الْحَجّ
Al-Hajj: 22
بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ
يَا أَيُّهَا النَّاسُ اتَّقُوا رَبَّكُمْ ۚ إِنَّ زَلْزَلَةَ السَّاعَةِ شَيْءٌ عَظِيمٌ ﴿١﴾
1. Enyi watu! Mcheni Rabb wenu. Hakika zilizala la Saa ni jambo kuu.
يَوْمَ تَرَوْنَهَا تَذْهَلُ كُلُّ مُرْضِعَةٍ عَمَّا أَرْضَعَتْ وَتَضَعُ كُلُّ ذَاتِ حَمْلٍ حَمْلَهَا وَتَرَى النَّاسَ سُكَارَىٰ وَمَا هُم بِسُكَارَىٰ وَلَـٰكِنَّ عَذَابَ اللَّـهِ شَدِيدٌ ﴿٢﴾
2. Siku mtakapoiona kila mnyonyeshaji atamsahau anayemnyonyesha, na kila mwenye mimba ataizaa mimba yake, na utawaona watu wamelewa, kumbe hawakulewa lakini ni adhabu ya Allaah kali.
وَمِنَ النَّاسِ مَن يُجَادِلُ فِي اللَّـهِ بِغَيْرِ عِلْمٍ وَيَتَّبِعُ كُلَّ شَيْطَانٍ مَّرِيدٍ ﴿٣﴾
3. Na miongoni mwa watu kuna ambao wanaobishana kuhusu Allaah bila ya elimu, na wanafuata kila shaytwaan asi.
كُتِبَ عَلَيْهِ أَنَّهُ مَن تَوَلَّاهُ فَأَنَّهُ يُضِلُّهُ وَيَهْدِيهِ إِلَىٰ عَذَابِ السَّعِيرِ ﴿٤﴾
4. Ameandikiwa (shaytwaan) kwamba atakayemfanya rafiki, basi yeye atampoteza na atamuongoza katika adhabu ya moto uliowashwa vikali mno.
يَا أَيُّهَا النَّاسُ إِن كُنتُمْ فِي رَيْبٍ مِّنَ الْبَعْثِ فَإِنَّا خَلَقْنَاكُم مِّن تُرَابٍ ثُمَّ مِن نُّطْفَةٍ ثُمَّ مِنْ عَلَقَةٍ ثُمَّ مِن مُّضْغَةٍ مُّخَلَّقَةٍ وَغَيْرِ مُخَلَّقَةٍ لِّنُبَيِّنَ لَكُمْ ۚ وَنُقِرُّ فِي الْأَرْحَامِ مَا نَشَاءُ إِلَىٰ أَجَلٍ مُّسَمًّى ثُمَّ نُخْرِجُكُمْ طِفْلًا ثُمَّ لِتَبْلُغُوا أَشُدَّكُمْ ۖ وَمِنكُم مَّن يُتَوَفَّىٰ وَمِنكُم مَّن يُرَدُّ إِلَىٰ أَرْذَلِ الْعُمُرِ لِكَيْلَا يَعْلَمَ مِن بَعْدِ عِلْمٍ شَيْئًا ۚ وَتَرَى الْأَرْضَ هَامِدَةً فَإِذَا أَنزَلْنَا عَلَيْهَا الْمَاءَ اهْتَزَّتْ وَرَبَتْ وَأَنبَتَتْ مِن كُلِّ زَوْجٍ بَهِيجٍ ﴿٥﴾
5. Enyi watu! Mkiwa mko katika shaka ya kufufuliwa; basi hakika Sisi Tumekuumbeni kutokana na mchanga, kisha kutokana na manii, kisha pande la damu linaloning’inia, kisha, kinofu cha nyama na kinachotiwa umbo, na kisichotiwa umbo, ili Tukubainishieni. Na Tunakikalisha katika fuko la uzazi Tukitakacho mpaka muda maalumu uliokadiriwa. Kisha Tunakutoeni hali ya mtoto, kisha ili mfikie umri kupevuka kwenu; na miongoni mwenu yule anayefishwa, na miongoni mwenu yule anayerudishwa kwenye umri mbaya na dhaifu zaidi hata awe hajui kitu chochote kile baada ya elimu (yake). Na utaona ardhi kame, lakini Tunapoiteremshia maji hutikisika na kuumuka, na inaotesha mimea ya kila namna; anisi mizuri.
ذَٰلِكَ بِأَنَّ اللَّـهَ هُوَ الْحَقُّ وَأَنَّهُ يُحْيِي الْمَوْتَىٰ وَأَنَّهُ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ ﴿٦﴾
6. Hivyo ni kwa kuwa Allaah Ndiye wa Haki, na kwamba Yeye Anahuisha wafu, na kwamba Yeye juu ya kila kitu ni Muweza.
وَأَنَّ السَّاعَةَ آتِيَةٌ لَّا رَيْبَ فِيهَا وَأَنَّ اللَّـهَ يَبْعَثُ مَن فِي الْقُبُورِ ﴿٧﴾
7. Na kwamba Saa itafika tu haina shaka ndani yake, na kwamba Allaah Atafufua waliomo kaburini.
وَمِنَ النَّاسِ مَن يُجَادِلُ فِي اللَّـهِ بِغَيْرِ عِلْمٍ وَلَا هُدًى وَلَا كِتَابٍ مُّنِيرٍ ﴿٨﴾
8. Na miongoni mwa watu wako wanaobishana kuhusu Allaah bila ya elimu, wala mwongozo na wala Kitabu chenye Nuru.
ثَانِيَ عِطْفِهِ لِيُضِلَّ عَن سَبِيلِ اللَّـهِ ۖ لَهُ فِي الدُّنْيَا خِزْيٌ ۖ وَنُذِيقُهُ يَوْمَ الْقِيَامَةِ عَذَابَ الْحَرِيقِ ﴿٩﴾
9. Mwenyekugeuza shingo yake kwa kibri ili apoteze (watu) njia ya Allaah. Atapata duniani hizaya, na Tutamuonjesha Siku ya Qiyaamah adhabu ya kuungua.
