الْفُرْقان
Al-Furqaan: 25


بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ


تَبَارَكَ الَّذِي نَزَّلَ الْفُرْقَانَ عَلَىٰ عَبْدِهِ لِيَكُونَ لِلْعَالَمِينَ نَذِيرًا ﴿١﴾
1. Amebarikika Ambaye Ameteremsha kwa mja Wake Pambanuo la haki na batili ili awe muonyaji kwa walimwengu.


الَّذِي لَهُ مُلْكُ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ وَلَمْ يَتَّخِذْ وَلَدًا وَلَمْ يَكُن لَّهُ شَرِيكٌ فِي الْمُلْكِ وَخَلَقَ كُلَّ شَيْءٍ فَقَدَّرَهُ تَقْدِيرًا ﴿٢﴾
2. Ambaye ni Wake Pekee ufalme wa mbingu na ardhi, na hakujichukulia mwana wala hakuwa na mshirika katika ufalme, na Ameumba kila kitu; kisha Akakikadiria kipimo cha sawa sawa.


وَاتَّخَذُوا مِن دُونِهِ آلِهَةً لَّا يَخْلُقُونَ شَيْئًا وَهُمْ يُخْلَقُونَ وَلَا يَمْلِكُونَ لِأَنفُسِهِمْ ضَرًّا وَلَا نَفْعًا وَلَا يَمْلِكُونَ مَوْتًا وَلَا حَيَاةً وَلَا نُشُورًا ﴿٣﴾
3. Na wakachukua badala Yake (Allaah) waabudiwa wasioumba chochote na hali wao wanaumbwa wala hawamiliki kwa ajili ya nafsi zao dhara wala manufaa wala hawamiliki mauti wala uhai wala kufufuliwa.


وَقَالَ الَّذِينَ كَفَرُوا إِنْ هَـٰذَا إِلَّا إِفْكٌ افْتَرَاهُ وَأَعَانَهُ عَلَيْهِ قَوْمٌ آخَرُونَ ۖ فَقَدْ جَاءُوا ظُلْمًا وَزُورًا ﴿٤﴾
4. Wakasema wale waliokufuru: “Hii (Qur-aan) si chochote isipokuwa ni uzushi alioutunga (Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم), na wamemsadia watu wingine.” Kwa yakini wameleta dhulma na uongo.


وَقَالُوا أَسَاطِيرُ الْأَوَّلِينَ اكْتَتَبَهَا فَهِيَ تُمْلَىٰ عَلَيْهِ بُكْرَةً وَأَصِيلًا ﴿٥﴾
5. Na wakasema: “Ni hekaya za kale ameziandikisha kisha anasomewa asubuhi na jioni.”


قُلْ أَنزَلَهُ الَّذِي يَعْلَمُ السِّرَّ فِي السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ ۚ إِنَّهُ كَانَ غَفُورًا رَّحِيمًا ﴿٦﴾
6. Sema (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم): “Ameiteremsha Ambaye Anajua siri katika mbingu na ardhi. Hakika Yeye daima ni Mwingi wa kughufuria, Mwenye kurehemu. 


وَقَالُوا مَالِ هَـٰذَا الرَّسُولِ يَأْكُلُ الطَّعَامَ وَيَمْشِي فِي الْأَسْوَاقِ ۙ لَوْلَا أُنزِلَ إِلَيْهِ مَلَكٌ فَيَكُونَ مَعَهُ نَذِيرًا﴿٧﴾
7. Na wakasema: “Ana nini huyu Rasuli anakula chakula na anatembea masokoni. Kwa nini asiteremshiwe Malaika akawa muonyaji pamoja naye?”


أَوْ يُلْقَىٰ إِلَيْهِ كَنزٌ أَوْ تَكُونُ لَهُ جَنَّةٌ يَأْكُلُ مِنْهَا ۚ وَقَالَ الظَّالِمُونَ إِن تَتَّبِعُونَ إِلَّا رَجُلًا مَّسْحُورًا ﴿٨﴾
8. “Au aangushiwe hazina juu yake au awe na bustani awe anakula humo?” Na wakasema madhalimu: “Hamfuati isipokuwa mtu aliyerogwa.”


انظُرْ كَيْفَ ضَرَبُوا لَكَ الْأَمْثَالَ فَضَلُّوا فَلَا يَسْتَطِيعُونَ سَبِيلًا ﴿٩﴾
9. Tazama vipi walivyokupigia mifano, wamepotea, hawatoweza kupata njia (ya haki).


