهٌ غَيْرُ اللَّـهِ يَأْتِيكُم بِلَيْلٍ تَسْكُنُونَ فِيهِ ۖ أَفَلَا تُبْصِرُونَ ﴿٧٢﴾
72. Sema: “Je, mnaonaje kama Allaah Angelikufanyieni mchana unaendelea daima dawamu mpaka Siku ya Qiyaamah, nani mwabudiwa ghairi ya Allaah Atakayekuleteeni usiku mpate utulivu humo? Je, basi hamuoni?”
وَمِن رَّحْمَتِهِ جَعَلَ لَكُمُ اللَّيْلَ وَالنَّهَارَ لِتَسْكُنُوا فِيهِ وَلِتَبْتَغُوا مِن فَضْلِهِ وَلَعَلَّكُمْ تَشْكُرُونَ ﴿٧٣﴾
73. Na kutokana na rahmah Yake, Amekufanyieni usiku na mchana ili mpate utulivu humo, na ili mpate kutafuta katika fadhila Zake, na ili mpate kushukuru.
وَيَوْمَ يُنَادِيهِمْ فَيَقُولُ أَيْنَ شُرَكَائِيَ الَّذِينَ كُنتُمْ تَزْعُمُونَ ﴿٧٤﴾
74. Na Siku (Allaah) Atakayowaita, Atasema: “Wako wapi hao mliokuwa mnadai kwa dhana kuwa ni washirika Wangu?”
وَنَزَعْنَا مِن كُلِّ أُمَّةٍ شَهِيدًا فَقُلْنَا هَاتُوا بُرْهَانَكُمْ فَعَلِمُوا أَنَّ الْحَقَّ لِلَّـهِ وَضَلَّ عَنْهُم مَّا كَانُوا يَفْتَرُونَ﴿٧٥﴾
75. Na Tutachomoa katika kila Ummah shahidi kisha Tutasema: “Leteni ushahidi wenu wa wazi.” Basi watajua kwamba haki ni ya Allaah Pekee; na yamewapotea yale waliyokuwa wakiyatunga.
إِنَّ قَارُونَ كَانَ مِن قَوْمِ مُوسَىٰ فَبَغَىٰ عَلَيْهِمْ ۖ وَآتَيْنَاهُ مِنَ الْكُنُوزِ مَا إِنَّ مَفَاتِحَهُ لَتَنُوءُ بِالْعُصْبَةِ أُولِي الْقُوَّةِ إِذْ قَالَ لَهُ قَوْمُهُ لَا تَفْرَحْ ۖ إِنَّ اللَّـهَ لَا يُحِبُّ الْفَرِحِينَ ﴿٧٦﴾
76. Hakika Qaaruwn alikuwa miongoni mwa kaumu ya Muwsaa, lakini aliwafanyia uonevu kwa kutakabari. Na Tulimpa katika hazina ambazo funguo zake zinalemea kundi la watu wenye nguvu (kuzibeba). Walipomwambia watu wake: “Usifurahi kwa kujigamba. Hakika Allaah Hapendi wanaofurahi kwa kujigamba.”
وَابْتَغِ فِيمَا آتَاكَ اللَّـهُ الدَّارَ الْآخِرَةَ ۖ وَلَا تَنسَ نَصِيبَكَ مِنَ الدُّنْيَا ۖ وَأَحْسِن كَمَا أَحْسَنَ اللَّـهُ إِلَيْكَ ۖ وَلَا تَبْغِ الْفَسَادَ فِي الْأَرْضِ ۖ إِنَّ اللَّـهَ لَا يُحِبُّ الْمُفْسِدِينَ ﴿٧٧﴾
77. “Na tafuta katika yale Aliyokupa Allaah makazi ya Aakhirah. Na wala usisahau fungu lako katika dunia. Na fanya ihsaan kama Alivyokufanyia Allaah ihsaan, na wala usitake ufisadi ardhini. Hakika Allaah Hapendi mafisadi.”
قَالَ إِنَّمَا أُوتِيتُهُ عَلَىٰ عِلْمٍ عِندِي ۚ أَوَلَمْ يَعْلَمْ أَنَّ اللَّـهَ قَدْ أَهْلَكَ مِن قَبْلِهِ مِنَ الْقُرُونِ مَنْ هُوَ أَشَدُّ مِنْهُ قُوَّةً وَأَكْثَرُ جَمْعًا ۚ وَلَا يُسْأَلُ عَن ذُنُوبِهِمُ الْمُجْرِمُونَ ﴿٧٨﴾
78. (Qaaruwn) Akasema: “Hakika nimepewa haya kwa sababu ya elimu yangu.” Je, hajui kwamba Allaah Ameangamiza kabla yake karne ambazo zilikuwa ni zenye nguvu zaidi kuliko yeye na zenye mkusanyiko (wa mali) mwingi zaidi? Na wala hawatoulizwa kuhusu dhambi zao wahalifu.
فَخَرَجَ عَلَىٰ قَوْمِهِ فِي زِينَتِهِ ۖ قَالَ الَّذِينَ يُرِيدُونَ الْحَيَاةَ الدُّنْيَا يَا لَيْتَ لَنَا مِثْلَ مَا أُوتِيَ قَارُونُ إِنَّهُ لَذُو حَظٍّ عَظِيمٍ ﴿٧٩﴾
79. Akawatokea watu wake katika pambo lake. Wale wanaotaka uhai wa dunia wakasema: “Ee laiti tungelipata mfano wa yale aliyopewa Qaaruwn, hakika yeye ana bahati kuu.”