ذَٰلِكَ بِمَا قَدَّمَتْ يَدَاكَ وَأَنَّ اللَّـهَ لَيْسَ بِظَلَّامٍ لِّلْعَبِيدِ ﴿١٠﴾
10. (Ataambiwa): “Hivyo ni kwa sababu ya yale yaliyotanguliza mikono yako; na kwamba Allaah si Mwenye kudhulumu waja.”
وَمِنَ النَّاسِ مَن يَعْبُدُ اللَّـهَ عَلَىٰ حَرْفٍ ۖ فَإِنْ أَصَابَهُ خَيْرٌ اطْمَأَنَّ بِهِ ۖ وَإِنْ أَصَابَتْهُ فِتْنَةٌ انقَلَبَ عَلَىٰ وَجْهِهِ خَسِرَ الدُّنْيَا وَالْآخِرَةَ ۚ ذَٰلِكَ هُوَ الْخُسْرَانُ الْمُبِينُ ﴿١١﴾
11. Na miongoni mwa watu yuko anayemwabudu Allaah ukingoni. Inapompata kheri, hutumainika kwayo; Na inapompata mtihani hugeuka nyuma juu ya uso wake (kurudia kufru). Amekhasirika duniani na Aakhirah. Hiyo ndiyo khasara bayana.
يَدْعُو مِن دُونِ اللَّـهِ مَا لَا يَضُرُّهُ وَمَا لَا يَنفَعُهُ ۚ ذَٰلِكَ هُوَ الضَّلَالُ الْبَعِيدُ ﴿١٢﴾
12. Humwomba badala ya Allaah yule visivyomdhuru na wala visivyomnufaisha. Huo ndio upotofu wa mbali.
يَدْعُو لَمَن ضَرُّهُ أَقْرَبُ مِن نَّفْعِهِ ۚ لَبِئْسَ الْمَوْلَىٰ وَلَبِئْسَ الْعَشِيرُ ﴿١٣﴾
13. Humwomba yule ambaye dhara yake iko karibu kuliko manufaa yake. Bila shaka ni mlinzi muovu kabisa, na bila shaka ni rafiki muovu kabisa.
إِنَّ اللَّـهَ يُدْخِلُ الَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ جَنَّاتٍ تَجْرِي مِن تَحْتِهَا الْأَنْهَارُ ۚ إِنَّ اللَّـهَ يَفْعَلُ مَا يُرِيدُ ﴿١٤﴾
14. Hakika Allaah Atawaingiza wale walioamini na wakatenda mema Jannaat zipitazo chini yake mito. Hakika Allaah Anafanya Atakavyo.
مَن كَانَ يَظُنُّ أَن لَّن يَنصُرَهُ اللَّـهُ فِي الدُّنْيَا وَالْآخِرَةِ فَلْيَمْدُدْ بِسَبَبٍ إِلَى السَّمَاءِ ثُمَّ لْيَقْطَعْ فَلْيَنظُرْ هَلْ يُذْهِبَنَّ كَيْدُهُ مَا يَغِيظُ ﴿١٥﴾
15. Yeyote yule anayedhani kwamba Allaah Hatomnusuru (Rasuli) duniani na Aakhirah, basi na afunge kitanzi juu, kisha akikate (ajinyoge), na atazame. Je, hila zake zaweza kuondoa yaliyomghadhibisha?
وَكَذَٰلِكَ أَنزَلْنَاهُ آيَاتٍ بَيِّنَاتٍ وَأَنَّ اللَّـهَ يَهْدِي مَن يُرِيدُ ﴿١٦﴾
16. Na hivyo ndivyo Tumeiteremsha (Qur-aan yenye) Aayaat bayana, na kwamba Allaah Humwongoza Amtakaye.
إِنَّ الَّذِينَ آمَنُوا وَالَّذِينَ هَادُوا وَالصَّابِئِينَ وَالنَّصَارَىٰ وَالْمَجُوسَ وَالَّذِينَ أَشْرَكُوا إِنَّ اللَّـهَ يَفْصِلُ بَيْنَهُمْ يَوْمَ الْقِيَامَةِ ۚ إِنَّ اللَّـهَ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ شَهِيدٌ ﴿١٧﴾
17. Hakika wale walioamini, na ambao Mayahudi, na Wasabai; waabudiao nyota, na Manaswara, wa Majusi; waabudiao moto, na wale wanaoshirikisha; hakika Allaah Atahukumu baina yao Siku ya Qiyaamah. Hakika Allaah juu ya kila kitu ni Mwenye kushuhudia.
أَلَمْ تَرَ أَنَّ اللَّـهَ يَسْجُدُ لَهُ مَن فِي السَّمَاوَاتِ وَمَن فِي الْأَرْضِ وَالشَّمْسُ وَالْقَمَرُ وَالنُّجُومُ وَالْجِبَالُ وَالشَّجَرُ وَالدَّوَابُّ وَكَثِيرٌ مِّنَ النَّاسِ ۖ وَكَثِيرٌ حَقَّ عَلَيْهِ الْعَذَابُ ۗ وَمَن يُهِنِ اللَّـهُ فَمَا لَهُ مِن مُّكْرِمٍ ۚإِنَّ اللَّـهَ يَفْعَلُ مَا يَشَاءُ ۩﴿١٨﴾
18. Je, huoni kwamba wanamsujudia Allaah walioko mbinguni na ardhini, na jua, na mwezi na nyota, na majabali na miti na viumbe vinavyotembea, na wengi miongoni mwa watu? Na wengi imewastahiki adhabu. Na ambaye Allaah Amemdhalilisha, basi hatopata wa kumkirimu. Hakika Allaah Anafanya Atakavyo.