تَبَارَكَ الَّذِي إِن شَاءَ جَعَلَ لَكَ خَيْرًا مِّن ذَٰلِكَ جَنَّاتٍ تَجْرِي مِن تَحْتِهَا الْأَنْهَارُ وَيَجْعَل لَّكَ قُصُورًا﴿١٠﴾
10. Amebarikika Ambaye Akitaka Atakujaalia kheri kuliko hayo; ni Jannaat zipitazo chini yake mito na Akujaalie maqasri.


بَلْ كَذَّبُوا بِالسَّاعَةِ ۖ وَأَعْتَدْنَا لِمَن كَذَّبَ بِالسَّاعَةِ سَعِيرًا ﴿١١﴾
11. Bali wameikadhibisha Saa. Na Tumeandaa kwa anayeikadhibisha Saa, moto uliowashwa vikali mno.” 


إِذَا رَأَتْهُم مِّن مَّكَانٍ بَعِيدٍ سَمِعُوا لَهَا تَغَيُّظًا وَزَفِيرًا ﴿١٢﴾
12. (Moto huo) Utakapowaona kutoka mahali mbali, watausikia ghadhabu zake na upumuaji pumzi kwa mngurumo.


وَإِذَا أُلْقُوا مِنْهَا مَكَانًا ضَيِّقًا مُّقَرَّنِينَ دَعَوْا هُنَالِكَ ثُبُورًا ﴿١٣﴾
13. Na watakapotupwa humo mahali pa dhiki wakiwa wamefungashwa pamoja wataomba huko kuteketea. 


لَّا تَدْعُوا الْيَوْمَ ثُبُورًا وَاحِدًا وَادْعُوا ثُبُورًا كَثِيرًا ﴿١٤﴾
14. “Msiombe leo kuteketea kumoja; bali ombeni kuteketea kwingi!”


قُلْ أَذَٰلِكَ خَيْرٌ أَمْ جَنَّةُ الْخُلْدِ الَّتِي وُعِدَ الْمُتَّقُونَ ۚ كَانَتْ لَهُمْ جَزَاءً وَمَصِيرًا ﴿١٥﴾
15. Sema: “Je, hayo ni bora, au Jannah ya yenye kudumu ambayo wameahidiwa wenye taqwa?” Itakuwa kwao ni jazaa na mahali pa kuishia.


لَّهُمْ فِيهَا مَا يَشَاءُونَ خَالِدِينَ ۚ كَانَ عَلَىٰ رَبِّكَ وَعْدًا مَّسْئُولًا ﴿١٦﴾
16. Watapata humo kila wanachokitaka ni wenye kudumu milele. Imekuwa ni ahadi juu ya Rabb wako ya kuombwa.


وَيَوْمَ يَحْشُرُهُمْ وَمَا يَعْبُدُونَ مِن دُونِ اللَّـهِ فَيَقُولُ أَأَنتُمْ أَضْلَلْتُمْ عِبَادِي هَـٰؤُلَاءِ أَمْ هُمْ ضَلُّوا السَّبِيلَ﴿١٧﴾
17. Na Siku Atakayowakusanya pamoja na yale wanayoyaabudu badala ya Allaah; Atasema: “Je, ni nyinyi ndio mliowapoteza waja Wangu, au wao ndio waliopotea njia?


قَالُوا سُبْحَانَكَ مَا كَانَ يَنبَغِي لَنَا أَن نَّتَّخِذَ مِن دُونِكَ مِنْ أَوْلِيَاءَ وَلَـٰكِن مَّتَّعْتَهُمْ وَآبَاءَهُمْ حَتَّىٰ نَسُوا الذِّكْرَ وَكَانُوا قَوْمًا بُورًا ﴿١٨﴾
18. Watasema: “Subhaanak! Utakasifu ni Wako haikutupasa sisi kuchukua badala Yako walinzi wowote; lakini Uliwastarehesha na baba zao mpaka wakasahau ukumbusho na wakawa watu wa kuteketea.”