وَقَالَ الَّذِينَ أُوتُوا الْعِلْمَ وَيْلَكُمْ ثَوَابُ اللَّـهِ خَيْرٌ لِّمَنْ آمَنَ وَعَمِلَ صَالِحًا وَلَا يُلَقَّاهَا إِلَّا الصَّابِرُونَ﴿٨٠﴾
80. Na wale waliopewa elimu wakasema: “Ole wenu! Thawabu za Allaah ni bora zaidi kwa yule aliyeamini na akatenda mema. Na wala hazipati isipokuwa wenye kusubiri.”
فَخَسَفْنَا بِهِ وَبِدَارِهِ الْأَرْضَ فَمَا كَانَ لَهُ مِن فِئَةٍ يَنصُرُونَهُ مِن دُونِ اللَّـهِ وَمَا كَانَ مِنَ الْمُنتَصِرِينَ﴿٨١﴾
81. Basi Tukamdidimiza yeye na nyumba yake ardhini; basi hakikuweko kikosi chochote cha kumnusuru dhidi ya Allaah, na wala hakuwa miongoni mwa wanaojinusuru.
وَأَصْبَحَ الَّذِينَ تَمَنَّوْا مَكَانَهُ بِالْأَمْسِ يَقُولُونَ وَيْكَأَنَّ اللَّـهَ يَبْسُطُ الرِّزْقَ لِمَن يَشَاءُ مِنْ عِبَادِهِ وَيَقْدِرُ ۖلَوْلَا أَن مَّنَّ اللَّـهُ عَلَيْنَا لَخَسَفَ بِنَا ۖ وَيْكَأَنَّهُ لَا يُفْلِحُ الْكَافِرُونَ ﴿٨٢﴾
82. Na wakapambaukiwa wale waliotamani mahali pake jana, wakisema: “Ee kumbe Allaah Hukunjua riziki na Hudhikisha kwa Amtakaye kati ya waja Wake. Ingelikuwa Allaah Hakutufanyia fadhila bila shaka Angelitudidimiza. Ee kumbe makafiri hawafaulu!”
تِلْكَ الدَّارُ الْآخِرَةُ نَجْعَلُهَا لِلَّذِينَ لَا يُرِيدُونَ عُلُوًّا فِي الْأَرْضِ وَلَا فَسَادًا ۚ وَالْعَاقِبَةُ لِلْمُتَّقِينَ ﴿٨٣﴾
83. Hiyo ni nyumba ya Aakhirah, Tunaijaalia kwa wale wasiotaka kujitukuza katika ardhi na wala ufisadi. Na hatima njema ni kwa wenye taqwa.
مَن جَاءَ بِالْحَسَنَةِ فَلَهُ خَيْرٌ مِّنْهَا ۖ وَمَن جَاءَ بِالسَّيِّئَةِ فَلَا يُجْزَى الَّذِينَ عَمِلُوا السَّيِّئَاتِ إِلَّا مَا كَانُوا يَعْمَلُونَ ﴿٨٤﴾
84. Atakayeleta jema, basi atapata bora kuliko hilo. Na atakayeleta ovu, basi hawalipwi wale wanaotenda maovu isipokuwa yale waliyokuwa wanayatenda.
إِنَّ الَّذِي فَرَضَ عَلَيْكَ الْقُرْآنَ لَرَادُّكَ إِلَىٰ مَعَادٍ ۚ قُل رَّبِّي أَعْلَمُ مَن جَاءَ بِالْهُدَىٰ وَمَنْ هُوَ فِي ضَلَالٍ مُّبِينٍ ﴿٨٥﴾
85. Hakika Yule Aliyekufaridhishia Qur-aan (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم,) bila shaka Atakurudisha mahali pa marejeo. Sema: “Rabb wangu Anajua zaidi yule aliyekuja na uongofu na yule aliyomo katikaupotofu bayana.”
وَمَا كُنتَ تَرْجُو أَن يُلْقَىٰ إِلَيْكَ الْكِتَابُ إِلَّا رَحْمَةً مِّن رَّبِّكَ ۖ فَلَا تَكُونَنَّ ظَهِيرًا لِّلْكَافِرِينَ ﴿٨٦﴾
86. Na wala hukuwa unataraji kwamba utapewa Kitabu isipokuwa ni rahmah kutoka kwa Rabb wako. Basi usijekuwa msaidizi kwa makafiri.
وَلَا يَصُدُّنَّكَ عَنْ آيَاتِ اللَّـهِ بَعْدَ إِذْ أُنزِلَتْ إِلَيْكَ ۖ وَادْعُ إِلَىٰ رَبِّكَ ۖ وَلَا تَكُونَنَّ مِنَ الْمُشْرِكِينَ ﴿٨٧﴾
87. Na wala wasikuzuie kabisa kufuata Aayaat za Allaah baada ya kuteremshwa kwako; na lingania kwa Rabb wako na wala usiwe miongoni mwa washirikina.
وَلَا تَدْعُ مَعَ اللَّـهِ إِلَـٰهًا آخَرَ ۘ لَا إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ ۚ كُلُّ شَيْءٍ هَالِكٌ إِلَّا وَجْهَهُ ۚ لَهُ الْحُكْمُ وَإِلَيْهِ تُرْجَعُونَ﴿٨٨﴾
88. Na wala usiombe pamoja na Allaah mwabudiwa mwingine. Hakuna Muabudiwa wa haki ila Yeye. Kila kitu ni chenye kuhiliki isipokuwa Wajihi Wake. Hukumu ni Yake Pekee na Kwake Pekee mtarejeshwa.
0 Comments