هَـٰذَانِ خَصْمَانِ اخْتَصَمُوا فِي رَبِّهِمْ ۖ فَالَّذِينَ كَفَرُوا قُطِّعَتْ لَهُمْ ثِيَابٌ مِّن نَّارٍ يُصَبُّ مِن فَوْقِ رُءُوسِهِمُ الْحَمِيمُ ﴿١٩﴾
19. Hawa ni makhasimu wawili wamekhasimikiana kuhusu Rabb wao. Basi wale waliokufuru watakatiwa nguo za moto watamwagiwa juu ya vichwa vyao maji yachemkayo.
يُصْهَرُ بِهِ مَا فِي بُطُونِهِمْ وَالْجُلُودُ ﴿٢٠﴾
20. Yatayeyusha kwayo (maji hayo) yaliyomo matumboni mwao na ngozi zao.
وَلَهُم مَّقَامِعُ مِنْ حَدِيدٍ ﴿٢١﴾
21. Na watapata marungu ya vyuma.
كُلَّمَا أَرَادُوا أَن يَخْرُجُوا مِنْهَا مِنْ غَمٍّ أُعِيدُوا فِيهَا وَذُوقُوا عَذَابَ الْحَرِيقِ ﴿٢٢﴾
22. Kila watakapotaka kutoka humo kwa dhiki, watarudishwa humo; na (wataambiwa): “Onjeni adhabu ya kuunguza.”
إِنَّ اللَّـهَ يُدْخِلُ الَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ جَنَّاتٍ تَجْرِي مِن تَحْتِهَا الْأَنْهَارُ يُحَلَّوْنَ فِيهَا مِنْ أَسَاوِرَ مِن ذَهَبٍ وَلُؤْلُؤًا ۖ وَلِبَاسُهُمْ فِيهَا حَرِيرٌ ﴿٢٣﴾
23. Hakika Allaah Atawaingiza wale walioamini na wakatenda mema Jannaat zipitazo chini yake mito watapambwa humo vikuku vya dhahabu na lulu, na mavazi yao humo ni hariri.
وَهُدُوا إِلَى الطَّيِّبِ مِنَ الْقَوْلِ وَهُدُوا إِلَىٰ صِرَاطِ الْحَمِيدِ ﴿٢٤﴾
24. Na wataongozwa kwenye kauli nzuri na wataongozwa kwenye njia ya Mwenye kustahiki kuhimidiwa kwa yote.
إِنَّ الَّذِينَ كَفَرُوا وَيَصُدُّونَ عَن سَبِيلِ اللَّـهِ وَالْمَسْجِدِ الْحَرَامِ الَّذِي جَعَلْنَاهُ لِلنَّاسِ سَوَاءً الْعَاكِفُ فِيهِ وَالْبَادِ ۚ وَمَن يُرِدْ فِيهِ بِإِلْحَادٍ بِظُلْمٍ نُّذِقْهُ مِنْ عَذَابٍ أَلِيمٍ ﴿٢٥﴾
25. Hakika wale waliokufuru na wanazuia njia ya Allaah na Al-Masjid Al-Haraam ambao Tumeujaalia kwa watu kuwa ni sawasawa; kwa wakaao humo na wageni. Na yeyote anayekusudia humo kufanya upotofu kwa dhulma Tutamuonjesha adhabu iumizayo.
وَإِذْ بَوَّأْنَا لِإِبْرَاهِيمَ مَكَانَ الْبَيْتِ أَن لَّا تُشْرِكْ بِي شَيْئًا وَطَهِّرْ بَيْتِيَ لِلطَّائِفِينَ وَالْقَائِمِينَ وَالرُّكَّعِ السُّجُودِ ﴿٢٦﴾
26. Na (taja) Tulipomwonyesha Ibraahiym mahali pa Nyumba; Al-Ka’bah, (Tukamwambia): “Usinishirikishe na chochote; na twaharisha Nyumba Yangu kwa wafanyao Twawaaf, na wanaosimama kuswali na wanaorukuu na kusujudu.
وَأَذِّن فِي النَّاسِ بِالْحَجِّ يَأْتُوكَ رِجَالًا وَعَلَىٰ كُلِّ ضَامِرٍ يَأْتِينَ مِن كُلِّ فَجٍّ عَمِيقٍ ﴿٢٧﴾
27. Na tangaza kwa watu Hajj; watakufikia kwa miguu na juu ya kila ngamia aliyekonda, watakuja kutoka katika kila njia pana za milima zilioko mbali kabisa.
لِّيَشْهَدُوا مَنَافِعَ لَهُمْ وَيَذْكُرُوا اسْمَ اللَّـهِ فِي أَيَّامٍ مَّعْلُومَاتٍ عَلَىٰ مَا رَزَقَهُم مِّن بَهِيمَةِ الْأَنْعَامِ ۖ فَكُلُوا مِنْهَا وَأَطْعِمُوا الْبَائِسَ الْفَقِيرَ ﴿٢٨﴾
28. Ili washuhudie manufaa yao; na walitaje Jina la Allaah katika siku maalumu kwa yale Aliyowaruzuku kati ya wanyama wenye miguu minne wa mifugo. Basi kuleni humo, na lisheni mwenye shida fakiri.
ثُمَّ لْيَقْضُوا تَفَثَهُمْ وَلْيُوفُوا نُذُورَهُمْ وَلْيَطَّوَّفُوا بِالْبَيْتِ الْعَتِيقِ ﴿٢٩﴾
29. Kisha wamalize ‘ibaadah zao; wajisafishe taka zao na watimize nadhiri zao, na watufu kwenye Nyumba ya Kale. (Al-Ka’bah).
ذَٰلِكَ وَمَن يُعَظِّمْ حُرُمَاتِ اللَّـهِ فَهُوَ خَيْرٌ لَّهُ عِندَ رَبِّهِ ۗ وَأُحِلَّتْ لَكُمُ الْأَنْعَامُ إِلَّا مَا يُتْلَىٰ عَلَيْكُمْ ۖفَاجْتَنِبُوا الرِّجْسَ مِنَ الْأَوْثَانِ وَاجْتَنِبُوا قَوْلَ الزُّورِ ﴿٣٠﴾
30. Ndio hivyo iwe na yeyote anayeadhimisha vitukufu vya Allaah basi hivyo ni kheri kwake mbele ya Rabb wake. Na mmehalalishiwa wanyama wa mifugo isipokuwa wale mnaosomewa. Basi jiepusheni na uchafu wa (kuabudu) masanamu, na jiepusheni na kauli za uongo.