فَقَدْ كَذَّبُوكُم بِمَا تَقُولُونَ فَمَا تَسْتَطِيعُونَ صَرْفًا وَلَا نَصْرًا ۚ وَمَن يَظْلِم مِّنكُمْ نُذِقْهُ عَذَابًا كَبِيرًا ﴿١٩﴾
19. Basi wamekwisha kukadhibisheni kwa yale myasemayo; hivyo hamtoweza kujiondoshea na wala kujinusuru. Na yeyote Yule atakayedhulumu miongoni mwenu Tutamuonjesha adhabu kubwa.


وَمَا أَرْسَلْنَا قَبْلَكَ مِنَ الْمُرْسَلِينَ إِلَّا إِنَّهُمْ لَيَأْكُلُونَ الطَّعَامَ وَيَمْشُونَ فِي الْأَسْوَاقِ ۗ وَجَعَلْنَا بَعْضَكُمْ لِبَعْضٍ فِتْنَةً أَتَصْبِرُونَ ۗ وَكَانَ رَبُّكَ بَصِيرًا ﴿٢٠﴾
20. Na Hatukupeleka kabla yako (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) Rusuli wowote isipokuwa bila shaka wakila chakula, na wanatembea masokoni. Na Tumejaalia baadhi yenu nyinyi kwa nyinyi kuwa ni majaribio je mtasubiri? Na Rabb wako ni Mwenye kuona daima.


وَقَالَ الَّذِينَ لَا يَرْجُونَ لِقَاءَنَا لَوْلَا أُنزِلَ عَلَيْنَا الْمَلَائِكَةُ أَوْ نَرَىٰ رَبَّنَا ۗ لَقَدِ اسْتَكْبَرُوا فِي أَنفُسِهِمْ وَعَتَوْا عُتُوًّا كَبِيرًا ﴿٢١﴾
21. Na walisema wale wasiotaraji kukutana Nasi: “Kwa nini hatuteremshiwi Malaika, au hatumwoni Rabb wetu?”  Kwa yakini wametakabari katika nafsi zao na wakavuka mipaka ya ufidhuli na uasi mkubwa.


يَوْمَ يَرَوْنَ الْمَلَائِكَةَ لَا بُشْرَىٰ يَوْمَئِذٍ لِّلْمُجْرِمِينَ وَيَقُولُونَ حِجْرًا مَّحْجُورًا ﴿٢٢﴾
22. Siku watakayowaona Malaika hakutakuwa na bishara njema Siku hiyo kwa wahalifu na (Malaika) watasema: “Marufuku! (Mafanikio) yamepigwa marufuku.”


وَقَدِمْنَا إِلَىٰ مَا عَمِلُوا مِنْ عَمَلٍ فَجَعَلْنَاهُ هَبَاءً مَّنثُورًا ﴿٢٣﴾
23. Na Tutayaendea yale waliyoyatenda ya ‘amali yoyote ile, Tutayafanya   chembechembe za vumbi zinazoelea hewani zinazotawanyika.


أَصْحَابُ الْجَنَّةِ يَوْمَئِذٍ خَيْرٌ مُّسْتَقَرًّا وَأَحْسَنُ مَقِيلًا ﴿٢٤﴾
24. Watu wa Jannah Siku hiyo wako katika makazi bora ya kustakiri, na mahali pazuri kabisa pa kupumzikia.


وَيَوْمَ تَشَقَّقُ السَّمَاءُ بِالْغَمَامِ وَنُزِّلَ الْمَلَائِكَةُ تَنزِيلًا ﴿٢٥﴾
25. Na Siku itakayoraruka mbingu kwa mawingu; na Malaika watateremshwa mteremsho mkubwa wa mfuatano.


الْمُلْكُ يَوْمَئِذٍ الْحَقُّ لِلرَّحْمَـٰنِ ۚ وَكَانَ يَوْمًا عَلَى الْكَافِرِينَ عَسِيرًا ﴿٢٦﴾
26. Ufalme wa haki Siku hiyo utakuwa ni  wa Ar-Rahmaan. Na itakuwa ni siku ngumu kwa makafiri.


وَيَوْمَ يَعَضُّ الظَّالِمُ عَلَىٰ يَدَيْهِ يَقُولُ يَا لَيْتَنِي اتَّخَذْتُ مَعَ الرَّسُولِ سَبِيلًا ﴿٢٧﴾
27. Na siku dhalimu atakapotafuna mikono yake akisema: “Laiti ningeshika njia pamoja na Rasuli. 