حُنَفَاءَ لِلَّـهِ غَيْرَ مُشْرِكِينَ بِهِ ۚ وَمَن يُشْرِكْ بِاللَّـهِ فَكَأَنَّمَا خَرَّ مِنَ السَّمَاءِ فَتَخْطَفُهُ الطَّيْرُ أَوْ تَهْوِي بِهِ الرِّيحُ فِي مَكَانٍ سَحِيقٍ ﴿٣١﴾
31. Muelemee haki kwa kumwabudu Allaah Pekee bila ya kumshirikisha. Na yeyote anayemshirikisha Allaah basi kama kwamba ameporomoka kutoka mbinguni, wakamnyakua ndege au upepo ukamtupa mahali mbali mno.
ذَٰلِكَ وَمَن يُعَظِّمْ شَعَائِرَ اللَّـهِ فَإِنَّهَا مِن تَقْوَى الْقُلُوبِ ﴿٣٢﴾
32. Ndivyo hivyo, na yeyote anayeadhimisha Ishara za Allaah, basi hayo ni katika taqwa ya nyoyo.
لَكُمْ فِيهَا مَنَافِعُ إِلَىٰ أَجَلٍ مُّسَمًّى ثُمَّ مَحِلُّهَا إِلَى الْبَيْتِ الْعَتِيقِ ﴿٣٣﴾
33. Katika hao (wanyama) mnapata humo manufaa mpaka muda maalumu uliokadiriwa. Kisha kuhalalika kwake kuchinjwa ni kwenye Nyumba ya Kale. (Haram ya Makkah)
وَلِكُلِّ أُمَّةٍ جَعَلْنَا مَنسَكًا لِّيَذْكُرُوا اسْمَ اللَّـهِ عَلَىٰ مَا رَزَقَهُم مِّن بَهِيمَةِ الْأَنْعَامِ ۗ فَإِلَـٰهُكُمْ إِلَـٰهٌ وَاحِدٌ فَلَهُ أَسْلِمُوا ۗ وَبَشِّرِ الْمُخْبِتِينَ ﴿٣٤﴾
34. Na kwa kila Ummah Tumeweka taratibu za ‘ibaadah ili wataje Jina la Allaah kwa yale Aliyowaruzuku ya wanyama wa miguu minne wa mifugo. Kwa hiyo Muabudiwa wenu wa haki ni Ilaah Mmoja Pekee, basi kwake jisalimisheni. Na wabashirie wanyenyekevu.
الَّذِينَ إِذَا ذُكِرَ اللَّـهُ وَجِلَتْ قُلُوبُهُمْ وَالصَّابِرِينَ عَلَىٰ مَا أَصَابَهُمْ وَالْمُقِيمِي الصَّلَاةِ وَمِمَّا رَزَقْنَاهُمْ يُنفِقُونَ ﴿٣٥﴾
35. Ambao Anapotajwa Allaah nyoyo zao zinajaa khofu na wanaosubiri juu ya yale yaliyowasibu, na wanaosimamisha Swalaah na katika vile Tulivyowaruzuku wanatoa.
وَالْبُدْنَ جَعَلْنَاهَا لَكُم مِّن شَعَائِرِ اللَّـهِ لَكُمْ فِيهَا خَيْرٌ ۖ فَاذْكُرُوا اسْمَ اللَّـهِ عَلَيْهَا صَوَافَّ ۖ فَإِذَا وَجَبَتْ جُنُوبُهَا فَكُلُوا مِنْهَا وَأَطْعِمُوا الْقَانِعَ وَالْمُعْتَرَّ ۚ كَذَٰلِكَ سَخَّرْنَاهَا لَكُمْ لَعَلَّكُمْ تَشْكُرُونَ ﴿٣٦﴾
36. Na ngamia na ng’ombe Tumekufanyieni kuwa ni miongoni mwa Ishara za Allaah; kwa hao mnapata kheri nyingi. Basi tajeni Jina la Allaah juu yao wanapopangwa safu (kuchinjwa). Na waangukapo ubavu, basi kuleni kutoka humo, na lisheni waliokinai na wanaolazimika kuomba. Hivyo ndivyo Tulivyowatiisha kwa ajili yenu ili mpate kushukuru.
لَن يَنَالَ اللَّـهَ لُحُومُهَا وَلَا دِمَاؤُهَا وَلَـٰكِن يَنَالُهُ التَّقْوَىٰ مِنكُمْ ۚ كَذَٰلِكَ سَخَّرَهَا لَكُمْ لِتُكَبِّرُوا اللَّـهَ عَلَىٰ مَا هَدَاكُمْ ۗ وَبَشِّرِ الْمُحْسِنِينَ ﴿٣٧﴾
37. Haimfikii Allaah nyama zake wala damu yake, lakini inamfikia taqwa kutoka kwenu. Hivyo ndivyo Tulivyowatiisha kwenu ili mpate kumtukuza Allaah; Allaahu Akbar, kwa yale Aliyokuongozeni; na wabashirie wafanyao ihsaan.
إِنَّ اللَّـهَ يُدَافِعُ عَنِ الَّذِينَ آمَنُوا ۗ إِنَّ اللَّـهَ لَا يُحِبُّ كُلَّ خَوَّانٍ كَفُورٍ ﴿٣٨﴾
38. Hakika Allaah Anawalinda wale walioamini. Hakika Allaah Hampendi kila mwingi wa kukhaini, mwingi wa kukufuru.
أُذِنَ لِلَّذِينَ يُقَاتَلُونَ بِأَنَّهُمْ ظُلِمُوا ۚ وَإِنَّ اللَّـهَ عَلَىٰ نَصْرِهِمْ لَقَدِيرٌ ﴿٣٩﴾
39. Wameruhusiwa (kupigana) kwa wale wanaopigwa kwa kuwa wamedhulumiwa. Na kwamba Allaah bila shaka ni Muweza wa kuwanusuru.
الَّذِينَ أُخْرِجُوا مِن دِيَارِهِم بِغَيْرِ حَقٍّ إِلَّا أَن يَقُولُوا رَبُّنَا اللَّـهُ ۗ وَلَوْلَا دَفْعُ اللَّـهِ النَّاسَ بَعْضَهُم بِبَعْضٍ لَّهُدِّمَتْ صَوَامِعُ وَبِيَعٌ وَصَلَوَاتٌ وَمَسَاجِدُ يُذْكَرُ فِيهَا اسْمُ اللَّـهِ كَثِيرًا ۗ وَلَيَنصُرَنَّ اللَّـهُ مَن يَنصُرُهُ ۗ إِنَّ اللَّـهَ لَقَوِيٌّ عَزِيزٌ ﴿٤٠﴾
40. Ambao wametolewa majumbani mwao bila ya haki isipokuwa kwa kuwa wanasema: “Rabb wetu ni Allaah.” Na lau ingelikuwa Allaah Hawakingi watu baadhi yao kwa wengine, bila shaka yangelivunjwa mahekalu na makanisa, na masinagogi na misikiti inayotajwa humo Jina la Allaah kwa wingi. Na bila shaka Allaah Atamnusuru yeyote yule anayenusuru Dini Yake. Hakika Allaah bila shaka ni Mwenye nguvu zote, Mwenye enzi ya nguvu Asiyeshindika.
الَّذِينَ إِن مَّكَّنَّاهُمْ فِي الْأَرْضِ أَقَامُوا الصَّلَاةَ وَآتَوُا الزَّكَاةَ وَأَمَرُوا بِالْمَعْرُوفِ وَنَهَوْا عَنِ الْمُنكَرِ ۗوَلِلَّـهِ عَاقِبَةُ الْأُمُورِ ﴿٤١﴾
41. Ambao Tukiwamakinisha katika ardhi, husimamisha Swalaah na hutoa Zakaah, na huamrisha mema na hukataza munkari. Na kwa Allaah Pekee ndio hatima ya mambo yote.
وَإِن يُكَذِّبُوكَ فَقَدْ كَذَّبَتْ قَبْلَهُمْ قَوْمُ نُوحٍ وَعَادٌ وَثَمُودُ ﴿٤٢﴾
42. Na wakikukadhibisha, basi wamekwishakadhibisha kabla yao watu wa Nuwh na ‘Aad na Thamuwd.
وَقَوْمُ إِبْرَاهِيمَ وَقَوْمُ لُوطٍ ﴿٤٣﴾
43. Na watu wa Ibraahiym, na watu wa Luutw.
وَأَصْحَابُ مَدْيَنَ ۖ وَكُذِّبَ مُوسَىٰ فَأَمْلَيْتُ لِلْكَافِرِينَ ثُمَّ أَخَذْتُهُمْ ۖ فَكَيْفَ كَانَ نَكِيرِ ﴿٤٤﴾
44. Na watu wa Madyan na alikadhibishwa Muwsaa, basi Nikawapa muhula makafiri, kisha Nikawachukua. Basi vipi ilikuwa adhabu Yangu.
فَكَأَيِّن مِّن قَرْيَةٍ أَهْلَكْنَاهَا وَهِيَ ظَالِمَةٌ فَهِيَ خَاوِيَةٌ عَلَىٰ عُرُوشِهَا وَبِئْرٍ مُّعَطَّلَةٍ وَقَصْرٍ مَّشِيدٍ ﴿٤٥﴾
45. Miji mingapi Tumeiangamiza iliyokuwa ikidhulumu basi ikaanguka juu ya mapaa yake, na visima vilivyohamwa na makasri madhubuti?
أَفَلَمْ يَسِيرُوا فِي الْأَرْضِ فَتَكُونَ لَهُمْ قُلُوبٌ يَعْقِلُونَ بِهَا أَوْ آذَانٌ يَسْمَعُونَ بِهَا ۖ فَإِنَّهَا لَا تَعْمَى الْأَبْصَارُ وَلَـٰكِن تَعْمَى الْقُلُوبُ الَّتِي فِي الصُّدُورِ ﴿٤٦﴾
46. Je, basi hawatembei katika ardhi ili wapate kuwa na nyoyo za kutia akilini au masikio ya kusikilizia; kwani hakika hayapofuki macho, lakini zinazopofuka ni nyoyo ziliomo vifuani.
وَيَسْتَعْجِلُونَكَ بِالْعَذَابِ وَلَن يُخْلِفَ اللَّـهُ وَعْدَهُ ۚ وَإِنَّ يَوْمًا عِندَ رَبِّكَ كَأَلْفِ سَنَةٍ مِّمَّا تَعُدُّونَ ﴿٤٧﴾
47. Na wanakuhimiza kwa adhabu, na Allaah Hakhalifu ahadi Yake. Na hakika siku moja kwa Rabb wako ni kama miaka elfu katika yale mnayoihesabu.
وَكَأَيِّن مِّن قَرْيَةٍ أَمْلَيْتُ لَهَا وَهِيَ ظَالِمَةٌ ثُمَّ أَخَذْتُهَا وَإِلَيَّ الْمَصِيرُ ﴿٤٨﴾
48. Na miji mingapi Nimeipa muhula na hali imedhulumu, kisha Nikaikamata (kuiadhibu) na Kwangu Pekee ni mahali pa kuishia.