يَا وَيْلَتَىٰ لَيْتَنِي لَمْ أَتَّخِذْ فُلَانًا خَلِيلًا ﴿٢٨﴾
28. “Ee ole wangu! Laiti nisingelimfanya fulani kuwa rafiki mwandani.”



لَّقَدْ أَضَلَّنِي عَنِ الذِّكْرِ بَعْدَ إِذْ جَاءَنِي ۗ وَكَانَ الشَّيْطَانُ لِلْإِنسَانِ خَذُولًا ﴿٢٩﴾
29. “Kwa yakini amenipoteza mbali na Ukumbusho baada ya kunijia.” Na shaytwaan kwa insani daima ni mwenye kutelekeza.


وَقَالَ الرَّسُولُ يَا رَبِّ إِنَّ قَوْمِي اتَّخَذُوا هَـٰذَا الْقُرْآنَ مَهْجُورًا ﴿٣٠﴾
30. Na Rasuli akasema: “Rabb wangu! Hakika watu wangu wameifanya hii Qur-aan yenye kuhamwa.


وَكَذَٰلِكَ جَعَلْنَا لِكُلِّ نَبِيٍّ عَدُوًّا مِّنَ الْمُجْرِمِينَ ۗ وَكَفَىٰ بِرَبِّكَ هَادِيًا وَنَصِيرًا ﴿٣١﴾
31. Na hivyo ndivyo Tumemfanyia kila Nabiy adui miongoni mwa wahalifu. Na Rabb wako Anatosheleza kuwa ni Mwenye kuongoza na Mwenye kunusuru.


وَقَالَ الَّذِينَ كَفَرُوا لَوْلَا نُزِّلَ عَلَيْهِ الْقُرْآنُ جُمْلَةً وَاحِدَةً ۚ كَذَٰلِكَ لِنُثَبِّتَ بِهِ فُؤَادَكَ ۖ وَرَتَّلْنَاهُ تَرْتِيلًا﴿٣٢﴾
32. Na wakasema wale waliokufuru: “Kwa nini hakuteremshiwa Qur-aan   kwa ujumla mara moja tu?” Ndio hivyo hivyo, ili Tukithibitishe kifua chako; na Tumeifunulia Wahyi punde kwa punde kwa kuratibu.

وَلَا يَأْتُونَكَ بِمَثَلٍ إِلَّا جِئْنَاكَ بِالْحَقِّ وَأَحْسَنَ تَفْسِيرًا ﴿٣٣﴾
33. Na wala hawakujii kwa mfano wowote isipokuwa Tunakuletea haki na tafsiri nzuri kabisa.



الَّذِينَ يُحْشَرُونَ عَلَىٰ وُجُوهِهِمْ إِلَىٰ جَهَنَّمَ أُولَـٰئِكَ شَرٌّ مَّكَانًا وَأَضَلُّ سَبِيلًا ﴿٣٤﴾
34. Wale ambao watakusanywa juu ya nyuso zao kueleleka Jahannam, hao wana mahali pabaya mno, wamepotea zaidi njia.


وَلَقَدْ آتَيْنَا مُوسَى الْكِتَابَ وَجَعَلْنَا مَعَهُ أَخَاهُ هَارُونَ وَزِيرًا ﴿٣٥﴾
35. Na kwa yakini Tulimpa Muwsaa Maandiko (ya Tawraat) na Tukamjaalia pamoja naye kaka yake Haaruwn kuwa msaidizi.


فَقُلْنَا اذْهَبَا إِلَى الْقَوْمِ الَّذِينَ كَذَّبُوا بِآيَاتِنَا فَدَمَّرْنَاهُمْ تَدْمِيرًا ﴿٣٦﴾
36. Tukasema: “Nendeni kwa watu ambao wamekadhibisha Aayaat (ishara, dalili) Zetu, basi Tukawadamirisha kwa kuteketeza.



وَقَوْمَ نُوحٍ لَّمَّا كَذَّبُوا الرُّسُلَ أَغْرَقْنَاهُمْ وَجَعَلْنَاهُمْ لِلنَّاسِ آيَةً ۖ وَأَعْتَدْنَا لِلظَّالِمِينَ عَذَابًا أَلِيمًا ﴿٣٧﴾
37. Na watu wa Nuwh walipowakadhibisha Rusuli, Tuliwagharikisha, na Tukawafanya kuwa Aayah (ishara, funzo) kwa watu. Na Tumewaandalia madhalimu adhabu iumizayo.