قُلْ يَا أَيُّهَا النَّاسُ إِنَّمَا أَنَا لَكُمْ نَذِيرٌ مُّبِينٌ ﴿٤٩﴾
49. Sema: “Eenyi watu! Hakika mimi kwenu ni mwonyaji dhahiri.
فَالَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ لَهُم مَّغْفِرَةٌ وَرِزْقٌ كَرِيمٌ ﴿٥٠﴾
50. Basi wale walioamini na wakatenda mema, watapata maghfirah na riziki karimu.
وَالَّذِينَ سَعَوْا فِي آيَاتِنَا مُعَاجِزِينَ أُولَـٰئِكَ أَصْحَابُ الْجَحِيمِ ﴿٥١﴾
51. Na wale waliokwenda mbio katika kupinga Aayaat (na ishara) Zetu, hao ni watu wa moto uwakao vikali mno.
وَمَا أَرْسَلْنَا مِن قَبْلِكَ مِن رَّسُولٍ وَلَا نَبِيٍّ إِلَّا إِذَا تَمَنَّىٰ أَلْقَى الشَّيْطَانُ فِي أُمْنِيَّتِهِ فَيَنسَخُ اللَّـهُ مَا يُلْقِي الشَّيْطَانُ ثُمَّ يُحْكِمُ اللَّـهُ آيَاتِهِ ۗ وَاللَّـهُ عَلِيمٌ حَكِيمٌ ﴿٥٢﴾
52. Na Hatukutuma kabla yako Rasuli yeyote na wala Nabiy yeyote isipokuwa anaposoma Kitabu cha Allaah au kubalighisha ujumbe, shaytwaan humtupia (batili) ya matamanio yake; lakini Allaah Hufuta yale anayoyatupia shaytwaan kisha Allaah Anathibitisha Aayaat Zake, na Allaah ni Mjuzi wa yote, Mwenye hikmah wa yote.
لِّيَجْعَلَ مَا يُلْقِي الشَّيْطَانُ فِتْنَةً لِّلَّذِينَ فِي قُلُوبِهِم مَّرَضٌ وَالْقَاسِيَةِ قُلُوبُهُمْ ۗ وَإِنَّ الظَّالِمِينَ لَفِي شِقَاقٍ بَعِيدٍ ﴿٥٣﴾
53. Ili (Allaah) Afanye yale aliyoyatupa shaytwaan kuwa ni fitnah kwa wale wenye maradhi katika nyoyo zao na nyoyo zao ni ngumu. Na hakika madhalimu bila shaka wamo katika upinzani wa mbali.
وَلِيَعْلَمَ الَّذِينَ أُوتُوا الْعِلْمَ أَنَّهُ الْحَقُّ مِن رَّبِّكَ فَيُؤْمِنُوا بِهِ فَتُخْبِتَ لَهُ قُلُوبُهُمْ ۗ وَإِنَّ اللَّـهَ لَهَادِ الَّذِينَ آمَنُوا إِلَىٰ صِرَاطٍ مُّسْتَقِيمٍ ﴿٥٤﴾
54. Na ili wajue wale waliopewa elimu kwamba hii (Qur-aan) ni haki kutoka kwa Rabb wao, hivyo waiamini, na zijisalimishe kwayo kwa unyenyekevu nyoyo zao. Na kwamba hakika Allaah Ndiye Anayewaongoza wale walioamini kuelekea njia iliyonyooka.
وَلَا يَزَالُ الَّذِينَ كَفَرُوا فِي مِرْيَةٍ مِّنْهُ حَتَّىٰ تَأْتِيَهُمُ السَّاعَةُ بَغْتَةً أَوْ يَأْتِيَهُمْ عَذَابُ يَوْمٍ عَقِيمٍ ﴿٥٥﴾
55. Na hawatoacha wale waliokufuru kuwa katika shaka nayo (Qur-aan), mpaka iwafikie Saa ghaflah, au iwafikie adhabu ya siku kame (isiyokuwa na kheri kwao).
الْمُلْكُ يَوْمَئِذٍ لِّلَّـهِ يَحْكُمُ بَيْنَهُمْ ۚ فَالَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ فِي جَنَّاتِ النَّعِيمِ ﴿٥٦﴾
56. Ufalme Siku hiyo ni wa Allaah Pekee; Atahukumu baina yao; basi wale walioamini na wakatenda mema, watakuwa katika Jannaat za neema.
وَالَّذِينَ كَفَرُوا وَكَذَّبُوا بِآيَاتِنَا فَأُولَـٰئِكَ لَهُمْ عَذَابٌ مُّهِينٌ ﴿٥٧﴾
57. Na wale waliokufuru na wakakadhibisha Aayaat (na ishara) Zetu; basi hao watapata adhabu ya kudhalilisha.
وَالَّذِينَ هَاجَرُوا فِي سَبِيلِ اللَّـهِ ثُمَّ قُتِلُوا أَوْ مَاتُوا لَيَرْزُقَنَّهُمُ اللَّـهُ رِزْقًا حَسَنًا ۚ وَإِنَّ اللَّـهَ لَهُوَ خَيْرُ الرَّازِقِينَ ﴿٥٨﴾
58. Na wale waliohajiri katika njia ya Allaah, kisha wakauawa, au wakafa, bila shaka Allaah Atawaruzuku riziki nzuri. Na hakika Allaah bila shaka Yeye Ndiye Mbora wa wenye kuruzuku.
لَيُدْخِلَنَّهُم مُّدْخَلًا يَرْضَوْنَهُ ۗ وَإِنَّ اللَّـهَ لَعَلِيمٌ حَلِيمٌ ﴿٥٩﴾
59. Atawaingiza mahala watakaouridhia. Na hakika Allaah bila shaka ni Mjuzi wa yote, Mpole wa kuwavumilia waja.
ذَٰلِكَ وَمَنْ عَاقَبَ بِمِثْلِ مَا عُوقِبَ بِهِ ثُمَّ بُغِيَ عَلَيْهِ لَيَنصُرَنَّهُ اللَّـهُ ۗ إِنَّ اللَّـهَ لَعَفُوٌّ غَفُورٌ ﴿٦٠﴾
60. Ndivyo hivyo, na yeyote anayejilipiza mfano wa alivyoadhibiwa, kisha akakandamizwa; bila shaka Allaah Atamnusuru. Na hakika Allaah bila shaka ni Mwingi wa kusameh, Mwingi wa kughufuria.
ذَٰلِكَ بِأَنَّ اللَّـهَ يُولِجُ اللَّيْلَ فِي النَّهَارِ وَيُولِجُ النَّهَارَ فِي اللَّيْلِ وَأَنَّ اللَّـهَ سَمِيعٌ بَصِيرٌ ﴿٦١﴾
61. Hivyo ni kwa kuwa Allaah Anaingiza usiku katika mchana, na Anaingiza mchana katika usiku; na kwamba Allaah ni Mwenye kusikia yote, Mwenye kuona yote.
ذَٰلِكَ بِأَنَّ اللَّـهَ هُوَ الْحَقُّ وَأَنَّ مَا يَدْعُونَ مِن دُونِهِ هُوَ الْبَاطِلُ وَأَنَّ اللَّـهَ هُوَ الْعَلِيُّ الْكَبِيرُ ﴿٦٢﴾
62. Hivyo ni kwa kuwa Allaah Ndiye wa Haki na kwamba vile wanavyoomba badala Yake ndiyo batili; na kwamba Allaah Ndiye Mwenye ‘Uluwa, Ametukuka, Mkubwa wa dhati, vitendo na sifa.
أَلَمْ تَرَ أَنَّ اللَّـهَ أَنزَلَ مِنَ السَّمَاءِ مَاءً فَتُصْبِحُ الْأَرْضُ مُخْضَرَّةً ۗ إِنَّ اللَّـهَ لَطِيفٌ خَبِيرٌ ﴿٦٣﴾
63. Je, huoni kwamba Allaah Ameteremsha kutoka mbinguni maji kisha ardhi ikawa chanikiwiti. Hakika Allaah bila shaka ni Mwenye kudabiri mambo kwa ulatifu, Mwenye upeo wa khabari za dhahiri na za kufichika.
لَّهُ مَا فِي السَّمَاوَاتِ وَمَا فِي الْأَرْضِ ۗ وَإِنَّ اللَّـهَ لَهُوَ الْغَنِيُّ الْحَمِيدُ ﴿٦٤﴾
64. Ni Vyake pekee vyote vile viliomo mbinguni na vile viliomo ardhini. Na hakika Allaah bila shaka Yeye Ndiye Mkwasi, Mwenye kustahiki kuhimidiwa kwa yote.
أَلَمْ تَرَ أَنَّ اللَّـهَ سَخَّرَ لَكُم مَّا فِي الْأَرْضِ وَالْفُلْكَ تَجْرِي فِي الْبَحْرِ بِأَمْرِهِ وَيُمْسِكُ السَّمَاءَ أَن تَقَعَ عَلَى الْأَرْضِ إِلَّا بِإِذْنِهِ ۗ إِنَّ اللَّـهَ بِالنَّاسِ لَرَءُوفٌ رَّحِيمٌ ﴿٦٥﴾
65. Je, huoni kwamba Allaah Amevitiisha kwa ajili yenu vile viliomo katika ardhi na merikebu zipitazo baharini kwa amri Yake. Na Anazuia mbingu zisianguke juu ya ardhi isipokuwa kwa idhini Yake. Hakika Allaah kwa watu ni Mwenye huruma mno, Mwenye kurehemu.
وَهُوَ الَّذِي أَحْيَاكُمْ ثُمَّ يُمِيتُكُمْ ثُمَّ يُحْيِيكُمْ ۗ إِنَّ الْإِنسَانَ لَكَفُورٌ ﴿٦٦﴾
66. Naye Ndiye Ambaye Anakuhuisheni, kisha Anakufisheni, kisha Atakuhuisheni. Hakika insani ni mwingi wa kukufuru.
لِّكُلِّ أُمَّةٍ جَعَلْنَا مَنسَكًا هُمْ نَاسِكُوهُ ۖ فَلَا يُنَازِعُنَّكَ فِي الْأَمْرِ ۚ وَادْعُ إِلَىٰ رَبِّكَ ۖ إِنَّكَ لَعَلَىٰ هُدًى مُّسْتَقِيمٍ ﴿٦٧﴾
67. Kwa kila Ummah Tumejaalia taratibu za ‘ibaadah wanazozifuata. Basi wasizozane nawe (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) kabisa katika jambo hili; na walinganie kwa Rabb wako. Hakika wewe bila shaka uko juu ya Mwongozo ulionyooka.
وَإِن جَادَلُوكَ فَقُلِ اللَّـهُ أَعْلَمُ بِمَا تَعْمَلُونَ ﴿٦٨﴾
68. Na wakibishana nawe (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم), basi sema: “Allaah Anajua zaidi yale mnayoyafanya.”
اللَّـهُ يَحْكُمُ بَيْنَكُمْ يَوْمَ الْقِيَامَةِ فِيمَا كُنتُمْ فِيهِ تَخْتَلِفُونَ ﴿٦٩﴾
69. “Allaah Atahukumu baina yenu Siku ya Qiyaamah katika yale mliyokuwa mnakhitilafiana.”
أَلَمْ تَعْلَمْ أَنَّ اللَّـهَ يَعْلَمُ مَا فِي السَّمَاءِ وَالْأَرْضِ ۗ إِنَّ ذَٰلِكَ فِي كِتَابٍ ۚ إِنَّ ذَٰلِكَ عَلَى اللَّـهِ يَسِيرٌ ﴿٧٠﴾
70. Je, hujui kwamba Allaah Anajua yale yote yaliyomo katika mbingu na ardhi? Hakika hayo yamo katika Kitabu. Hakika hayo kwa Allaah ni mepesi.