وَعَادًا وَثَمُودَ وَأَصْحَابَ الرَّسِّ وَقُرُونًا بَيْنَ ذَٰلِكَ كَثِيرًا ﴿٣٨﴾
38. Na kina ‘Aad na Thamuwd na watu wa Ar-Rass na karne nyingi zilokuwa baina yao.



وَكُلًّا ضَرَبْنَا لَهُ الْأَمْثَالَ ۖ وَكُلًّا تَبَّرْنَا تَتْبِيرًا ﴿٣٩﴾
39. Na kila mmoja Tuliwapigia mifano na kila mmoja Tuliwateketeza mateketezo kamilifu.


وَلَقَدْ أَتَوْا عَلَى الْقَرْيَةِ الَّتِي أُمْطِرَتْ مَطَرَ السَّوْءِ ۚ أَفَلَمْ يَكُونُوا يَرَوْنَهَا ۚ بَلْ كَانُوا لَا يَرْجُونَ نُشُورًا﴿٤٠﴾
40. Na kwa yakini walipita katika mji ambao ulinyeshewa mvua mbaya. Je, basi hawakuwa wakiuona? Bali walikuwa hawataraji kufufuliwa.


وَإِذَا رَأَوْكَ إِن يَتَّخِذُونَكَ إِلَّا هُزُوًا أَهَـٰذَا الَّذِي بَعَثَ اللَّـهُ رَسُولًا ﴿٤١﴾
41. Na wanapokuona (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) hawakuchukulii isipokuwa mzaha; (wakisema): “Je, ndiye huyu ambaye Allaah Amemtuma kuwa Rasuli?”



إِن كَادَ لَيُضِلُّنَا عَنْ آلِهَتِنَا لَوْلَا أَن صَبَرْنَا عَلَيْهَا ۚ وَسَوْفَ يَعْلَمُونَ حِينَ يَرَوْنَ الْعَذَابَ مَنْ أَضَلُّ سَبِيلًا ﴿٤٢﴾
42. “Kwa yakini alikaribia kutupoteza na waabudiwa wetu, ingelikuwa hatukuvumilia kuwaabudu.” Na watakuja kujua wakati watakapoona adhabu, ni nani aliyepotea zaidi njia.


أَرَأَيْتَ مَنِ اتَّخَذَ إِلَـٰهَهُ هَوَاهُ أَفَأَنتَ تَكُونُ عَلَيْهِ وَكِيلًا ﴿٤٣﴾
43. Je, umemuona yule aliyefanya hawaa yake kuwa ndio mwabudiwa wake?  Je, basi utaweza wewe kuwa ni mdhamini wake?



أَمْ تَحْسَبُ أَنَّ أَكْثَرَهُمْ يَسْمَعُونَ أَوْ يَعْقِلُونَ ۚ إِنْ هُمْ إِلَّا كَالْأَنْعَامِ ۖ بَلْ هُمْ أَضَلُّ سَبِيلًا ﴿٤٤﴾
44. Je, unadhania kwamba wengi wao wanasikia au wanatia akilini? Wao si chochote isipokuwa kama wanyama, bali wao wamepotea zaidi njia.


أَلَمْ تَرَ إِلَىٰ رَبِّكَ كَيْفَ مَدَّ الظِّلَّ وَلَوْ شَاءَ لَجَعَلَهُ سَاكِنًا ثُمَّ جَعَلْنَا الشَّمْسَ عَلَيْهِ دَلِيلًا ﴿٤٥﴾
45. Je, huoni vipi Rabb wako Alivyotandaza kivuli? Angelitaka Angelikifanya kitulie tu kisha Tukalifanya jua kuwa kielekezo juu yake.


ثُمَّ قَبَضْنَاهُ إِلَيْنَا قَبْضًا يَسِيرًا ﴿٤٦﴾
46. Kisha Tunakivutia kwetu Kwetu mvuto wa pole pole.


وَهُوَ الَّذِي جَعَلَ لَكُمُ اللَّيْلَ لِبَاسًا وَالنَّوْمَ سُبَاتًا وَجَعَلَ النَّهَارَ نُشُورًا ﴿٤٧﴾
47. Naye Ndiye Ambaye Amekujaalieni usiku kuwa ni libasi na usingizi mapumziko ya kama kufa na Amefanya mchana ni wa kuinuka na kutawanyika.