وَيَعْبُدُونَ مِن دُونِ اللَّـهِ مَا لَمْ يُنَزِّلْ بِهِ سُلْطَانًا وَمَا لَيْسَ لَهُم بِهِ عِلْمٌ ۗ وَمَا لِلظَّالِمِينَ مِن نَّصِيرٍ﴿٧١﴾
71. Wanaabudu badala ya Allaah ambayo Hakuyateremshia mamlaka, na ambayo hawana elimu nayo. Na madhalimu hawana yeyote mwenye kunusuru.
وَإِذَا تُتْلَىٰ عَلَيْهِمْ آيَاتُنَا بَيِّنَاتٍ تَعْرِفُ فِي وُجُوهِ الَّذِينَ كَفَرُوا الْمُنكَرَ ۖ يَكَادُونَ يَسْطُونَ بِالَّذِينَ يَتْلُونَ عَلَيْهِمْ آيَاتِنَا ۗ قُلْ أَفَأُنَبِّئُكُم بِشَرٍّ مِّن ذَٰلِكُمُ ۗ النَّارُ وَعَدَهَا اللَّـهُ الَّذِينَ كَفَرُوا ۖ وَبِئْسَ الْمَصِيرُ ﴿٧٢﴾
72. Na wanaposomewa Aayaat Zetu bayana, utatambua katika nyuso za wale waliokufuru karaha. Wanakaribia kuwashambulia wale wanaowasomea Aayaat Zetu. Sema (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم): “Je, nikujulisheni yaliyo shari zaidi kuliko hayo kwenu? Ni moto; Aliowaahidi Allaah wale waliokufuru. Na ni ubaya ulioje mahali pa kuishia.
يَا أَيُّهَا النَّاسُ ضُرِبَ مَثَلٌ فَاسْتَمِعُوا لَهُ ۚ إِنَّ الَّذِينَ تَدْعُونَ مِن دُونِ اللَّـهِ لَن يَخْلُقُوا ذُبَابًا وَلَوِ اجْتَمَعُوا لَهُ ۖ وَإِن يَسْلُبْهُمُ الذُّبَابُ شَيْئًا لَّا يَسْتَنقِذُوهُ مِنْهُ ۚ ضَعُفَ الطَّالِبُ وَالْمَطْلُوبُ ﴿٧٣﴾
73. Enyi watu! Imepigwa mfano basi isikilizeni kwa makini! Hakika wale mnaowaomba badala ya Allaah hawawezi kuumba nzi japo wakijumuika kwa hilo. Na nzi akiwapokonya kitu chochote kile hawawezi kukiambua tena. Amedhoofika mwenye kutaka matilabu na mwenye kutakiwa.
مَا قَدَرُوا اللَّـهَ حَقَّ قَدْرِهِ ۗ إِنَّ اللَّـهَ لَقَوِيٌّ عَزِيزٌ ﴿٧٤﴾
74. Hawakumkadiria Allaah kama inavyostahiki kumkadiria. Hakika Allaah bila shaka ni Mwenye nguvu zote, Mwenye enzi ya nguvu Asiyeshindika.
اللَّـهُ يَصْطَفِي مِنَ الْمَلَائِكَةِ رُسُلًا وَمِنَ النَّاسِ ۚ إِنَّ اللَّـهَ سَمِيعٌ بَصِيرٌ ﴿٧٥﴾
75. Allaah Anakhitari Wajumbe miongoni mwa Malaika na miongoni mwa watu. Hakika Allaah ni Mwenye kusikia yote, Mwenye kuona yote.
يَعْلَمُ مَا بَيْنَ أَيْدِيهِمْ وَمَا خَلْفَهُمْ ۗ وَإِلَى اللَّـهِ تُرْجَعُ الْأُمُورُ ﴿٧٦﴾
76. Anajua yale yaliyoko mbele yao, na yale yaliyoko nyuma yao. Na kwa Allaah yanarejeshwa mambo yote.
يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا ارْكَعُوا وَاسْجُدُوا وَاعْبُدُوا رَبَّكُمْ وَافْعَلُوا الْخَيْرَ لَعَلَّكُمْ تُفْلِحُونَ ۩﴿٧٧﴾
77. Enyi walioamini! Rukuuni, na sujuduni na mwabuduni Rabb wenu, na fanyeni ya kheri ili mpata kufaulu.
وَجَاهِدُوا فِي اللَّـهِ حَقَّ جِهَادِهِ ۚ هُوَ اجْتَبَاكُمْ وَمَا جَعَلَ عَلَيْكُمْ فِي الدِّينِ مِنْ حَرَجٍ ۚ مِّلَّةَ أَبِيكُمْ إِبْرَاهِيمَۚ هُوَ سَمَّاكُمُ الْمُسْلِمِينَ مِن قَبْلُ وَفِي هَـٰذَا لِيَكُونَ الرَّسُولُ شَهِيدًا عَلَيْكُمْ وَتَكُونُوا شُهَدَاءَ عَلَى النَّاسِ ۚفَأَقِيمُوا الصَّلَاةَ وَآتُوا الزَّكَاةَ وَاعْتَصِمُوا بِاللَّـهِ هُوَ مَوْلَاكُمْ ۖ فَنِعْمَ الْمَوْلَىٰ وَنِعْمَ النَّصِيرُ ﴿٧٨﴾
78. Na fanyeni jihaad katika njia ya Allaah kama inavyostahiki kufanyiwa jihaad. Yeye Ndiye Amekuteueni na Hakukufanyieni ugumu wowote ule katika Dini. Mila ya baba yenu Ibraahiym. Yeye (Allaah) Ndiye Aliyekuiteni Waislamu hapo zamani na pia katika hii (Qur-aan). Ili Rasuli (Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) awe shahidi juu yenu, nanyi muwe mashahidi juu ya watu. Basi simamisheni Swalaah na toeni Zakaah, na shikamaneni pamoja kwa ajili ya Allaah, Yeye Ndiye Mola Mlinzi wenu. Basi Mzuri Alioje Mola Mlinzi na Mzuri Alioje Mwenye kunusuru.
0 Comments