وَهُوَ الَّذِي أَرْسَلَ الرِّيَاحَ بُشْرًا بَيْنَ يَدَيْ رَحْمَتِهِ ۚ وَأَنزَلْنَا مِنَ السَّمَاءِ مَاءً طَهُورًا ﴿٤٨﴾
48. Naye Ndiye Ambaye Ametuma upepo wa kheri kuwa bishara njema kabla ya rahmah Yake. Na Tunateremsha kutoka mbinguni maji yaliyo safi.


لِّنُحْيِيَ بِهِ بَلْدَةً مَّيْتًا وَنُسْقِيَهُ مِمَّا خَلَقْنَا أَنْعَامًا وَأَنَاسِيَّ كَثِيرًا ﴿٤٩﴾
49. Ili Tuhuishe kwayo nchi iliyokufa, na Tuwanyweshe kwayo kati ya wale Tuliowaumba; wanyama na watu wengi.


وَلَقَدْ صَرَّفْنَاهُ بَيْنَهُمْ لِيَذَّكَّرُوا فَأَبَىٰ أَكْثَرُ النَّاسِ إِلَّا كُفُورًا ﴿٥٠﴾
50. Na kwa yakini Tumeigawa (mvua) baina yao ili wakumbuke (neema za Allaah), lakini watu wengi wanakataa kabisa; (hawana) isipokuwa kukufuru tu.


وَلَوْ شِئْنَا لَبَعَثْنَا فِي كُلِّ قَرْيَةٍ نَّذِيرًا ﴿٥١﴾
51. Na lau Tungelitaka, bila shaka Tungelipeleka katika kila mji mwonyaji.



فَلَا تُطِعِ الْكَافِرِينَ وَجَاهِدْهُم بِهِ جِهَادًا كَبِيرًا ﴿٥٢﴾
52. Basi usiwatii makafiri, na fanya jihaad dhidi yao kwayo (Qur-aan) jihaad kubwa.


وَهُوَ الَّذِي مَرَجَ الْبَحْرَيْنِ هَـٰذَا عَذْبٌ فُرَاتٌ وَهَـٰذَا مِلْحٌ أُجَاجٌ وَجَعَلَ بَيْنَهُمَا بَرْزَخًا وَحِجْرًا مَّحْجُورًا ﴿٥٣﴾
53. Naye Ndiye Aliyeunganisha bahari mbili; hii ni tamu ikatayo kiu, na hii ni ya chumvi, kali. Na Akajaalia baina yao kitenganisho na kizuizi kinachozuia kabisa.   


وَهُوَ الَّذِي خَلَقَ مِنَ الْمَاءِ بَشَرًا فَجَعَلَهُ نَسَبًا وَصِهْرًا ۗ وَكَانَ رَبُّكَ قَدِيرًا ﴿٥٤﴾
54. Naye Ndiye Aliyeumba mtu kutokana na maji, kisha Akamjaalia kuwa na unasaba wa damu na uhusiano wa ndoa. Na Rabb wako daima ni Mweza wa yote.


وَيَعْبُدُونَ مِن دُونِ اللَّـهِ مَا لَا يَنفَعُهُمْ وَلَا يَضُرُّهُمْ ۗ وَكَانَ الْكَافِرُ عَلَىٰ رَبِّهِ ظَهِيرًا ﴿٥٥﴾
55. Na wanaabudu badala ya Allaah vile visivyowafaa na wala visivyowadhuru. Na kafiri daima ni msaidizi dhidi ya Rabb wake.


وَمَا أَرْسَلْنَاكَ إِلَّا مُبَشِّرًا وَنَذِيرًا ﴿٥٦﴾
56. Na Hatukukutuma (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) isipokuwa ni mbashiriaji na mwonyaji.


قُلْ مَا أَسْأَلُكُمْ عَلَيْهِ مِنْ أَجْرٍ إِلَّا مَن شَاءَ أَن يَتَّخِذَ إِلَىٰ رَبِّهِ سَبِيلًا ﴿٥٧﴾
57. Sema: “Sikuombeni ujira juu yake isipokuwa atakaye achukue njia kwa Rabb
wake.”


وَتَوَكَّلْ عَلَى الْحَيِّ الَّذِي لَا يَمُوتُ وَسَبِّحْ بِحَمْدِهِ ۚ وَكَفَىٰ بِهِ بِذُنُوبِ عِبَادِهِ خَبِيرًا ﴿٥٨﴾
58. Na tawakali kwa Aliye hai Ambaye Hafi, na sabbih kwa Himidi Zake; na Inamtosheleza kuwa ni Mwenye upeo wa khabari za dhahiri na za kufichika kuhusu dhambi za waja Wake.


الَّذِي خَلَقَ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ وَمَا بَيْنَهُمَا فِي سِتَّةِ أَيَّامٍ ثُمَّ اسْتَوَىٰ عَلَى الْعَرْشِ ۚ الرَّحْمَـٰنُ فَاسْأَلْ بِهِ خَبِيرًا ﴿٥٩﴾
59. Ambaye Ameumba mbingu na ardhi na vilivyo baina yake katika siku sita, kisha Istawaa juu ya ‘Arsh[1], Ar-Rahmaan, basi ulizia kuhusu Yeye; kwani ni Mwenye upeo wa khabari za dhahiri na za kufichika.


وَإِذَا قِيلَ لَهُمُ اسْجُدُوا لِلرَّحْمَـٰنِ قَالُوا وَمَا الرَّحْمَـٰنُ أَنَسْجُدُ لِمَا تَأْمُرُنَا وَزَادَهُمْ نُفُورًا ۩﴿٦٠﴾
60. Na wanapoambiwa: “Msujudieni Ar-Rahmaan” husema: “Ni nani huyo Ar-Rahmaan? Tumsujudie unayetuamrisha, na inawazidishia kukengeuka kwa chuki.


تَبَارَكَ الَّذِي جَعَلَ فِي السَّمَاءِ بُرُوجًا وَجَعَلَ فِيهَا سِرَاجًا وَقَمَرًا مُّنِيرًا ﴿٦١﴾
61. Amebarikika Ambaye Amejaalia buruji katika mbingu na Amejaalia humo taa yenye mwanga mkali na mwezi wenye nuru.


وَهُوَ الَّذِي جَعَلَ اللَّيْلَ وَالنَّهَارَ خِلْفَةً لِّمَنْ أَرَادَ أَن يَذَّكَّرَ أَوْ أَرَادَ شُكُورًا ﴿٦٢﴾
62. Naye Ndiye Aliyejaalia usiku na mchana ufuatane kwa atakaye kukumbuka au atakaye kushukuru.


وَعِبَادُ الرَّحْمَـٰنِ الَّذِينَ يَمْشُونَ عَلَى الْأَرْضِ هَوْنًا وَإِذَا خَاطَبَهُمُ الْجَاهِلُونَ قَالُوا سَلَامًا ﴿٦٣﴾
63. Na waja wa Ar-Rahmaan ni wale wanaotembea katika ardhi kwa unyenyekevu na upole, na majahili wanapowasemesha, wao husema: Salaam!


وَالَّذِينَ يَبِيتُونَ لِرَبِّهِمْ سُجَّدًا وَقِيَامًا ﴿٦٤﴾
64. Na wale wanaokesha usiku kwa ajili ya Rabb wao wakisujudu na kusimama.


وَالَّذِينَ يَقُولُونَ رَبَّنَا اصْرِفْ عَنَّا عَذَابَ جَهَنَّمَ ۖ إِنَّ عَذَابَهَا كَانَ غَرَامًا ﴿٦٥﴾
65. Na wale wanaosema: “Rabb wetu! Tuepushe adhabu ya Jahannam. Hakika adhabu yake ni yenye kugandamana daima; isiyomwacha mtu.”


إِنَّهَا سَاءَتْ مُسْتَقَرًّا وَمُقَامًا ﴿٦٦﴾
66. “Hakika hiyo (Jahannam) ni mahali paovu mno pa kustakiri na mahali pa kuishi.



وَالَّذِينَ إِذَا أَنفَقُوا لَمْ يُسْرِفُوا وَلَمْ يَقْتُرُوا وَكَانَ بَيْنَ ذَٰلِكَ قَوَامًا ﴿٦٧﴾
67. Na wale ambao wanapotoa huwa hawafanyi israfu na wala hawafanyi uchoyo na wanakuwa wastani baina ya hayo.



وَالَّذِينَ لَا يَدْعُونَ مَعَ اللَّـهِ إِلَـٰهًا آخَرَ وَلَا يَقْتُلُونَ النَّفْسَ الَّتِي حَرَّمَ اللَّـهُ إِلَّا بِالْحَقِّ وَلَا يَزْنُونَ ۚوَمَن يَفْعَلْ ذَٰلِكَ يَلْقَ أَثَامًا ﴿٦٨﴾
68. Na wale ambao hawaombi pamoja na Allaah mwabudiwa mwengine na wala hawaui nafsi ambayo Allaah Ameiharamisha isipokuwa kwa haki, na wala hawazini. Na atakayefanya hivyo atakutana na adhabu.


يُضَاعَفْ لَهُ الْعَذَابُ يَوْمَ الْقِيَامَةِ وَيَخْلُدْ فِيهِ مُهَانًا ﴿٦٩﴾
69. Ataongezewa adhabu maradufu Siku ya Qiyaamah, na mwenye kudumu humo akiwa amedhalilika.


إِلَّا مَن تَابَ وَآمَنَ وَعَمِلَ عَمَلًا صَالِحًا فَأُولَـٰئِكَ يُبَدِّلُ اللَّـهُ سَيِّئَاتِهِمْ حَسَنَاتٍ ۗ وَكَانَ اللَّـهُ غَفُورًا رَّحِيمًا ﴿٧٠﴾
70. Isipokuwa yule aliyetubu na akaamini na akatenda ‘amali njema; basi hao Allaah Atawabadilishia maovu yao kuwa mema.  Na Allaah daima ni Mwingi wa kughufuria, Mwenye kurehemu.


وَمَن تَابَ وَعَمِلَ صَالِحًا فَإِنَّهُ يَتُوبُ إِلَى اللَّـهِ مَتَابًا ﴿٧١﴾
71. Na atakayetubu na akatenda mema, basi hakika yeye anatubia kwa Allaah tawbah ya kweli.



وَالَّذِينَ لَا يَشْهَدُونَ الزُّورَ وَإِذَا مَرُّوا بِاللَّغْوِ مَرُّوا كِرَامًا ﴿٧٢﴾
72. Na wale ambao hawashuhudii uongo, na wanapopita kwenye upuuzi hupita kwa heshima.



وَالَّذِينَ إِذَا ذُكِّرُوا بِآيَاتِ رَبِّهِمْ لَمْ يَخِرُّوا عَلَيْهَا صُمًّا وَعُمْيَانًا ﴿٧٣﴾
73. Na wale ambao wanapokumbushwa Aayaat za Rabb wao, hawapinduki kuzifanyia uziwi na upofu.


وَالَّذِينَ يَقُولُونَ رَبَّنَا هَبْ لَنَا مِنْ أَزْوَاجِنَا وَذُرِّيَّاتِنَا قُرَّةَ أَعْيُنٍ وَاجْعَلْنَا لِلْمُتَّقِينَ إِمَامًا ﴿٧٤﴾
74. Na wale wanaosema: “Rabb wetu! Tutunukie katika wake zetu na dhuria wetu viburudisho vya macho yetu, na Tujaalie kuwa waongozi kwa wenye taqwa. 



أُولَـٰئِكَ يُجْزَوْنَ الْغُرْفَةَ بِمَا صَبَرُوا وَيُلَقَّوْنَ فِيهَا تَحِيَّةً وَسَلَامًا ﴿٧٥﴾
75. Hao ndio watakaolipwa maghorofa ya juu (Jannah) kwa kuwa walisubiri, na watapokelewa humo kwa maamkizi na amani.


خَالِدِينَ فِيهَا ۚ حَسُنَتْ مُسْتَقَرًّا وَمُقَامًا ﴿٧٦﴾
76. Ni wenye kudumu humo. Uzuri ulioje wa mahali pa kustakiri na makazi ya kushi daima.


قُلْ مَا يَعْبَأُ بِكُمْ رَبِّي لَوْلَا دُعَاؤُكُمْ ۖ فَقَدْ كَذَّبْتُمْ فَسَوْفَ يَكُونُ لِزَامًا ﴿٧٧﴾
77. Sema (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم): “Rabb wangu Asingekujalini lau kama si du’aa zenu; kwa yakini mmekadhibisha, basi adhabu itakuwa ya lazima kukugandeni tu!



 
[1] Yuko juu kwa namna inayolingana na Utukufu Wake Yeye Mwenyewe Allaah.